Not_Yet_Uhuru
JF-Expert Member
- Oct 11, 2010
- 1,304
- 431
SERIKALI YATEKELEZA KAULI ZA DR SLAA NA SERA ZA CHADEMA TAYARI!!
Serikali ya CCM wanakimbiana kutokana na Nguvu na ukweli wa Uwezo wa Dr Slaa, yaogopa kila kitu kinachosemwa katika Sera za CHADEMA. Sasa imefikia kujikanyaga hadi kuamuru waziri wake afanye jinsi ashushe bei za Saruji, nondo na bidhaa nyingine...Aibuu!
WanaJF, taarifa ya nipashe ipo chini hapa....
----------------------------------
NA GAZETI LA NIPASHE
20th October 10
Serikali: Bei za saruji, nondo zishushwe
Richard Makore
Serikali imeviagiza viwanda vya saruji na nondo nchini kuhakikisha vinapunguza bei ya bidhaa hizo kwa kuwa hakuna sababu yoyote ya msingi inayochangia zipande mara kwa mara.
Agizo hilo lilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara Viwanda, Biashara na Masoko, Joyce Mapunjo, alipozungumza na NIPASHE kuhusu upandaji holela wa bidhaa hizo.
Alisema uzalishaji wa saruji na nondo ni mkubwa lakini hajui kwanini wazalishaji hao wanazipandisha na kuwafanya wananchi wa kawaida kushindwa kuzinunua.
Aliahidi kufuatilia kwenye viwanda hivyo ili aelezwe sababu zinazowafanya wazidi kupandisha bidhaa zao kwa mauzo ya jumla na hivyo kuwafanya wauzaji wa rejareja nao kupandisha bei.
Bei ya nondo yenye milimita 10 yenye urefu wa futi 40 kwa sasa ni Sh.10,000 kutoka Sh. 8,000 milimita 12 Sh. 13,000 badala ya Sh. 12,000 na bei ya mfuko mmoja wa saruji hivi sasa ni Sh. 13,000 badala ya Sh. 12,000.
Na katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Wakala wa Serikali Biashara na Leseni nchini (Brela), Esteriamo Mahingila, aliwataka wazalishaji na wakulma kujiwekea malengo ili kuhakikisha wanaziwekea nembo bidhaa zao zote wanazozalisha.
Mahingila alikuwa akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wataalamu wa masuala ya hakimiliki duniani ambao wanahakikisha bidhaa zinakuwa na nembo na alama kabla ya kuuzwa.
------------------------------------
CCM TUNAWAARIFU UKWELI HUU! Subirini KIDOGO muone nchi inavyoongozwa kuanzia hapo baada ya kura hapo 31 Oct. Wananchi watafumbuka macho na gharama zitakuwa chini wafurahie maziwa na asali katika nchi yao. Mtasahaulika mara moja katika historia!!