Njilembera
JF-Expert Member
- May 10, 2008
- 1,496
- 607
Kule rumande hata mahabusi wanaingizwaga watu wa usalama kwa kazi maalumu, nadhani sasa CCM wana kila sababu ya kutumia mbinu za akiba kuwapoteza baadhi ya watu. Msihofu watanzania.
atakayenyoosha mkono na kukudhuru ni mtanzania mwenzako ambaye anaimba ana mapenzi mema na nchi yake ilhali ni mapenzi mema kwa genge lake.
Asante kwa kujibu kero iliyokuwa inanisumbua! Maana sikuweza kuona ni kwa nini mahabusu wafanye walichokifanya. Mahabusu sio watu wa kukata tamaa, maana wanatuhumiwa tu, na kila siku inayokuja wana matumaini ya kutoka. Hizo chuki gani walikuwa nazo na huyu baba wampige walivyofanya! Hili la kwanza.
Pili nilikuwa nawaza pengine alipelekwa mahabusu ya watuhumiwa wale waliokwishakata tamaa. Mahabusu ya watu sugu waliokwisha ua au kufanya maasi kiasi wao ni raha kumwongezea mwenzao mateso. Lakini nalo hili halikukaa sawasawa. Kwa nini mtu huyu awekwe na hao. Au polisi wetu wanawachanganya mahabusu bila kujali asilia za makosa yao. Hili sikuliweza kabisa, nilipata na msongo wa mawazo.
Baada ya kukusoma sasa napata afueni. Walifanya janja apigwe na watu wa usalama...Lakini UWT ni watu wabaya kiasi hicho..hmmmm naweza nikaamini, niliwahi kuwasikia jinsi walivyokuwa wanatesa watu wakati ule wa Presidential Dentation, enzi zile,,,,,inawezekana! Kumbe BADO SSSEMU wanaendeleza kale ka mchezo. Jamani wagombea kuweni makini. Simu zenu zina sehemu ya kubonyeza kuashiria hatari moja kwa moja kwa watu wa karibu nanyi (hasa kama una Samsun, unabonyeza kwa pembeni mara 4 na watu uliowaorodhesha wanapata onyo kwamba uko na shida, watakufuatilia watafanya wanachoweza usiwahishwe mahabusu, watatumaliza hao!)