Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

SALMA2015

Container la futi 40 kutoka India mpaka hapa ni Dollar 400? nipe hiyo kampuni inayosafirisha kwa bei hii, kila kontena mimi ntakupa wewe commission ya dollar 100. Niko tayari, sasa hivi hata container 200 kuzi reserve meli nzima.

Wacha kudanganya umma.

Ndio unaamka nini shekhe zomba?
 
Last edited by a moderator:
Kaka umeongea ukweli mtupu .mimi huwa nawaambia watu TZ bila ccm ni sawa na paradiso .
 
JF mtaelewa lini? sisi tunajua haya kwa kuwa tuna-access na jamvi. Wenzetu ambao ndo mtaji wa ccm hawajui. Tuwaelimishe
 
Halafu hiyo hesabu yako mfuko mmoja ni shillingi ngapi? ukiweka gharama za usafiri wa meli (zilizo sawa hiyo ya 400 kwa container la futi 40 ni porojo), gharama za bandari? usafiri wa nchi kavu? gharama za kuhifadhi (storage)? gharama za kuuza (sales cost)? kwi kwi kwi teh teh teh, bado ni elfu tano tu kwa mfuko? sasa wewe mbona juu huko kwa gharama porojo na unauza 10,000 kwa mfuko? umempita bei Slaa kwa 100%, sasa nani porojo zaidi wewe, au yeye?

Mambumbu ni wengi sana Tanzania, wanasifia uongo! hizo ndio shule za kina mtakatifu. Tukiwaambia mnsaidiwa na NECTA mnakataa, mmeshazitazama hizo hesabi za bi salma lakini au mnachekelea kama misukule tu?

Wee gamba la Kipemba hebu tulia! Hata kama kuna makosa madogomadogo ya kimahesabu uchambuzi wake ni murua na tunaweza kununua simenti atmost kwa Tshs. 8,000 (elfu nane tu) na siyo hii ya elfu 15.
 
Watu kama zomba huhitaji kubishana nao. wanyonyaji wakubwa. Mahafidhina wenye ukurutu kwenye masaburi.
 
Kunaambao mpaka leo hawajui kwanini watanzania ni maskini.

Rafiki si mbali kijijini bali hata mkuu wa nchi alishawahi kutamka mbele ya mkutano wa kimataifa kuwa hata yeye hajuwi kwanini Tanzania ni maskini.
 
Kaka hongera umenena na kuichambua vizuri

Mi naona mtoa mada kakumbuka shuka wakati kumepambazuka! Alimsikia Dokta akisema bei halisi ya simenti ni sh. 5,000/- kichwa kikawa kizito kuelewa. Leo uchaguzi ushapita ati ndio kaelewa. Uoga wa RISK ni umaskini, tungemchagua daktari huenda angepunguza bei ya cement.
 
Kwa kweli inatia hasira kuona kuwa viongozi wetu hawako makini na hawa majangili wa kizungu, kiarabu, kihindi n.k. Jamaa wanakuja kutunyonya tu kila sekta. Madini wanachukua, gesi wanatupimia kwenye kibaba, umeme wanatuhujumu, wanyama wetu wanachukua wazimawazima, bandarini nako wako, kwenye mabenki wanatuibia, shirika letu la ndege wameua, reli wameihujumu, kwenye makampuni ya simu wanatubia, yaani inatia hasira.

Mkuu, hasira yako ihamishie kwa Serikali iliyoko madarakani, kwani ndiyo iliyokubali hao wageni wanyonye mali yetu kwa wao kupewa hisa kidogo kwenye hayo makampuni, au watoto wao kusomeshwa nje au hata kufadhiliwa kwenye kampeni zao za kisiasa.
 
Watu kama zomba huhitaji kubishana nao. wanyonyaji wakubwa. Mahafidhina wenye ukurutu kwenye masaburi.
 
Mkuu, hasira yako ihamishie kwa Serikali iliyoko madarakani, kwani ndiyo iliyokubali hao wageni wanyonye mali yetu kwa wao kupewa hisa kidogo kwenye hayo makampuni, au watoto wao kusomeshwa nje au hata kufadhiliwa kwenye kampeni zao za kisiasa.

Ni kweli mkuu, huo ndo usaliti wanaotufanyia viongozi wetu wa kiafrika. Na ukiingia ndani zaidi unagundua kuwa huo mgao wanaopewa hawa viongozi wetu ni mapesa mengi mno kiasi kwamba hawana hata cha kuyafanyia, mwisho wake wanakufa na kuyaancha kwenye mabenki yakiwemo ya nje ya nchi huku watanzania wenzao wakitaabika na maisha magumu. This is too wicked kwa kweli.
 
Ndugu mtz asikudanganye mtu, maisha bora yanaletwa na mtu binafsi na si vinginevyo. Achana na wanasiasa watakupa pressure; chemsha akili yako fanyakazi halali kwa bidii utafanikiwa.
 
Ndugu mtz asikudanganye mtu, maisha bora yanaletwa na mtu binafsi na si vinginevyo. Achana na wanasiasa watakupa pressure; chemsha akili yako fanyakazi halali kwa bidii utafanikiwa.

Taratibu mkubwa,
Utafanikiwaje ikiwa unafanya biashara na kisha unaletewa kimemo uchangie CCM na ukikataa unaletewa watu wa TRA waje wakufilisi?,Utafanikiwaje ikiwa biashara yako inategemea umeme na bei yake ni kubwa tena ni wa mgawo na bidhaa zako zinaoza? Utafanikiwaje ikiwa wewe ni mtoa huduma na mojawapo wa wateja wako wakubwa ni taasisi za serikali ambazo huwezi kupewa kazi mpaka utoe 20 %? Utafanikiwaje kujenga hata kibanda chako ikiwa mfuko wa simenti ni sh. 18,000? Utafanikiwaje ikiwa shughuli zako zinahitaji mali ghafi za ubora wa hali ya juu wakati Ekelege wa TBS ameruhusu bidhaa feki kuingia sokoni akishirikiana na wakubwa wake? Utafanikiwaje wakati tu ndo umemaliza shule huna mtaji wa kujiajiri na kazi hupati kwasababu huna mtu wa kukuandikia kimemo? n.k Fikiri!
 
Angalau cement ina process ndefu kidogo!nilishangaa sana nilipotembelea kiwanda cha mbolea ya minjingu phosphate,mchakato wa uzalishaji wake hauzidi kwenye karatasi moja ya daftari dogo kuuandika!ni kiasi cha kuchimba udongo ule mweupe mweupe kutoka kwenye umbali usiozidi mita 3 kwenda chini,kutoka mgodini hadi kiwandani kuna umbali usiozidi mita 400,ambapo udongo huo huchekechwa ili kuondoa mawemawe na vitu vingine vigumu kisha hujazwa kwenye mifuko tayari kwa matumizi!!bei yake sasa!!usishangae mh pinda na jk wakijigeuza maafisa mosoko wa bidhaa hii,kama kuna yeyote mwenye uwezo na afanye utafiti na atashangaa jinsi gani wakulima wetu masikini wanavyoibiwa kupitia mbolea hii,Bila ccm mengi yatawezekana.
 
Ilikuwa kweli
Salma kadhihirisha ukweli kuwa haiwezekani, anaona haya saa hizi, Slaa mfuko 5,000 Salma mfuko 10,000 wapi na wapi? halafu bei ya Salma ya kukodi container hata nusu container haupati wacha container la futi 40. Kwi kwi kwi teh teh teh!
 
Nadhani tafiti kama hizi ziingeendelea ili tuweze kujitambua wakati ujao na kufanya maamuzi sahihi ahsante kwa kutuchanganua
 
attachment.php


Kauli aliyoitoa Dr Slaa wakati wa vuguvugu la kampeni za kisiasa kwamba mfuko wa sement utakuwa Tshs 5,000, badala ya Tshs16,500 kwa sasa kwa wakazi wa DSM na zaidi ya Tshs18,000 kwa wakazi wa nje ya mji huu, nimekuwa nikizitafakari kwa kina sana kwa muda mrefu. Kutokana na Uzoefu wangu wa masuala machache alonijalia mola, nilioona kama ni sentensi ya kisiasa zaidi ya kimatendo, lakini sasa nakiri ni sentenSi makini na ya kweli. Na si 5000 tu bali pia 2,500 au 3000 kwa mfuko wa 50kgs.

Hivi majuzi, nilikuwa namsikiliza Waziri Viwanda na Biashara Dr. Kigoda akizungumzia masuala ya Kiuchumi kwenye kipindi cha TBC asubuhi. Kauli aliyotoa Abdala Kigoda ilinifanya kile kisifa cha kuitwa Dr nikiondoe haraka na natamani nikiingia ofisini kwake nimwite Mr Abdala. Mkongwe Huyu adui mkubwa wa mabango ya “sigara ni hatari kwa Afya yako” alisema , ‘AMESIKIA” wafanya biashara wa hapa wakimweleza kwamba bei ya mfuko wa sement inayouzwa hapa ni ghali sana kulinganisha na bei ya mfuko utaouagiza kutoka India

Nikawaza kama mzee huyu, waziri wetu amesikia tu, ameshindwa kufanya tathimini kutumia ziada kidogo ya akili yake iliyompelekea kuitwa DR, kwamba kama hali iko hivyo kwa India km 4,600 tu kutoka TZ, sawa na kwenda kigoma na kurudi dsm mara mbili, ana mipango gani mbadala ya kuhakikisha na hapa kwetu unafuu wa neema unaonekana kwenye gharama ya mifuko ya cement, watu tukajenga?

Sentensi yake hiyo ilinisukumia na kuamsha mawazo yale niliyokuwa nayo awali aliyoyasema Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CHADEMA Dr Wilbroad Slaa-2010, kwamba Bei ya sement ni ghali sana, Serikali yake itaipunguza hadi kufikia Tsh5,000. Na hapo ndipo nilipoona nifanye kauchunguzi kadogo sana ambako mdau wa jamvi unaweza kunikosoa lakini uwezo wa kuchunguz kwangu ndipo ulipofikia..

Cha kwanza nikawapigia “madalali wa wagonjwa” (india kuna watu kazi yao ni udalali wa wagonjwa, wanatengeneza dili zao kwa kuwasaka wagonjwa kutoka kwenye nchi zao kama Africa na hata penginepo kupitia mashirika mengi kama LIONS CLUB na mengineyo na kuwa connect na daktari husika na kufanya protocal zote za maandalizi na ndivyo nao wanavyopata kula ..anyway that is not ma topic)..nikawauliza wanitajie bei ya mfuko wa sement kwenye soko la kawaida .. baada ya muda wakaniambia ni Rupia 230. Rupia moja ni sawa na Tsh28.

Kwa hiyo mfuko mmoja wa Kg 50 wa sement kule India ni sawa na Tsh 6,440 (28 x 230). Kwa Kontena la 20ft lina uwezo wa kuchukua tani 35-40, lakini meli nyingi zina standard ya kujaza 40ft kwa tani 20 tu. Sasa tani 20 ni mifuko 400 a cement. Kwa bei ya meli zinazosafirisha 40ft kwa 20ton ni dolar 400 (sawa na tzs 632,000 (1,580 x 400).. tukiacha vikodi vidogo vidogo vya asilimia 2.

so mzigo utafika TZ kwa gharama ya (400[20ton] x 6,440[mfuko] + 632,000[Usafiri] =3,208,000 so Mifuko 400 utaifikisha Tz kwa gharama ya Tshs 3,208,000 na Mifuko 400 utainunua Tz kwenye soko letu kwa gramama ya (400 x 16,500) = 6,600,000 tofauti ya zaidi ya (6,600,000 -3,208,000) = 3,392,000 .. he he he!

Mifuko 400, ukiinunua India na kuiuza TZ Tsh 10,000 tu kwa mfuko utapata Tshs (10,000 x 400)= 4,000,000 na kutengeneza faida chap ya (4,000,000-3,208,000)=792,000.

Biashara ya haraka sana na mifuko itagombaniwa kama njugu na wewe unaifanya biashara yako yote ukiwa nyumbani nyuma ya laptop yako tu na simu ya mkononi basi.

Nikaenda mbali kidogo na kujiuliza kwanini India cement ni bei rahisi. Nikagundua kwamba, kasheshe kubwa ya kutengenza sement iko kwenye maandalizi yake hasa hasa uzalishaji wa vijiwe vidoho vigumu sana vinavyoitwa Clinker. Mchakato wa Kutengeneza malighafi hii clinker ndio mgumu na ghali zaidi. Kwa utafiti mfupi nilioufanya nimegundua utengenezaji wa Clinker Kule India Ni Ghali sana Kulinganisha na hapa kwetu TZ. Nilibahatika kutembelea kiwanda cha Lafarge Mbeya Cement maarufu kwa kutengeneza Cement ya Mnyama (TEMBO CEMENT). --Simba ni Tanga na Twiga ni DSM.

Mchakato wa Kutengeneza Clinker unaanzia kwenye machimbo ya miamba geu yenye vichambuzi (ingredients na Ore mbalimbali) miamba hii hutoka machimboni na kuingizwa kwenye ngome ya mapondo (Crushers) ambapo hupondwa na kuwa miamba midogo mithili ya kokoto na kuzukumizwa kwenye mkanda, na vile vile huchimbwa udongo wa mfinyanzi nao hukimbizwa kwenye mkanda wake mwingine kwa viwango vyao.

Mikanda hii miwili huingizwa kwenye ngome kubwa ya mapondo na kusagwa kwa kuchanganywa kiasi cha kuwa vumbi, hapa ndipo kiasi kikubwa cha Vumbi huzalishwa, kutokana na shughuli pevu inayofanyika. Vumbi hili hudhibitiwa sana ila kiasi kidogo hutolewa nje na kuwa wingu zito sana la Vumbi hatari kwa mazingira. Vumbi hukusanywa kwenye Kiwiko kikubwa na kirefu sana nadhani ndio point ndefu kuliko zote kwenye kiwanda cha simenti, kinachoitwa Cyclone. Cyclone Hili hupokea vumbi hilo na kulisafirisha likahifadhiwe kweye maghala makubwa (Silos) Sasa Vumbi hili laini ndio malighafi ya kutengenezea hizo Clinker.

Vumbi hili hukimbizwa kwenye kinu kikubwa (KILN). Na huko huchomwa kwenye jotoridi la takriban nyuzijoyo 1400. Udongo huyeyushwa na kuchangamana. Chanzo cha moto huwa ni makaa ya mawe ambayo hupondwa na kuwa vumbi kisha husukumwa kwa upepo wenye gandamizo kubwa na kuzalisha moto kama jehanam ya ajabu sana ndani ya jiko hilo. Moto ule (Carbon) na udongo huo ukijumlisha na mzunguko wa jiko lenyewe, manake linachoma huku linazunguka basi huzaa vijiwe vidogo vyeusi vinavyoitwa Clinker.

Clinker hizo hupozwa kwenye ghala (hydrous)na baadae hukimbizwa kwenye mpipa mkubwa unaozunguka wenye magololi ya chuma na vikwazo ndani yake, huko clinker hugongwagongwa na kuwa vumbi laini sana ambalo huchanganywa na vumbi jingine linaloitwa gypsum (udongo unaochimbwa Tanga) na hapo kutoa vumbi ambalo likipata maji hukauka na kuwa jiwe linaloitwa CEMENT.

Baada ya chochezi hilo nikapeleleza na utengenezji wa Clinker kule India, ambapo mawe hununuliwa, mfinyanzi hununuliwa na zaidi ya hayo wao huchoma kwa kutumia mafuta ambapo ni gharama sana sisi tunatumia makaa ya mawe ambayo kusini ni mengi tu..

Ukiangalia mchakato huo HAPA KWETU, Miamba geu iko mingi na bure kabisa, Makaa ya Mawe Tunayo Kusini ya Kumwaga tu, Gypsum ni udongo unaopatikana Tanga mwingi sana na Bure tu. Sasa nani katuroga mpaka Cement isiwe na bei ya Tsh 2500 au 3000 tu????!!!????

Nikagundua gharama Kubwa za Cement ni Unyonyaji tu, Viwanda vingi vinaendesha mataifa ya nje na si tanzania. Mfano waholanzi hawa Lafarge wanamlipa MZUNGU Technician tu mwenye certificate ya ufundi karibia Dola 8,500 sawa na (8500 x 2580) = Tshs 13,400,000/=kama mshahara wake mwezi, wakati Mhandisi Mtanzania mwenye Jiwe lake moja au mawili, aliyekokotoa shule ngumu ya FoE na term system that time, na kuvivuka vikwazo vyote vya kina Prop Chambega, Luhanga , Masuha Nk ambaye ndiye mkuu wa sekta mojawapo labda project manager, au Chief Electrical, mechanical, Civil nk kiasi cha Tsh 820,000 kwa mwezi. Usawa uko wapi?. Wakati huyu fundi wa kizungu maelekezo na miongozo ya kazi anaipata kwa Mtanzania huyu ambaye ni meneja wa kitengo husika. Hivi usawa uko .. kama Fundi tu anakula madolali yote hayo je Eng wa kizungu, je Chief of DPt je manager je CO wa kizungu anajichotea mangapi.. kama hiyo haitoshi je wanajilipia kwenye serikali yao kiasi gani kwa External security, BIMA, INSUARANCE nk (maana huduma hizi zote wanajitegmezea huko kwao) na kiasi gani wanarundika kwenye mabenki yao na kuimarisha uchumi wao?

Fedha nyingi na Utajiri Mwingi wazawa hawafaidi, tunanyonywa na kukubali kunyonyeka. Kiwanda sio Inshu kubwa, Serikali ikiamua kujenga Kiwanda hiki ni kazi nyepesi na laini sana. Kama Hawa wazungu wanaleta makandamizi haya basi tuwaalike Wajerumani waliowajengea hawa waholanzi na wengineo viwanda waijengee serikali kupitia vichwa makini chini ya PSRC ikaendesha kiwanda hiki kwa ukombozi wa wananchi wake. INAWEZEKANA..

Alamsik..!!


NB: Kwa muda wako jisomee:

Tanzania: Cement sh 5,000 yawezekana!

&
Maisha BORA: Songea mfuko wa cement sh 20, 000 per bag!
you are real brialiant,uchambuzi safi kabisa,mbeya cement kiwanda cha songwe Injinia mwandamizi Maro ni alikuwa injinia mkuu toka kiwanda kinajengwa mpaka kinaanza uzalishaji,aliacha kazi kwa ajili ya mzungu asiyejua kazi kulipwa Milioni 13 ili hali yeye akipokea milioni 1.5,alipatwa na uchungu akaacha kazi.meneja mkuu Diyami alimshauri Mkapa kutobinafisisha kiwanda cha Songwe ila mkapa hakusikia,kwa hiyo bei ya saruji ingeweza kuwa nafuu tatizo ni ufisadi toka kwa hawa wageni tuliowapa viwanda kwa bei ya kutupa,lengo ni kupata super profit,so THE MISSION OF CAPITALIST WHEREVER THEY ARE IS EXPLOITATION by any means,hivyo saruji kuuzwa 5000 kama alivyosema Dr slaa ni kweli,kweli tupu.
 
inawezekana kabisa kuuzwa kwa bei kama huamini angalia wenzetu Rwanda hakuna nyumba za udongo kule

tena hawa wanyarwanda hawana bandari, sukari wanaagiza kutoka india kupitia bandari ya dar, halafu ikifika kwao wanauza kilo 1 kwa franc 370 kama sikosei, ambayo uki exchange kwa hela za madafu kilo moja inakuwa kwenye sh. 480. Sisi tuna bandari, hata sukari ya nje tunauziwa 2500. Wizi mtupu! Ee bwana tenda miujiza tu!
 
Back
Top Bottom