Dr Ulimboka atoa tamko, amtaja Ramadhani Ighondu

Status
Not open for further replies.

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,734
405
Kwa mujibu wa ripoti iliyoandaliwa na Dr. Ulimboka na kusomwa na wakili wake,ametamka bayana kuwa mtu aliyekuwa akiwasiliana nae muda mfupi kabla ya kutekwa ni Bw. Ramadhani Igondu yule yule aliyetajwa kwenye gazeti la Mwanahalisi
Ikulu matatani

• Msemaji wa Rais adai kauli ya Dk. Ulimboka ni ya kipuuzi

na Waandishi wetu

SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk. Stephen Ulimboka, kusisitiza kwamba alitekwa na mtu anayefanya kazi Ikulu, Ramadhan Ighondu, Ikulu imehamanika na kujitetea kwamba madai hayo ni ya kipuuzi.

Juzi, Dk. Ulimboka alitoa tamko akisema kwamba Ighondu ndiye aliyehusika na sakata la kuteka na kumtesa vibaya, ambalo wengine wamekuwa wakiliita jaribio la kumuua; lakini jana katika hali inayoonyesha kwamba Ikulu haiko tayari kumchukulia hatua mtumishi wake anayetuhumiwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu, alisisitiza: "Ikulu iliishajibu. Tulisema haihusiki, na Rais Jakaya Kikwete amepata kuzungumza juu ya jambo hili mara nyingi."

Wakati Ikulu ikimtetea mtuhumiwa huyo na kujaribu kujivua lawama, Jeshi la Polisi, ambalo lilimtia mbaroni raia wa Kenya na kumpeleka mahakamani kujibu tuhuma za kumteka na kumtesa daktari huyo, nalo limesita kubainisha kama litamkamata na kumhoji Ighondu, ambaye ametajwa rasmi na shahidi wa kwanza halisi katika suala hili, Dk. Ulimboka.

Badala yake maofisa wa jeshi hilo wametupiana mpira kila mmoja akidai hahusiki na suala hilo.

Katika tamko lake la kiapo lililotolewa kwa waandishi wa habari juzi, Dk. Ulimboka, kupitia kwa wakili wa kujitegemea, Nyaronyo Kicheere, alisema anamfahamu mtesaji wake, na kwamba hata akikamatwa leo hii, atakwenda kufanya utambuzi.

Alisema anashangaa kwamba polisi wameshindwa kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo, licha ya kwamba alishatajwa na gazeti la MwanaHALISI na katika mtandao wa YouTube.

Alisema: "Nathibitisha kwamba Ramadhan Ighondu alitambulishwa kwetu kwa jina la Abeid. Binafsi ninamfahamu sana bwana huyu kwa sababu alikuwa akitumwa mara kwa mara kuja kukutana na mimi na tumekutana mara kadhaa kabla ya tukio lile.

"Nathibitisha kwamba mfanyakazi huyu wa Ikulu, ndiye aliyenipigia simu na kuniita kwenye kikao ambacho muda mfupi baadaye nilitekwa. Katika mawasiliano hayo, Abeid alikuwa anatumia simu namba 0713 760473."

Dk. Ulimboka aliongeza kuwa anakumbuka kuwa Abeid alitambulishwa kwake na kigogo mmoja, akiwa na wawakilishi wengine wa madaktari, kuwa ndiye angehusika katika kuchukua madai na hoja za madaktari katika mgogoro kati ya madaktari na serikali.

Lakini Rweyemamu hakutaka kufafanua zaidi badala yake alisema, "Naomba uninukuu; haya madai ni upuuzi…hiki kitu kilishajibiwa."
Alipoulizwa kama anamfahamu Ramadhan Ighondu, Rweyemamu alikwepa swali, huku akisisitiza kuwa Ikulu haihusiki naye.

Baada ya kuona swali hilo analikwepa, mwandishi alimuuliza Rweyemamu ni hatua gani ambazo Ikulu itamchukulia Ighondu kama mfanyakazi wao.

Swali hilo lilionekana kumkera Rweyemamu, akajibu kwa ukali, "Kama Ikulu haihusiki, hatuna cha kufanya juu ya jambo hilo; mnakaa mnalea maneno ya kipuuzi…Ikulu imwajibishe kuhusu nini? Haihusiki!"

Alipobanwa zaidi alisema kama kuna watu wanasema hivyo waende wakaripoti polisi.

Kauli ya jana ya Rweyemamu ni ya pili kutolewa na Ikulu kuhusu Dk. Ulimboka. Mara ya kwanza, ilipotolewa na Rais Jakaya Kikwete alipokutana na baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, akasema, "Dk. Ulimboka ana nini mpaka Ikulu imteke? Tumteke ili iweje?"

Kikwete alikwenda mbali zaidi na kusema hata Dk. Ulimboka mwenyewe alipokwenda Ikulu akiwa na viongozi wenzake alinyamaza kimya tu na kwamba waliokuwa wakizungumza ni wengine.

Hata hivyo, kwa kuwa Ikulu imesema haihusiki, na Dk. Ulimboka mwenyewe ametamka kwamba anamjua aliyemtesa, na kwamba anafanya kazi Ikulu, ni juu ya umma kuamua nani anasema ukweli.

Kwa upande wa polisi, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alijitetea akisema suala hilo liko kwa mkubwa wake wa kazi, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Maanumba, na kwamba atafutwe kwa ajili ya kulitolea ufafanuzi.

"Gazeti lenu juzi nililisifia sana nikalitolea mfano mzuri; watu hawawezi kutuchezea tu na kutishia mamlaka iliyopo kama hakuna sheria. Lazima kila mmoja afuate sheria. Hilo suala liko kwa DCI na sisi polisi tuna nidhamu ya kazi. Suala likiwa kwa mkubwa wako huwezi kulizungumzia. Tambua faili lipo kwao na mimi sina uwezo wa kulizungumzia," alisema.

Alipobanwa zaidi kuwa Dk. Ulimboka ameshamtaja aliyemtesa na kwamba yuko tayari kuwapa ushirikiano na kutoa ushahidi mbele ya tume huru, Kova alisema, "Hivi wewe unanitafuta nini? Nimekwambia sina uwezo nalo; au hutaki ushirikiano na mimi? Hilo swali lako ni sawa na kumuuliza kipofu pale unapaonaje!?"

Naye DCI Manumba alipopigiwa simu, alijibu kwa kifupi akisema aulizwe msemaji wa jeshi hilo. Akakata simu.

Msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso, alipoulizwa alisema suala hilo liko kwenye uchunguzi, hivyo hawezi kulitolea ufafanuzi.

Kama walivyofanya wenzake, Senso naye alipobanwa zaidi, alisisitiza, "Tafadhali, sina maelezo zaidi ya hayo. Kukiwa na kitu kipya tutaandaa."

Mwanaharakati alonga
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Deus Kibamba, alizungumzia sakata hilo akisema kuwa serikali haipaswi kuishi kwenye kukanusha kutohusika kwake bali ina wajibu wa kuchunguza na kutafuta ukweli wa jambo hilo.

"Serikali ama imehusika au haikuhusika kumteka Dk. Ulimboka, haitoshi kukanusha tu, maana ni sawa na baba nyumbani anaelezwa mboga imeibiwa anasema hahusiki bila kutafuta muafa wa nani kaiba," alisema.

Alisema kuwa Dk. Ulimboka amewataja watu kwa majina na namba zao za simu, hivyo ni vyema wakajitokeza kujitetea wenyewe na kama hawafanyi hivyo serikali iwakamate na kuwahoji kwa nguvu.

Kibamba alisema kuhojiwa na kufikishwa mahakamani si tatizo bali kinachokuwa kinatafutwa ni ukweli, lakini akatilia shaka kuwa siku hizi mahakama zinabagua aina ya watu kwani wapo wanaokamatwa na kufikishwa siku hiyo na wengine hawafikishwi huko kabisa.

"Naunga mkono tamko la Dk. Ulimboka na hivyo iundwe tume huru ya kuchunguza tukio la kutekwa kwake na hata kuuawa kwa Kamanda Liberatus Barlow, maana usalama wa nchi sasa uko shakani," alisema.
 
Baada ya kimya kirefu leo dr ulimboka ametoa taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na wanasheria wake shayo pamoja na nyaroro kicheere.ameshangazwa na serikali kutomkamata mtu huyo na amesema yupo tayari kutoa ushirikiano kwa tume huru japo mpaka sasa haijaundwa.

Source clouds news ya 18:00pm
my take: kumbe MWANAHALISI walikua very right
 
Kwa mujibu wa ripoti iliyoandaliwa na Dr. Ulimboka na kusomwa na wakili wake,ametamka bayana kuwa mtu aliyekuwa akiwasiliana nae muda mfupi kabla ya kutekwa ni Bw. Ramadhani Igondu yule yule aliyetajwa kwenye gazeti la Mwanahalisi

Hana jipya huyo Dr. Ameishafungwa mdomo!
It is just a boredom story at present!
 
itakuwa wamemrusha hela za ahadi,na leo nimeona watoto wanaandamana kudai chao serikal haina ela baba mwanaasha kasafri na ufunguo wa store ya mahela
 
ni kweli hata mimi nimemskia iyo radio clouds, tatizo ameenda kwenye wrong media, angeitisha vyombo vya habari then awape release, ni bahati mbaya kuwa pia amechelewa, na huenda isije ikawa strategy kuwa baada ya kuchommwa makanisa hata akiongea hamna tatizo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom