Dr. Ulimboka: Hali ya afya (Updates)

Mwenyenzi MUNGU mwenye mamlaka Mbinguni na Duniani,fanya mwujiza na huyu Ndg yetu anyanyuke na kushuhudia kwa kinywa chake alichotendewa na hw majambazi wa serikali tawala dhaifu.

Nina Imani MUNGU mwenye uweza wa yote atatenda mwujiza.
Liverpool,
Unaomba miujiza ifanyike? Mbona imeshafanyika tayari... Wewe huoni kuwa mijitu iliagizwa kutoa roho ya Dr Ulimboka, inakula na kushiba na ina uzoefu na mafunzo ya kuuwa bila kuacha ushahidi. Hujuwi kuwa aliyewatuma ana nguvu zote kifedha, ki-cheo, na madaraka ... hivyo halikuwa jambo la kubahatisha? Dr Ulimboka amelindwa na Mungu tu na muujiza umeshafanyika.

Maana ya muujiza huu ni kuwa, Mungu amekwishachoka na udhalimu wa CCM na viongozi wake. Kikombe cha uovu wa CCM kimejaa. Ukuta umekwisha andikwa hukumu ya CCM, ndiyo maana unayaona yanayoendelea KUTOKEA KILA SIKU.

Halitabaki jiwe juu ya jiwe.. subiri kidogo tu CCM yangu haiponi kamwe
 
get well soon doctor! na huyu Mgaya atuondolee upuuzi hapa hatijasahau alivotu betray ss wafanyakazi!
 
Hivi vifaa ukienda mtu wa kawaida wanakuambia avifanyi kazi ............ Inakuwaje kwa doctor ulimnboka vinafanya kazi au ni india
 

Attachments

  • DR ULIMBOKA.JPG
    DR ULIMBOKA.JPG
    88.8 KB · Views: 1,259
Ndiyo maana hawa madaktari siwatofautishi na hiyo serikali wanayogombana nayo. Wote ni "Mafia" tu!
 
Masaburi wewe ulisha wahikuingia icu za moi au unalopoka tu hujui kitu sasa vitaje majina vifaa hivyo kama unavijua wewe kilaza kazi yenu kuhalisha tu humu.
 
Hivi vifaa ukienda mtu wa kawaida wanakuambia avifanyi kazi ............ Inakuwaje kwa doctor ulimnboka vinafanya kazi au ni india

Na kama ulishalazwa humo au ndugu yako kama vifaa havikufanya kazi ungalikuwa mzima kweli wewe au huyo nduguyo? Na ulivyoambiwa havifanyi kazi ulichukua hatua gani?
 
Nchi hii watu waliosomea propaganda vilaza kweli kweli...wanaongea ongea tu kama wako vijiweni. Utaemaje muhimbili ni India!
 
Madaktari siku zote wapo kwenye mgomo. Wana ma agent wao ambao ni manesi kwa ajili ya kuwapokelea vijihela vya rushwa ndogo ndogo, unakuta mwananchi katoka kimanzichana kaja hapo Muhimbili ukiangalia mtu hajiwezi kutoa hata sh 500 lakini dokta ana demand 20,000 au mtu wa X-Ray anasema mashine mbovu wakati akija mwengine na chambi anapitishwa mlango huo huo anapigwa X-Ray anaondoka fasta.

Kuweni na moyo wa ubinadamu hamna aliyewalazimisha kuwa madaktari mliamua wenyewe.
 
Hivi vifaa ukienda mtu wa kawaida wanakuambia avifanyi kazi ............ Inakuwaje kwa doctor ulimnboka vinafanya kazi au ni india
Umeshawahi kulazwa ICU? Kwa taarifa hakuna kifaa kigeni hapo. hiyo ndo ICU, usilete hoja za kujenga fitna!
 
Hivi vifaa ukienda mtu wa kawaida wanakuambia avifanyi kazi ............ Inakuwaje kwa doctor ulimnboka vinafanya kazi au ni india

Wewe kwenye hiyo picha umeona vifaa gani? si useme kitanda kimoja kinachotembea? au umeona hizo gadgets za umeme na mashuka kuu kuu? Tutajia hivyo vifaa tafadhali ili thread yako iwe na maana.
 
Hivi vifaa ukienda mtu wa kawaida wanakuambia avifanyi kazi ............ Inakuwaje kwa doctor ulimnboka vinafanya kazi au ni india


Ndugu usikurupuke!hiyo ndio ICU ya MOI, ndivyo ilivo kama unaovyoona katika picha, pili elewa MOI ni private sio shamba la bibi kama MNH. MOI na MUHIMBILI ni mashirika 2 tofauti, garama za matibabu MOI ni tofauti na MNH.

Tangu MOI ifunguliwe hivyo vifaa vipo na watu wanaolazwa pale wanalipa ghali hata ukiangalia word zao ni tofauti na za MNH zina grade kuna za mtu 1 ambazo ni VIP A, kuna za watu 2 ambazo ni VIP-B, kuna za watu 3 na 4 na moja kamasijakosea inalaza watu 6 ambazo ni wanaziita standard word na bei zao ni tofauti. Vile vile elewa MOI ni kitengo kinachojitegemea hakiusiani na MNH ingawa kuna baadhi ya madaktari wachache wanatibu kotekote, hata wasemaji wa hizo hospital ni watu wawili tofauti.
Pia kuna some case ambazo MOI huwa wanazishughulikia kusaidia MNH.

Na kama waijua MNH vizuri pale jengo la sewahaji kuna floor MOI wanaihudumia kama MOI kwa ajili ya wagonjwa wa MNH, hata majerui wanaopata ajali wakisha shughulikiwa na MOI wanapelekwa pale sewahaji.
 
All human being are equal but some are more EQUAL. Hiyo ndiyo bongo yetu nzuri.
 
  • Thanks
Reactions: R.B
Back
Top Bottom