Dudu baya mahakamani

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
images

MSANII wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’ (pichani) hivi karibuni alitupwa selo baada ya kukamatwa na polisi wilayani Geita kwa kudaiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, Ijumaa lina kisanga kamili.

Kwa mujibu wa mlalamikaji, Warwa Nkurunzinza, Desemba 31, 2010 alimtumia Dudubaya fedha shilingi 250,000 kupitia akaunti yake ya Benki ya NBC Tawi la Geita kwa lengo la kufanya shoo kwenye mkesha wa kuamkia Januari Mosi, mwaka huu.

Hata hivyo, Nkurunzinza alidai kuwa, pamoja na kufanya hivyo, Dudubaya hakutokea hali iliyofanya amfungulie kesi msanii huyo katika kituo cha polisi na kupewa RB yenye namba GE/RB/1829/04 ili akamatwe.

Msanii huyo alipokamatwa alifikishwa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo ya Nyankumbu, wilayani Geita, Mbauro Mbauro na kusomewa mashtaka yake.

Mbele ya Hakimu Mbauro, Nkurunzinza alidai kuwa, alikuwa ameandaa shoo katika Kijiji cha Rwamgasa nje kidogo ya Mji wa Geita iliyokuwa itumbuizwe na Dudubaya lakini akaingia mitini hadi alipokamatwa Mei 28, mwaka huu.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti kwa kupeleka wadhamini watatu ambao ni wakazi wa wilaya hiyo na fedha taslimu shilingi 100,000.

Katika hatua nyingine, mwandishi wa habari hii chupuchupu apewe mkong’oto na wapambe wa msanii huyo baada ya ‘kumfotoa’ Dudubaya akiwa mahakamani hapo.
Kesi hiyo ilihairishwa hadi Juni 8, mwaka huu itakapotolewa hukumu.
 
Who's Dudubaya by the way?:tonguez:

umetoka usingizini nini? yaani hujasoma habari yenyewe umepitia kichwa cha habari na kujibu
tusiwe wavivu wa kusoma,rudia tena kusoma utamjuwa dudubaya ni nani kama utakavyo

walioelimika wanasema Ukitaka kumnyima habari Mtanzania basi we iweke ktk maandishi
 
Umeisha ambiwa hilo dudubaya ! Unalipaje kidole ? Damn ! Kill them dudus.
 
wasanii wetu keweli hawana value kabisa, yaani dhamana ni laki moja tu? duh
hii si ni dharau jamani?
 
Karibu sana, ni wewe au mwingine maana isije ikawa umebadilisha ID, karibu sana

Nonsense!
Unachangia mada au unataka kujibishana na watu, kama wewe unamjua huyu dudu**** si kila mtu anaweza mjua
kwani tunatofautiana hobbies hizo. Tuwe wastaarabu jamani, this is for great thinkers not for insane! Please.
 
Back
Top Bottom