Dr. Slaa ondoeni huyu ndani ya CHADEMA

PMNBuko

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
967
154
Diwani wa Kata ya Kibeta mjini Bukoba amefunga barabara ya wapigakura wake kwa zaidi ya miaka 5 sasa. Kutokana na hali hiyo barabara hiyo imetelekezwa na Manispaa ya Bukoba kwa kuachwa bila matengenezo yoyote.

Wananchi zaidi ya 250 wanaruka mawe na maji kama ngedere bila msaada wa Diwani wao kwa kukosa uongozi wake ambao ungezaa matunda kwa wapigakura hao kupata huduma ya barabara inayopitika.

Rai yangu kwa Dr Slaa, ondoeni mtu huyu maana ameshindwa kutekeleza ahadi zake na anakidhalilisha Chama chetu.
 
Muwe mnamtanguliza Mungu kwanza, kabla hamjamchagua mtu wa kuwaongoza. Mfano uliohai tumeuona kwa "jua kali", tuliridhika sana na maneno ya viongozi wetu wa dini eti ni "chaguo la Mungu" bila kuchanganya akili zetu mwisho wa siku tunalia na kusaga meno. Wengine mpaka imefikia wameanza kumkumbuka Mwalimu na maamuzi yake ya busara wakati ule wa mwaka 95, dhidi ya Bw. Ben na Mzee wa upepo.
 
Diwani wa Kata ya Kibeta mjini Bukoba amefunga barabara ya wapigakura wake kwa zaidi ya miaka 5 sasa.

Achana na barabara ya kata, Mbowe anakutaka muwape nchi miaka 5 wataondoa umasikini.
 
Hii nikazi yenu wapga kula,na ikiwezekana siku ya mkutano katika mtaa wenu msikose kumuuliza jambo ili,kikubwa zaidi kaguweni mapato na matumizi,isije ikawa hakuna hata Tsh iliyo letwa mtaani kwenu.
 
kaifunga kwa sababu gani?labda kuna mabomu ya ardhini!!!uliza sababu za kuifunga halafu urudi utuhabarishe
 
Mimi si mkazi wa pale nilipata kuon ahali hii wakati wa mazoezi ya sensa nikakuta malalamiko kwa Diwani huyu. Kwa ujumla wake wananchi wamemchoka. Hafanyi lolote kabisa.
 
Slaa hana namna yoyote ya kumwondoa Diwani, vinginevyo ataanzisha mgogoro kama uliopo Arusha.
Hii ndiyo shida ya nafasi za kidemokrasia!...Katiba yetu mpya inabidi isisahau mambo ya jinsi hii!
 
Muwe mnamtanguliza Mungu kwanza, kabla hamjamchagua mtu wa kuwaongoza. Mfano uliohai tumeuona kwa "jua kali", tuliridhika sana na maneno ya viongozi wetu wa dini eti ni "chaguo la Mungu" bila kuchanganya akili zetu mwisho wa siku tunalia na kusaga meno. Wengine mpaka imefikia wameanza kumkumbuka Mwalimu na maamuzi yake ya busara wakati ule wa mwaka 95, dhidi ya Bw. Ben na Mzee wa upepo......

For sure kiongozi bora si sura, kabila, tabasam wala mwonekano bali atoka kwa Mungu, japo sasa naamini ni bakora tumepigwa na sijajua kama tumejifunza mpaka 2015 ndo ntakuwa na jibu.
 
Hii nikazi yenu wapga kula,na ikiwezekana siku ya mkutano katika mtaa wenu msikose kumuuliza jambo ili,kikubwa zaidi kaguweni mapato na matumizi,isije ikawa hakuna hata Tsh iliyo letwa mtaani kwenu.....

we unadhani watu kama hawa wanafanya mikutano basi?
 
Muwe mnamtanguliza Mungu kwanza, kabla hamjamchagua mtu wa kuwaongoza. Mfano uliohai tumeuona kwa "jua kali", tuliridhika sana na maneno ya viongozi wetu wa dini eti ni "chaguo la Mungu" bila kuchanganya akili zetu mwisho wa siku tunalia na kusaga meno. Wengine mpaka imefikia wameanza kumkumbuka Mwalimu na maamuzi yake ya busara wakati ule wa mwaka 95, dhidi ya Bw. Ben na Mzee wa upepo....

HEBU NI FAFANULIE "JUA KALI" na "CHAGUO LA MUNGU"..........UNAMAANISHA MUNGU ANACHAGUA MAFISADI?
 
mbona rahisi tu kumng'oa,itisha mkutano wa hadhara hapo kijijini then mchukue hatua ya kumiondoa+kufunga ofisi yake
 
For sure kiongozi bora si sura, kabila, tabasam wala mwonekano bali atoka kwa Mungu, japo sasa naamini ni bakora tumepigwa na sijajua kama tumejifunza mpaka 2015 ndo ntakuwa na jibu.

Diwani mwenyewe ni Mchungaji wa Kanisa liitwalo Chemchem. So what should these people do, how can the choice be done rightly???
 
Slaa alishatangaza kuwa nchi haitatawalika diwani kaamua kuanzisha mamlaka yake shida iko wapi?
 
Baada ya maoni yenu nimemtafuta WEO (Ward Executive Officer) wa Kata hiyo kujua kama Barabara hiyo ina mpango wa kutengenezwa na kama Diwani huyo hafungui njia je barabara itapita wapi?? Nimeelezwa hakuna mpango huo maana Diwani huyo hazingatii njia hiyo maana ana maslahi tofauti nayo.
 
Back
Top Bottom