Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

Kwa hii taarifa yako mkuu, basi uduni wa maisha tulionao watanzania ni wa kujitakia wenyewe, tena kwa kuukumbatia kwa mapenzi makubwa kiasi cha kushindwa kuihukumu CCM kupitia sanduku la kura. Hakuna maendeleo ya maana hapa Tanzania mpaka kuwe na mabadiliko ya maana katika serikali inayotawala.


ni wakujitakia mkuu tena kwa asilimia zote....
 
Walahhi tenah! Mi na nyinyiemu 2015, mungu aendelee kumpa nguvu mheshimiwa rais, Dr. Wilbroad Slaa..AMeN
 
ooh man JF is back....well analytical and constructive thread ever
 
Nazdi kupata hasira na serikal ilioko madarakan! 'wananchi wasiopiga kura ndio wanaowachagua viongoz wasiofaa' lazma 2badilike jaman
 
Salma kwa uchambuzi na utafiti ulofanya una haki ya kusema ulosema hasa kuwa bei ya cement yaweza shuka hadi chini ya 5,000/- ya Ki-TZ. I salute you and you deserve my (our) respect!!! Wewe ni GREAT THINKER...!!!

Viongozi mlo madarakani endeleeni kubisha tu ila ipo siku mambo yatageuka na watakuja watu makini washike serikali na ndo wata-prove kuwa inawezekana na nyie kama mtakuwa hai au wana wenu watakuja ona aibu kuwa why nyie mlitunyonya na kutukandamiza watanzania kwa maisha magumu na nyie ndo muishi kwenye maisha bora kwa kila mnyonyaji na Fisadi!!

Mtu mmoja nilisoma kitabu chake nikiwa shule enzi hizo, alimsimulia mtu mmoja aitwaye Rashidi kama sikosei ambaye alikuwa Kuli bandarini...kwa shida alizo kuwa anazipata alihitimisha hivi..."YANA MWISHO HAYA".

So hata ufisadi ulokubuhu nao Una mwisho wake na OLE WENU MAFISADI NA WANYONYAJI WOTE WA TAIFA HILI...Wakati ukifika Mtalia na kusaga meno....
 
Halafu hiyo hesabu yako mfuko mmoja ni shillingi ngapi? ukiweka gharama za usafiri wa meli (zilizo sawa, hiyo ya dola 400 kwa container la futi 40 ni porojo), gharama za bandari? usafiri wa nchi kavu? gharama za kuhifadhi (storage)? gharama za kuuza (sales cost)? kwi kwi kwi teh teh teh, bado ni elfu tano tu kwa mfuko? sasa wewe mbona juu huko kwa gharama porojo na unauza 10,000 kwa mfuko? umempita bei Slaa kwa 100%, sasa nani porojo zaidi wewe, au yeye?
 
Mambumbu ni wengi sana Tanzania, wanasifia uongo! hizo ndio shule za kina mtakatifu. Tukiwaambia mnasaidiwa na NECTA mnakataa, mmeshazitazama hizo hesabu za bi Salma lakini au mnachekelea kama misukule tu?
 
Dada naomba ruhusa niprint utafiti huu niusambaze mtaani kwa gharama yangu nikuatribute tafadhali.
 
Hongera sana kwa uchambuzi makini, wacha Kigoda na serekali wasome labda wataelewa pia TBC wanaweza kukanusha makala zao
 
asante mkuu kwa info,,,,,,,,hatuna utashi kwa vile hatuna uzalendo,,,,chadema valien njuga mambo haya,,,kampen futa nyumba za tope na nyasi tz au op makazi bora,,,
 
Ubaya ni kwamba ndugu zetu wakina Nape huwezi kuwaona huku waki reason kwa issue badala ya propaganda.

Wakina rejao wao wanajua mambo laini laini tu!
 
Mheshimiwa, kwa maana iyo ni nafuu zaidi kuagiza contena la cement toka nje kwaajili ya ujenzi kuliko kununua hapa nchini..kama option hii ipo kwann tuna endelea kung'ang'ana na cement za hapa nchini au serikali inakata kodi ya juu mno kwenye iyo
 
Uchambuzi mzuri sana, na ni kweli hilo linawezekana kabisa
na kwa kuongezea tu, bei inawezaje kuwa sawa nchi zima? yaani kama Dar ni 5000 basi na Kigoma, Lindi na Shinyanga bei inakuwa hiyohiyo ya 5000tsh

Kwa nchi zenye kujali raia wake na kuwapunguzia kasi ya ugumu wa maisha, utaratibu unaotumika ni wa kuwapa punguzo la kodi na kuwashushia bei ya mafuta kwa wasafirishaji wote wanaopewa tenda ya kusafirisha hiyo cement kwenda mikoa husika, mwenye roli anayepeleka cement Morogoro anakuwa na kiwango chake cha kodi na bei yake ya mafuta ambayo itakuwa juu kidogo kuliko ya yule anayepeleka Kigoma ama mwanza, utaratibu huu unasaidia sana kwa kuweka uwiano sawa wa bei kwa nchi nzima
 
Yawezekana kama viongozi wetu wataacha ulafi uliopitiliza. Wamekula wameshiba bado wanajitapisha ili waendelee kula huku wananchi wa kawaida wakiteseka kwa njaa na umasikini uliokithiri. Hawana aibu kabisa wameshatufanya misukule yao wao na familia zao wakineemeka kwa jasho letu.AIBU YAO MILELE
 
Mkuu kwanza nashukuru kwa shule kubwa uliyotupa.., Mimi naamini kabisa kila kitu kinawezekana ila kama unavyosema TZ kila kitu ni Udalali ambao unaanzia kwa waziri hadi watendaji wa chini.

Mfano the same inatokea kwenye Sukari, Unga nk...

Tufike mahali kama Dr Anasema inwezekana Mfuko wa Cement kuwa 5000/=, Elimu Bure, Afya Bure etc Tumpe hii Nchi atuonyeshe the wengine wafuate... Tatizo hapa ni CCM na Mafisasi wanatumia sana Pesa ili kupotosha ukweli huu...

Mimi namwamini sana huyu Mzee... Nakumbuka Mara ya kwanza wakati anagombea ubunge kule Karatu alisema... Kusambaza maji viji vyote vya Karatu inawezekana, Kupunguza kodi ya kichwa kutoka 5000 hadi 2000 inawezekana, Wanafunzi wa karatu kusoma bure inawezekana, Kila kijiji kuwa na Dispensary inawezekana... Wakati jamaa wa CCM anahubiri maji hakuna TZ nzima si karatu tu...

Watu wa Karatu wakaona isiwe taabu.. Wakampa Ubunge pamoja na halimashauri... Unajua alifanyaje? Kwanza alifuatilia kodi ya kichwa inakusanywa kiasi gani kwa mwaka, akakuta zaidi ya 80% inatumika kwenye process ya ukusanyaji.

Simply akasema kama atatengeneza kodi ndogo ambayo watu watailipa wenyewe then amemaliza Kazi ndiyo ikawa 2000/= na 500/= kwa ajili ya kuwasomesha wanafunzi kutoka olevel hadi Alevel.

Badala yake wakazi wa Halimashauri zinazoizunguka Karatu wakawa wanalipa kodi zao Karatu. Mapato yakawa mengi ndiyo CCM wakaamua kuifuta.


Sasa ni muda wa kuangalia tusichague tena hawa wazee wa mades tuchagu Rais mwenye IQ, I mean Ram, HDD pamoja na Processor speed kubwa ambaye si Rahisi kumdanya sikufichi hata mchwa na vipandikizi Pale CDM vinashindwa kufanya kazi pale CDM kwa sababu ya huyu Mzee.

Mtu mwingine ambaye namkubali ni Freeman Mbowe huyu bwana anastahili kuwa kwenye nafasi ya Juu maana hata Nyerere alijua hili kabla hajafariki, IQ yake ni kubwa huwezi kukuta mahali ukawakusanya interlectuls kama alivyofanya kule marekani then ukawaambia nataka tufanye QA session kwa maana yeye atoe maelezo then wao wamwuulize maswali na majibu na tumeona ameweza kuwa convince wote na badala yake sasa ni balaa tupu CCM wanahaha.
 
Back
Top Bottom