Duka la Dawa Muhimu za Binadamu (Pharmacy): Utaratibu wa Kufuata na Mtaji wa Kuanzisha Biashara

Mtaji utategemea na namna ya duka unalotaka kuanzisha lakini ili duka lionekane hasa ni duka si chini ya 20M.

Taratibu za kisheria ni lazima uwe na cheti cha mfamasia ambacho ndy utatumia kufungua hilo duka,pia uwe na muuzaji

au wauzaji waliosoma kozi za maduka ya dawa muhimu na pia kozi hiyo ipo pia kwa wamiliki wa maduka pia inatakiwa

usomee,hizo kozi zilikuwa zinafanyika wilayani na mikoani kuanzia mwaka jana sijui sasa kwa ambao hawakusoma mwaka

jana utaratibu ukoje na pia sina uhakika kama imeshaisha tanzania nzima.

Walikuwa wanasisitiza hivyo ndiyo vitakuwa vigezo hasa sijui lakini tofauti na hapo inakuwaje,watakuja wengine kukujuza

zaidi.

Kuhusu usimamizi sijaelewa unamaanisha usimamizi wa namna gani?..

Ili mali yako isipotee wengine wanauza mtu wako unayemwamini kazi yake ni kupokea pesa.

Ni biashara inayolipa sana ukiwa sehemu nzuri na wahudumu wazuri bila kusahau kuwa kidigitali zaidi..
 
Kwa vile fani yako ni mwalimu, nakushauri ufungue biashara kutokana na fani yako ili usije angukia pua mkuu.
Afungue shule watoto wa awali - inalipa
Afungue Stationary - inalipa
Sasa bwana mifugo na karani wapi na wapi.
Fanyeni biashara kulingana na taaluma mlizo nazo
 
Kwa vile fani yako ni mwalimu, nakushauri ufungue biashara kutokana na fani yako ili usije angukia pua mkuu.
Bila shaka umenena. Kuna askari wa kikosi cha mbwa yeye anafuga mbwa binafsi jioni anawapeleka kwenye malindo. Mwisho wa mwezi anavuta pesa zake.
 
Naona hapo juu wajanja washaanza kukuotesha mbawa(kumbuka ukitaka kumuua sisimizi muoteshe mbawa!akiruka juu anakutana na kunguru wakidhani ni kumbikumbi,akishuka chini anakutana na binadamu atamkanyaga).

Ushauri wangu: Ulikuwa sahihi kuwaza kufungua duka la dawa muhimu na siyo Pharmacy kwani capital ni ndogo kwa kuangalia yafuatayo.

Gharama ya pango la chumba kikubwa angalau ft 20 x12 na height 10 vinalipiwa kwa mwaka sh.1,800,000,mlango wa kioo(aluminium)600,000,shelves za gharama ya chini kabisa sh.1,500,000,Ac 700,000. Gharama nyingine ndogo ndogo pamoja na rangi fanya 1,000,000. Gharama za kumlipa mfamasia angalau kwa miezi sita(jamaa huwa wanachukua kwa miezi sita hadi mwaka)6,000,000 ie 1M kila mwezi ukipiga hesabu unabaki na 8.4M kwa ununuzi wa dawa.

Hapo unaweza kufungua Pharmacy ingawa kuna gharama za kulipia kibali leseni na mapato.

Pia gharama za kumlipa muuzaji kwani mfamasia hawezi kukaa dukani kuuza kwa hiyo M.1 ya kila mwezi huyu atakuwa ama ameajiriwa na serkali au mashirika/makampuni ambako ndipo atatumia muda wake mwingi.

Hapo kwako ataweka cheti tu.

Hata hivyo ni Muhimu kupata sehemu inayofikika kwa urahisi na watu wengi kitu ambacho unalazimika umuhamishe mtu kwa gharama zaidi.

Uwe makini usidanganywe kuwa biashara hii ina faida kubwa saana!La hasha,hii ilikuwa zamani.

Ukiweza kufanya biashara ya jumla unaweza kupata zaidi kwani kwenye retail ushindani ni mkubwa sana.

Mwisho nakushari anza na duka la dawa muhimu kwa kiasi kidogo cha pesa halafu,ukizijua changamoto zilizopo,unaweza kuamua kwenda mbele kufungua pharmacy.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Wasaalam nyote.

Shukrani kwa Kibaravumba na nyote mliotoa constructive comments.

King kong, sina hizo sifa za kutafuta PM za wadada kama unavyohisi. Baadirisha ur negativity thinking ndugu yangu maana unafkiria watu wote wana tabia kama hizo

Nilifanikiwa kuanzisha duka mwezi May baada ya kuongeza kamtaji na kufikia around Tshs. 30m. In my road map, after one year nilipanga kuombea kamkopo bank or other financial institution for about Tsh. 40m kwaajili ya kufungua sehemu nyingine hapa hapa Dar after analyse the market and all other relevant info.

Najitahidi kukeep all info (financial and non-financial) updated ili inisaidie kujua wapi natakiwa kufanya nini kwa wakati gani.

Naelewa biashara ina challange nyingi sana na najua ntapata challange zaidi sku zijazo lakini naamaini kila kunapo challange njia inapatikana kama una malengo

Nakaribisha michago yenu ambayo itakayojenga na sio kubomoa maana naamini humu ndani kuna watu wanaofanya hii biashara na wanaelewa uendeshaji wake unavyokuwa.

Shukrani sana na nawatakia mapumziko mema.
 
Mkuu hongera sana kwa kuanza biashara.
 
Gud start kwani hata philips sijui megido walianzia chini leo wapo juu mbaya.
 
Kaka hongera saana kwa mafanikio na uthubutu wako wa kuanzisha biashara hii ambayo ni ya fani tofauti na taaluma yako....kama inawezekana tafadhari share kwa manufaa yetu wengi tulio na ndoto ya kufanya biashara hii mchanganuo wa gharama haliso ulizotumia hadi kuisimamisha biashara hii, pamoja na challenges faced.
Wasaalam nyote.

Shukrani kwa Kibaravumba na nyote mliotoa constructive comments.

King kong, sina hizo sifa za kutafuta PM za wadada kama unavyohisi. Baadirisha ur negativity thinking ndugu yangu maana unafkiria watu wote wana tabia kama hizo

Nilifanikiwa kuanzisha duka mwezi May baada ya kuongeza kamtaji na kufikia around Tshs. 30m. In my road map, after one year nilipanga kuombea kamkopo bank or other financial institution for about Tsh. 40m kwaajili ya kufungua sehemu nyingine hapa hapa Dar after analyse the market and all other relevant info.

Najitahidi kukeep all info (financial and non-financial) updated ili inisaidie kujua wapi natakiwa kufanya nini kwa wakati gani.

Naelewa biashara ina challange nyingi sana na najua ntapata challange zaidi sku zijazo lakini naamaini kila kunapo challange njia inapatikana kama una malengo

Nakaribisha michago yenu ambayo itakayojenga na sio kubomoa maana naamini humu ndani kuna watu wanaofanya hii biashara na wanaelewa uendeshaji wake unavyokuwa.

Shukrani sana na nawatakia mapumziko mema.
 
Hiyo biashara inalipa sana kitu cha muhimu ni kupata location ambayo ina flow ya watu kwa wingi.Vitu vya kuzingatia ni

  • Location
  • Competitors
  • Wafanyakazi waaminifu
  • Vifaa (frame,Ac,)
  • Kibali toka TFDA
Kwa maelezo zaidi tembelea website ya TFDA

Inabidi uwaone pia Balaza la Pharmacy Tanzania.
 
Ndugu yangu, naomba na mimi nikupe mwanga zaidi kwa faida ya wengine.

Kama baadhi walivyosema, kutokana na mabadiliko ya sheria, Tanzania kwa sasa hakuna maduka ya dawa baridi. Tuna maduka ya dawa muhimu (DLDM). Maduka haya yameanzishwa kutokana na utafiti uliofanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) mwaka 2001, na kubainisha mapungufu mengi ambayo yalikuwa yanafanywa katika maduka ya dawa baridi (DLDB). Mojawapo ni kuuza dawa zisizoruhusiwa kisheria kwa kutumia watoa dawa wasio na sifa; kugeuza maduka kuwa maabara na dispensaries na kadhalika.

Kwa ufupi tu, kutokana na hali hiyo, na kwa kuwa Tanzania ilikuwa ina huduma duni ya dawa kwa wananchi walio wengi, (ambao wanapatikana na vijijini na miji midogo), serikali ikaamua kuanzisha mpango wa DLDM kwa lengo la kuondoa matatizo yote yaliyobainishwa kwa utafiti. Pili ilikuwa kuruhusu dawa chache za msingi (few essential medicines) ziwepo kwenye maduka hayo, na watoa dawa wake wapate mafunzo maalumu, ili huduma ziwe bora na za uhakika katika maeneo ya rural, periurban na maeneo maalum yaliyoruhusiwa ambayo hakuna duka la Famasi.

Ili kuweza kuhakikisha haya, ngazi zote za utendaji, yaani ngazi ya kijiji au mtaa, ngazi ya kata, ngazi ya wilaya na mkoa wanahusishwa moja kwa moja katika utekelezaji wa mpango huu.

Sasa utaratibu ni huu:
1. Chukua fomu ya kuanzisha fomu ya kuanzisha DLDM kwa mfamasia wa wilaya unayotaka kufungua duka. Ijaze sehemu A, ukiwa umeambatanisha vyeti vya kuhitimu mafunzo maalumu yaani mmiliki na mtoa dawa, mkataba wa kazi baina ya mmiliki na mtoa dawa, pia commitment letter ya mtoa dawa katika duka hilo. Kama wewe ni mmiliki na pia ni mtoa dawa, huna haja ya kukusanya mkataba huo.
2. Fomu ipeleke ofisi ya kijiji au mtaa ambao duka litakuwepo. Wao watajaza sehemu B.
3. Fomu itapelekwa kwa ofisi ya Kata, watajaza sehemu C. Wakaguzi zaidi ya mmoja watakuja kufanya ukaguzi wa eneo na jengo kama linakidhi vigezo.
4. Fomu itapelekwa ngazi ya wilaya, na kabla hawajajaza sehemu D, watatakiwa kufanya ukaguzi tena kwenye eneo na jengo lako, na kuhakikisha mtoa dawa wako amepatiwa mafunzo. Kama kuna marekebisho utaelezwa na uyafanyie kazi. Lakini kwa kupitia kamati yao ya Chakula na Dawa inayoongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri au Manispaa, itakaa kikao na kuyapitia taarifa za ngazi zote, na za ukaguzi. Maduka yaliyokidhi vigezo, yanapendekezwa sasa kwenda Baraza la Famasi (Pharmacy Council) waweze kutoa vibali. Ukishapata kibali unatakiwa urudi tena kwenye halmashauri au wilayani ukapate Leseni ya Biashara.

Nahisi nimekupa mwanga kidogo zaidi, ila kama ningekuwa na email yako, ningekutumia Kitabu cha mwongozo kinachosimamia mpango huu.

Thank you
Mwananchi mwenzenu.

wisepeny@gmail.com
Thanx in advance
 
Naomba kufahamu kwa mtu kuuza duka la dawa za binadamu anatakiwa asome kozi gani na chuo gan?

Ahsante
 
Habarini,

Jamani najua kwenye jukwaa kuna watu wenye fani mbali mbali humu ndani. Mimi nina wazo la kufungua Duka la Dawa mkoani Singida. Nahitaji anaye fahamu utaratibu wa kufungua duka hili anipe mawazo juu ya utaratibu wa ufunguzi wa duka hili.

Pia kwa anayejua maduka yanayouza dawa za jumla kwa bei nafuu hapa Dar es salaam hata mawasiliano ya maduka hayo pia. Natanguliza shukrani zangu za Dhati kwa mawazo yenu mbalimbali ili niyafanyie kazi.
 
Hongera kwa wazo lako zuri

1. Tafuta eneo unalokusidia kufanya hiyo bishara.
2. Nenda ofisi za TFDA hapo Singida, kachukue form ya maombi utaijaza utakapoijaza na kuirudisha ukirudisha watakupangia siku yakuja kuangalia na kuikagua, kama utakidhi vigezo utapewa kibali, kama haitakuwa na vigezo watakufahamisha hayo mapungifu.

Kuhusu maduka ya jumla, pia kuna tofauti ya vigezo kati ya pharmacy na duka la dawa muhimu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom