Duka la Mariedo na bidhaa bandia

SWAZI

Member
Aug 2, 2011
87
19
duka la mariedo na bidhaa FEKI na CHEAP

Kwanza maduka yao yako so depressing...rangi rangi nyingii utafkiri yale cover ya sinema za porn za 1960's

pili sijui kwa nini wanauza vitu feki feki tena kwa bei za juu

na mbaya zaidi wameingi akwenye mkumbo wa network za ufisadi na baadhi ya maofisa wa mashirika ya serikali kwa kuwauzia staff uniform ambazo hazina chembe ya Quality...soma taarifa za mkaguzi mkuu wa serikali CAG juu ya ifisadi wa Mariedo na aliyekuwa spika samuel sitta

Sasa kuna mtu aliwa blast kule kwenye siasa lakini nimeona ma celebrity wetu nao wanaingizwa kwenye mkumbo wa kuwasafisha hawa jamaa wakati wanawaliza watu

ndio mshaonywa tena
 
mh! Ufisadi kwenye nguo???? Kweli Allah atuhurumie hadi basic needs ka makazi, mavazi na chakula zoote tunapigwa cheusi chekundu hata huruma hawana looooooh!
 
Nimesikia pia wameingia mkataba na benki fulani iliyozindua mastercard yake hivi karibuni, je huu pia ni muendelezo wa ufisadi?
 
Maduka mengi ya nguo mjini hapa wanatuuzia vitu feki, you have to be extra careful
 
Mi Ze shoping yangu nafanyiwa na mama watoto K-Koo...suti nzuriiii laki moja u nusu tu!!
 
Hapo mwanzo uliposema bidhaa FEKI na CHEAP nilistuka by cheap unamaanisha nini! Manake wanauza bei ghali unnecessarily! Duka lao la BW Mkapa, ukienda next shop tu unakuta exactly the same thing tofauti ya bei na Mariedo ni laki 1 au 2! Kupanga ni kuchagua!
 
Sinatatizo na ulichoandika ila nashindwa kujua SITA ametoka wapi katika hili !!
 
JAMANI UNUNUZI KATIKA TAASISI ZETU UNAFUATA "minimum procurement procedures" na sheria za manunuzi ya UMAMA za PPRA, na kila mtu anajua sheria hii ilivyoboreshwa hivi karibuni.....!! sasa kama wameshinda tenda husika sioni tatizo linatoka wapi....!! kuna vitu vingi vya kujenga tunavyotakiwa kuendelea kuadress.:A S embarassed:
 
Hapo mwanzo uliposema bidhaa FEKI na CHEAP nilistuka by cheap unamaanisha nini! Manake wanauza bei ghali unnecessarily! Duka lao la BW Mkapa, ukienda next shop tu unakuta exactly the same thing tofauti ya bei na Mariedo ni laki 1 au 2! Kupanga ni kuchagua!


heehhehe King'asti....imebidi nicheke....maana ...kila JIJI lina mitaa yake na maduka yake ya ghali! Inabidi mtu apapase mfuko na kujielewa yuko wapi kwenye "mashopping"
Ukienda Pariiiiiiiii ( Paris) mitaa ya Champs Elysee -- bei zake usipime hata kama vitu vinafanana na mitaa mingine .Nenda London - huwezi kulinganisha bei za Oxford Street na Shepherds Bush . Huwezi kulinganisha bei za Harrods na maduka mengine.
New York - go shop at Conway achana na Macy's hahahhah.

DSM ukiingia Mariedo na laki zako 3 utaambulia pea ya kiatu au handbag. Wakati Kariakoo hiyo hiyo utavaa suit na accessories lol.

Msilaumu bei ati kwa vile bidhaa zafafanana.
Kumbuka kuna suala la being "excusive" na "buying a brand"!
 
heehhehe King'asti....imebidi nicheke....maana ...kila JIJI lina mitaa yake na maduka yake ya ghali! Inabidi mtu apapase mfuko na kujielewa yuko wapi kwenye "mashopping"
Ukienda Pariiiiiiiii ( Paris) mitaa ya Champs Elysee -- bei zake usipime hata kama vitu vinafanana na mitaa mingine
.Nenda London - huwezi kulinganisha bei za Oxford Street na Shepherds Bush . Huwezi kulinganisha bei za Harrods na maduka mengine.
New York - go shop at Conway achana na Macy's hahahhah.

DSM ukiingia Mariedo na laki zako 3 utaambulia pea ya kiatu au handbag. Wakati Kariakoo hiyo hiyo utavaa suit na accessories lol.

Msilaumu bei ati kwa vile bidhaa zafafanana.
Kumbuka kuna suala la being "excusive" na "buying a brand"!
si kweli

na kama tofauti ipo nasi ni paundi moja au mbili
 
Eh huyu mama sijui bado yupo na NSSF kwenye mkataba wa uniform? maana kuna kipindi alikuwa anasupply uniforms za NSSF , jamani suruali zinaharibika baaada ya kuvaa mara tatu tu! halafu anasupply nyingine Mh!! , tie hazina ubora hata kidogo yaani ni UFISADI! lakini msimlaumu sana huyu mama inabidi muangalie mambo ya procurement hapo NSSF inawezekana ni 10% kwa kwenda mblel! halafu ni MJANJA SANA! amekodi eneo hapo Benjamin Mkapa plaza na kodi inajilipa kwa kuwauzia nguo hao hao NSSf tena ZISIZO NA UBORA! mimi nasema kama nguo zingekuwa na ubora wala si shida sana kwa sababu ingekuwa ni NSSf wanafaidika na yeye pia lakini nguo hazina ubora! na wafanyakazi wanalalama sana! ila watakimbilia wapi??? na kitu kingine kinasikitisha watavaa nguo hizo baada ya mwenzi wanaacha WANAVAA NGUO ZAO ZA KAWAIDA! PESA YETU JAMANI MWAIFISIDI KWANINI????? Bora hata tungepewa wenyewe mikopo!
 
Hapa tutasema mpaka makoo yatakauka,wala hao wahusika hawajali wanajali mifuko yao kujaa noti.Mariedo kwa sasa atapeta akija mwenzie mwenye dau kubwa atapigwa chini mwenzie ataendelea....
 
si kweli

na kama tofauti ipo nasi ni paundi moja au mbili
Na quality ni tofauti.

Miezi mitatu iliyopita nilikuwa london, nikaenda kufanya Shopping Debenhams,3 pack of boxer shorts nilinunua kwa paundi 20. Rafiki yangu mkenya akanishauri twende Shephards Bush market, nilipoona paki ya boxer tatu kwa paundi 5, nikaanza kujuta kwa nini nimenunua Oxford Street, lakini kabla hata sijapanda ndege zile za paundi tano zilishaanza kuchanika

Kama mtu alivyosema hapo juu, cheap is dear in the long run. Kuna tofauti kubwa ya quality ya nike tracksuit utakayo nunua Oxford street paundi 70 na nike utakayo nunua Shephard Bush kwa paundi 25.

Kwa hapa Bongo ni tofauti, bidhaa zinatoka same source lakini ukienda kwenye maduka yenye majina makubwa bei ni za juu sana na kulinganisha na maduka mengine bei niza kawaida lakini quality zote ni kama za Shephard Bush
 
Still ni tofauti lol....MARIEDO ni kama HARRODS YA BONGO... LOL usilianzishe tu
...soma kwamba " you should peg urself where u belong" hata kama the difference is a dime.
Harrods imekuwa famous kwa ajili ya nice products, high quality and good services.Mtu yoyote anapokwenda Harrods anatazamia TOP QUALITY.

Lakini Mariedo, kama mtu alivyolalamika hapo juu, unaweza kununua nguo baada ya siku tatu inaanza kufumuka.Kwa Harrods ikitokea hivyo mara kwa mara ni Skendo
 
kuvaa kitu cha thamani ina raha yake hata kitu hikohiko unaweza kukipata sehemu nyingine kwa bei rahisi..........simple but expensive is my motto!halafu vyombo vikae mwilini!
 
Napenda sana kuvaa vizuri,nadhani ndio maana mademu wananizimia kinoma..
 
Back
Top Bottom