Dr. SLAA sasa atoa facts suala la CCM & silaha, amvaa Amiri Jeshi Mkuu na Mwenyekiti

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,642
6,070
Wakuu

Jana Jumanne, timu kadhaa zinazounda timu moja ya Operesheni Sangara-M4C ilikuwa inamalizia kiporo cha Mvomero, ambako kabla ya mapumziko ya siku mbili kwa ajili ya Siku Kuu ya Eid-El-Fitr, kata kadhaa zilibaki katika mashambulizi makali ya Jumamosi. Mashambuzi hayo yamemng'oa Amos Makalla kutoka huko Dar es Salaam kuja jimboni kusalimia wananchi! Anakumbuka shuka kumekucha...

Katika mikutano aliyofanya jana na timu yake, Dkt. Slaa alitoa more facts juu ya zile tuhuma nzito alizotoa juzi kwenye press conference kuwa CCM wamekuwa wakiingiza nchini silaha bila vibali wala kulipia leseni, kisha wanawapatia vijana wao wanaowekwa kwenye makambi mbalimbali (kama ile ya Ulemo, Iramba, Singida, wakati wa uchaguzi mdogo Igunga) ambayo hutumika kuandaa na kufundisha vijana kwa ajili ya kufanya utekaji, utesaji na hata kuua...

Katika hatua ya mbele zaidi, amesisitiza kuwa kama ambavyo hawajawahi kuchomoka katika mtego mwingine wowote ule hasa katika masuala ya ufisadi na kuhujumu maendeleo ya watu wa nchi hii, katika hili la kuingiza silaha nchini kwa nia ya kudhibiti CHADEMA na kudhuru viongozi wake (wapinzani wao wa kisiasa) "CCM hawatachomoka pia".

"Kwa hili pia CCM hawachomoki, wamo kwenye mtego wetu tena kwa mara nyingine, leo naanza kwa kutoa kidogo tu, wakiendelea kuja na maneno matupu nitatoa facts na nyaraka zingine zaidi, na sasa katika hatua hii suala hili linamhusu Kikwete akiwa kama Mwenyekiti wa CCM na Amiri Jeshi Mkuu, ndiye anayehusika na masuala haya, afanyie kazi suala hili ili Watanzania wapate majibu ya kina na ukweli.

"Wakati wa uchaguzi mdogo Igunga waliweka vijana kwenye makambi kama pale Ulemo, Iramba mkoani Singida, wakifundishwa mbinu za kuteka, kutesa na kuua, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya CCM kudhibiti wapinzani wao kisiasa, wakilenga CHADEMA na hasa kudhuru viongozi wake. Waliwapatia bunduki, mojawapo ni silaha iliyotengenezwa China, yenye uwezo wa kubeba risasi 8 kwenye magazine yenye namba J137, walikuwa nayo vijana hao kambini.

"Tunamtaka Kikwete, kama Amiri Jeshi Mkuu na pia akiwa Mwenyekiti wa CCM atuambie, silaha hii iliingiaje nchini na kwa nini ilikuwa mikononi mwa CCM, tutashusha nondo zaidi, kuendelea kuivua nguo CCM na mikakati ya kumaliza wananchi wa nchi hii wasiokuwa na hatia," alisema Dkt. Slaa katika vijiji mbalimbali vya Kata za Langali na Mlali, Mvomero, Morogoro.
 
Labda hao ndio baadhi ya wahuni walioshiriki kumteka Dr. Ulimboka. Aibu kubwa kwa CCM kuanzisha kundi la kigaidi chini ya ulezi wa Mwigulu.
 
Jamani kama ni kweli hiyo ni kashfa nzito sana kwa taifa letu, lakini kama siyo ni hatari pia! Ni muhimu vyombo vya usalama vikachunguza!
 
Nape anachezea moto natamani aendelee kuchemka wanaume wamshukie boss wake mazima. Nape jana kabeep leo Dr kapiga simu.

Nape atuamnbie je hiyo bunduki waliitoa wapi na nani aliisajili kwa nini ilikwenda kwenye makambi yao. Nape akumbuke alikubali kuwa huwa CCM wana makambi ya kufundisha vijana wao vita na kuteka sasa aseme bunduki za nini wakati kuna polisi, mgambo, nk na kama wanahitaji bunduki kwanini wasisajili wakati ni ruksa mtu kumiliki silaha???

Nape akumbuke CCM wameteka, wameua na wanatoa kauli chafu na za dharau kama zile za Igunga sasa wanalia.
Mahakama zikifanya kazi vizuri Tanzania tutaheshimiana na wehu watapungua.
 
Bunduki za nini?
Mbona yeye alikamatwa na mbili mfukoni kule Arusha?
Hivi ile kesi iliishia wapi?
 
CCM au Chama Cha Mafioso wamekuwa wakifanya vitu bila kujali kuwa kuna kubadilika kwa wakati. Ule mfumo uliowazaa na kuwapa kiburi wa chama kimoja ulishakufa ingawa wao wanadhani bado uko hai. Heri wangekuwa na akili wakatumia japo moja ya common sense wangejifunza kilichojiri Kenya mwaka 2002 KANU ilipodondoshwa na kufurushwa madarakani. Kwa vile CCM ni Chama Cha Mafedhuli hawana uwezo wa kujifunza hadi yawakute.
 
Mbona hapa kuna upuuzi mtupu.
Andiko lote haluna fact hata moja kusubstantiate hizi serious allegations.

Ndo matatizo ya monologue, wanakijiji watshangilia tu Dr Slaa.
Leo akija mtu akasema CDM wameficha mabomu sehemu fulani kwa kujiandaa na uchaguzi , bila vielelezo si mtaamini ? Au siyo
 
Album mpya ya chadema ni "bubu". Tutasema, tutataja.

Na kuna misukule inashangilia, wanafanywa kama kama watoto wa kuku, "mtanyonya kesho".
 
wewe usiwe mtumwa wa mawazo namba ya siraha (bunduki) iko hapo waitolee ufafanuzu wala sio siasa
Ni mtu mjinga mjinga tu anaweza kuamini hii trend of thoughts, kuwa silaha moja ndo ina wawinda viongozi wa CDM wakati mwenyewe DrSlaa alikutwa ana mbili!

Wakuu April Fools day ilishapita!
 
Back
Top Bottom