Dkt. Wilbert Kleruu - Utata wa kifo chake, historia na maisha yake

gm,

1...malengo ya kuanzisha vijiji vya ujamaa ilikuwa ni pamoja na kuwaweka wananchi karibu na, pamoja na kurahisisha kuwapatia, huduma za kijamii, kama barabara,maji,shule,..

..sasa kwa kigezo hicho tu, tayari kulikuwa na maeneo,haswa ya kule uchagani,ambako kwa kweli misingi ya infrastuctures mbalimbali ilishakuwepo.

..pia haikuwa busara kuwahamisha wakulima wa zao la kudumu kama kahawa.

..sikumbuki kahawa iliingia lini Kilimanjaro, lakini naamini ilikuwa miaka zaidi ya 50 kabla ya operesheni vijiji.

..maeneo ya Upareni settlements zao ziko kijamaa-jamaa. zaidi, wana tatizo kubwa sana la ardhi, na hakuna mapori ambayo ungeweza kupima vijiji vipya vya ujamaa.

.2..nadhani utakubaliana na mimi kwamba Kilimanjaro was a unique case, na kulikuwa hakuna ulazima wa zoezi wa operesheni vijiji.
..halafu things went so wrong ktk mikoa mingine, ilibidi zoezi zima lisitishwe.

NB:

kwa upande mwingine napingana na wale wanaodai kwamba alichofanya Mwawindi ilikuwa ni ushujaa.

..ppl had not exhausted every peaceful option ktk kupinga operesheni vijiji.

..hata UHURU wetu hatukupata kwa mapambano ya silaha.

Je yale malengo ya kuanzishwa vijiji yalifanikiwa?
Iliwahi kufanyika tathmini yoyoye kuona kama kulikuwa na ufanisi ama lah?..
Je itakuwa sahihi kusema kuwa operesheni Vijiji ilipelekea sehemu nyingine za Tanzania kurudi nyuma kimaendeleo badala ya kupiga hatua?
 
Kithuku said:
Kwa kumbukumbu yangu wakati wa mchakato vijiji vya ujamaa Peter Abdallah Kisumo alikuwa waziri wa serikali za mitaa na maendeleo vijijini (ndivyo ilivyoitwa wakati huo). Wakati huo alikuwa kijana na alikuwa anavaa zile suti za "Chou en Lai" aina fulani kama zile anazopenda Mzee Malecela. Angalao ninayo sababu fulani ya kukumbuka hilo, lakini mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro wa wakati huo simkumbuki.

Kithuku,

..asante kwa marekebisho kwamba Peter Kisumo alikuwa waziri wa serikali za mitaa na maendeleo vijijini.

..kuna wanaodai kwamba Kisumo alikuwa na ushawishi mkubwa kwa Mwalimu kuhusu Kilimanjaro, na kupelekea wananchi wa huko wasisumbuliwe na zoezi la operesheni vijiji.
 
gm,alnabady,kjnne46,

..pamoja na taabu zote hizo mbona hakukuwa na maandamano au harakati zozote zile kupinga operesheni vijiji?

The Serpent General,

Watanzania ni watu wenye silika za passive resistance! Tumeambiwa na kufundishwa kuwa wenzetu Wakenya walikuwa magangwe na kupigana na vita kama MauMau.

Sisi vita ya kweli dhidi ya mkoloni ilikuwa ni ya Majimaji kama sikosei. Hata kule Uhehe kwa Mkwawa, Tabora kwa Isike, Abushiri, Sina hata Meli, vita vyao havikupewa manjonjo kama vita vya Majimaji.

Huu ugonjwa wa Passiveness sijui tumeutoa wapi. Je tulikuwa nao tangu tukiwa koloni la Uingereza, tukajirithisha wakati wa Nyerere na tunazeeka nalo sasa hivi na Kikwete?

Kwenye mjadala wa vifo vya watoto Tabora, Mwanakijiji kahoji, pamoja na uchungu na kilio kutokana na kufiwa, hasira iko wapi kuonyesha kuchukizwa au kupingana na kilichotokea?

Same could be stated kuhusu Operesheni ya Vijiji vya Ujamaa.

Ukiangalia pamoja na nia yake nzuri, Operesheni hii ilikuwa na mipango mibaya, utendaji mmbovu na mbaya zaidi, wananchi walikosa kauli na hawakushirikishwa.

Lakini ukirudia maandiko ya Nyerere kati ya mwaka 1961-1967, inaelekea kuwa mipango ilikuwa ni mizuri na pasingetokea tatizo lolote wakati wa utendaji na utimilizaji wa kuhamisha watu.

Je ni kitu gani kilisababisha process nzima ya Vijiji vya Ujamaa kuharibika?

Je Sensa ya 1968 ilichangia vipi kubadilika kwa mipango ya awali ya sera hii?

Je waliokuwa viongozi wa Serikali na TANU ambao walikuwa madarakani na Nyerere wakati wa uanzishaji na utekelezaji wa Sera hii, watakuwa tayari leo hii kutupa hadithi zao ama za mafanikio au kushindwa kwa zoezi zima la Vijiji vya Ujamaa?

Naamini kama Nyerere angekuwa hai, angekuja kijiweni na kujitetea ni vipi utekelezaji wa Vijiji vya Ujamaa ulikwenda mrama!

Je angekuwa mbishi kuhusu udhalimu na ubabe wa Serikali yake au angekuwa muungwana na kukiri makosa yaliyotokea? No body knows but Nyerere himself!

Makosa ya sera ya vijiji vya Ujamaa wa kulaumiwa si mwingine bali ni muasisi wa sera Mwalimu Nyerere.

Kama alikubaliana na Kisumo kutosukuma vijiji vya ujamaa Kilimanjaro na kufanya panga pangua, lakini kwingineko kama Iringa jinsi tulivyoelezwa hapa akavurunda mpaka
 
Kithuku,

..asante kwa marekebisho kwamba Peter Kisumo alikuwa waziri wa serikali za mitaa na maendeleo vijijini.

..kuna wanaodai kwamba Kisumo alikuwa na ushawishi mkubwa kwa Mwalimu kuhusu Kilimanjaro, na kupelekea wananchi wa huko wasisumbuliwe na zoezi la operesheni vijiji.

Ni kweli kipindi hicho kulikuwa na watu wengi wa Kilimanjaro waliokuwa na ushawishi mkubwa na Mwalimu Nyerere. Wakati huo Kisumo akiwa waziri, walikuwepo wenzie pia baadhi wakiwa mawaziri kutoka Kilimanjaro, akiwemo mpare mwenzie Chediel Yohana Mgonja, Eliufoo, Nsilo Swai, na mwaka 1975 akaingia Lucy Lameck, na Cleopa Msuya ambaye Mwalimu alimwamini sana kwenye technical details. Wote hawa walikuwa na ushawishi mkubwa sana kwa Mwalimu. Fikiria miaka ile ya ujamaa na vyama vya ushirika jinsi biashara binafsi zilivyokuwa zinapigwa vita, lakini Mzee Mberesero (wa huko Mwanga kwa Msuya) alimudu kuwa na kampuni ya mabasi ya Ngorika ambayo ilikuwa inashindana na KAMATA ya serikali, na hakuguswa na mtu tangu mwaka 1970. Huo ni mfano mmoja tu, kulikuwa na "untouchables" wengi. Arusha familia ya kina Maeda wamekula good time tangu hizo enzi za ujamaa, si kwa wizi au mshahara wa uma, bali kwa biashara ambazo wengine walikuwa wanawekewa vigingi kuingia (Joel Maeda alikuwa mwenyekiti wa TANU mkoa), walikuwa na mabasi yanaitwa Kilimanjaro (KBS), pia walijenga mahoteli makubwa na yanatesa hadi leo (kama mnajua Golden Rose ni mojawapo). Kwa hiyo siasa ya ujamaa ilisema viongozi wasiwe na hisa kwenye kampuni (lakini walikuwa si na hisa tu, bali waliendesha biashara kubwa), ilisema wahimize ujamaa na ushirika (lakini walisaidia watu binafsi "wateule" wachache)! Wakati huo ilikuwa mbinde, ukitaka kuanzisha japo genge tu la kuuzia nyanya na mishumaa, lazima upate kwanza kibali kutoka kwa "Afisa Ujamaa na Ushirika" wa wilaya, ambae hawezi kutoa kibali kama hujaja na barua kutoka mwenyekiti wa kijiji na katibu kata, halafu uje na orodha ya watu mnaoshirikiana ili genge lako lipate sifa ya "duka la ushirika", ndipo akuandikie kibali cha kwenda kuomba leseni. Na hata leseni ukipata, unalazimika kuwa bidhaa zote za dukani kwako ukazinunue RTC, ambako utafungua faili (lilikuwa kama kadi fulani gumu, unawekewa tiki kila unapopata mgao wako wa bidhaa!) Huwezi kununua bidhaa kuendana na mahitaji ya wateja wako, utanunua kwa mgao, kama wakisema sukari si zaidi ya kilo 50, basi huwezi kupata zaidi! Na kuna wakati walikuwa wanasukuma bidhaa fulani kwa nguvu, kwa mfano wanasema bidhaa zilizopo ni sukari, sabuni, vibiriti, chumvi na kanga, na ni lazima ununue zote kwa ratio waliyoweka, ukikataa moja umekataa zote! Sasa shangaa kwamba katika mazingira kama hayo, kuna watu walimudu kufanya biashara kubwa na makampuni kama hayo niliyokupa mfano, jiulize waliwezaje? Kifupi ni kwamba Kilimanjaro ujanja waliujua siku nyingi, na ulipokuja huo ujamaa wakatunga mbinu za kuweza ku-survive humohumo, wakisaidiwa of course na wakubwa waliokuwa karibu na Nyerere ambao waliweka ushawishi wa kuwawezesha kuendelea na mambo yao.
 
Kitu kingine cha ajabu kuhusu hii sera ya vijiji vya ujamaa ambavyo vilikuja kwa cost kubwa kwa wananchi na serikali, kulikuwa na mbwebwe za kushangilia ambazo zilikuwa ni itikadi za kuonyesha kuwa sera hii inakubalika na kuonekana kuwa imefanikiwa. Maonyesho ya saba saba na sikukuu za wakulima zilitokea huku na pia kulikuwa na taratibu za kuwapeleka watu kwenye uwanja wa sabasaba kushindanisha mabeberu na kutoa zawadi kwa kijiji kilichofanya kazi haswa na kutoa mazao mengi. utashindwa kuelewa kuwa tunapatiana zawadi na kupongezana kwa kilimo ambacho hakikuweza kukidhi mahitaji yetu ya chakula hadi tunaletewa unga wa yanga miaka ya sera hizo.

Lingekuwa jambo la busara kwa kipindi kile viongozi na hasa Nyerere kukubali hadharani kuwa siasa ya ujamaa haifai na iachwe mara moja. Lini siasa hii iliachwa hakuna aliyesema, upi ulikuwa mkakati mbadala wa siasa hii hakuna aliyewaambia wananchi. Kwa kiasi kikubwa Nyerere anapewa heshima na pongezi kwa mambo mengi ila hapa hii lawama inamuangukia na siasa ya ujamaa ambayo haikuwa imefanyiwa utafiti wa kutosha.
 
Ni kweli kipindi hicho kulikuwa na watu wengi wa Kilimanjaro waliokuwa na ushawishi mkubwa na Mwalimu Nyerere. Wakati huo Kisumo akiwa waziri, walikuwepo wenzie pia baadhi wakiwa mawaziri kutoka Kilimanjaro, akiwemo mpare mwenzie Chediel Yohana Mgonja, Eliufoo, Nsilo Swai, na mwaka 1975 akaingia Lucy Lameck, na Cleopa Msuya ambaye Mwalimu alimwamini sana kwenye technical details. Wote hawa walikuwa na ushawishi mkubwa sana kwa Mwalimu. Fikiria miaka ile ya ujamaa na vyama vya ushirika jinsi biashara binafsi zilivyokuwa zinapigwa vita, lakini Mzee Mberesero (wa huko Mwanga kwa Msuya) alimudu kuwa na kampuni ya mabasi ya Ngorika ambayo ilikuwa inashindana na KAMATA ya serikali, na hakuguswa na mtu tangu mwaka 1970. Huo ni mfano mmoja tu, kulikuwa na "untouchables" wengi. Arusha familia ya kina Maeda wamekula good time tangu hizo enzi za ujamaa, si kwa wizi au mshahara wa uma, bali kwa biashara ambazo wengine walikuwa wanawekewa vigingi kuingia (Joel Maeda alikuwa mwenyekiti wa TANU mkoa), walikuwa na mabasi yanaitwa Kilimanjaro (KBS), pia walijenga mahoteli makubwa na yanatesa hadi leo (kama mnajua Golden Rose ni mojawapo). Kwa hiyo siasa ya ujamaa ilisema viongozi wasiwe na hisa kwenye kampuni (lakini walikuwa si na hisa tu, bali waliendesha biashara kubwa), ilisema wahimize ujamaa na ushirika (lakini walisaidia watu binafsi "wateule" wachache)! Wakati huo ilikuwa mbinde, ukitaka kuanzisha japo genge tu la kuuzia nyanya na mishumaa, lazima upate kwanza kibali kutoka kwa "Afisa Ujamaa na Ushirika" wa wilaya, ambae hawezi kutoa kibali kama hujaja na barua kutoka mwenyekiti wa kijiji na katibu kata, halafu uje na orodha ya watu mnaoshirikiana ili genge lako lipate sifa ya "duka la ushirika", ndipo akuandikie kibali cha kwenda kuomba leseni. Na hata leseni ukipata, unalazimika kuwa bidhaa zote za dukani kwako ukazinunue RTC, ambako utafungua faili (lilikuwa kama kadi fulani gumu, unawekewa tiki kila unapopata mgao wako wa bidhaa!) Huwezi kununua bidhaa kuendana na mahitaji ya wateja wako, utanunua kwa mgao, kama wakisema sukari si zaidi ya kilo 50, basi huwezi kupata zaidi! Na kuna wakati walikuwa wanasukuma bidhaa fulani kwa nguvu, kwa mfano wanasema bidhaa zilizopo ni sukari, sabuni, vibiriti, chumvi na kanga, na ni lazima ununue zote kwa ratio waliyoweka, ukikataa moja umekataa zote! Sasa shangaa kwamba katika mazingira kama hayo, kuna watu walimudu kufanya biashara kubwa na makampuni kama hayo niliyokupa mfano, jiulize waliwezaje? Kifupi ni kwamba Kilimanjaro ujanja waliujua siku nyingi, na ulipokuja huo ujamaa wakatunga mbinu za kuweza ku-survive humohumo, wakisaidiwa of course na wakubwa waliokuwa karibu na Nyerere ambao waliweka ushawishi wa kuwawezesha kuendelea na mambo yao.

Kithuku,

Kama kina Masawee (sic) walikuwa na ujanja ujanja na kumpiku Kifimbo, ina maana wengine walikuwa mafala?;)

If it was possible kwa Wachaga, Waarabu na Wadosi, iweje wengine manyanga yalibwagwa chini? je hawakuwa na viongozi wanaojiamini kuweza kujenga hoja hata kum-face Mwalimu kama hawa Wachaga na Wapare walivyofanya?

What went wrong? Okay, Mwalimu exploited the opportunity to increase his sphere of influence and his reign, but how did we end up surrendereing hands down without massive resistance? Are we in some way acknowledging the Ndivyo Tulivyo doctrine?
 
@gm,

GM,

Nimesema kule kwenye Nyerere na influence za Ujamaa na Siasa. Tatizo si sera au siasa, bali ni watu na uongozi na la nyongeza kumnukuu Bob Mkandara ni Mazingira.

Leo hii hata tukiletewa Ubepari kama tulivyoishi nao kwa miaka karibu 16, bado tunachechemea na hatuna mbele wala nyuma.

Hivyo ukikaa chini na kutafakari, unakuta si Sera au Siasa, bali ni Watu, Uongozi na Mazingira.

Tutakakapoweza kubadilisha mawazo na namna ya vitu hivi vitatu na kuvipa nguvu chanya tutaweza kuona mabadiliko. Wa kwanza katika hilo kuhojiwa ni sisi kama Watu. Je tuna nia na utashi wa maendeleo?

Niliposema kwenye hoja hiyo ya Nyerere, Ujamaa na Azimio kuwa Watanzania ni wavivu, ilibidi nirudi nije nitoe ufafanuzi wa kauli yangu.

Nitayasema hapa, kwa nini Tanzania tunashindwa sera na siasa za kuongoza Taifa.

Kwanza ni Watu, pili ni Uongozi na tatu ni Mazingira. Kama akija Mzungu na kuwa mnyapara, nakuambia watu wangehamia vijijini kwa mwendokasi wa mwanga, wangejituma bila kuwa na ubishi na kama enzi za Ukoloni na Utumwa, tungefanya kazi marudufu kumfurahisha "Bwana Mkubwa".

Lakini katika kujitawala kwetu, ni wachache ambao waliendelea kujituma bila mijeledi. Hawa ndio kina Mwanamwindi, ambao walikataa kupigwa mijeledi na "Wazungu Weusi" kwa kuwa walishafikia upeo wa kujituma na kujitosheleza.

Nimeongelea mara kadhaa suala la Mtanzania kujitegemea na kusema siku Mtanzania atakapokuwa na Uhuru wa Fikra, Mawazo na Kujitosheleza kwa mali na hata kuwa na ziada kwa hiari yake mwenyewe, siku hiyo itakuwa siku ya Ukombozi. Siku hiyo ndipo wana wa Israeli watafika Kaanani nchi tuliyoahidiwa.

Mwanamwindi alikuwa muasisi wa Mtanzania huyu aliye huru na anayejitegemea, bahati mbaya safari yake ilifupishwa kutokana na ubabe wa Mzungu mweusi na hasira za kukataa kuwa mnyonge.
 
Rev. Kishoka,

Nimekupata hii ni safari ya kujituma bila kuangalia mwenzako anafanya nini na nani anakusupport au hakusupport. Ni safari ambayo kila mwenye moyo atajituma kwa nafasi yake na opportunity zilizopo na kutengeneza ambazo hazipo katika swala zima la kujikomboa kiakili na kimtazamo.
 
... je hawakuwa na viongozi wanaojiamini kuweza kujenga hoja hata kum-face Mwalimu kama hawa Wachaga na Wapare walivyofanya?

What went wrong? Okay, Mwalimu exploited the opportunity to increase his sphere of influence and his reign, but how did we end up surrendereing hands down without massive resistance? Are we in some way acknowledging the Ndivyo Tulivyo doctrine?

Ndivyo tukoje ?

Katika hao tulio hivyo, sisi kina nani, na hao Wachaga na Wapare wamo humo ? Huyo Nyerere na wewe mwenyewe mmo humo kwenye kundi la hivyo mlivyo ?

Ile idea ya ndivyo mlivyo labda huwa tunaongelea kitu tofauti. Rev. Kishoka ukitamka hicho kitu sehemu yeyote duniani, hususan mbele ya watu wanaofuatilia masuala ya mahusiano ya races za binadamu utaeleweka unazungumzia idea yenye mizizi ya kinazi, iliyoenezwa zaidi na Dokta Watson, aliyegundua structure of DNA, ambae alipokuwa senile uzeeni, akaanza kudai kwamba katika level ya DNA, watu weusi wote tuna inferior cerebral prowess kulinganisha na Wazungu. Sasa kama unakubali hivyo, basi si Nyerere, si hao Wachaga wala Wapare ambao wanaweza kujenga hoja mbele ya Nyerere ambao wanaepuka kundi hilo. Hiyo bigoted idea haina walakini. Wewe Rev. Kishola unadhani kwamba inawezekana wewe na race yako nzima mme evolve kuwa inferior kwa mzungu ? (tunachoongelea kukilinganisha hapa ni nguvu za kufikiri, down at the DNA level, sio utajiri wa uchumi au umahiri wa mbio za kuogelea, au urefu wa viungo vya mwili, au utaalam wa asili wa kupiga mdundiko). Unadhani inawezekana tuko inferior kwa weupe kwa kufikiri?

Manaka, labda tuelewane, tunaongelea kina nani tuko hivyo ? Halafu, haswa haswa, tukoje ? Let's work out the definitions first.
 
Rev. Kishoka,

Wengine hawakuwa mafala, nadhani kuna waliokubali na kumwamini Mwalimu kama nabii (hasa waliogawiwa mashamba), kuna walioogopa kukosa vyote wakaamua kuufyata, na kuna walioamua kumkabili waziwazi kumpinga, na kwa kweli hawa walipata tabu sana. Lakini kuna walioamua "kula na kipofu", kuwa wanafiki kumwimbia mtu sifa ambazo hawaziamini moyoni, ili watakachomwambia awakubalie, "kumtumikia kafiri wapate mradi wao" nk. Wajua hata msichana mrembo ukitaka kumpata kiulaini kwanza unamjengea imani, akishakuamini pasi shaka lolote, basi sema chochote utapata!

Hiyo ndiyo tabia ya jamaa zetu wachaga na wapare (samahani kama kuna watakaodhani kuwa huu ni ukabila, lakini ni uzoefu wangu wa kuishi kwao, na pia nadhani ni sifa nzuri maana imewasaidia sana). Mchaga au mpare akitaka kitu kwako iwe ni cha biashara au ni chochote cha faida, haji directly "naomba hiki" au "nataka hiki", huwa wanaanza mbali, anajenga urafiki, anakuwa upande wako anakutetea hadi unamwamini sana, halafu siku ikifika akakutajia anachotaka, utaona kama ni kitu kidogo tu kwa kuzingatia ukaribu wenu, na kamwe hutajua ndicho kilichomleta! Hiyo wamechukua tangu zamani za wale machifu "Mangi", ilikuwa ukitaka kitu kwa Mangi unafanya mambo ambayo yatamfanya akujue: kama kumpelekea vizawadi, kumwalika kwenye sherehe zako na kumchomea "ndafu", kupeleka watoto wako wakafanye kazi kwake bure, halafu siku ya siku unamtokea unasema "Mangi naomba shamba", wallahi atanyang'anywa mwingine upewe! Au ikitokea sababu ya kunyang'anya shamba, la kwako halichukuliwi. Kwa hiyo hawa walimchezea Nyerere kwa kutumia uleule utamaduni wao. Kuna wimbo fulani wachaga walikuwa wanamuimbia Mangi wao Marealle kabla ya uhuru, lakini baada ya uhuru walipogundua kuwa Nyerere na Marealle "haziivi", na Nyerere sasa ana nguvu kuliko Marealle (ambaye alishatorokea UK), walimwalika Nyerere wakam-"crown" Umangi kwa kumvisha vazi linaitwa "mbelele", linavaliwa na Mangi tu hilo, halafu ule wimbo wakafuta jina "Marealle" wakaweka "Nyerere", na unaimbwa hadi leo. Kichekesho ni kwamba huwa wachaga wanauimba huo wimbo kwenye harusi "Nyerere kasema tupige matuta" (pengine kwa kukosa nyimbo nyingine za kichaga)! Ndivyo kina Kisumo na Nsilo Swai "walivyomshika masikio" Nyerere.
 
Kithuku,

Naona umenipa siri ya wachaga hapa, itabidi niifanyie kazi sasa! LOL teh teh teh!
 
Ninachoweza kusema ni kuwa wananchi hawakuwa na pa kwenda kumshtaki Nyerere au namna ya kumshughulikia Nyerere mwenye Serikali,bunge na mahakama.

Wakuu naomba kusema hivi, mimi simchukii Mwalimu as a person, isipokuwa nina tatizo sana na some of his policies, lakini pia ninajua na kuamini as a fact kua kama kiongozi, kuna mazuri aliyotufanyia na mabaya, aliyoyafnya kwa kibin-adam, na menigne kwa makusudi mazima,

Lakini hapa ni pahali pa elimu, basi tuwe fair japo kidogo, tuweke mabaya yake na mazuri yake, ili msomaji ambaye ni bina-adam mwenye mapungufu kama Mwalimu, aweze kujona kwenye picha inayokuwa-painted hapa kuhusu uongozi wa Mwalimu, lakini kufikia mahali pa kudai alitakwia afikishwe kwenye sheria ina maana sasa tunamuweka kundi moja la kina Lowassa, ambao tunataka wafikishwe kwenye sheria, sasa tukifanya hivyo Mungu atatuletea noma kwenye taifa letu,

Ingawa pia sio rahisi kuya-overcome mapungufu ya Mwalimu, kwa sababu yapo all over to be seen, lakini bado siamini kuwa alitakwia kufikishwa kwenye mikono ya sheria, unless kuna something I am missing, au tuwekeni sawa maana wakuu huenda kuna something mnajua hamsemi?
 
Haya mnayoandika ni madogo makubwa ipo siku yatatolewa huko usoni na wengi watashangazwa na ukweli wa hali halisi ya nchi
 
Field Marshall ES,

Heshima mkuu,

Nafikiri mengi mazuri ya Mwalimu tunayaongea kila siku ikiwa ni pamoja na kuleta uhuru na kutuunganisha kwa lugha na undugu, sidhani kama kuna mtu anaweza kusahau hayo kamwe, ni mengi siwezi hata kumaliza kuyataja.

Ila hapa hili la dr. Kleruu na sera za ujamaa pia haliwezi kuwa overlooked pia, kama mimi binafsi sikuwa najua chochote kumhusu huyu Dr. hadi siku mbili zilizopita, nimekuwa nikiimba wimbo wa Marehemu Mwinshehe bila kujua ila baada ya kuona na kusikia yaliyotokea hata wimbo nauogopa tena hivo. Nafikiri umeleta point nzuri sana ila mazuri ya Nyerere hayawezi kusahaulika!
 
Ndivyo tukoje ?

Katika hao tulio hivyo, sisi kina nani, na hao Wachaga na Wapare wamo humo ? Huyo Nyerere na wewe mwenyewe mmo humo kwenye kundi la hivyo mlivyo ?

Ile idea ya ndivyo mlivyo labda huwa tunaongelea kitu tofauti. Rev. Kishoka ukitamka hicho kitu sehemu yeyote duniani, hususan mbele ya watu wanaofuatilia masuala ya mahusiano ya races za binadamu utaeleweka unazungumzia idea yenye mizizi ya kinazi, iliyoenezwa zaidi na Dokta Watson, aliyegundua structure of DNA, ambae alipokuwa senile uzeeni, akaanza kudai kwamba katika level ya DNA, watu weusi wote tuna inferior cerebral prowess kulinganisha na Wazungu. Sasa kama unakubali hivyo, basi si Nyerere, si hao Wachaga wala Wapare ambao wanaweza kujenga hoja mbele ya Nyerere ambao wanaepuka kundi hilo. Hiyo bigoted idea haina walakini. Wewe Rev. Kishola unadhani kwamba inawezekana wewe na race yako nzima mme evolve kuwa inferior kwa mzungu ? (tunachoongelea kukilinganisha hapa ni nguvu za kufikiri, down at the DNA level, sio utajiri wa uchumi au umahiri wa mbio za kuogelea, au urefu wa viungo vya mwili, au utaalam wa asili wa kupiga mdundiko). Unadhani inawezekana tuko inferior kwa weupe kwa kufikiri?

Manaka, labda tuelewane, tunaongelea kina nani tuko hivyo ? Halafu, haswa haswa, tukoje ? Let's work out the definitions first.

Kuhani,

Kama ukisoma majibu yangu vizuri, utabainisha ni kwa nini nimesema tunakubali kuwa ndivyo tulivyo!

Ndivyo Tulivyo pamoja na kuwa ni gumzo kule kwenye hoja ya kauli na misemo ya Tanzania, bado itabakia kuwa general and ambigous!

Matumizi yangu hapa ya Ndivyo Tulivyo ni kwa maana ya kuburuzwa bila kujitutumua bila kupinga! Hali hiyo si ya Dr. Watson au lolotem ni ukweli wa mambo na pamoja na kuuma kwake na hata kuwasha, bado sisi tu wepesi kuburuzwa. Iwe ni Azimio la Arusha, Ujamaa Vijijini, Mbio za Mwenge, Azimio la Zanzibar, Soko Huria, Cost Sharing, OIC, Muungano, Rada, UFISADI, IPTL na mengine mengi ambayo kama Raia ama kwa njia moja au nyingine tumeburuzwa bila kuleta mgomo au kudai kwa hasira tuwe na majadiliano au kuwa na nguvu katika kutoa maamuzi ambayo tumeyakabidhi kwa Wanasiasa wetu!
 
Ni kweli kipindi hicho kulikuwa na watu wengi wa Kilimanjaro waliokuwa na ushawishi mkubwa na Mwalimu Nyerere. Wakati huo Kisumo akiwa waziri, walikuwepo wenzie pia baadhi wakiwa mawaziri kutoka Kilimanjaro, akiwemo mpare mwenzie Chediel Yohana Mgonja, Eliufoo, Nsilo Swai, na mwaka 1975 akaingia Lucy Lameck, na Cleopa Msuya ambaye Mwalimu alimwamini sana kwenye technical details. Wote hawa walikuwa na ushawishi mkubwa sana kwa Mwalimu.

Mkuu Kithuku, hivi ni kweli kwamba Lucy Lameck alikufa kwa ngoma??!!
 
@gm,

Tatizo si kujadili mazuri na mapungufu, tatizo ni zile chuki zinazosema Mwalimu alikuwa Mhaini, akamatwe, tumnyonge au tufukue Maiti yake tuihukumu!

Kuna watu tayari wanamfananisha na Charles Taylor, Bokasa na Idi Amini!

Ukiuliza ni vipi alikuwa mhaini, unaambiwa aliweka watu kizuizini, alituletea Umasikini kwa Azimio na Ujamaa wake, alituingiza kwenye vita na Amin, alinyanyasa Waislamu, tumpeleke The Hague kwenye mahakama ya dunia tumshitaki!

This is what FMES is against na anaomba tusijipeleke kwenye huo ukanda!
 
Mkuu Kithuku, hivi ni kweli kwamba Lucy Lameck alikufa kwa ngoma??!!

Lucy Lameck alifariki baada ya kuugua muda mrefu. Alilazwa muda mrefu tu pale hospitali ya KCMC, lakini kwa hakika sifahamu ni nini kilichokuwa kikimsumbua.
 
Jiepushe na yule Binti anayejizungusha zungusha karibu nawe, ataomba kabati la baridi (jokofu);)

Du kumbe umemuona huyo binti, balaa hii tena mie nilifikiri ndio nimepata siri ya kumtokea tena hapa! Hilo kabati tena basi!!LOL
 
Back
Top Bottom