Elections 2010 Duh; nini kilitaka kumtokea JK kule Lindi Jukwaani?

mungu wangu.....

Yani askari anaonyesha kabisa ana-move.... na walio pembeni tayari wameanza kuamka
 
Wale wanaokaa nyuma ya Marais wote duniani wakiwa na nguo za jeshi si body guards ni wapambe kwa ajili ya huduma kwa Marais kwa mfano kubeba makabrasha ya Rais na kusogeza kiti vizuri endapo Rais anasimama, inavyoelekea bwana wa kushoto alikuwa anamkumbusha mpambe wa Rais kuzogeza kiti mbele kidogo ili Rais atakapomaliza kusalimia wananchi asije akaanza kukaa kumbe kiti kiko mbali. Mjeshi anaonekana anamjibu usiwe na hofu niko imara. Ni wazo langu tu kutokana na ninavyoangalia movies hasa zile zilizoegizwa kama Marais. I stand to be corrected kwa wale walio na ufahamu zaidi.
 
hili jamvi ni watu waliojaa chuki tu, hamna lolote la kuanguka wala kutetereka, ndio maan wengi wamelihama, hamtaki
maendeleo ila uzushi tu

Ni kweli wakati fulani tunatakiwa kusema mambo baada ya kuwa na uhakika. mambo ya kupika yanaweza kushusha hadhi ya JF. Kwa ninavyowajua waandishi wa habari kama Rais alitaka kuanguka wasingesika kuripoti tukio hilo kama walivyofanya jangwani na zaidi gazeti la mtanzania lisingeweza kutoa picha hivyo kwa kuwa ni la kada wa CCM
 
JK ana mvi japo si nyingi na zinaonekana vizuri tu hapaki chochote, kwa wale wazee vijana wangekuwa wanapaka Yazuu kuzifanya nyeusi. Sina chama lakini Brovoooo kikwete kwa hili unatakiwa kupewa big up.

wana ccm wanafurahisha sana. huyu kishakimbilia kusema kuwa hana chama
 
Jamani ivi jamii forum ni kwa ajili ya kumpingakikwete? Mbona mnaspeculate vitu visivyo jamani. Ebu acheni kupoteza value ya iki kitu bwana!
jk-lindi+crowd1.jpg

source: Press kikwete 2010/ mtanzania 21 oct. 2010

jk alikuwa anaenda chini nini, akawahi kushika meza? Ingekuwa mwananchi kaweka picha hii front page kama alivyofanya mtanzania ingekuwa ni uchochezi? Ila akifanya roastam aziz sio?
 
Wale wanaokaa nyuma ya Marais wote duniani wakiwa na nguo za jeshi si body guards ni wapambe kwa ajili ya huduma kwa Marais kwa mfano kubeba makabrasha ya Rais na kusogeza kiti vizuri endapo Rais anasimama, inavyoelekea bwana wa kushoto alikuwa anamkumbusha mpambe wa Rais kuzogeza kiti mbele kidogo ili Rais atakapomaliza kusalimia wananchi asije akaanza kukaa kumbe kiti kiko mbali. Mjeshi anaonekana anamjibu usiwe na hofu niko imara. Ni wazo langu tu kutokana na ninavyoangalia movies hasa zile zilizoegizwa kama Marais. I stand to be corrected kwa wale walio na ufahamu zaidi.

Acha kamba hizo. Wangapi wa aina huyo wanakaa nyuma ya Obama?
 
Hebu tuambie kwanza hapo ni kina nani waliostuka hapo? Ukimwacha mwenyewe mbona kama mtu 4 hapo wote wako standby?
 
Angalieni video ya Lindi kwenye blog ya Michuzi. Membe kaongea kwa dakika saba ushee. Kikwete kaongea dakika moja tu na nusu akamaliza.
Kachoka!
 
wana ccm wanafurahisha sana. huyu kishakimbilia kusema kuwa hana chama
Wengine utawasikia wakianza na gia ya mimi sidanganyiki 2010 ili wapate supoti ya upande fulani, kama mtu unajiamini hakuna haja ya kujitambulisha uko upande fulani wewe shusha nondo tu utaeleweka.
 
Nina wasiwasi Jk anaweza kwenda chini kabla ya tarehe 31 oct, kwanini huwa wanampa dakika tano hadi kumi za kuhutubia?
 
waungwana nisaidieni hv sheria inaruhusu chama kubadilisha mgombea urais. maana huyu wa ccm anaumwa.
 
Duuh ushabiki mwingine... yani jamaa katika picha mnato kaona JK kapoteza balance?? Duh ama kweli Tz tumeendelea. tuna wang'amuzi wa mambo hata picha mwenendo hatuzihitaji...

Wewe hukusoma 'photo interpretation nini kwenye Geography yako?
 
Jamani ivi jamii forum ni kwa ajili ya kumpingakikwete? Mbona mnaspeculate vitu visivyo jamani. Ebu acheni kupoteza value ya iki kitu bwana!

speculation ni sehemu ya great thinking!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom