Duka la Dawa Muhimu za Binadamu (Pharmacy): Utaratibu wa Kufuata na Mtaji wa Kuanzisha Biashara

mjasiria

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
4,156
1,849
Masi.jpg

Wakuu nina maswali kadhaa kuhusu hii biashara.
  1. Je, ninahitaji vibali gani? Na vinapatikana katika ofisi zipi na pia itakuwa msaada sana kama itawezekana kuweka gharama zinazolipwa kwa kila kibali.
  2. Je, mtaji kiasi unatosha kufungua biashara hii.
Natanguliza shukrani zangu.


WADAU WENGINE WANAOHITAJI MUONGOZO WA BIASHARA HII
Mimi ni muhitimu wa course ya uuguzi, nimejiminya kitaa maana ajira ni ngumu hivyo nilipigana kufanya vitu mbalimbali na sasa nimepata million2 sasa nafikiria kuanzisha duka la dawa muhimu ! naombeni ushauri kwa mtaji huo naweza fanikisha?

Changamoto zake kwa anaefahamu anaweza nisaidia!! mm nipo Dar kwa sasa hata kama kuna allocation nzuri karibu na Dar ambapo naweza anzisha pia mnaweza nisaidia coz bado cjapata sehemu!!

Naomba msaada sana
Heshima mbele waungwana,

Mimi ni mjasiliamali aambye Nimekuwa nafanya biashara mbalimbali kwa muda sasa, pamoja na kuwa nimeajiliwa, lakini bado namudu kufanya biashara na kusimamia kwa kiasi kikubwa.

Baada ya kufanya utafiti mdogo nimegundua kwamba kuna maduka makubwa machache sana ya kuuza madawa yenye kiwango cha Pharmacy, na kwa kuwa kazi kubwa ya mjasiliamali ni kubeba Risk na Ku - Capitalise on Discripancies, nataka kujaribu biashara hii.

TafadhaLI WAUNGWANA, kwa mwenye UELEWA wa:
1. mtaji unaohitajika
2. Namna ya kusimamia
3. Taratibu za kisheria zinazotakiwa
na mambo mengine mengi ambayo yanaweza kunisaidia kufanya biashara hii.

Nawasilisha.


MICHANGO YA WANA JF
MAANA YA PHARMACY, HATUA ZA KUANZISHA NA MAZINGATIO


Habari wakuu!!

Kama wafanyavyo wengine kwenye hii Forum nimeona nami leo nije kwa maelezo kifupi namna mtu anaweza kuanzisha hatua kwa hatua biashara ya Dawa au kama inavyojulikana na wengi yaani Retail Pharmacy.

Lakini kabla sijaenda moja kwa moja kwenye hatua hizo, ni muhimu basi kuweza kujua Pharmacy ni kitu gani hasa?
Kwa mujibu wa sheria ya Famasi au PHARMACY ACT, Pharmacy ni sehemu ambayo chini ya usimamizi wa mfamasia ambaye amepewa dhamana ya uangalizi wa shughuli zake (Pharmaceutical services) itauza au kununua dawa zilizo kwenye makundi ya moto au Baridi nikiwa na maana dawa zinazohitaji uangalizi au prescription na dawa za kawaida au Over the counter medicines (OTC Medicines).

Watu wengi huchanganya kati ya Duka la dawa Muhimu (DLDM) na Pharmacy. Hivi ni vitu viwili tofauti na utofauti wake unakuja kuwa DUKA LA DAWA MUHIMU au kama yanavyojulikana kitaalamu (Accredited Drug Dispensing Outlets au ADDO) hayaruhusiwi kuuza baadhi ya dawa za moto kisheria, na ukikuta wanauza basi ujue ni kinyume na Sheria na Taratibu za Pharmacy Act na ni vyema ukatoa taarifa kwa vyombo husika au Baraza la Wafamasia.

Mtu yoyote anaweza kumiliki Famasi hata kama hana Taaluma ya Ufamasia ila atalazimika kumuajiri mfamasia kwa Part time au Full time na malipo mara nyingi hutegemea na makubaliano kati ya mmiliki na Mfamasia mwenyewe. Wengine huamua kuingia partnerships na wengine huamua kuwa huru kwa kuajiriwa kwa muda.

Hatua Ya Kwanza
Kama zilivyo biashara zingine ni vyema kwanza ukafanya utafiti binafsi kwa kuangalia Location, economic status ya watu wanaozunguka eneo hilo na ushindani wa kibiashara au kama kuna Famasi maeneo hayo ambayo yanaweza kukuletea ushindani mkubwa na kushindwa kufanikiwa kibiashara.

Baada ya kufanya hayo na kujiridhisha na eneo husika unalotaka kutoa huduma hiyo, mfuate mfamasia wa wilaya wa eneno hilo ili uweze kumweleza dhumuni lako na kukupa maelezo kama kuna maombi mengine yoyote ya uanzishwaji wa Famasi yaliyokwisha pelekwa kwenye eneo ulilochagua kufanya huduma hiyo.

Wengi huwa wanakurupuka kwa kulipia chumba cha biashara na baadae huingia hasara kwani wanakuta kuna mtu teyari kwenye eneo hilo ameshapeleka maombi ya kuanzisha Famasi kama yeye. Kisheria kuna umbali ambao lazima uwepo kati ya Famasi na Famasi na ili usiingie hasara hiyo ni vyema kabla hujalipia chumba cha biashara basi onana na mfamasia wa wilaya kwanza.

Ukubwa wa chumba cha Biashara pia ni kitu muhimu sana kuzingatia kwenye Biashara hii. Kama utataka kufungua Famasi ya rejareja, basi utatakiwa kuwa na chuma kisichopungua 25 meter square ili uweze kukigawa na kupata chumba cha mbele yaani counter, chumba cha kutolea dawa au Dispensing room na stoo ya dawa.

Hatua Ya Pili
Baada ya kuhakikisha eneo lako la biashara ni salama na chumba chako kina ukubwa unaotakiwa kadiri mfamasia wa wilaya alivyokushauri, basi lipia chumba chako na anza marekebisho kama utakavyoelekezwa na mfamasia wa wilaya ili pawe na muonekano wa kisasa na kuvutia kwa kuweka hizo partitioning kwa ajili ya chumba cha mbele, kutolea dawa na stoo! Wengi hupendelea kuweka partitioning za Aluminium lakini hata ceiling board na gypsum hukubalika na huokoa gharama.

Hakikisha hicho chumba kina mzunguko mzuri wa hewa kwa kuweka feni na Air conditioner! Sheria pia inataka kuwe na vigae chini ili kurahisisha usafi na kuzua maambukizi ya magonjwa au vumbi ambayo hupunguza nguvu za dawa au kuharibika. Pia unaweza kuweka mbwembwe zingine za kibiashara ili kuvutia wateja wako kama rolling adverts na vioo ukutani.

Hatua Ya Tatu
Ukishamaliza kufanya marekebisho yako na kama ulivyoshauriwa na Mfamasia wa Wilaya, unatakiwa kumwita ili aje kukukagua Jengo (Premise Inspection) na kukuandikia kibali ambacho utalazimika kulipia hizo form za ukaguzi na maombi ya kibali ambayo yakishajazwa hutumwa baraza la Famasi uweze kupewa leseni na ruhusa ya kuanzisha biashara yako (Licence and Permitt). Kwa kawaida hapa huwa kuna gharama za kulipia na gharama huongezeka kama mmiliki sio mfamasia, hulazimika kulipia professional fee ya Mwaka. Hii hatua huweza kucuhukua hata miezi mitatu au sita kukamilika au kupata kibali chako kwani Baraza la Wafamasia lazima likae vikao kupitia maombi yako.

Tukumbuke pia hii biashara ni tofauti na biashara zingine kwani ni huduma pia kwa jamii na ni ya kitaalamu. Mikataba ya ajira ya wataalamu kama Dispensing Nurse,Pharmaceutical Technician au Mfamasia wako lazima iwepo wakati wa ukaguzi na ujazaji wa form za leseni za Baraza la Wafamasia. Hii ina maana kwamba kama huna Medical background kwenye dawa utalazimika kuajiri hao watu muhimu ambao ni kati ya mfamasia au technician ili aweze kukusaidia kutekeleza majukumu ya utoaji huduma za dawa.

Hatua Ya Nne
Wengi wakishakaguliwa hukurupuka kwa kwenda kununua mzigo (Dawa) na kuziweka au kuzipanga stoo)!Cha msingi hutakiwi kuwa na papara, subiri vibali vyote vya baraza la Famasi umepata na leseni ya biashara kutoka kwa Afisa Biashara wa wilaya ndio ujihakikishie kuanza kununua dawa kutoka kwa whole salers au distributors.

Hatua Ya Tano
Hatua hii ni ya kufungua Famasi yako na teyari kwa kuanza huduma, kumbuka siku zote biashara ni ubunifu hivyo basi hakikisha wahudumu wako ni competent na wana ueledi wa kutosha kwenye kutoa maelezo sahihi ya dawa na matumizi yake!Hakikisha pia wahudumu muda wote ni wenye lugha nzuri kwa wateja wa rika zote na tabasamu muda wote!
Kama unajiweza kifedha ni vyema wahudumu wakawa na uniforms au makoti ya kitabibu(Medical coat) ili kuonekana professional zaidi na kuwavutia wateja.

Inashauriwa pia uwe na Water dispenser ili wateja wenye uhitaji wa lazima kuanza kunywa dawa papo hapo waweze kupata huduma hiyo bila kusahahu kipimo cha uzito kiwepo kuwawezesha wahudumu kutoa dozi za dawa sahihi kwa wateja hasa watoto chini ya miaka mitano.

Cha Kuzingatia
Kama zilivyo biashara zingine ni muhimu kujiandaa kwa fedha japo si lazima kiasi kikubwa (At least 20M), na biashara hii utalazimika kumuajiri mfamasia ili akusimamie Famasi yako na kwa sasa wafamasia hutoza si chini ya Tsh. 1,000,000/ kwa mwezi na huyo ni wa part time tu, hivyo basi ni vyema ukawa na kiasi cha kuanzia cha kutosha kwa ajili ya kumlipa advance hata ya miezi sita kabla biashara yako haija stabilize au kuzoeleka na kufanya vizuri.

Kwa sasa pia kuna makampuni au Distributors wanaokopesha dawa kwa wateja wake, hivyo unaweza pia kujihusiha na haya makampuni ili waweze kukukopesha dawa na kulipia baadae.

Ni hayo tu machache niliyoona niwashirikishe, wengi wana pesa lakini hawajui waifanyie nini, hivyo basi kama umeelewa vizuri biashara hii kwa maelezo hapo juu nakushukuru na nikutakie upambanaji wenye kheri..Pamoja sana!
KWA MTAJI MDOGO, FANYA HIVI

Ushauri wangu: Ulikuwa sahihi kuwaza kufungua duka la dawa muhimu na siyo Pharmacy kwani capital ni ndogo kwa kuangalia yafuatayo.

Gharama ya pango la chumba kikubwa angalau ft 20 x12 na height 10 vinalipiwa kwa mwaka sh.1,800,000,mlango wa kioo(aluminium)600,000,shelves za gharama ya chini kabisa sh.1,500,000,Ac 700,000. Gharama nyingine ndogo ndogo pamoja na rangi fanya 1,000,000. Gharama za kumlipa mfamasia angalau kwa miezi sita(jamaa huwa wanachukua kwa miezi sita hadi mwaka) 6,000,000 ie 1M kila mwezi ukipiga hesabu unabaki na 8.4M kwa ununuzi wa dawa.

Hapo unaweza kufungua Pharmacy ingawa kuna gharama za kulipia kibali leseni na mapato.

Pia gharama za kumlipa muuzaji kwani mfamasia hawezi kukaa dukani kuuza kwa hiyo M.1 ya kila mwezi huyu atakuwa ama ameajiriwa na serkali au mashirika/makampuni ambako ndipo atatumia muda wake mwingi.

Hapo kwako ataweka cheti tu.
Hata hivyo ni Muhimu kupata sehemu inayofikika kwa urahisi na watu wengi kitu ambacho unalazimika umuhamishe mtu kwa gharama zaidi.

Uwe makini usidanganywe kuwa biashara hii ina faida kubwa saana!La hasha,hii ilikuwa zamani.
Ukiweza kufanya biashara ya jumla unaweza kupata zaidi kwani kwenye retail ushindani ni mkubwa sana.

Mwisho nakushari anza na duka la dawa muhimu kwa kiasi kidogo cha pesa halafu,ukizijua changamoto zilizopo,unaweza kuamua kwenda mbele kufungua pharmacy.
Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
KUANZISHA BIASHARA HII, FUATA UTARATIBU HUU

Ndugu yangu, naomba na mimi nikupe mwanga zaidi kwa faida ya wengine.

Kama baadhi walivyosema, kutokana na mabadiliko ya sheria, Tanzania kwa sasa hakuna maduka ya dawa baridi. Tuna maduka ya dawa muhimu (DLDM). Maduka haya yameanzishwa kutokana na utafiti uliofanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) mwaka 2001, na kubainisha mapungufu mengi ambayo yalikuwa yanafanywa katika maduka ya dawa baridi (DLDB). Mojawapo ni kuuza dawa zisizoruhusiwa kisheria kwa kutumia watoa dawa wasio na sifa; kugeuza maduka kuwa maabara na dispensaries na kadhalika.

Kwa ufupi tu, kutokana na hali hiyo, na kwa kuwa Tanzania ilikuwa ina huduma duni ya dawa kwa wananchi walio wengi, (ambao wanapatikana na vijijini na miji midogo), serikali ikaamua kuanzisha mpango wa DLDM kwa lengo la kuondoa matatizo yote yaliyobainishwa kwa utafiti.

Pili ilikuwa kuruhusu dawa chache za msingi (few essential medicines) ziwepo kwenye maduka hayo, na watoa dawa wake wapate mafunzo maalumu, ili huduma ziwe bora na za uhakika katika maeneo ya rural, periurban na maeneo maalum yaliyoruhusiwa ambayo hakuna duka la Famasi.

Ili kuweza kuhakikisha haya, ngazi zote za utendaji, yaani ngazi ya kijiji au mtaa, ngazi ya kata, ngazi ya wilaya na mkoa wanahusishwa moja kwa moja katika utekelezaji wa mpango huu.

Sasa utaratibu ni huu:
1. Chukua fomu ya kuanzisha fomu ya kuanzisha DLDM kwa mfamasia wa wilaya unayotaka kufungua duka. Ijaze sehemu A, ukiwa umeambatanisha vyeti vya kuhitimu mafunzo maalumu yaani mmiliki na mtoa dawa, mkataba wa kazi baina ya mmiliki na mtoa dawa, pia commitment letter ya mtoa dawa katika duka hilo. Kama wewe ni mmiliki na pia ni mtoa dawa, huna haja ya kukusanya mkataba huo.

2. Fomu ipeleke ofisi ya kijiji au mtaa ambao duka litakuwepo. Wao watajaza sehemu B.

3. Fomu itapelekwa kwa ofisi ya Kata, watajaza sehemu C. Wakaguzi zaidi ya mmoja watakuja kufanya ukaguzi wa eneo na jengo kama linakidhi vigezo.

4. Fomu itapelekwa ngazi ya wilaya, na kabla hawajajaza sehemu D, watatakiwa kufanya ukaguzi tena kwenye eneo na jengo lako, na kuhakikisha mtoa dawa wako amepatiwa mafunzo. Kama kuna marekebisho utaelezwa na uyafanyie kazi. Lakini kwa kupitia kamati yao ya Chakula na Dawa inayoongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri au Manispaa, itakaa kikao na kuyapitia taarifa za ngazi zote, na za ukaguzi. Maduka yaliyokidhi vigezo, yanapendekezwa sasa kwenda Baraza la Famasi (Pharmacy Council) waweze kutoa vibali. Ukishapata kibali unatakiwa urudi tena kwenye halmashauri au wilayani ukapate Leseni ya Biashara.

Nahisi nimekupa mwanga kidogo zaidi, ila kama ningekuwa na email yako, ningekutumia Kitabu cha mwongozo kinachosimamia mpango huu.
Thank you
Mwananchi mwenzenu.


KUTOKA TFDA
Angalia hii habari iliyotoka 2012 nadhani itakupa mwanga.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imesema ni ruksa Mtanzania yeyote mwenye umri unaozidi miaka 18, kufungua duka la dawa muhimu za Binadamu na Mifugo (DLDM), hasa katika maeneo ya Vijiji na Miji midogo ambapo upatikanaji wa dawa muhimu ni wa matatizo.

Ofisa Uhusiano wa TFDA, Gaudensia Simwanza, aliwaambia waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba watakaofungua maduka Vijijini watapewa kipaumbele kwani watu wengi yamejikita kufungua maduka hayo maeneo ya mijini.

Alisema mwombaji anapaswa kuwa tayari kupitia mafunzo ya mwezi mmoja ili kujua sheria na kanuni za uendeshaji wa maduka hayo, ili kuonyesha utofauti wa uedeshaji duka la dawa baridi na moto ambapo wamiliki wake walikuwa hawana uelewa.

Simwanza alisema kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa DLDM, mmiliki na mtoa dawa wanalazimika kuingia mkataba wa kazi kwa lengo la kusimamia utendaji, kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ili kulinda maslahi ya pande zote mbili.

Alisema DLDM ni maduka ya kutunza na kuuza dawa zisizohitaji cheti cha daktari na baadhi ya dawa hizo kuhitaji cheti cha daktari.

Mtoa dawa katika maduka hayo ni lazima awe na sifa za awali kama fundi sanifu, ofisa muuguzi, tabibu na mhudumu wa afya au wawe wasaidizi katika ngazi hizo.

Chanzo: NIPASHE


USHUHUDA BAADA YA KUFUATA USHAURI WA WANAJF
BIASHARA HII INA CHANGAMOTO

Wasaalam nyote.
Shukrani kwa Kibaravumba na nyote mliotoa constructive comments.

Nilifanikiwa kuanzisha duka mwezi May baada ya kuongeza kamtaji na kufikia around Tshs. 30m. In my road map, after one year nilipanga kuombea kamkopo bank or other financial institution for about Tsh. 40m kwaajili ya kufungua sehemu nyingine hapa hapa Dar after analyse the market and all other relevant info.

Najitahidi kukeep all info (financial and non-financial) updated ili inisaidie kujua wapi natakiwa kufanya nini kwa wakati gani.

Naelewa biashara ina challange nyingi sana na najua ntapata challange zaidi sku zijazo lakini naamaini kila kunapo challange njia inapatikana kama una malengo

Nakaribisha michago yenu ambayo itakayojenga na sio kubomoa maana naamini humu ndani kuna watu wanaofanya hii biashara na wanaelewa uendeshaji wake unavyokuwa.
Shukrani sana na nawatakia mapumziko mema.
 
Mkuu kila kitu kinawezekana na kwa mtaji wa kiasi ulichosema, naamini lengo litatimia.

Wahusika wakuu wa hii kitu ni TFDA ambao ofisi zao zinapatikana mabibo external.

Nenda katika ofisi zao watakupa majibu ya maswali yako yote na mengine ambayo haukuuliza hapa.

Naogopa kukupa majibu hapa kutokana na mapinduzi makubwa yaliyofanywa na TFDA katika biashara hii ya dawa baridi ambayo kwa sasa wanaziita dawa muhimu.

Make sure you have all the details before jumping into it, si vibaya ukajaribu kuonana na watu ambao tayari wanafanya hii biashara, uhakika nilionao ni kwamba hii biashara inalipa, unachohitaji ni umakini na subira kwa siku za mwanzo za biashara.
 
Kwa ufupi maeneo ya mijini huwezi kuanzisha tena duka la dawa baridi. TFDA ilishatoa tamko. Unatakiwa kuanzisha duka la dawa muhimu vijijini na pembezoni mwa mji ambapo inaelekeana na rural settings.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na TFDA, email info@tfda.or.tz . Pia kumbuka kuwa vibali vya maduka ya dawa baridi vinashughuliiwa na Halmashauri ya wilaya/mji/manispaa husika.

Kama upo Kinondoni basi unawasiliana na mfamasia wa manispaa (Kinondoni anaitwa mabonesho) ila kama mdau aliyetangulia alivyosema nenda TFDA kaonane nao.

Specifically kutana na Kitengo kinachohusika na Maduka ya Dawa muhimu (kwa Kiingereza wanayaita ADDO).

Upo hapo kama unataka namba zao ni-PM
 
NISAIDIN JINSI YA KUPATA LESSEN YA DUKA LA MADAWA. Nataka kufungua duka la madawa ya binadamu mkoa songea naomba jamani anayefahamu njia za kupita ili nifanikiwe lengo langu anisaidie nawatakia siku njema.
 
Mkuu hapo kwenye hospitali ya wilaya kuna mfamasia wa wilaya, nenda ukamwone atakupa utaratibu wote.
 
Nenda kwa mfamasia wa mkoa au TFDA. TFDA wana ofisi ya Kanda pale Mbeya. ila kumbuka kwa Songea kuna maduka ya dawa aina mbili:
  1. Duka la dawa muhimu- ADDO
  2. Pharmacy
Sasa wewe unataka kuanzisha lipi mana requirements zinatofautiana.
 
Habari za asubuhi wana JF.

Wakuu kunasehemu nimeona naweza kufungua duka la dawa, naomba watalaam wanisaidie mahitaji yanayohitajika na gharama zake. Ningependelea kuweka dawa nyingi coz mi dr, kama kuna mtu anifafanulie madaraja ya maduka ya dawa. Natarajia ushirikiano wenu wakuu. Asante.
 
Nenda kamwone mfamasia wa wilaya ya eneo husika atakupa imput zote lakini kwa sasa tuna madaraja wa2 tu ya duka la dawa.
Duka la dawa Muhimu na Pharmacy inayohitaji uwe na mfamasia wa degree.
Mahitaji mengine ni vyumba viwili.
 
Naomba mwenye uzoefu na utaalamu wa biashara ya duka la dawa anisaidie, nataka kuanzisha hii biashara.
 
Sio ya kulevya

Nataka kufanya biashara ya kuingiza dawa za binadamu toka nje je nahitaji kibali gani.

Pia, kama nataka kuingiza solution ya unga wa maziwa ya watoto je nayo nahitaji vibali vipi?

Vitu kama pedi za wanawake na pampers za watoto pia nataka kuingiza je zaidi ya TBS nahitaji vibali toka wapi? Na process ikoje?
 
Ndugu wanajamii forum,

Nahitaji kujua taarifa kuhusu biashara ya dawa baridi. Naomba msaada wa kujua mawazo yenu kuhusu hio biashara, walau mtaji kiasi cha chini ni kiasi gani inatakiwa, namna gani ya kuendesha na taratibu zote za kufungua hadi kuweza isimamisha. n

Asante.
 
Milioni mbili hadi tatu, pia tafuta mfanyakazi mzoefu kidogo usije nunua madawa mengine yaka-expire store kukosa wtj.
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom