Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 301
Maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam jana walijitokeza kumlaki mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilibroad Slaa, ambaye wakati akihutubia wananchi pamoja na mambo mengine, ameahidi kuanza mchakato wa utengenezaji wa katiba mpya ndani ya miezi minne kama atapewa dhamana ya kuongoza nchi.
Dk. Slaa ambaye hadi jana asubuhi alikuwa ameshadhaminiwa na Watanzania 1,397,757 kutoka mikoa 20 Tanzania Bara na Visiwani, alikuwa akitokea Zanzibar alikokwenda kutafuta wadhamini, akiwa ameambatana na viongozi wakuu wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, ambapo aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere majira ya saa 6:50 mchana na baadaye kuhutubia umati mkubwa wa wananchi waliojitokeza kumsikiliza katika viwanja vya Jangwani.
Wakati akitoa hutuba, Dk. Slaa alisema kero nyingi zinazoikabili nchi kwa sasa zinatokana na Katiba ya nchi kuwa na kasoro nyingi na kwamba iwapo itaandikwa upya kwa kuzingatia matakwa ya wananchi wengi, itasaidia kutatua kero hizo.
"Siku hizi kila mahali ni foleni, ukienda polisi ni foleni, mahakamani, benki, barabarani kote ni foleni huku chai ya 'wakubwa' kwa mwaka inagharimu zaidi ya bilioni 30, wabunge wanapandishiwa mishahara kila siku na kulipwa posho kubwa wakati mwananchi wa kawaida akiteseka kwenye lindi la umaskini, hizi ni kero zinazohitaji ufumbuzi wa haraka," alisema Dk. Slaa na kushangiliwa.
Dk. Salaa, ambaye alihutubia kwa takribani dakika 40 kuanzia saa 12:03 jioni, alisema Tanzania inahitaji viongozi watakaoweza kupanga matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo ili zinufaishe umma badala ya kuwanufaisha wachache huku wengi wakiumia.
Kwa wakati wote ambao Dk. Slaa alikuwa akihutubia wananchi walikuwa wakimshangilia kwa kumwita 'Rais, Rais' jambo lililokuwa likimlazimu kukatisha hotuba yake kila mara.
Awali, Mbowe alisema Chadema kinamuunga mkono Maalim Seif Hamad Sharif ambaye anawania Urais kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF) visiwani Zanzibar.
Alisema kuwa chama hicho hakitasimamisha mgombea urais kwa upande wa Zanzibar na kwamba wafuasi wake watampa kura za urais Maalim Seif. Hata hivyo, alisema Chadema kitasimamisha wagombea wa ubunge na uwakilishi visiwani humo ili kuweka nguvu ya upinzani ndani ya Baraza la Wawakilishi.
Hata hivyo, alisema Chadema haiungi mkono uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar kwa maelezo kwamba uundwaji wake hautamaliza siasa za chuki visiwani humo.
Kwa upande wa Bara, alisema chama hicho kimeshindwa kuungana na vyama vingine kwa kuwa baadhi ya vyama vya siasa vimekuwa vikifanya mzaha kwa kushabikia CCM.
Alisema katika uchaguzi wa mwaka huu, Chadema kitapambana ipasavyo ili kuhakikisha kinapata ushindi na kueleza kwamba wamechoshwa na wizi wa kura aliosema umekuwa ukifanywa na Chama Cha Mapinduzi.
"Chadema tumeamua kumuunga mkono Maalim Seif kule Zanzibar lakini tutasimamisha wagombea ubunge na uwakilishi wa Baraza. Kwa upande wa Bara, nadhani wote mnafahamu kwamba tunavyama 17 vya siasa, vya kweli na vya mzaha. Hatuwezi kuungana na vyama vinavyocheza ngoma ya CCM," alisema na kuongeza "Haki ya Mungu, ama zao ama zetu...lugha ya kusema tumeibiwa kura mwaka huu tutaiacha. Chadema tunapenda amani lakini mwaka huu ikibidi na sisi tutaiba kura, tumechoka."
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Said Arf, alisema afya ya Dk. Slaa ni imara na kwamba anaweza kufanyakazi bila tatizo lolote hivyo kuwaomba wananchi wamchague kuwa rais wakati wa uchaguzi. Alionya kwamba chama hicho hakiwezi kugawanywa na propaganda ya udini ambayo imeanza kunadiwa na wapinzani wao wa kisiasa wanaodai kwamba Dk. Slaa ni chaguo la Kanisa Katoliki.
Wakili wa maarufu nchini, Mabere Marando, ambaye ni miongoni mwa mawakili wanaowatetea watuhumiwa wa wizi wa EPA, alisema washtakiwa waliofikishwa mahakamani ni matawi na kwamba CCM haitaweza kuwakamata watuhumiwa wakubwa.
Alisema kuwa watuhumiwa waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa EPA ni watu wadogo, lakini vigogo waliohusika hawajachukuliwa hatua yoyote na kwamba ushahidi anao.
Hata hivyo, akisoma dua ya kufungua mkutano huo, Sheikh Said Mwaipopo, alisababisha wananchi kushangilia katikati ya swala alipomwomba Mungu awadhalilishe wezi wote wa rasilimali za nchi.
Aidha, msafara wa Dk. Slaa ambao uliwasili uwanja wa ndege wa zamani majira ya saa 6:50 mchana, ulikuwa ukisimama kila wakati njiani wakati ukielekea Jangwani, kutokana na magari ya wananchi kuingilia jambo lililoibua mgogoro baina ya vijana wa usalama wa Chadema na askari wa usalama barabarani, katika mataa ya Tazara.