Sam GM
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 535
- 28
- Thread starter
- #61
Masanja,
..unajua kuna watu wanafikiri kutoa visingizio vya ajabu-ajabu kama hivyo hapo juu wanamtetea, kumlinda, na kumuenzi, Baba wa Taifa.
..ku-suggest kwamba Mwalimu Nyerere alikasimisha mamlaka yake ya kusaini death-warrants kwa watu wengine ni kumtukana matusi makubwa kabisa.
Mwikimbi,
..Peter Kisumo, akiwa mkuu wa mkoa, ndiye aliyemshawishi Mwalimu kutokupeleka operesheni vijiji Kilimanjaro.
..kuna sababu nyingi tu zikiwemo za kihistoria, kisiasa, kijiografia, na hata kiuchumi, kwamba zoezi hilo lingeleta madhara makubwa, na lilikuwa halitekelezeki, katika maeneo mengi ya Kilimanjaro.
..Kithuku ameleta maelezo ya kina kuhusu maeneo ambayo vijiji vya ujamaa vilianzishwa Kilimanjaro. lakini utaona kwamba zoezi hilo lilitekelezwa ktk maeneo ambayo kiasili yamekuwa hayakaliwi na makabila makubwa ya Kilimanjaro--Wachaga na Wapare.
Jokakuu,
Maelezo yako ni mazuri na yanaleta mwanga kidogo kuhusu nini kiliendelea wakati ule, kwa mtizamo wangu ninaona kama hii siasa ya ujamaa na vijiji ilikuwa tayari haifai hata kabla haijaanza, kwa sababu huwezi ukalazimisha watu wa sehemu au mikoa fulani kuhama wakati sehemu zingine hawafanyi hivyo. Kwa mtizamo wangu Nyerere angechukua mda yeye na washauri wake kuangalia jambo hilo katika angle nyingi tofauti kabla hawajaamua kuwatoa watu baruti katika maeneo yao kwa jina la kujenga taifa!!