Dr Slaa na mchumba wake watakiwa kufika mahakamani

Kazaa naye mtoto hivi majuzi, ni ajabu ya tatu kabla hata mahakama haijatoa taraka. Mahimbo anaweza kufungua kesi nyingine ya kuzaa na mke wake.
Mkuu kuna wakati nilisikia kuwa Mahimbo ameweka pingamizi mahakamani kwamba Dr. asimguse huyo mama, imekuwaje akazaa naye tena na jamaa yuko kimya kama kweli ni mke wake? Hii si ni contempt of the court au?
 
Mkuu nilikuwa na maana kwamba afunge ndoa kanisani au kama hawataki aende kwa DC. Kumbe sasa hata ndoa ya mwanzo ya mchumba wake bado haijavunjika! Basi kuna kazi hapa. Inabidi kwanza ndoa ivunjwe ndio kuwe na mchakato wa kufunga ndoa. Mambo yananichanganya haya: Kama ndoa haijavunjwa inakuwaje awe mchumba wa mtu? Kwa mila za kwetu damu ingeishamwagika kitaaaambo.

Bila shaka Dr Slaa ameshindwa kufunga ndoa kwa sababu ndoa ya mwanzo haijavunjwa kwa taraka (sheria). Nadhani hata hili neno mchumba sio mahali pake kwa sasa hadi hapo taratibu za kisheria zitakapokamilika.
 
mbona hamumuongelei jamaa yetu, yeye akienda ughaibuni lazima aibukie kwa muswati sijui wana biashara gani kule.
 
Mkuu kuna wakati nilisikia kuwa Mahimbo ameweka pingamizi mahakamani kwamba Dr. asimguse huyo mama, imekuwaje akazaa naye tena na jamaa yuko kimya kama kweli ni mke wake? Hii si ni contempt of the court au?
Nchi hii ndugu yangu vigogo wako juu ya sheria,kwetu sisi walala hoi ndio sheria msumeno utaona kama slaa atafanywa kitu,ataachiwa tu,namuonea huruma sana mwenye mke maana jambo hilo lisikie kwa mwenzako tu usiombe likutokee wewe yani mke wako au mume wako achukuliwe na mtu mwingine hata kwa usiku mmoja tu..
 
Kazaa naye mtoto hivi majuzi, ni ajabu ya tatu kabla hata mahakama haijatoa taraka. Mahimbo anaweza kufungua kesi nyingine ya kuzaa na mke wake.
Ingekuwa enzi za Mussa angepigwa mawe.Any way waende kwenye case inayowahusu
 
Mkuu kuna wakati nilisikia kuwa Mahimbo ameweka pingamizi mahakamani kwamba Dr. asimguse huyo mama, imekuwaje akazaa naye tena na jamaa yuko kimya kama kweli ni mke wake? Hii si ni contempt of the court au?

Hadi amezaa na Josephine, Dr Slaa yuko kimya sana angetoka kufafanua hili jambo litamchafua pasipo sababu. Kama ameamua kuishi na huyo mama hana sababu za kukaa kimya wakati jamii inaumba maneno mengi juu ya uhusiano huo wa kimapenzi.
 
suala hili liko mahakamani hairuhusiwi kuendeleza mjadala hadi pale kesi ya msingi itakapoisha. kuendelea kujadili ni kuingilia uchunguzi na upelelezi.

JF itafungwa kwa amri ya mahakama.
 
hakimu aagiza slaa, mchumba wake wafike mahakamani
imeandikwa na veronica mheta, arusha; tarehe: 21st february 2012
habari zaidi:
hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi arusha, charles magesa ameagiza katibu mkuu wa chadema, dk. Willibrod slaa na mchumba wake josephine, kufika mahakamani hapo leo asubuhi kabla ya kuanza kwa kesi dhidi yao na kinyume na hapo atatoa hati ya kuwakamata.

Magesa alitoa amri hiyo jana baada ya washitakiwa hao na mwenzao, aquiline chuwa kutofika mahakamani hapo na wakili wao, albert msando alipoulizwa akawatetea kuwa wamechanganya siku ya usikilizwaji wa kesi ya kufanya maandamano yasiyo halali na kesi ya kutoa matamshi ya uchochezi.

Jana katika kesi hiyo, usikilizwaji wa awali ulikuwa uanze kwa washitakiwa 19 akiwemo dk. Slaa kusomewa mashitaka mapya 13 yanayowakabili.

Awali wakili wa serikali, edwin kakolaki aliiomba mahakama kutoa hati ya kuwakamata washitakiwa hao na kuwaleta mahakamani kwa nguvu kutokana na kudharau mahakama.

“si kweli kuwa wamechanganya tarehe ya kesi kutokana na wingi wa kesi walizonazo kwa kuwa wanaowadhamini wangepaswa kufanya nao mawasiliano pamoja na wakili wao.

“naomba mahakama itoe hati ya kuwakamata na kuwaleta hapa kwa nguvu ili wasipate mkanganyiko wa kuchanganya tarehe,” aliomba wakili kakolaki.

Kakolaki pia aliiambia mahakama kuwa washitakiwa hao wanadharau mahakama hiyo kwa sababu januari 17 mwaka huu waliambiwa wakumbushane ili wasikose mahakamani siku hiyo kwa sababu ndiyo usikilizwaji wa awali wa kesi hiyo utafanyika, lakini hawakufanya hivyo.

“mimi nasema hawajasahau wamefanya makusudi, kwa sababu wangeweza kutumia njia ya kuandika katika kumbukumbu zao ili wasisahau tarehe za kesi zao, pamoja na kudai wana kesi nyingi zinazowachanganya lakini hiyo siyo sababu ya msingi,” alisema kakolaki.

Baada ya wakili kakolaki kutoa ombi hilo, aliomba mahakama iendelee na usikilizwaji wa kesi hiyo kama walivyokubaliana na washitakiwa ambao hawakuwepo, wasomewe mashitaka yao siku watakapofika leo.

Kakolaki baada ya kutoa ombi hilo, hakimu magesa alimwamuru aendelee na usomaji wa mashitaka ya awali.

Wakili kakolaki alidai washitakiwa wote 19 wanashtakiwa katika kosa la kwanza, kula njama januari 3 na 5 mwaka jana katika manispaa ya arusha ya kutenda kosa la kufanya fujo.

Katika kosa la pili linalowahusu washitakiwa 18, wameshitakiwa kula njama kufanya mkusanyiko usio halali na kufanya vurugu baada ya katazo halali.

Katika shitaka linawahusu dk. Slaa na mbunge wa moshi mjini, philemon ndesamburo, wanashitakiwa kwa kutoa matamshi yenye lengo la kuleta uchochezi.

Pamoja na mashitaka mengine, pia walishitakiwa kwa kufanya mkusanyiko usio halali kwa ajili ya lengo moja la kukataa kutii amri ya ocd iliyowataka watawanyike.

huyo josephine ni mchumbaaa au hawara!!!!!! I dont get it
 
Hivi Slaa, akiamua kufunga ndoa kwa Mkuu wa Wilaya atakatazwa?
 
Kazaa naye mtoto hivi majuzi, ni ajabu ya tatu kabla hata mahakama haijatoa taraka. Mahimbo anaweza kufungua kesi nyingine ya kuzaa na mke wake.

usilolijua nikama usiku wa giza.akili za wanywa pombe kupita kiasi.
 
Hivi Slaa, akiamua kufunga ndoa kwa Mkuu wa Wilaya atakatazwa?
Mkuu hawezi kukatazwa. Hata mimi nilikuwa na mawazo hayo, lakini kuna hili jingine eti kwamba ndoa ya awali ya mama Josephine haijavunjwa. Hivyo basi DC hawezi kufungisha hii ndoa itakuwa ni kuvunja sheria. Ila najua pia kwamba kusuio la ndoa yoyote lazima litangazwe sasa isije ikatokea tena Dr. anatangaza kufunga ndoa na mtu ambaye ni wa mtu. Tuayaache hayo nadhani ni mambo ya wenyewe japokuwa wenyewe ni wetu kwa kuwa wanatuongoza/wanataka kutuongoza.
 
Ndoa ya kanisa haivunjwi kirahisi rahisi hivyo labda akimbilie mahakamani kuivunja nasikia kanisani walikataa.

siyo lazima uwe mwanasheria kujua sheria,unaweza kujisomea vifungu na kuelewa.
Cha ajabu kiko ,wapi?napoamua kuomba Talaka.nani alikwambia kanisha ilikataa!

NILIPOINGIA KWENYE NDOA MAAMUZI YALIKUWA YAKWANGU,SASA NAPOTAKA KUTOKA KWANINI MNATAKA KUSHIRIKISHWA.

Tujifunze kuheshimu maamuzi ya watu,mnachotakiwa kufanya ni kushahuri the step ahead.
 
Hadi amezaa na Josephine, Dr Slaa yuko kimya sana angetoka kufafanua hili jambo litamchafua pasipo sababu. Kama ameamua kuishi na huyo mama hana sababu za kukaa kimya wakati jamii inaumba maneno mengi juu ya uhusiano huo wa kimapenzi.

pamoja na haki mliyonayo yakutujadili,naomba mtupe mda,haya ni maswala ya mda.
 
Mkuu kuna wakati nilisikia kuwa Mahimbo ameweka pingamizi mahakamani kwamba Dr. asimguse huyo mama, imekuwaje akazaa naye tena na jamaa yuko kimya kama kweli ni mke wake? Hii si ni contempt of the court au?
"Great Thinkers..."
Sasa hapa mada ni Dr. Slaa aitwa mahakamani au Dr. Slaa "kazaa na "mke" wa mtu"?.
Kuna mambo ya maana mengi sana ya kuzungumzia badala ya kupiga umbea wa mahusiano ya watu wengine.
 
Maendeleo ya lesi vipi hapo Arusha? Dr. Slaa na Josephine wamefika? mliopo Mahakamani tunaomba mtujuze kinachoendelea tafadhali
 
Back
Top Bottom