Dr. Ulimboka Stephen na harakati za kuimarisha mfumo wa afya Tanzania

kebepa

Senior Member
Dec 20, 2009
133
14
Masomo ya udaktari ni magumu na yanachukua miaka mingi (miaka mitano ya darasani na kufuatiwa na mwaka mmoja wa mafunzo kwa vitendo) kwa mtu kuwa daktari wa kawaida, miaka huongezeka zaidi kutokana na daktari mhusika anataka kubobea katika kitu gani.

Hivyo, ilikuwa ni lazima kufunga mkanda kuhakikisha kuwa mtu anapita vikwanzo mbalimbali katika masomo ili mwisho wa siku awe daktari.

Mwaka wa kwanza, masomo ni magumu kiasi kwamba kuna kipindi wanafunzi hukimbiana kwa maana kwamba inabidi kutafuta mahali palipotulia pa kusomea na kurudi mtu akiwa amechoka na hivyo kulala mara nyingine bila hata kuwa na maongezi na rafiki anakaa nao chumba kimoja
Namfahamu daktari huyu tangia alipokuwa chuo kikuu.

Dr. Ulimboka ni miongoni mwa wanafunzi waliokuwa wanajituma sana. Dkt Ulimboka Stephen wakati huo akiwa mwanafunzi , alikuwa ni mmoja kati ya wanafunzi wenye bidii na wenye udadisi wa hali ya juu katika mambo mbalimbali yanayohusu taaluma pamoja na mambo mbalimbali ya kijamii ambayo yanaonekana kutokwenda sawa. Ni mtu ambaye anaweza kujenga hoja kwa utulivu na hivyo kama hujajipnaga siku zote atakushinda.

Kuna watu ambao wanapenda kurahisisha mambo bila kuumiza vichwa vyao kuangalia mantiki ya kila jambo linalotokea walikuwa wanamwita mbishi na pengine wasingeweza kuendelea kuchangia katika hoja hizo kwa maana kwamba mazungumzo au mabishano na kijana huyu yalikuwa yanaweza kuzifikisha akili zao kule wasikoweza kuendelea kujenga hoja na hivyo kushindwa kutetea mantiki ya hoja zao.

Kwa sababu ya uwingi wa wanafunzi katika chuo hiki wakati huo, na mfumo wa malazi ya wanafunzi kutokuwa unaeleweka, ilipelekea wanafunzi wengi wa udaktari kutofahamiana na hivyo kuna wengi tu ambao hawakujua undani wa Ulimboka Stephen, lakini kwa waliokuwa karibu naye waliweza kuona kuwa hii ni hazina katika maendeleo ya nchi hususani katika sekta ya afya maana ni mtu ambaye anaweza kujenga hoja na kukemea mfumo usioridhisha kwa hoja zenye mantiki na zinazohitaji mtu kufikiria ‘nje ya boksi’’.

Katika mijadala mbalimbali iliyokuwa imeibuka katika mazingira ya kimasomo au nje ya masomo hasa wakati wa majadiliano ya kimakundi, pale panapokuwa na utata aliweza kudadisi na mwishowe kufikia muafaka katika suala husika.

Mazingira ya elimu ya juu katika nchi yetu bado ipo katika mazingira ambayo yanavutia migomo na migogoro ya mara kwa mara, hivyo basi kama wanafunzi wakati huo tulalikumbwa na migomo na migogoro hiyo, kwa wakati huo uhusika wake katika migomo na migogoro hii haukuwa wa hali ya juu kwani dhamira yake ilijikita kwenye weredi wa fani ya udaktari hata kama ni katika mazingira magumu ya kusoma. Hivyo basi kama ilitokea kuwa kuna mgomo au mgogoro ambao unawagusa wanafunzi wote naye alikuwa ni mmoja wa walikokuwa wnapata adhabu ambazo wanafunzi wengi wanakuwa wamepata.

Alikazana kusoma miaka yote mitano na hatimaye kumaliza na kupata shahada ya udaktari.

Harakati za kuendesha mapambano ya kudai haki na maboresho katika sekta ya afya zilianza wakati akiwa daktari katika mafunzo (intern doctor) katika hospital ya Muhimbili mnamo mwaka 2005, katika hali isiyo ya kawaida alijitokeza na kuwa mwenye msimamo mkali na kuibuka kama kiongozi (bila kuchaguliwa rasmi na watu) kutokana na hoja zake zenye mantiki ambazo alikuwa anazijenga na hivyo watu mbalimbali kuanza kuvutiwa naye na hatimaye kumhalalisha kuwa kiongozi wa mapambano hayo ambayo hasa yalilenga kuinua maslahi ya madaktari ili waeze kuhudumia watanzania jinsi inavyotakiwa. Mgomo ulijikita katika falsafa ya kuifanya serikali kuinua maslahi ya watumishi wa afya ili huduma bora zitolewa kwa wananchi kupitia kwa watumishi ambao hawana kinyongo na wanafanya kazi kwa moyo wote “ well motivated health workers”.

Katika mgomo huu, mazungumzo yaliweza kufanyika na serikali wakati huo Mh. Professor David Mwakyusa ndiye alikuwa Waziri wa afya na kufikia maamuzi ya kupandisha mshahara wa watumishi wa sekta ya afya nchini. Mabadiliko hayo ya maslahi kwa watumishi wa sekta ya afya yamekuwa na mafanikio makubwa sana katika taifa letu kwa maana kuwa; Mosi, madaktari wengi ambao walikuwa huwa wanakimbilia nchi za jirani kwa ajili ya kufuata maslahi mazuri waliweza kubaki na kuajiriwa na serikali hapa hapa nchi ni, pili, upatikananji wa wahudumu wa afya wenye sifa katika wilaya mbalimbali uliongezeka tatu, udahili wa wanafunzi katika vyuo vikuu katika fan iza afya uliongezeka.

Vile vile, kutokana na kuwa na watumishi wa afya wenye sifa katika hospitali mbalimbali za ngazi ya mikoa na wilaya, msukumo wa kuboresha mazingira ya kazi uliongezeka (ambao pengine umechangia kuwepo kwa mgomo huu wa sasa wa kudai upatikanaji wa vifaa tiba na kudai kuboreshwa kwa mazingira ya kazi kwa watumishi wa afya walioko vijijini).

Mgomo wa madaktari unaoendelea sasa umedumu kwa takribani miezi saba kufikia sasa. Mgomo huu ulitokana na uzembe uliofanywa na viongozi wa wizara ya afya na usitawi wa jamii baada ya kutowalipa intern doctors posho zao za mwezi , na wanapodai haki zao, wakafukuzwa hospital ya Muhimbili kibabe na kurudishwa wizarani (hata hivyo, viongozi hawa wazembe wamewajibishwa, ila amebaki mmoja ambaye ni mkurugenzi wa Muhimbili ambaye alishindwa kutumia busara na kutii aliyoambiwa na wakubwa wake bila kuhoji na kujadiliana na menejimenti yake na kutoa mapendlezo kuhusu suala hilo).

Mkurugenzi huyu, naye hana muda mrefu wa kuendelea kuongoza taasisi iliyomshinda.

Katika kuhakikisha intern doctors wanarudishwa Muhimbili bila mashariti yeyote, chama cha madaktari Tanzania (MAT) kiliitisha mkutano wa wanachama wote, ili pamoja na mambo mengine, kujadili suala hili la intern doctors. Mjadala uliishia kuwa intern doctors warudishwe bila masharti na viongozi wa wizarani wawajibike.

Vile vile katika mijadala hii zikaja hoja za madai ya kuboresha sekta ya afya na kuwa na madai kama ifuatavyo: .

i. Kuondolewa kwa viongozi wakuu katika W/Afya kutokana na ushahidi wa uovu wao
ii. Kuboresha huduma za Afya hospitalini(ongeza vitanda, watumishi, madawa, zana za kazi)
iii. Kuwapatia watumishi wa sekta ya Afya kadi ya kijani ya Bima.
iv. Kudai posho ya kuitwa kazini kwa 5%.
v. posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi (30%)
vi. Posho katika mazingira magumu (30%).

vii. Mshahara kuwa mil.3.5, (sawa na ongezeko la 70%)

Katika kuhakikisha madai haya yanafuatiliwa, madaktai walipendekeza kuwe na kamati maalumu ya kufuatilia madai haya.

Kutokana na uzoefu kutoka mgomo wa 2005, Dr Ulimboka alichaguliwa kuongoza kamati hii ambayo itaratibu ufuatiliaji wa suala hili.

Itaendelea toleo lijalo
 
Back
Top Bottom