Dr Walid Amani Kabourou yuko wapi?

CAMARADERIE

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
4,419
1,920
Ningependa kujuzwa alipo huyu bwana mkubwa aliyekuwa mwiba wa CCM akiwa CHADEMA na hatimaye kuhamia CCM.
 
Ni mbunge wa bunge la Africa Mashariki kupitia CCM ambao alipewa kama asante kwa kuwasaidia CCM kushinda jimbo la Kigoma mjini alilokuwa akiliongoza yeye. Pia anaendesha chuo chake kikuu kiitwacho "Western Tanganyika Collage" kilichopo Kigoma mjini ambapo kwa sasa kinatoa kozi za computer.
 
Are you sure Mkuu?? Nilifikiri alikuwa huko bunge lililopita.
 
Wakuu,
Huyu jamaa alitingisha sana enzi zile Kigoma akiwa mbunge kwa tiketi ya chadema. Niseme tu kuwa huyu alikuwa mmoja wa watu walioufanya mkoa wa Kigoma kuwa ngome ya upinzani hasa chadema kwa wakati huo.

Ili kudhibiti upinzani, baadaye alirubuniwa na magamba na kujiunga nao. Alipewa ubunge wa Afrika mashariki.

Tangu wakati huo sijamsikia tena miaka takribani kumi.

Amepotelea wapi Dr. Warid Kabouru?
 
Yupo anajilia pensheni kama msataafu katika kitengo cha kuvuruga upinzani nchini. Ila bado amekuwa msaada sana kwa watu kama Shibuda wanaweza kumcheki kubadirishana uzoefu kisiasa.
 
Yupo anajilia pensheni kama msataafu katika kitengo cha kuvuruga upinzani nchini. Ila bado amekuwa msaada sana kwa watu kama Shibuda wanaweza kumcheki kubadirishana uzoefu kisiasa.
Au pengine amepewa ukurugenzi kwenye taasisi ama mwenyekiti wa bodi fulani hivi.
 
Hata mimi nilikua najiuliza kuhusu huyu jamaa. Ila alikosea sana kurudi gambani huyu ni sawa na akina Masumbuko Lamwai wamepotea kabisa hata ndugu yangu Tambwe Hiza wote hawa kushinei baada kurudia gamba
 
Wapo na Makamba Sr wanawaandalia makao magamba wenzao maana yeye ndiye aliyempeleka ccm.
 
Sikilizeni! Dr Aman Walid Kabourou aliihama CDM kwa pesa ya EPA. Mwenye jukumu la kuhakikisha anahamia CCM alikuwa Maranda ambaye magamba wammefunga jela. Maranda na Dr Kabourou wana uhusiano wa kidugu, na ndiyo sababu kila siku kesi ya Maranda ilipokuwa inatajwa ama kusikilizwa pale Kisutu Dr Kabourou alikuwepo. Baada ya kukwapua pesa ya EPA, Mangulla akampa Maranda kazi ya kuhakikisha analirejesha jimbo la Kigoma Mjini CCM. Kumbuka waratibu wakuu wa EPA ndani ya CCM walikuwa Mangulla, Rostam, Mama Meghji na Salome Mbatia. Dr Kabourou akapewa sh 147 millioni kutoka zile za EPA, aliandikiwa hundi na Maranda. Ushahidi upo kwenye ripoti ya uchunguzi ya Hosea, Mwanyika na Mwema. Dr Kabourou akaahidiwa ubunge wa Afrika Mashariki, akapata. Siku hizi sijui alipo! Atakuwa anatafutiwa nafasi, subirini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom