Dr ULIMBOKA,Nembo ya Sekta ya Afya Nchini.

ludoking

Senior Member
Oct 5, 2008
124
71
Nikumbushe kidogo, Makaburu wa Africa Kusini walipoinyofoa roho ya kijana mzalendo wa nchi hiyo STEVEN B. Biko mwaka 1977 walidhani wamepunguza kwa kiasi kikubwa utawala wao dhalimu. Walikosea kwani walikuwa wameuchochea moto. Baada ya kuinyofoa roho ya Biko Makaburu wakawa wamezalisha roho za akina Biko wasiohesbika, Biko mwenyewe akabaki kutumika kama roho ya UKOMBOZI. Kwa hiyo waliodhani wamemuua Biko wakawa wamemtengenezea maisha yasiyokatika. Biko anaishi mpaka leona anaendelea kuenziwa wakati walioshoriki kifo chake wao wakiwa wamesha kufa na majina yao kuzikwa na mjina yao na hatuwakumbuki tena
Kwa hiyo hata waliohusika na unyama dhidi ya Dr Ulimboka anapaswa kuelewa kwamba walichokifanya hata kama hakikufanikiwa kama walivyokusudia kisingekuwa na matazamo waliyoyatarajia (kuwanyamazisha madaktari). Katika mazingira haya ni vigumu kumpoteza Dr Ulimboka na kutoweka na kusahaulika. Kinyume chake jina la Ulimboka litachapwa kwa muhuriwa moto kwenye roho za watanzania 'wanaopenda kuona mabadiliko kwenye sekta ya Afya nchini mwao'.

Source: Tanzania Daima, Jumapili 08 July 2012 (pg 12-13)
 
Thafi thana makala imetulia hiyo makabulu wa bongo ni chama cha mabwepande ccm
 
Back
Top Bottom