Dr SLAA: Wana TABORA mtuunge mkono

asimamishwe pro SAFARI nahakika ilo jimbo litakuja upinzani

kwani Safari ni mtu wa huko?.......ingependeza zaidi kama mgombea akawa ni mwana Igunga, itasaidia sana kusukuma mashambulizi ya kampeni
 
Mbona muiran aliweza kuwa mbunge kwa miaka kibao? Sema waweke mislamu kwa vile TBR inawaislamu kibao!

Siku hizi watu hawaangalii mgombea anatoka chama gani ama dini gani...watanzania siku hizi wanamchangua mtu anayekubalika, basi mradi awe na uwezo wa kugusa hisia za watu.
 
Katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA amekaririwa akisema "watanzania mtuunge mkono tunataka Igunga Iwe Ngome ya CHADEMA". Dr slaa ameyasema hayo makao mapema leo asubuhi katika makao makuu ya CHADEMA eneo la Kinondoni Ufipa jijini Dar es salaam.

Wito huo wa mwanasiasa huyo anayeonekana kuitikisa ilivyo ngome ya CCM inafuatia hatua ya mbunge wa Igunga, mfanyabiashara na rafiki mkubwa wa rais Jakaya Kikwete Bw Rostam Aziz kujiuzulu huku akiwaacha wana CCM wenzake midomo wazi kwa hotuba yake iliyokuwa imejaa hasira, visasi na ubabe, huku akibainisha wazi kuwa hakubaliani na misimamo ya Nape na Chiligati.
 
Dr__Slaa.jpg

Katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA amekaririwa akisema "watanzania mtuunge mkono tunataka Igunga Iwe Ngome ya CHADEMA". Dr slaa ameyasema hayo makao mapema leo asubuhi katika makao makuu ya CHADEMA eneo la Kinondoni Ufipa jijini Dar es salaam.Wito huo wa mwanasiasa huyo anayeonekana kuitikisa ilivyo ngome ya CCM inafuatia hatua ya mbunge wa Igunga, mfanyabiashara na rafiki mkubwa wa rais Jakaya Kikwete Bw Rostam Aziz kujiuzulu huku akiwaacha wana CCM wenzake midomo wazi kwa hotuba yake iliyokuwa imejaa hasira, visasi na ubabe, huku akibainisha wazi kuwa hakubaliani na misimamo ya Nape na Chiligati.
 
Wala asijulikane kwa sasa kama niwa Cdm mana hawa Magamba hawatabiriki hata chembe moja wasijemuhujumu huyo mtu,maana hawa ni wazee wa fitna

Mtu kama huyo hata CDM haimtaki, kama akijulikana leo atakula za magamba hata akijulikana kesho atakula za magamba. Ndio maana CDM inatakiwa kujenga viongozi wasio ndumilakuwili na wenye tamaa ya fedha na madaraka. Tunahitaji viongozi wanoweka maslahi ya nchi mbele na kizazi cha sasa na kijacho.
 
magamba yatachelewesha huo uchaguzi yakisoma upepo na kama yakijiridhisha jimbo watalikosa,yataitisha uchaguzi mwezi september 2015

Sheria zipo wazi, labda watumie mchezo wa kutopeleka barua tume ya uchaguzi na bungeni. Ila nahisi bungeni kuna sheria kama mbunge hahudhurii vikao kadhaa bila sababu anakuwa amejiuzulu? Wakikalia ndio CDM wanakwenda na twanga kote kote ukizingatia jimbo halina mwenyewe.
 
Nimesoma Maoni wengi wameandika vizuri tu, mimi maoni yangu ni haya;

Chadema wanayo nafasi ya kushinda ikiwa watamchagua mtu miongoni mwa wanaigunga na awe ni mtu anayekubalika na kufahamika.
Swala la Dini halina msingi sana hapo igunga na hata watanzania walio wengi kote nchini hawalipi nafasi.
Swala la Wapinzania kuungana halina maana na halifai kusikilizwa kabisa, utamwachia CUF then akiingia bungeni anafundwa kuwa mpinzani wa Chadema badala ya CCM.

Kuhusu watu waliomlilia RA ni kwamba kwanza njaa mbaya na pili ndugu zangu wa Tabora yaani wanyamwezi wengi wao wavivu wa kujishugulisha na huwa wanaridhika kwa kitu kidogo sana, na hiyo siri RA aliifahamu na ndio maana akawa anawadaganya kwa vitu vidogo sana kama kuwapa vijisenti, kofia, fulana , khanga n.k
ila Watu hawa wakieleweshwa vizuri wakaelewa huwa wanabadilika na kufanya maamuzi magumu na huwa hawarudi nyuma tena.

Chadema wanapaswa kuwapeleka watu makini Igunga watakao ongea kwa lugha rahisi itakayowaingia wanaIgunga na hatimaye kuamua kufanya mabadiliko ya kweli, Waelezwe jinsi mkoa wao ulivyo na dhuluma amabayo ccm imeufanyia, kwa mfano waelezwe kwamba TBR ni kitovu cha elimu lakini hausaminiwi, ni kati kati ya nchi lakini ulitengwa kwa kutokuwa na miundombinu ya kunganisha na mikoa mingine, waelezwe jinsi walivyokuwa wakikopwa Tumbaku yao ilihali watoto wao wakifukuzwa shule kwa kukosa ada, waelezwe jinsi amabvyo Afya, maji , umeme vinayowasumbua katika maisha yao.

Naamini wakielezwa kwa Lugha sahihi wataigeuka ccm ambayo naamini walishaigeuka tangu mwanzo ila walitishwa na wengine kuhongwa na hata kuibiwa kura.
 
tena wanamlilia mtu aliyetufilisi! Wametia aibu kwa kweli.
Waswahili walipima, wakadadisi, wakachunguza na kutafiti na baadaye wakaja na usemi ambao hapa tunaweza kuutohoa: "Fisadi akufaae si mpiganaji asiyekufaa" au "Fisadi mbaya kiatu chake dawa". Mwanangu ungefika Igunga na kuona hali zao halisi za kimaisha zilivyo, kuondokewa na mtu anayewapa maslahi (hata vikiwa ya wizi) ni msiba mkubwa. Huoni hata mkulu wa ikulu anamlilia. Acha walie! Wamekuwa kama kuku wa kisasa, hawajui wakiachiwa watajitafutia vipi ulaji. Mazoea mabaya. Wako mashakani! Kwa taarifa yako, wakati wa kampeni hata kwenye nyumba za ibada Wanyamwezi hawa walikuwa wanaambiwa na wahubiri wao kuwa atakayemnyima kura lazima ataenda jehanamu. Kwa uelewa finyu ulioko kule, athari ya mahubiri kama hayo, usipime!


Acha walie Igunga, fisadi kujiondoa
Za maisha walifunga, pingu naye kama ndoa,
Kwao alikuwa kinga, Ingunga siyo Kondoa,
Japo fisadi mbaya, kiatu chake ni dawa.
 
Back
Top Bottom