uttoh2002
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 14,597
- 26,226
Pole please find a way to talk through ili awe huru tena kwako, Noma hiyo kaka.
Jamani ukistaajabu ya Musa utaona sijui ya nani, mwenzio nimepata aibu ya mwaka nikiwa na mama mkwe wangu. Kwa kifupi ni kwamba nilikua nimetembelewa na mama yangu mkwe kutoka huko Katavi mkoa mpya na kwa bahati mbaya ndo mara yake ya kwanza kuja Dar. Kutokana na mihangaiko ya kazi za mchana na ratiba kuwa tight siku za weekend na siku za weekdays sikufanikiwa hata siku moja kumtoa dina, juzi usiku ikabidi twende zetu dina mimi mke wangu na mama mkwe maeneo ya posta maana yeye alikua anaondoka siku inayofuata yaani jana kurudi Katavi. Sasa tukawa tumechelewa kutoka mpaka kwenye saa nne na nusu usiku, wakati wa kurudi njiani maeneo ya Africa Sana Sinza tukapata pancha nikawaambia mke wangu na mama mkwe wakae kwenye gari tu ili nitafute kijana maeneo ya standi ya daladala Africa sana au hata pale kwenye kituo cha mafuta anisaidie kubadilisha tairi hata kwa kumlipa maana sikutaka kuchafua suti yangu.
Ile kushuka ndani ya gari kutembea tu hatua kama tano nikavamiwa na machangu kama wawili wote wakafikiri nataka huduma kumbe mimi natafuta kijana wa kunisadia kubadilisha tairi. Lakini kilichonistua ni kumwona dada ambae ni jirani yangu na pia tunafanya nae ofisi za karibu maeneo ya mjini nae akiwa miongoni mwa wale wasichana wawili waliokuwa wanafikiri nataka huduma.Alivoniona alijiskia vibaya alitamani ardhi ipasuke. Sasa mimi sielewi hivi wasichana wanajiuza for only finding satisfactions, au shida za maisha au ni hulka tu ya wasichana? Nasema hivo kwa sababu huyo dada ana kazi nzuri tu ingawa sijui mshahara wake lakini kazi yake inaweza kumfanya aishi mjini bila wasi wasi. Nimekutana nae leo wakati naelekea lunch yaani hana amani hata kidogo lakini mimi nayachukulia kama mapito.