Dr. Steven Ulimboka anarudi leo saa sita mchana

Mungu amempa 2nd chance ya kuishi, ye anaichezea. Kina Rama hawatamuacha!!

Angebaki tu hukohuko!!!
 
home is home hata kama haki hakuna,karibu na ueleze ukweli juu ya unyama wa serikali ya tanzania isiyojali haki za binadamu

Nabii hakubaliki nyumbani, wakati mnaiponda Serikali kwa majungu tu na sababu za kisiasa, Nchi zingine zinakuja Tanzania kujifunza mfumo mzuri wa uongozi. Hata MALAWI wanaotuchokoza wiki mbili zilizopita walikuwa bungeni kujifunza. Hivi mnafikiri kutekwa kwa Ulimboka ni mtaji tosha kwa wanaharakati, wanasiasa na maadui wengine kujijengea umaarufu? La hasha, watanzania wataujua tu ukweli wa mambo na kutambua kuwa maendeleo ya nchi yao yanacheleweshwa na wanasiasa na wanaharakati ambao,badala ya kuchangisha fedha kwa ajili ya majimbo yao wanafanya hivyo ili kushibisha matumbo yao na kufanya mikutano yenye kuhamasisha wananchi kugomea shughuli za maendeleo na huduma za jamii kama ambavyo Ulimboka alivyoingizwa mkenge.
 
Ni vyema tumshukuru mungu wale wote tunaojali haki na utu wa binadamu,kutekwa na kudhuriwa dr.ulimboka na sasa anarudi tz baada ya matibabu ughaibuni wakati bado uchunguzi wa wahusika na utekaji huo haujajulikana kama umefanyika na pia serikali ikilifutia gazeli pendwa la mwanahalisi hasa juu ya utafiti wake wa kina na kuweka bayana mhusika nambari wani wa sakata la utekaji huo,je nini hatima ya ujio wake akiwa mzima wa afya?
 
Nadhani ni nafasi nzuri kwa yeye sasa kujifunza kuwa uhai wa mtu ni kitu cha thamani kuliko vyote duniani na kujutia kitendo chake cha kuhamasisha madaktari kugoma na kusababisha watu kupoteza uhai ambao kama yeye pia angeupoteza angeacha pengo kubwa sana kwa familia yake kama ambavyo waliofariki kutokna na mgomo huo walivyoacha pengo katika familia zao
 
hivi kwani anamhitaji huyo ulimboka . si abaki huko huko . au huko alipo hakuna hospital . si aombe kazi afanye huko.
 
Rama ndo nani kwani?
Atakuwa anamjua KUBENEA pekee si unajua tena habari za kughushi, zinavyokuwa na utaa. Unajua hayo ndiyo baadhi ya madhara ya kukuwa kwa technojia ya habari na mawasiliano. Mtu anaweza kkuwa na visasi na jirani yake akamzushia jambo na akenda katika taasisi ambazo anweza kupata taarifa za adui yake kama vile tume ya uchaguzi, benki, kampuni za simu, hospitali, RITA na kuchapisha uzushi dhidi yake, Jambao ambalo nadhani KUBENEA amefanikiwa kwa huyo adui yake anayemuuita kwa jina RAMA. Nasema ni za kughushi kwa sababu nakumbuka Kubenea alipohujiwa alivyozipata habari za Rama alisema alizipata tume ya uchaguzi, sasa nikashangaa zaidi pale alipoandikwa kwenye gazeti kuwa Simu ya Rama iliwahi kuishiwa salio na kubaki na shilingi moja, hapa nikajiuliza tume ya uchaguzi inawezaje kujua salio la mteja wa kampuni ya simu.
 
Aiseee baba yangu ngoja niende njia panda nikatafute fuso la kuja dar kumpokea mbunge mtarajiwa dr ulimboka
 
hivi kwani anamhitaji huyo ulimboka . si abaki huko huko . au huko alipo hakuna hospital . si aombe kazi afanye huko.
Unajua nchi kama ya Rwanda ULIMBOKA alikuwa wa kupigwa risasi hadharani na kufa. Kagame hana sababu ya kuona mtu anasababisha vifo vya mamia ya watu kuliko kuiondoa hiyo nafsi moja. Hakuna nchi inayoweza kumpa ULIMBOKA uraia wala kazi wakati ikijua kaibisa ni mtu asiyejali uhai wa watu.
 
Nabii hakubaliki nyumbani, wakati mnaiponda Serikali kwa majungu tu na sababu za kisiasa, Nchi zingine zinakuja Tanzania kujifunza mfumo mzuri wa uongozi. Hata MALAWI wanaotuchokoza wiki mbili zilizopita walikuwa bungeni kujifunza. Hivi mnafikiri kutekwa kwa Ulimboka ni mtaji tosha kwa wanaharakati, wanasiasa na maadui wengine kujijengea umaarufu? La hasha, watanzania wataujua tu ukweli wa mambo na kutambua kuwa maendeleo ya nchi yao yanacheleweshwa na wanasiasa na wanaharakati ambao,badala ya kuchangisha fedha kwa ajili ya majimbo yao wanafanya hivyo ili kushibisha matumbo yao na kufanya mikutano yenye kuhamasisha wananchi kugomea shughuli za maendeleo na huduma za jamii kama ambavyo Ulimboka alivyoingizwa mkenge.

nini maana ya kuhimiza wananchi kugomea shughuli za maendeleo?je ni kuwaambia ukweli?shughuli gan ya maendeleo serikali yetu imefanya tangu uhuru kama sio kusimamia miradi ya iMf na wB na wanaoitwa wakubwa?tz hakuna kitu kinaitwa uongoz bora ila kuna 'utawala bora' chini ya tume yake, so Malawi walikuja kujifunza utawala bora. Kazi ya upinzani katika dunia ya demokrasia ni kukosoa serikali na watendaji wake!kazi hiyo hufanyika kwenye majukwaa ya siasa,mikutano ya bunge, makongamano, vyombo vya habari,nk. Si kazi ya upinzani kusifia na vilevile si busara kwa serikali kupita kwenye 'media' na kuanza kulalamika kuwa wapinzani ni wachochezi na wavunjifu wa amani. Hilo ni swala la kisheria na vyombo vipo,tuache kuwajaza wananchi maneno ambayo hakuna anaeyaamini. Bora kunyamaza kimya kuliko kuwa wasema hovyo.
 
Welcome back, tumesikia mengi, tunataka kusikia tena kutoka kwako bila shaka ni wakati mgumu sana kwa wale waliojaribu kufanya walichofanya bila mafaniko. Tunasubiri ukweli zaid ili tuwe huru.
 
Aiseee baba yangu ngoja niende njia panda nikatafute fuso la kuja dar kumpokea mbunge mtarajiwa dr ulimboka

Mafia wote lazima wawe wabunge wa jimbo la kaskazini, hatuwataki huku kwetu. kwani lazima fikie huku Dar kwa nini asifikie huko KILIMANJARO kabisa ili apewe jimbo la MAFIA mwenzake Lema.
 
nini maana ya kuhimiza wananchi kugomea shughuli za maendeleo?je ni kuwaambia ukweli?shughuli gan ya maendeleo serikali yetu imefanya tangu uhuru kama sio kusimamia miradi ya iMf na wB na wanaoitwa wakubwa?tz hakuna kitu kinaitwa uongoz bora ila kuna 'utawala bora' chini ya tume yake, so Malawi walikuja kujifunza utawala bora. Kazi ya upinzani katika dunia ya demokrasia ni kukosoa serikali na watendaji wake!kazi hiyo hufanyika kwenye majukwaa ya siasa,mikutano ya bunge, makongamano, vyombo vya habari,nk. Si kazi ya upinzani kusifia na vilevile si busara kwa serikali kupita kwenye 'media' na kuanza kulalamika kuwa wapinzani ni wachochezi na wavunjifu wa amani. Hilo ni swala la kisheria na vyombo vipo,tuache kuwajaza wananchi maneno ambayo hakuna anaeyaamini. Bora kunyamaza kimya kuliko kuwa wasema hovyo.

Upinzania maana yake siyo kukataza wananchi kjihusisha na shughuli za maendeleo. Upinzania unatakiwa uwaeleze wananchi nini sera yao na si kuponda sera ya chama tawala ili wananchi wenyewe wapime ipi ni sera safi. Kamwe watanzania hawawezi kupata maendeleo zaidi ya yale ya sasa kwa kuwaandaa mabwanyeye wa baadaye kwa kuwachangisha fedha katika mahoteli makubwa, Upinzani siyo kuhamasisha Watumishi wa Serikali kuigomea serikali iiliyoko madarakani hata siku moja, hetu tupe mifano ya upinzani wowote katika bara la afrika na nje ya afrika. Sera ya kujitenga kwa baadhi ya mikoa(NAASARI'S SPEECH)na ile ya umajimbo kamwe ina lengo la kutugawa watanzania. Sera ya kuwabagua viongozi ndani ya chama kutokana na maeneo wanayotoka kama ambavyo anafanyiwa ZITTO kabwe unafikiri ina lengo zuri kwa watanzania? Umenichekesha sana uliposema kuwa serikali haipaswi kulalamikia wapizani. Serikali inao wajibu wa kusimamia mipaka ya demokrasia ili kulinda usalama, amani na mshikamano wa watu wake.
 
Kwa watakaokuwa na nafasi wafike Airport Saa Saba Mchana 12/8/2012 (Mwalimu Nyerere Internationa Airport)
 
Atakuwa anamjua KUBENEA pekee si unajua tena habari za kughushi, zinavyokuwa na utaa. Unajua hayo ndiyo baadhi ya madhara ya kukuwa kwa technojia ya habari na mawasiliano. Mtu anaweza kkuwa na visasi na jirani yake akamzushia jambo na akenda katika taasisi ambazo anweza kupata taarifa za adui yake kama vile tume ya uchaguzi, benki, kampuni za simu, hospitali, RITA na kuchapisha uzushi dhidi yake, Jambao ambalo nadhani KUBENEA amefanikiwa kwa huyo adui yake anayemuuita kwa jina RAMA. Nasema ni za kughushi kwa sababu nakumbuka Kubenea alipohujiwa alivyozipata habari za Rama alisema alizipata tume ya uchaguzi, sasa nikashangaa zaidi pale alipoandikwa kwenye gazeti kuwa Simu ya Rama iliwahi kuishiwa salio na kubaki na shilingi moja, hapa nikajiuliza tume ya uchaguzi inawezaje kujua salio la mteja wa kampuni ya simu.

Kama ndo hivyo uyu Kubbenea atakuwa na uadui na kila mtu(kuanzia rais,wawaziri,wabunge,wakurugenzi wa baadhi ya makampuni,usalama,nk). Wakulima ( watz) wanaamini maneno ya KUBE kwasababu 1. Hajachukuliwa hatua zozote za kisheria. 2. Kufungiwa kwa gazeti lake kwa kile kinachoonekana na wasomi,wachambuzi,na wanasheria sababu hafifu. 3. Kufukuzwa kwa wafanyakaz tigo kukiashiria upendeleo (bias) kwani wamewajibishwa hao uku watajwa kwenye sakata hilo wakila bata. Hii inaonesha serikali (watendaji wake) wasivyojiweza kwenye kutengeneza matukio. Hii ni kwa sababu ya kazi za kujuana na kulewa sifa za madaraka na kudhan kuw mtu ukiwa usala.m.a wa taifa unakuwa mungu mtu. Nchi za ng'ambo hupanga matukio kwa miaka na kutumia watu wenye akili nyingi na sio watu wenye nguvu nyingi.
 
Unafikiri kila mtu ni wa udaku tu! chanzo changu ni yeye mwenyewe!

Ulimboka siyo siri hata yeye mwenyewe anakuja akiwa katika mazingira magumu sana. Atazungukwa na waathirika wa mgomo ambao yeye ndiye mwanzilishi. Atakuwa kati kati ya watu ambao ni maadui zake wa zamani na wangependa kutumia upotoshwaji wa aina yoyote kuhusu kutekwa kwake ili kumdhuru kwa namna yoyote ile. Atakuwa anajifariji kuwa watanzania wengi wanamuona kama shujaa, lakini kwa namna moja au nyingine nafsi yake itakuwa inamsuta kwa kitendo chake cha kusababisha wagonjwa wafe, madaktari wengine wapoteze kazi na kuzusha uongo kwa vyombo vya dola kuwa vilihusika kumdhuru huku akiwataja wengine kwa majina kule hospitalini Muhimbili na baadaye akiwa Afrika ya kusini. Hakika ujasiri wake utakuwa ni kujihami 2 lakini si kwa sababu eti aliweza kutaabika kwa sababu ya kuwatetea wanyonge, la hasha.
 
mtahaha sana mwaka huu.ulimboka is back na hataikimbia nchi yake.
 
Back
Top Bottom