Dr Slaa: Nionyesheni hati ya muungano ili nami niutambue muungano!

IYO NI ndoa ila si halali kabisa imefungiwa vichochoroni huko na ni kazi sana kupata watoto wenye akili timamu ndio maana watoto wa ndoa iyo wanalala lala hovyo bungeni na wanaropoka ujinga ujinga kila siku mfano mzuri ni huyu makamba na magamba wenzake
 
Watanzania kwa unafiki hawajambo hii katiba rais akiifuata mnasema hii katiba mbaya inampa rais madaraka makubwa...hii katiba ikitumika kwenye sehemu ambayo kuna maslahi na Chadema mnaikubali.

Kinyume na unavyotaka kutuaminisha hapa, Rais ameshindwa kabisa kuifuata, kuisimamia, na kuihifadhi Katiba ya JMT; hilo halina ubishi. Mfano rahisi sana: Katiba ya JMT inatambua uwepo wa taasisi inayoitwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, viongozi wakuu wakiwa vyeo vya Rais na Waziri Kiongozi wa Mapinduzi ya Zanzibar.

Tuthibitishie hapa kwamba serikali hiyo na vyeo hivyo vipo kwa mujibu wa katiba ya JMT! Huu ni mfano mdogo unaoonesha failure ya kutisha ya Rais wa JMT kushindwa kuisimamia Katiba aliyoapa kuilinda! Una jingine?
 
Ritz hili lingewezekana tu kama tungekuwa tumeunda serikali tatu na kila nchi inachangia asilimia fulani ktk mfuko wa serikali kuu, kwa mfano Bara wanatoza kodi ya asilimia 15 kati ya hizo asilimia 7 ni ya nchi (bara) na asilimi 8 ni ya serikali kuu. Zanzibar nao watatakiwa kuchangia asilimi 8 ya mapato ya kodi ktk serikali kuu lakini wanaweza kutoza kodi pungufu ya asilimia 7 kama bara au zaidi - wapendavyo kulingana na mahesabu yao. Kwa maana kwamba kodi ya nchi (ile asilimia 7) haihusiani na sehemu yoyote ua muungano isipokuwa nchi husika, ila mchango wa Serikali kuu ndio lazima iwe kiwango kimoja.

Sasa inapofikia maswala ya Madini na vitu vingine kila nchi itafaidika na rasilimali zake na ule mchango wa serikali kuu utatazama maswala muhimu ya Kitaifa tu na sio manendeleo ya kila nchi. Zanzibar wakipata mafuta watachangia asilimia 8 tu ya kodi ktk mauzio iwe ndani au nje nyinginezo ni kwa maendeleo yao.

Bob Mkandara,
Ngoja tusubiri huu mchakato wa katiba kama suala ili litaweza kuongelewa.
 
Vipi Gesi, Dhahabu, Almasi, Tanzanite, Uranium...Wazanzibar wanapata mgao sawa?
Sasa kuna tofauti gani nilichouliza na wewe unachouliza au Slaa alichoomba aonyeshwe, maana mimi nimeuliza mafuta wewe unauliza dhahabu, IQ? ndiyo maana nimekuambia hujui hata Slaa alikuwa ana maana gani kuomba aonyweshwe hati.
 
Bob Mkandara,
Ngoja tusubiri huu mchakato wa katiba kama suala ili litaweza kuongelewa.

Lakini upanue fikra zako kabla ya kuchangia hili suala,unajua hawa watawala wanaogopa kugusia suala la muungano.kabla ya kuandaa katiba mpya ilitakiwa ipigwe kura ya kuangalia n muungano unafaa.Pana kasoro nyingi sana ktk muungano ambazo zilitakiwa zipatiwe ufumbuzi,mfano gar toka Zanzibar ikija Bara inalipiwa tena kodi,je hizo n nchi tofauti?Zanzibar wana vitambulisho vya uraia na katiba yao,Bara je?
 
Lakini upanue fikra zako kabla ya kuchangia hili suala,unajua hawa watawala wanaogopa kugusia suala la muungano.kabla ya kuandaa katiba mpya ilitakiwa ipigwe kura ya kuangalia n muungano unafaa.Pana kasoro nyingi sana ktk muungano ambazo zilitakiwa zipatiwe ufumbuzi,mfano gar toka Zanzibar ikija Bara inalipiwa tena kodi,je hizo n nchi tofauti?Zanzibar wana vitambulisho vya uraia na katiba yao,Bara je?

Ndio maana CCM wanaambiwa hili suala la Katiba Mpya ni ngoma nzito sana kwao lakini hawaelewi! Ajenda ya Katiba haikuwahi kuwepo katika Ilani ya CCM lakini katika "kutafuta umaarufu" wakadhani hili litawasaidia ikiwa ni pamoja na kuwapiku waasisi wa wazo lenyewe yaani CHADEMA.

Kimsingi, wasipokuwa makini mchakato huu ndio mazishi ya CCM na kufutika kwake katika orodha ya vyama vya siasa.
 
Slaa, yaani leo ndio unaomba hati ya muungano umekaa bungeni miaka mingi hata siku moja ujaomba hati.

Halafu nakushangaa utaki muungano wakati unagombea urais mgombea mwenza wako alitoka Zanzibar kupitia huu muungano.

Kwa nini mnakaa na mbunge wa Zanzibar Raya Ibrahimu ambae katokana na huu muungano.

Na wewe si ndio ulituambia mnakubalika Uzini sijui ulikwenda Zanzibar kufanyaje wakati huu muungano hautambui.


Mheshimiwa Ritz,

Hata mimi simwelewi Dr Slaa kama anamaanisha hautambui Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambao sasa unaitwa JMT. Yeye aligombea u-Rais mwaka wa 2010, kwa hiyo alionyesha kutambua Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ili kumpa "benefit of the doubt", nadhani Dr Slaa alitaka kuona ile hati original. Hii hati, inaeleweka ilijumuisha mambo Kumi na moja tu ambayo yangeshughulikiwa na Serikali ya Muungano. Kumekuwa na nyongeza nyingi katika kipindi hiki cha miaka 48, na baadhi ya hayo ya nyongeza hayakutangazwa au hayakubaliki.

Dr Slaa akiona ile hati ya Muungano original ataweza kusaidia hata kutatua baadhi ya kero za Muungano.
 
Sometimes watu wasipende kujipatia umaarufu kwa vitu vidogo. Siku zote alikuwa wapi asiyaseme haya? Mbona miaka yote ameshiriki sherehe za muungano? Huyu mzee naona anazeeka vibaya. Ni kiherehere gani kilimpeleka Uzini kama hautambui Muungano.

Dr Slaa kwa hili inabidi awaombe radhi viongozi wote wa CDM wanaotokea Visiwani.

Ni upofu wako unaotokana na kufunikwa mwili mzima na gamba unaokufanya usimwelewe Slaa(PhD). Msimamo wa Slaa upo wazi siku nyingi na hata uzini alipokwenda alitamka kuwa kama suala ni muungano basi wananchi waulizwe wanataka muungano wa namna gani maana huu uliopo UMEKOSA UHALALI wa kuwepo kutokana na wananchi kutoshirikishwa wakati unaanzishwa. Zilikuwa fikra na ubabe wa Nyerere na Karume bila kutaka kujua maoni ya wananchi. Lakini akasema, wao kama chadema wanapenda muungano wa serikali tatu (kisiasa).
Sasa awaombe msamaha viongozi wa cdm znz kwa kosa lipi?
 
si ajabu hata kikwete hajawahi kuiona hati hiyo...kweli uongozi kazi kubwa kikwete ulikimbilia ikulu haya sasa tunaiomba hati ya muungano na hao mawaziri wako masele na Tzeba ni hovyo angalau huyo januari na hamisi....

Duh Mkuu itakuwa balaha kama masele atapewa uwaziri,dogo kwa
sasa ana njaa kweli hela nyingi alipoteza kwenye uchaguzi analipa madeni tu
 
Kwakuwa Kikwete hataki wananchi tuamue hatma ya muungano, sasa analazimika kutuonyesha wananchi hati ya muungano ili walau tuwe na imani kwamba muungano tulio nao sasa japo wananchi wengi hatuukubali muundo wake, kwamba una uhalali wa kisheria na kimkataba.

Hii hati ya muungano kufichwa(kama ipo) ni muendelezo wa usiri wa serikali ya ccm usiokuwa na tija yoyote kwa maslahi ya ustawi wa nchi yetu.

Naomba kuuliza...Kama kuna yeyote anaweza nifafanulia faida za kuwa/au kutokuwa na muungano pamoja na hasara zake..
 
haya jamani sasa ndio mnataka kujuwa hati ya muungano kwakuwa kaseme dr slaa lakini pale wazanzibar walipokuwa wakisema tulikuwa tunawatukana na tukiwambia kuwa wanataka kuregesha usulutani haya sasa kazi ianziye kwetu mpaka itolewecheti cha ndoa
 
Hati ya muungano aijulikani iliko sasa huu ni ubwege au ufala?????????
Bora tuuvunje sasa lol!
Heko Dr.Slaa kwa kutuamsha usingizini kha!

wewe ndo umeamshwa na mawimbi ya Operation Sangara,mbona ishu ya kufichwa hati ya Muungano ishaongelewa sana even hii ni moja ya sababu ya kumng'oa Ikulu ya Znz Mzee Jumbe,huo usingizi alokuamsha Dr.Slaa itakuwa ni mdondo,wenzio tushalilia sana hiyo hati tangu enzi za Mwl Nyerere!
 
Kama kuna mtu simuamini kama kiongozi ni Dr. Slaa! Why would you need workings of the documents, data while you already have information. What I mean katiba ya serikali ya muungano ina-nullifying existence ya kitu chochote before! Meaning the fact katiba ya sasa ya 1977 inakubalika kwamba ni katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na fact kwamba UN inajua hivyo... You do not need to know any other documents prior to that! And if you need it, then it is just history or making baraza cheers.

ni wewe mwenyewe tu humwamini dr slaa kati ya watanzani mia moja manake wewe ni MAGAMBA NA ENDELEA KUMWAMINI HUYO VASCO DAGGAMA WAKO NA IKO SIKU UTAMWAMINI DR SLAA MKOMBOZI WETU
 
embu tufikirie Iko wapi TNGANYIKA? mbona ZANZIBARI ipo? yuko wapi Raisi wa Tanganyika? Mbona Zanzibari yupo?
tuoneshwe hati ya muungano kama ipo, kama haaipo ijadiliwe iandikwe na iwekwe wazi.
naomba viongozi wetu msikimbie kivuli chenu mchanamchana. Raisi funguka
 
Back
Top Bottom