Mikael Aweda
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 2,973
- 3,901
Nimeanza kazi ya kuajiriwa miaka 7 iliyopita. Jana jioni nikakwama kwenye foleni masaa mengi sana nikafika nyumbani saa 3 usiku. nikaanza kuwaza mgawanyo wa masaa yangu baada ya kukaa kwenye foleni. Nikaanza kutafakari kama ifuatavyo:
MUDA NILIOKA NJIANI.
Kwa siku napoteza masaa 4; Asubuhi 2 na jioni 2. Hii inatokana na foleni. Kama siyo foleni nisingetumia muda huo. Siku 6 za wiki natumia masaa hayo kwenda kazin na kurudi, kwa kuwa nafanya hadi jumamosi. Ni jumapili tu ndo siendi kazini.
Kwa hiyo, Ktk siku 30 nafanya kazi siku 26 za mwezi ( toa jumapili tu). Hivyo, masaa 4 kwa siku * 26 siku za mwezi ni sawa masaa 104 kwa mwezi zinapotea njiani.
Kwa mtazamo huo huo, Masaa 104 kwa mwezi ni sawa na masaa 1248 kwa mwaka.
Kwa mantiki hiyo, kwa miaka 7 niliyoajiriwa,muda niliokaa kwenye foleni ni swa na masaa 1248 (ya mwaka * miaka 7 = masaa 8736 kwa miaka 7.
Baada ya hapo nikataka kujua masaa haya 8736 ni miaka mingapi. Nikagundua kuwa masaa 8736 nikagawa kwa 24 (masaa kwa siku) ninapata siku 364. Mwaka una siku 365/366.
Hiyo ni kusema Dr Slaa nimekaa njiani (ndani ya daladala + gari binafsi) kwenda kazini au kurudi nyumbani muda wa mwaka moja kasoro siku moja ( 364). Je, una mawazo mapya ya kunisaidia?
MUDA NILITUMIA OFISI
Kwa siku nafanya kazi masaa 8 (Mara mbili ya muda niliokaa njiani) Kwa hiyo kwa mwezi natumia masaa 208 Ofisini (8 ya siku * siku 26 za mwezi toa jumapili). Kwa mwaka natumia masaa 2496 ofisini. Kwa miaka 7 nimetumia masaa 17,472 ofisini. Nikigawa kwa saa 24 ( idadi ya maasa kwa siku) ninapata siku 728 ambazo ni wastani wa miaka 2.
Kwa hiyo ndani miaka 7. Nimefanya kazi miaka 2 nimekaa njiani (dala dala au gari binafsi) mwaka 1 . Masaa yaliyobaki ni ya kulala, kupumpizika kazi nyinginezo ikiwepo kujenga Chadema nk.
Je, mgawanyo huu unaweza kunitoa ktk umaskini na kuniletea Maendeleo nikawa na malori na vituo vya mafuta Rizi1?. Mimi naona hapana ndio maana nihitaji ushauri wako.
Hoja yangu ni kuwa siwezi kukaa barabarani masaa manne (Mwaka1 ktk miaka 7) kila siku halafu nikategemea maendelea. Ninahitaji mawazo mapya ya kunitoa hapa. Dr Slaa unanishaurije?
Gharama.
Rafiki yangu anakaa Kibamba na anafanya kazi mjini. Anatumia Tsh 7,000 Kila siku kama gharama ya ziada ya foleni. Bila foleni angetumia 10,000 kwa gari yake ndogo. Lakini kutokana na foleni kwa siku anatumia 17,000/=
Ziada ya 7,000/= anayoingia rafiki yangu ni hasara ya Tsh ngapi ktk miaka 11 aliyofanya kazi? Je, WanaDar es Salaam wote wanapata hasara ya muda + pesa ya kiasi gani kwa siku, mwezi na mwaka?
Je,Dr Slaa ungenisaidiaje kama ungekuwa umeingia ikulu 2010? Na kama umechakachuliwa kura unanipa ushauri gani? Maana hata muda wa Kufanya kazi za Chadema niko bara barani.
Mawazo yangu tu yaliyonikuta kwenye foleni ya Jana.