Dr. Slaa, usigombee ubunge tafadhari nakuomba

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Aug 8, 2009
2,906
3,249
Kutokana na tetesi na maoni ya watu wengi ndani na nje ya JF yanayopendekeza na kushauri Dr. Slaa agombee ubunge, ni jambo zuri lakini binafsi nachukua fursa hii kumuomba, kama alikuwa na mpango huo au hata kama anapata ushawishi katika chama, namuomba sana aachane na mpango huo.
Kuna sababu nyingi lakini acha nitoe chache za msingi
1. Mahali popote penye mafanikio lazima kutatokea watu wasiopenda mafanikio yako licha kwa kutojionyesha kuwa hawapendi
2. CCM wana mbinu nyingi sana chafu ambazo najua bado hazijafutika kichwani kwako na kwa kila mtanzania kutokana na yaliyojitokeza kwenye uchaguzi uliopita(wizi wa kura) sasa usitarajie kuwa wameacha wizi
3. Kutokana na sababu hizo, kuna uwezekano licha atuombei, ukaja kushindwa kwenye hizi chaguzi za ubunge, bila shaka utakuwa umepoteza mvuto katika jamii, na ile ndoto ya watanzania kuwa utakuwa mgombea na hatimae kuwa rais ajae wa tanzania itakuwa imefutika.
Mwisho nikutakie kazi njema katika kujenga chama imara.

CDM DAIMA
 
kwanza hagombei hakuna mpango hakuna mpango kama huo kwani slaa ni presedential material yule
siyo mtu wa kugombea ubunge tena kazi alizonazo kwenye chadema zinamtosha na kama hakigombea
lazima atashinda lakini hatogombea kwani yeye ni kocha kazi yake ni kupanga mashambulizi na wewe
mwenyewe unashuudia makombola yanayotua bungeni ccm haina hamu.

ushauri wangu kwa chadema:
nendeni igunga muwape chance watu igunga wachague mtu wanayemtaka hawakilishe kwa ticket ya CDM kama huyo diwani wa chadema
wa igunga mjini basi agombee kama watu wengine na kamwe msiwateulie mtu watu awe yeyote yule.
 
Dr Slaa ni Presiential material hawezi kugombea ubunge huo ndio ukweli wenyewe
 
Nafikiri hatogombea. Kazi kubwa kwake iwe kukijenga chama, kuwajenga viongozi wa CHADEMA, kuwapa elimu ya uraia wananchi na kuwaeleza kwa ushahidi lile alikuwa akilisema wakati wa Kampeni 2010 ya kuwa kuirejesha CCM madarakani ni kuwaletea maafa watanzania. Hii dozi inatakiwa iingizwe vilivyo kwa kila mtanzania kabla 2014.
Najua CHADEMA wanakumbuka kuwa ilimlazimu Nyerere (JK halisi na wa ukweli) aache uwaziri mkuu aende kukijenga TANU.
 
Naunga mkono hoja kwa 100% muheshimiwa rais mtarajiwa wilbroad slaa awaachie vijana wagombee ubunge yy apambane na urais. TUNAMTEGEMEA SANA ACHUKUE MIKOBA YA JK
 
Mkuu huyo asidiliki wala kuwaza kugombea ubunge wowote ule kwa sasa hadhi yake ni HIYO HIYO ALIYOTUONYESHA KUPITIA KAMPENI ZAKE ZA URAIS ZILIZOPITA.Subira yavuta heri,akigombea UBUNGE atakuwa AMEWAANGUSHA BAADHI YA WATANZANIA WALIOANZA KUAMINI JUU YA DHAMILA YA KUWAKOMBOA TOKA MIKONONI MWA MAFISADI.
 
nami naungana na wenzangu asigombee ubunge hata ukitokea popote, atapoteza mvuto wake ikatokea akashindwa, tunamtegemea sana kuikomboa nchi na wananchi wake baadaye, aendelee kuimarisha chama chake hadi kwenye grassroot.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom