Dr. Willbroud Slaa on his TWITTER account today!

Status
Not open for further replies.
ukanda anauleta anaye zungumzia ukanda@ mohammed. acha kupaka watu matope ili wachukie fanya mambo mengine! yani ungejua vitamburisho tunavyo tayari tunasubiri tarehe ya kupiga kura! yani ulie tuu
 
A way forward ni kuwa kitu kimoja CDM kuna shutma zinaizonga pengine ni propaganda tu za wenye kuchukia maendeleo ya CDM lakini hakuna hata siku moja CDM imekanusha au kutolea maamuzi ambayo yatawafanya watu wapuuze shutma hizo.
1. Kuwa CDM ni chama cha kikanda na hata wabunge wake wengi ni wa kutoka kanda fulani.
2. CDM ina mkono wa kanisa (hapa nakumbuka shutma dhidi ya CUF wao walikuwa wanazikanusha ila kwa bahatio mbaya au sijapata kusikia popote CDM wakikanusha hili)

Mabadiliko yatapatikana watanzania wakiwa wamoja bila kujali kanda zao/koo zao wala dini zao je CDM wapo tayari kuonyesha njia?

hahahaha! kazi kweli kweli...
Mimi nilitegemea maswali ya msingi...kumbe ni upuuzi huu!
Endelea kusubiri jibu, wakati wengine wanafanya mabadiliko!
 
My friend!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
mind you, to everything you may think of, especially when had never excited b4, there is point zero then 1, 2 , 3 ......
Always we should think critically and avoid cheep thinking.

I believe CDM is the only political party that uses brain and the real vision seeing beyond fifty years to come. When is Nyerere going to redeem the Arusha vacant????????????????

Naomba kadi ya chadema tafadhari sana!!!!!!!!.
wapo watanzania wengi sasa wanataka kadi za chadema. Please chadema jitangazeni wapi tutapata kadi zenyu????????.
 
Akifukuzwa lowasa na chenge ccm km walivyowadanganya watz kidogo watz wataanza kurudisha mawazo yao ccm. .. La sivyo wasubiri maumivu zaidi kutokana na hasira za watz.
 
Mwanzo wa kitu huanzia location fulani, hata CHADEMA kilianzia kaskazini au waasisi wake wametoka kaskazini na wangeweza toka kusini au mashariki tatizo lako nini hapo. Basi chama kikianzishwa na watu wa kusini kitaitwa cha kanda ya kusini , Mashariki n.k? Na kama ni cha kikanda je kuna mtu toka kanda nyingine alishazuiliwa kuwa member simply haruhusiwi?. Hiv Mch. Msigwa , Sugu, Wenje, Mnyika woote ni wa kanda ya kaskazini? Hv Halima Mdee, zitto Zuberi Kabwe na wale wajumbe wa zenji ni Wakristo. Mkuu some time kama great thinker unatakiwa ufanye utafiti mwenyewe na siyo ku-support watu wa vijiweni; ukweli unatakiwa uwape ukweli na si wewe nawe kujichanganya na ujinga wakati we una maujanja na uwezo wa kupangua ujinga.

Tatizo watu wengine wanaufinyu wa mawazo, sijui chama mpaka kianzie DSM ndo yataona cha Tz nzima,hopeless kabisa
 
398925_395861980441474_100000530260857_1446109_465654622_n.jpg
Yes you can, Mimi sioni tofauti yako na Kikwete zaidi ya Umri na rangi
 
Tukichagua Viongozi kwa sababu wana pesa au wametoka koo za watawala hatupat haki POLISI,MAKAMANI na Katika vyombo vya mizani.History inasema Matajiri wote Hulisha MAKOMBO walio chini ya himaya yao.
Tukitambua hilo tutachukia matabaka na kujenga umoja wenye haki sawa kwa kila mtu.tutakula sahani moja badala ya wengine kula vinono na kundi jingine kula MAKOMBO.
Hatetwi mtu angalieni kesi za watawala na watawaliwa zinavyoendeshwa.kuna hukumu zingine zinatolewa bila hata watu kufikishwa mahakama kwa kupigwa bila ushahidi wa utendaji kosa wakati katiba inapiga marufuku mtuhumiwa kutendewa kama mtualiyetiwa hatiani mpaka mizani idhibitishe kuwa anahatia.
Watala wetu hawana woga tena maana wanaamini katika pesa zao na Nguvu ya UMMA wameisahau kuw inashinda pesa.
Shime Watanzania tutumie akili zote kuonyesha pesa na utawala bila PEOPLES POWER ni ANGUKO LA MENDE
Inauma sana...............
 
Huwa natembelea mara nyingi ktk ukurasa wa Dr.Slaa ktk mtandao wa kijamii wa twitter, leo(samahani niko via mobile hivyo siwezi kuleta LINK) amekuja na ujumbe huu.

"Maendeleo hayaletwi kwa kubahatisha, bali huletwa na mabadiliko, wewe na mimi(sisi) ndo tunaotakiwa kuleta mabadiliko"(nimeitafisiri kwa kiswahili, mtaniwia radhi kama nitakuwa nimepotosha). Je Mtanzania mwenzangu uko tayari kuleta mabadiliko? Umepigika na maisha magumu?

Umechoka kubambikiwa kesi, kuuwawa na kuonewa na jeshi la polisi?, umechoka kuona mhimili wa dola(mahakama) inatumikia serikali, kupendelea wenye pesa ktk maamuzi?, umechoka kuona bunge letu likigeuka taasisi ya CCM?, uko tayari kuona wachache wakivuna rasilimali za Taifa huku wengi tukiteseka kwa umasikini wa kutupwa?

Je umeridhika kuona hali ya elimu ya vijana wetu ilivyo sasa(unaweza kushindwa kutofautisha vijana waliomaliza kidato cha 4 na yule wa drs V11)? Nawasilisha!!!!!!
Ukinywa viroba na valeur lazima uwe na fikra hizi na kuzikazia na ndumu!
 
Lema alipata kura 2010 kwa sababu watu walikuwa hawamfamu. Kwa kipindi hiki cha mwaka na nusu watu wamemfahmu Lema ni mtu wa aina gani. Wameona matatizo aliyowaletea, vurugu za kila siku na kurudi nyuma kwa maendeleo ya Jimbo la Arusha mjini. Kwa sasa hawawezi kurudia tena kosa walilolifanya 2010. Watu wengi sana wamefurahia uamuzi wa maahakama...at last wameondoka na matatizo!!

Nakutuma kawaambie ccm hivi wanazo t actics 2 ambazo majibu yake nimeambatanisha.

1. Mahakama imeamuliwa itengue ili Chadema waende mahakamani na kwa kufanya hivyo mahakama itazungusha kesi hadi 2014 kisha Lema atashinda ila atakuwa na mwaka mmoja wa kufanyakazi hivyo watapata kitu cha kuongea kwenye kampeni za 2015 kuwa Lema alikalia vurugu na kesi tu kipindi chote cha ubunge wake hivyo hajadeliver.

Jibu: chadema hawaendi mahakamani wanakubali ngoma irudiwe ikiwa mbichi. Hapo ndo ccm watajinyea maana wanazikwa huko kaskazini kabisa.

2. chadema wakimrudisha Lema kugombea, ccm wanaweza kuja na hoja mahakamani kuwa hana sifa za kugombea

Jibu: Chadema kazi ni moja ni kuwamaliza ccm, kamanda Lema atakubali kuachia na kurudi kwenye ofisi ya chama Ili kujenga chama. Je wajua ni jembe lipi litasimama badala ya Lema? Chadema lazima itumie silaha zake za mwisho za mapambano ilimradi ccm wafutike kabisa........Dr. Slaa ni lazima atapeperusha bendera ya CDM Arusha na hapo ndipo kitakuwa kilio na kusaga meno !

Chadema wamejipanga ni kazi kwao CCM kuchagua kipi rahisi kwao kwenye hili.

lakini kumbuka pia chadema wanafurahia zaidi kitendo cha leo maana wanaendelea na kazi yao badala ya usumbufu wa kuomba kibali cha mikutano ya kuwaelimisha watanzania..

Kumbuka pia wakati huu masikio ya wanatanzania bado yako Arumeru na yatabaki hapo Arusha wakipata somo.

Hakuna namna yoyote itakayoishinda nguvu ya umma na haki ya mtu haipotei bali inacheleweshwa tu!

Mungu ibariki Chadema,Mungu ibariki Nchi yetu!
 
Upo Karatu, meru au Moshi? huko ndiko zipo highly demanded! Kwingine hamna mtu anataka kukisikia hicho chama

Ndio mnavyojidanganya? Tena we mnafiki sana ulikimbilia wapi na mash...g.. wenzio wakati matokeo ya Arumeru yanatangazwa naona ulikuwa kimya kama unamwagiwa.
 
A way forward ni kuwa kitu kimoja CDM kuna shutma zinaizonga pengine ni propaganda tu za wenye kuchukia maendeleo ya CDM lakini hakuna hata siku moja CDM imekanusha au kutolea maamuzi ambayo yatawafanya watu wapuuze shutma hizo.
1. Kuwa CDM ni chama cha kikanda na hata wabunge wake wengi ni wa kutoka kanda fulani.
2. CDM ina mkono wa kanisa (hapa nakumbuka shutma dhidi ya CUF wao walikuwa wanazikanusha ila kwa bahatio mbaya au sijapata kusikia popote CDM wakikanusha hili)

Mabadiliko yatapatikana watanzania wakiwa wamoja bila kujali kanda zao/koo zao wala dini zao je CDM wapo tayari kuonyesha njia?

Mwanamume lazima uwe na sifa za kuwa mwanaume. we ulivyofanya uchunguzi umeona nini? Viongozi wa kikanda unamaanisha nini? Mwenyekiti kaskazini, makamu Mpanda wa bara wa visiwani ni Mpemba na jamaa ni mashine. Katibu anajulikana naibu Kigoma utapata hiyo orodha hadi kamati kuu yao. Ukanisa ama ukristu ni baadhi yenu ninyi waislamu mnaoeneza huo ujinga kwa mashaka na hofu mlizonazo na mioyo ya giza. Kwa hiyo ccm ni chama cha waislamu kama cdm ni cha kikiristu maana kamati kuu na halmashauri kuu ya CcM imejaa waislamu. Chadema hawezi kuwa wanajibu kila ujinga wenu ndo maana hata arumeru pamoja na matusi ya kina Lusinde walikaa kimya na mwisho wananchi wamewaadhibu. we kama umetumwa timiza matakwa ya waliokutuma halafu subiri ujila mbuzi wako. sisi wengine chadema ni tegemeo letu
 
Nakutuma kawaambie ccm hivi wanazo t actics 2 ambazo majibu yake nimeambatanisha.

1. Mahakama imeamuliwa itengue ili Chadema waende mahakamani na kwa kufanya hivyo mahakama itazungusha kesi hadi 2014 kisha Lema atashinda ila atakuwa na mwaka mmoja wa kufanyakazi hivyo watapata kitu cha kuongea kwenye kampeni za 2015 kuwa Lema alikalia vurugu na kesi tu kipindi chote cha ubunge wake hivyo hajadeliver.

Jibu: chadema hawaendi mahakamani wanakubali ngoma irudiwe ikiwa mbichi. Hapo ndo ccm watajinyea maana wanazikwa huko kaskazini kabisa.

2. chadema wakimrudisha Lema kugombea, ccm wanaweza kuja na hoja mahakamani kuwa hana sifa za kugombea

Jibu: Chadema kazi ni moja ni kuwamaliza ccm, kamanda Lema atakubali kuachia na kurudi kwenye ofisi ya chama Ili kujenga chama. Je wajua ni jembe lipi litasimama badala ya Lema? Chadema lazima itumie silaha zake za mwisho za mapambano ilimradi ccm wafutike kabisa........Dr. Slaa ni lazima atapeperusha bendera ya CDM Arusha na hapo ndipo kitakuwa kilio na kusaga meno !

Chadema wamejipanga ni kazi kwao CCM kuchagua kipi rahisi kwao kwenye hili.

lakini kumbuka pia chadema wanafurahia zaidi kitendo cha leo maana wanaendelea na kazi yao badala ya usumbufu wa kuomba kibali cha mikutano ya kuwaelimisha watanzania..

Kumbuka pia wakati huu masikio ya wanatanzania bado yako Arumeru na yatabaki hapo Arusha wakipata somo.

Hakuna namna yoyote itakayoishinda nguvu ya umma na haki ya mtu haipotei bali inacheleweshwa tu!

Mungu ibariki Chadema,Mungu ibariki Nchi yetu!
Alietengua ubunge wa Lema ndie alisema anaweza kushiriki, atakeweka pingamizi la kushiki basi inabidi atangulize pingamizi la kuvuliwa ubunge. Sioni kama kutakuwa na pingamizi kwani jaji amesema Ruksa though unaweza kuwa mtego labda wanasheria watusaidie hapa
 
A way forward ni kuwa kitu kimoja CDM kuna shutma zinaizonga pengine ni propaganda tu za wenye kuchukia maendeleo ya CDM lakini hakuna hata siku moja CDM imekanusha au kutolea maamuzi ambayo yatawafanya watu wapuuze shutma hizo.
1. Kuwa CDM ni chama cha kikanda na hata wabunge wake wengi ni wa kutoka kanda fulani.
2. CDM ina mkono wa kanisa (hapa nakumbuka shutma dhidi ya CUF wao walikuwa wanazikanusha ila kwa bahatio mbaya au sijapata kusikia popote CDM wakikanusha hili)

Mabadiliko yatapatikana watanzania wakiwa wamoja bila kujali kanda zao/koo zao wala dini zao je CDM wapo tayari kuonyesha njia?

Kaka yangu nafikiri unajua kuhusu "Action Speaks Louder than words"waache cdm waproove kupitia hili, pia umejifunza kwa CUF kwamba walikanusha na bado mpaka leo hii watu wanasema ni chama cha kidini. Sasa unataka chadema wafe kwenye njia ile ile walipita cuf wakafa? tena ingawa kuna mambo yalionekana kwamba ni wadini kwa kuangalia na kwa matendo yao mfano mikutano msikitini,safu ya uongozi n.k lakn sio muhimu kwa sasa tumia akili ya kuzaliwa na si kuendeshwa na propaganda za ccm kuita wenziwe wadini katika lala salama ya kifo chake. My Opinion kikubwa ni cdm kuzidi kuelimisha na kutumia peoples power NOT CDM power kukomboa hii nchi. Sasa wewe unaletewa mtu wa kukuongoza kujikomboa kwa kutumia nguvu yako halafu bado unakataa ama unajiuliza mara 2 mbili. Wewe ni woga ama ujeuri unakufanya usijisikie huru
 
Upo Karatu, meru au Moshi? huko ndiko zipo highly demanded! Kwingine hamna mtu anataka kukisikia hicho chama

Hizo ni dadili za magonjwa nyemelezi kwenye ubongo wako. Wahi kwenye kituo cha afya ukaanzishiwe RVS.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom