Dr Slaa mgeni rasmi Kongamano la Wanafunzi Chuo Kikuu Cha Mzumbe Morogoro

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
864
Wakuu, Habari za Ijumaa.

Ni mataumaini yangu kuwa mnaendelea salama na shughuli zenu za kila siku.

Napenda kutumia jukwaa hili kuwataarifu kuwa kesho tarehe 21 Mei 2011 kutakuwa na Kongamano la CHADEMA Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Katika Kongamano hilo Dr Slaa ndiye mgeni rasmi ambapo atazungmza na wanazuoni hao kwa pamoja wakijadili mustakabali wa Taifa la Tanzania. Kongamano hilo linatarajiwa kuanza saa 4 asubuhi katika Ukumbi wa Paradise Mzumbe. Mada mbalimbali zitajadiliwa.

Pamoja na Dr Slaa, Makamanda wengine wa CHADEMA watakaokuwepo ambao ni Fredy Mpendazoe, John Mrema, Benson Kigaila na Regia Mtema ninayecheza uwanja wa nyumbani.

Pamoja na kuhudhuria Kongamano la kesho lakini pia leo baadhi yetu tutahudhuria Kongamano la Katiba lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe litakalofanyika Chuoni hapo kuanzaia saa 3 asubuhi.

Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke.

Aluta Continua

Kutoka Morogoro Mjini
Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira

================================
KATIKA PICHA:

CDM-MZUMBE2.jpg

CHANGARAWE3.jpg

CHANGARAWE2.jpg

MZUMBE4.jpg
 
aksante kwa kutujuza. du, natamani ningepata chance ya kumsiikiliza dr wa ukweli akitema moto hapo. shime wanamoro hii twanga kote kote si ya kukosa!
 
Asante dada Regia kwa taarifa hiyo. Tunategemea wanazuoni watajadili kwa ufasaha matatizo ya nchi yetu na kuonyesha njia ya ufumbuzi. Mungu isaidie Chadema imuonyeshe mwananchi wa Tanzania njia ya kufikia ukombozi wa kweli.

Aluta Continua......
 
Hongera sana dk slaa, kazi yako tunaiona tunakupongeza sana hakuna kulala.
 
Wakuu.Habari za Ijumaa.Nimataumaini yangu kuwa mnaendelea salama na shughuli zenu za kila siku.
Napenda kutumia jukwaa hili kuwataarifu kuwa kesho tarehe 21 Mei 2011 kutakuwa na Kongamano la CHADEMA Chuo Kikuu cha Mzumbe.Katika Kongamano hilo Dr Slaa ndiye mgeni rasmi ambapo atazungmza na wanazuoni hao kwa pamoja wakijadili mustakabali wa Taifa la Tanzania.Kongamano hilo linatarajiwa kuanza saa 4 asubuhi katika Ukumbi wa Paradise Mzumbe.Mada mbalimbali kujadiliwa.Pamoja na Dr Slaa Makamanda wengine wa CHADEMA watakuwepo ambao ni Fredy Mpendazoe, John Mrema,Benson Kigaila na Regia Mtema ninayecheza uwanja wa nyumbani.

Pamoja na kuhudhuria Kongamano la kesho lakini pia leo baadhi yetu tutahudhuria Kongamano la Katiba lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe litakalofanyika Chuoni hapo kuanzaia saa 3 asubuhi.

Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke.

Aluta Continua

Kutoka Morogoro Mjini
Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira

Hapo kwenye kijani.... kila la heri
 
Dada Regia,
Hapa mtakuwa mmefanya la maana sana kwa sababu kati ya Vyuo vya Vikuu vya Kipuuzi vinavyoshabikia CCM nchini ni MZUMBE. Wakati tunafanya mgoma usio na kikoma wa vyuo vikuu nchi nzima mwaka April 2007 vyuo vyote vilituunga mkongo vijana wa UDSM. Ni Mavuvuzela ya Mzumbe University ndiyo yaliendelea kuingia darasani. Nakumbuka mwisho wa ule mgomo ni kwa Profesa Peter Msola kusalimu amri kwa kufukuza wanafuzi wote na kukifunga UDSM na vyuo vyake vyote vishiriki.

Baadae Moto huu ulisambaa hadi kwenye vyuo binafsi lakini Mzumbe wao waliendelea na masomo utadhani tulikuwa tunayapigania yalikuwa hayawasu.

Dk Slaa (My President) nenda kawafunde hawa vijana maana ndio tawi pekee la Chipukizi la UVCCM lililobaki nchini.
 
Tukiwa elimisha wasomi juu ya mstakabali wa nchii nirahisi upinzani kutawala nchii!!Kwani tutakuwa tunapingana kwa hoja siyo kwa siasa za maji taka!PEOPLE POWER IS COMING SOON OUR SIDE!STAY TUNED!
 
mzumbe sidhani kama mmekwenda muda muafaka, mngefanya utfiti kwanza kabla ya kwenda huko
 
Twanga kote kote baba>>>>>>>>>>>>> mkulu alisoma nyakati akawahi kikombe loliondo vinginevyo ingekua kushnei>>>>
 
Back
Top Bottom