Dubai or Japan or UK?

esswaay

Member
Dec 21, 2010
28
0
Jamani magari yaliojazana hapa mjini mengi yalikuwa yanatoka Dubai kisha UK nao watu wakaanza kuingiza na sasa naona watu wanazungumzia kuagiza gari wenyewe direct from Japan

sasa nauliza kama nataka gari kama Rav 4 au Prado au gari tuu yoyote kwa ujumla ni nunue wapi kati ya nchi hizo 3 ?

na sababu ni zipi?
 
Kanunue Japani. Sasa ni Rav 4 au Prado ni gari za Japani.
 
Jamani magari yaliojazana hapa mjini mengi yalikuwa yanatoka Dubai kisha UK nao watu wakaanza kuingiza na sasa naona watu wanazungumzia kuagiza gari wenyewe direct from Japan

sasa nauliza kama nataka gari kama Rav 4 au Prado au gari tuu yoyote kwa ujumla ni nunue wapi kati ya nchi hizo 3 ?

na sababu ni zipi?

angalia urahisi wa bei mkuu...

lakini kwa quality mara nyingi gari za japan na uk ni bora kuliko za dubai...ila kama unapenda kipupwe kuwa makini na gari za uk...unaweza kununua gari isiwe na kipupwe bse kule ni baridi mwaka mzima hivyo gari nyingi hazina AC...

khs eti gari kuwa ni japanese si hoja...toyota wana plants huko uk na quality stds zinaangaliwa sana tu...

huwa kuna vitofauti vidogo vidogo ambavyo kama umezoea gari kutoka japan vinaweza kuwa kero mfano...uk made..indicator unawashia kushoto wakati wipers ni kulia...kuna interchange ya vile vistick vya ku-operate hivyo vitu viwili.

vinginevyo....... kipendacho roho............!!!!!!!!
 
Binafsi kwa ushauri nitakwambia ni kati ya Japan au UK. Na pia ushauru wangu sio static. Watu wanakariri tu Japan oh mara UK. Ukweli kuna vitu vingi vya kuangalia zaidi ya aina ya gari. Kwa mfano hivi karibuni gari kutoka Japan zilikuwa ghali saaana na bado ghali kutokana na pesa yao kuwa na nguvu kulinganisha na dollar. Pia pesa yetu nayo ilishuka thamani saana kwahiyo kununua gari Japan hakukuwa attractive. Kwa UK, tatizo la market yao haiko organise saana kwenye kuimport magari kwenda Tanzania km Japan. Lakini in some cases, cars are cheaper in the UK than Japan. Experience yangu nyingine pia ni kwamba, gari kutoka Japan kuja Tanzania inategmea na gari yenyewe. Kuna gari niliwahi kushuhudia body yake ni laini saana kulinganisha na brand ya UK. Pia aliyesema AC, nadhani anazungumzia magari ya siku nyingi saana lakini magari siku hizi yanaoptions za heater na AC. Kwahiyo uchaguzi wako, kama kwa choice ya price, durability etc.
 
Realtor naungana na hoja yako kamani gari moja ni bora kununua hapo hapo dar ! chengine muhimu ifahamike magari kutoka dubai karibu yote yamepelekwa pale kwa soko na sio magari ya dubai kwani gari za dubai ni left hand na sio right hand . nying ya gari hizi kutoka dubai huwa ni za ajali kiasi ambacho gari moja hukatwa kuungwa na gari nyengine mfano gari aliyopata ajali sehemu ya mbele inaunganishwa na gari ilyoharibika nyuma kitu unatakiwa kuwa makini kugundua .jengine huwaga zinafanyiwa mchezo mchafu katika speedo pale dubai. japan na uk zinalingana ila za japan mara nyingi ni chakavu popote utakapoamua japan au uk nunua la mwaka 1999 kwenda mbele utafurahi.
 
Altaaf umenisaidia sana pia coz i had no idea na michezo michafu hiyo!

vinginevyo kwa gari moja ni bora kununua hapa ni uhakika zaidi kwakua utapata nafasi ya kuthaminisha kabla ya kununua japo inakua ghali zaidi kidoggo ukilinganisha na kuagiza nje
 
Kuhusu hili la kununua gari kuna siri nyingi tu, kuna magari utaona yanauzwa rahisi na ni matoleo ya miaka ya karibuni kuanzia 2005 na kwa bodi utayaona yanapendeza lakini kumbe mengine yalipata ajali na kuwa right - off huko yalikotoka ama yameenda miles/km nyingi lakini yamefanyiwa maujanja wa clocking- (kurudisha speedometer)
Popote utaponunua ni muhimu sana jaribu kuomba full service history book na original registration book, hapo utaelewa ukweli kuhusu hiko chombo.
Mimi personal opinion yangu ni kwamba kuana grade 3 ambapo Grade 1, UK made, kwa sababu ya manufacture standard UK wana viwango vyao kwa kila gari na wanamlazimisha manufacture atimize viwango, kiusalama na umadhubuti viwango vyao viko juu ukilinganisha na Japan, mfano Rav 4 ya Japan na ile ya UK, ingawa ya Japan itakuwa na vikorombwezo (luxuries) zaidi (DVDs, navigation etc) lakini ya UK itakuwa na extra safety features,
Grade 2 ni Japan kwa sababu anagalau waweza pata history book ya kuiamini kidogo ingawa jamaa zetu wa Kipopo wamekuwa wanafoji, jitahidi kununua kwenye makumpuni ya kueleweka na sio wale ma-agenti wababaishaji.
Grade 3 ni Dubai huku kwa kweli ni kubahatisha, unaweza kupata gari kama inavosema kwenye registration book ama ukapata gari bodi tu, miezi 6 spana mkononi.
Mwisho kama unanunua huku kwetu Tanzania hapo ni akili na macho ndio muamuzi, unaweza kutafuta fundi unayemuamini ili akusaidie kukagua.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom