Elections 2010 Dr. Slaa usitunyang'anye tonge mdomoni

WANASIASA WANAOTAKA KURA ZETU ........WAMETUFANYIA NINI?......sio kukurupuka na kuzitaka kura zetu
 
Remmy na wewe umenunuliwa kwa vipande thalathini vya fedha? Lakini uzuri ni kuwa mkakati wenu umeshawekwa peupe, hivyo huo ni mkakati ambao umeshindwa kabla ya kuanza kufanya kazi. HATUDANGANYIKI.
 
Silaa tafadhali kutaka kwako kura kusikufanye ukatunyang"anya tonge wafanyakazi mdomoni. Tunazitaka sana hiyo nyongeza ya mshahara no matter imetangazwa wapi? we mbona umeahidi mengi? hizo ahadi si rushwa na si kinyume na maadili ya kampeni? kabla ya kuzinduliwa kwa kampeni ulizitaka kura zetu na ukaahidi kuongeza mshahara hiyo si rushwa? Nilikupenda sana niliapa kutopiga kura mwaka huu lakini ulipokuja wewe nikahamasika lakini kwa hili unaniboa na kinirudisha kulekule. Wafanyakazi hatudanganyiki na nyongeza ya mshahara hata akiongeza kama hatukumtaka tusimgempa na hata kama asipoongeza kama tulimtaka tungempa. NImegundua kuwa wagombea wote wapo kwaajili ya kura tu na wala si maslahi ya wananchi, kama kweli unamaslahi nasi ungeacha wafanyakazi mwezi huu wa nane japo tufikie hiyo 175,000/= tupambane na maisha. Khaa bee!!!!

Pesa zote zinapitishwa na bunge hasa nyongeza za mishahara na kutangazwa na waziri husika.Ukirejea
kipindi cha bunge la bajeti serikali ilitangaza kima cha chini cha sh 135,000/= na kusema serikali haiwezi
kuongeza pesa zaidi ya hiyo kutokana na ufinyu wa bajeti.Swali la kujiuliza hizo pesa zimetoka wapi za
nyongeza na ni nani kaidhinisha hizo pesa hapo ndo utakapoona ufinyu wa mawazo yako.Kinachoongelewa
na Dr.Slaa je zile taratibu za kuidhinisha hizo pesa zilifuatwa, kikao gani cha bunge kimekaa kuridhia ombi la
serikali nyongeza ya bajeti, je waziri husika alitangaza ongezeko hilo kupitia gazeti la serikali.Hizi pesa
zilizongezeka kama kima cha chini ni kodi za wanachi si za ccm lazima zifuate taratibu na sheria sio
unakurupuka baada ya kuona mambo yamekufikashingoni unaenda kwenye majukwaa ya kisiasa unatangaza
kima cha chini.Dr Slaa hatunyang'ani hilo tonge letu ila anachohoji hii si rushwa.
Jamani si huyu huyu raisi alitudharirisha pale Diomondi Jubilee na kutuambia hata tugome miaka 8 hicho
kima cha chini hatatoa sasa hizi za sasa katoa wapi?
 
Slaa ni silaha yetu, hatudanganyikiiiiiiiiiii wafanyakazi, hata tuongezwe mshahara mpk tsh 500,000 ila kama mfumuko wa bei haujathibitiwa ni bure tu, serikali lazima idhibiti mfumuko wa bei ili hela iwe na dhamani.Halafu mbona mimi sijaona hilo ongezeko la mishahara????? maana hata salary slip za july na agosti zinaonyesha mshahara wa zamani so bado nasema huu ni usanii wa CCM kuturubuni kisha hawatekelezi kama kawaida yao. 2010 HATUDANGANYIKIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII.
 
Pesa zote zinapitishwa na bunge hasa nyongeza za mishahara na kutangazwa na waziri husika.Ukirejea
kipindi cha bunge la bajeti serikali ilitangaza kima cha chini cha sh 135,000/= na kusema serikali haiwezi
kuongeza pesa zaidi ya hiyo kutokana na ufinyu wa bajeti.Swali la kujiuliza hizo pesa zimetoka wapi za
nyongeza na ni nani kaidhinisha hizo pesa hapo ndo utakapoona ufinyu wa mawazo yako.Kinachoongelewa
na Dr.Slaa je zile taratibu za kuidhinisha hizo pesa zilifuatwa, kikao gani cha bunge kimekaa kuridhia ombi la
serikali nyongeza ya bajeti, je waziri husika alitangaza ongezeko hilo kupitia gazeti la serikali.Hizi pesa
zilizongezeka kama kima cha chini ni kodi za wanachi si za ccm lazima zifuate taratibu na sheria sio
unakurupuka baada ya kuona mambo yamekufikashingoni unaenda kwenye majukwaa ya kisiasa unatangaza
kima cha chini.Dr Slaa hatunyang'ani hilo tonge letu ila anachohoji hii si rushwa.
Jamani si huyu huyu raisi alitudharirisha pale Diomondi Jubilee na kutuambia hata tugome miaka 8 hicho
kima cha chini hatatoa sasa hizi za sasa katoa wapi?

Wanaforum, hii ni janja ya CCM kutumia hela za serikali kwenye kampeni, walichofanya ni kwamba wamechukua fedha kwenye account ya OE-Other Expenditure na kujifanya inakwenda kulipa mishahara iliyoongezwa kwa hiyo mpaka waje waseme ni kiasi gani hasa kimetumika tayari uchaguzi umeisha na wameshashinda uchaguzi na serikali ni ya kwao. Hivyo itabaki kuwa CAG anasemaje, miaka inapita ni 2015 na watu hawakumbuki tena, na hivyo ndivyo itakavyokuwa.
Rais angeisemea si katika jukwaa la siasa wala kampeni ya CCM. Halafu mishahari kuboreshwa ni haki ya wafanyakazi na siyo huruma ya serikali.....
 
I was likely to get confused by the message from Remmy....! But thanks God that this is the home of Great Thinkers....! Completely encouraged....!
 
Hukusikiliza kwa makini hotuba yake Mwanahaki,.JK alisema hataweza kupandisha kiwango cha chini kufikia sh 315000 kama walizotaka TUCTA na akasema hata mkigoma kwa miaka 8 haiwezekani ni bora msinipe hizo kura zenu kuliko kuwadanganya kisa ni mwaka wa uchaguzi. HUkumuelewa, NImetamani sana niirudishe ile speech kwenye vyombo vya habari umma umsikilize tena, sina uwezo.
 
Kagemulo. Achana na pandikizi hili. Halina hoja mbali na kutumwa.

Hana hoja maana hata hoja anazolalamikia Dr Slaa hazijui. Yupo kuandika pumba akidhani tutamshangilia kumbe tumemgeuza sawa na karatasi ya kupangusa uchafu choon.

taratibu jamani, tuwaeleweshe polepolewatatuelewa tu mbona wetu hawa
 
Silaa tafadhali kutaka kwako kura kusikufanye ukatunyang"anya tonge wafanyakazi mdomoni. Tunazitaka sana hiyo nyongeza ya mshahara no matter imetangazwa wapi? we mbona umeahidi mengi? hizo ahadi si rushwa na si kinyume na maadili ya kampeni? kabla ya kuzinduliwa kwa kampeni ulizitaka kura zetu na ukaahidi kuongeza mshahara hiyo si rushwa? Nilikupenda sana niliapa kutopiga kura mwaka huu lakini ulipokuja wewe nikahamasika lakini kwa hili unaniboa na kinirudisha kulekule. Wafanyakazi hatudanganyiki na nyongeza ya mshahara hata akiongeza kama hatukumtaka tusimgempa na hata kama asipoongeza kama tulimtaka tungempa. NImegundua kuwa wagombea wote wapo kwaajili ya kura tu na wala si maslahi ya wananchi, kama kweli unamaslahi nasi ungeacha wafanyakazi mwezi huu wa nane japo tufikie hiyo 175,000/= tupambane na maisha. Khaa bee!!!!

Hivi una maana tonge ni JK au hiyo increment? Hivi maadili ya uchaguzi ya NEC unayajua; terms and conditions of political parties unazijua, sheria ya uchaguzi umeisoma vizuri? Kama bado basi kasome kwanza halafu hutuletee theses nzuri!!!
 
Sijadanganywa wana JFmtu mzima hadanganyiki.NIlipokuwa naandika nilijuakabisa humu ndani 90% ni CHADEMA original nilitegemea kuzongwana kutukanwa kabisa. TO be honest since naingia kazini 2007 JK kanipandishia mshahara more than 3times,nilianza na 392000 per month mpaka mwezi july,2010 kwa mshahara mpya nimefikia 709000. wale wa kima cha chini 2007walikuwa na only 61000 per month sasa wana 135000,wapi hakuongeza kama mnavyodai. CHADEMA si nguvu zao ila TUCTA na migomo ya wafanyakazi ndo wametufikisha hapa CHADEMA msijidai. I owe you alot Mgaya thanks to you,live longer!!!
 
Mimi mfanyakazi ndiye niliyesikia kutoka kwa kikwete kuwa hataki kura yangu...............mimi na watoto wangu na mke wangu na wajomba wangu na ndugu zangu wengine hatutampigia kura kikwete wala ccm tutaipa kura chadema........mimi cwezi kuwa mpiga kuwa wa kutangatanga kama mwandishi wa hii thread aliyefulia yaani ni mmoja kati ya wale watz mbayuwayu wasiokuwa na msimamo.................
Kwa kweli ha2danganyiki hata kwa pilau
 
WANASIASA WANAOTAKA KURA ZETU ........WAMETUFANYIA NINI?......sio kukurupuka na kuzitaka kura zetu
Usitoe kura yako kama shukrani kwa mtu aliyekufanyia jambo fulani, toa kwa yule unayedhani atakuonoza vizuri huko uendako. Kama kuna aliyekuongoza vizuri kwenye mitaa ya huko kijijini, siyo lazima umpe kura tena huyo eti akuongoza mjini bila kujua kama anaijua mitaa ya mjini.

Kutokana na kuwa wagombea wengi wa CCM wanategemea kura za shukrani huenda ndiyo maana wamekuwa mbele kutoa rushwa kusudi washukuriwe kwa kura. Hizi pilau, pombe, pesa, khanga, tisheti, simu, baisikeli, pikipiki, na kadhalika ni matokea ya kutegemea kura za asante badala ya kutegemea kura za uwezo kiungozi.
 
Silaa tafadhali kutaka kwako kura kusikufanye ukatunyang"anya tonge wafanyakazi mdomoni. Tunazitaka sana hiyo nyongeza ya mshahara no matter imetangazwa wapi? we mbona umeahidi mengi? hizo ahadi si rushwa na si kinyume na maadili ya kampeni? kabla ya kuzinduliwa kwa kampeni ulizitaka kura zetu na ukaahidi kuongeza mshahara hiyo si rushwa? Nilikupenda sana niliapa kutopiga kura mwaka huu lakini ulipokuja wewe nikahamasika lakini kwa hili unaniboa na kinirudisha kulekule. Wafanyakazi hatudanganyiki na nyongeza ya mshahara hata akiongeza kama hatukumtaka tusimgempa na hata kama asipoongeza kama tulimtaka tungempa. NImegundua kuwa wagombea wote wapo kwaajili ya kura tu na wala si maslahi ya wananchi, kama kweli unamaslahi nasi ungeacha wafanyakazi mwezi huu wa nane japo tufikie hiyo 175,000/= tupambane na maisha. Khaa bee!!!!

Ndugu yangu pole sana, huu wote ni umasikini uliosababishwa na ccm. Kama kweli mfanyakazi anaangalia kanyongeza ka mshahara halafu anashangilia!!! hii kwangu ni ajabu. Elimu ya uraia ni hii, kuangalia mbali si kuangalia kama kuku na kudonoa donoa tu pembeni, angalia kama Tai. Tunataka mabadiliko ya uongozi ili tujenge Tanzania yenye neema kwa wote kwa vizazi vyote. Wakati mwingine usifikiri wewe kufaidika, kuwa mpambanaji ili wanao na wajukuu wako hapo baadaye waone fahari juu yako. Si baadaye ukishazeeka wajukuu wakubeze waseme 'hivi baba mlikuwa na akili kweli mpaka mali zetu zinaporwa na kuisha na kutuachia umasikini?' usiangalie kanyongeza ka JK angalia Tanzania yenye neema baadaye.

Saa ya ukombozi ni sasa.
 
Sijadanganywa wana JFmtu mzima hadanganyiki.NIlipokuwa naandika nilijuakabisa humu ndani 90% ni CHADEMA original nilitegemea kuzongwana kutukanwa kabisa. TO be honest since naingia kazini 2007 JK kanipandishia mshahara more than 3times,nilianza na 392000 per month mpaka mwezi july,2010 kwa mshahara mpya nimefikia 709000. wale wa kima cha chini 2007walikuwa na only 61000 per month sasa wana 135000,wapi hakuongeza kama mnavyodai. CHADEMA si nguvu zao ila TUCTA na migomo ya wafanyakazi ndo wametufikisha hapa CHADEMA msijidai. I owe you alot Mgaya thanks to you,live longer!!!

Nina wasiwasi na wewe kama kweli ni muwajibikaji mzuri kazini. Haki bila wajibu si haki na wajibu bila haki si haki. Sasa wewe unaamini kuwa kuongezwa mshahara ulikokuonyesha kunalingana na kuhenya kazini kwa mwezi mzima? Kwa miaka mitano amekuongeza takribani asilimia themanini na moja hivi. Je, kuhusu bidhaa na mahitaji unajua vilivyopanda bei? Mwaka 2005 sembe, sukari, kodi ya nyumba, mchele, mafuta ya kula, nakadhalika vilikuwa bei gani? Umeshapata faraja ya kusahau machungu ya Chama Chetu? Lakini cha fedheha zaidi ni kutaka utu wako ulinganishwe na fedha. Huo ni utumwa mbaya mno, utumwa wa nafsi. Yalikwa matusi si ya nguoni tu (bali ya kila mahali) mfanyakazi kulinganishwa na mbayuwayu. Mfanyakazi kutishwa, kukejeliwa na dharau katika hutuba ya mtu waliyemweka wenyewe ofisini, vilivuka mpaka kwa maana zote. Kama kweli kama una chembe ya utu isiyonunulika kwa fedha iliyobaki nafsini mwako huwezi kumshutumu kiongozi wa CHADEMA kwa kudai iliyo haki kwa mfanyakazi lakini kwa njia zinazokubalika kisheria. Si kutumika kama takrima ili wafanyakazi mummiminie kura ambazo mwenyewe akiwa na akili timamu, bila kushawishiwa wala kushurutishwa tena mbele ya hadhara akitazamwa na dunia nzima, alizikataa.
CCM ni chama changu kwa miongo mingi lakini tukubali tu kuwa kimezeeka. Kama chuma huchakaa na kuwa chakavu, sembuse chama kilichoasisiwa na binadamu. CCM sasa kirefu chake ni Chama Chakavu Mkweche. Sera zao, porojo, ahadi hewa za miaka zaidi ya hamsini zimechosha masikioni na hata mioyoni pia. Unaweza kubahatisha kushikilia hilo tonge la ufisadi kwa sasa lakini litakukwama tu kooni kwa miaka mingine mitano na kukutokea puani.

Huamini?

Dawa ya mjinga ni kuumia.
 
Sijadanganywa wana JFmtu mzima hadanganyiki.NIlipokuwa naandika nilijuakabisa humu ndani 90% ni CHADEMA original nilitegemea kuzongwana kutukanwa kabisa. TO be honest since naingia kazini 2007 JK kanipandishia mshahara more than 3times,nilianza na 392000 per month mpaka mwezi july,2010 kwa mshahara mpya nimefikia 709000. wale wa kima cha chini 2007walikuwa na only 61000 per month sasa wana 135000,wapi hakuongeza kama mnavyodai. CHADEMA si nguvu zao ila TUCTA na migomo ya wafanyakazi ndo wametufikisha hapa CHADEMA msijidai. I owe you alot Mgaya thanks to you,live longer!!!

Remmy unaonekana kuwa unajua sana namna mishahara ilivyongezeka, bila ya kututajia athari za mfumuko wa bei kwa mishahara hii duni. kwa jinsi unaisifia nyongeza hizi kiduchu napata wasi wasi kuwa nafasi yako ya kazi unaitumia kuwadai wananchi rushwa au kushiriki wizi wa mali ya umma ndio maana haujui athari za mfumuko wa bei. Nyongeza ulizotaja ni ndogo sana ikilinganishwa na ongezeko la mishahara kwa kwa viongozi waandamizi wa serikali kama vile wabunge, mawaziri, makatibu wakuu, majaji, wakuu wa vyombo vya usalama n.k. Kwa hakika kuwa na mfanyakazi kama wewe anayethamini rushwa kuliko mshahara ni mzigo kwa taifa hili.

Hakuna mtu amabye amedai kuwa CHADEMA ndio imeleta nyongeza hizo, alichofanya Dr Slaa na CHADEMA ni kuongezea nguvu madai ya TUCTA; waliyoyadai muda mrefu na kuambulia matusi na vitisho miezi mitatu iliyopita kutoka kwa JK. Kutokana na uwezo wa DR Slaa kujenga hoja CCM ikagundua hoja za wafanyakazi ilizokuwa ikizipuuza zitakigharimu sana katika uchaguzi huu hivyo kuamua kutoa nyongeza hiyo.

Hata kama wewe hautambui mchango huo, mamilioni ya wafanyakazi wanatambua tafu iliyopigwa na DR Sla na CHADEMA na wamepania kuhakikisha kuwa hii ndio mara ya mwisho kwa madai ya wafanyakazi kuchezewa chezewa. Hivyo watashiriki katika harakati za kuliboresha Byunge letu kwa kupunguza wabunge wa chama tawala ambao hushindwa kutimiza amajukumu yao kutokana na mfumo wa ukiritimba wa CCM na kuongeza wabunge wa upinzani ili mijadala yenye masalahi ya taifa iweze kupatiwa kipumbela kama vile Serikali kuchukua hatuaza dhatui kumaliza tatizo sugu la misururu mirefu ya magari kila asubuhi na jioni katika karibu Majiji yote ya Tanzania; amabyo inawaathri sana wafanyakazi kiuchumi, kijamii n.k

Mfanyakzi yeyeote anayetazama maslahui ya muda mfupi yanayotokana na kutumia nafasi yake ya kazi kuwadai wananchi rushwa hivyo kujipatia mapato ya kificho ndio hawezi kuona faida za kuleta mabadiliko hapa nchini
Iko siku na wewe pia utatambua nini tunakigombea, lakini kwa hivi sasa inaelekea nafasi yako kikazi unapata vi rushwa rushwa kwa kuwakamua wananchi ambao unapaswa kuwahudumia bur ndio maana hauni ugumu wa maisha licha ya wafanyakzi kupata mishahara mdogo
 
Back
Top Bottom