Dr. Slaa, Mbowe wanguruma!

Status
Not open for further replies.
Anga lote limechafuka kwa press conference.
Lakini ndo tunazidi kuelimika ivo
twasubiria audio tukate ishu
kamata tano robot
 
Patiently waiting for the audio..coz jana Malecela wasted my time and that of the waandishi! Angekuja tu jf nakutoa maoni yake..the talk wasnt worth any media house airtime.
 
- Wamtetea Dk. Mwakyembe katika sakata la umeme
- Wamshukia vibaya Rostam...

Zaidi naja kukupasheni... Looking for the Audio version of this(these) Press Conference(s)

Hiyo conference wangeitisha wakiwa pamoja na Mh. Zitto.....sipati picha ingekuwaje hapo.....!
 
Na Mwakyembe nasikia ameamua kuwatolea uvivu kabisa... liwalo na liwe.. Sasa kina Mbowe hawakumsikiliza mzee Malecela jana? Kasema malumbano yakome, mbona hayakomi!! maana nasikia kuna msurururu wa mikutano ya waandishi sitoshangaa kesho ikawa "double dose"
 
Ni kuwa, kuna wanachama 12 ambao wamesimamishwa ama tuseme "Wamefukuzwa" uanachama na CHADEMA.

Inaelezwa kuwa hawa ni wale waliokuwa wanaendesha kampeni chafu dhidi ya chama chao ambao kwa namna moja ama nyingine wamekiri kuwa walikuwa financed na Guninita na wawili kati yao walikuwa planted na UwT.

Still searching for the audio version
 
Na Mwakyembe nasikia ameamua kuwatolea uvivu kabisa... liwalo na liwe.. Sasa kina Mbowe hawakumsikiliza mzee Malecela jana? Kasema malumbano yakome, mbona hayakomi!! maana nasikia kuna msurururu wa mikutano ya waandishi sitoshangaa kesho ikawa "double dose"

Si unajua siasa za Tanzania? ni malumbano kwa kwenda mbele. 2010 imekaribia tutayasikia mengi sana!!
 
Na Mwakyembe nasikia ameamua kuwatolea uvivu kabisa... liwalo na liwe.. Sasa kina Mbowe hawakumsikiliza mzee Malecela jana? Kasema malumbano yakome, mbona hayakomi!! maana nasikia kuna msurururu wa mikutano ya waandishi sitoshangaa kesho ikawa "double dose"
Yaah,

Lakini nimebahatika kuongea na mmoja wa watu wa ndani wa chama hicho, anadai wameshtuka kuona Press Conference ya Dr. Slaa inahudhuriwa na waandishi 62 kitu ambacho si cha kawaida
 
Mzee Mwanakijiji & Invisible,
Nafikiri huu sio tena wakati wa kutoa press conferences maana hazisaidii upinzani kabisaa. Hizi zinawaumiza zaidi CCM na ndio maana Malecela akawakataza wanaCCM wasizitumie na sio wapinzani.

Wapinzani inatakiwa sasa tuanze kuchukua hatua ngangari zaidi za kumuondoa au kummaliza nguvu Kikwete kama maandamano, migomo, mikutano ya hadhara n.k.

Hii ndio njia pekee iliyobaki maana kama tulivyomsikia Mzee Malecela ameshaeleza kuwa Kikwete anachoogopa ni upinzani ndani ya CCM na sio nje yake.
 
sina hakika wamezungumza kama msimamo wa Chama au wao wenyewe tu...as kama tulivyoona huko kwa Zitto na Lipumba...!!!

Kwanini Chadema au CUF kwa umoja au kwa ubinafsi wao wasicome up na alternative Plans za Power crisis...then watafute misimamo yao on the mjadala wa "Ki-Maslahi" unaoendelea sasa!!!!
 
Kama Mbowe na slaa wako kwa mwakyembe, where is Zitto??
Issue ya Zitto Dr. Slaa kairuka, kasema Bunge limekwishatoa 'statement' yake dhidi ya Dowans na wala asingependa kugusia hilo.

Suala la RA alikuwa akimjibu mwandishi ambaye alimwuliza anamwongeleaje RA, yeye akawambia waandishi kuwa yeye kishaieleza Serikali kuwa RA si safi na akasema yeye ni mmojawapo katika "list of shame" na alipendekeza afikishwe mahakamani na serikali ni kama inamwogopa ama inamkingia kifua.
 
Niweke rekodi ili wachangiaji waweze kujua kilichozungumzwa na kimezungumzwa wapi.

Tangu jana CHADEMA wamekuwa na Kamati Kuu ya chama TAIFA na leo wanaendelea na kikao cha Baraza Kuu la Chama Taifa.

Hivyo basi kutokana na mikutano hiyo Kamati Kuu jana ilifanya maamuzi mengi juu ya mwelekeo wa chama na Taifa kwa ujumla.

Ni kweli jana wanachama 12 wa chama walifukuzwa uanachama kutokana na ripoti maalum iliyokuwa imetokana na KAMATI NDOGO YA KAMATI KUU iliyoundwa mwaka jana mwezi wa kumi na moja ikiwa inaongozwa na mwanasheria mahiri mzee Bob Makani.

Wajumbe wengine wa kamati hiyo walikuwa ni pamoja na ;
Prof.Baregu, Mustafa Akoonay ambaye ni wakili wa kujitegemea na mjumbe wa kamati kuu, Edson Mbogoro mwanasheria wa kujitegemea kutoka Ruvuma,Mama Chiku Abwao .

Makatibu wa kamati hiyo walikuwa ndugu Tundu Lissu akisaidiana na Halima Mdee.

Baada kazi ya kamati hiyo walifulkuzwa wanachama 12 ambao walikuwa wakijiita wanachama wa Dar es salaam huku wakuwa wanatumiwa na CCM kukivuruga chama.

Mtakumbuka pia kuwa wakati wa mchakato wa uchaguzi Tarime hawa jamaa ile wiki ya mwisho waliandamana kupinga chama kushiriki uchaguzi Tarime kwa hoja kuwa kilihusika kumuua Wangwe.

Kuhusu Rostam.
Leo Dr.Slaa kaamua kuuvunja mzizi wa fitna pale alipoweka wazi kile ambacho kinaendelea kati ya Rostam , Mwakyembe e.t.c kwa kuweka ukweli hadharani juu ya kampuni ya kuzalisha umeme ambayo inamilikiwa na Rostam inaitwa PE (POWER ENERGY).

Kampuni hii inalitaka eneo la kijiji kinaitwa Kisasida , na kampuni ya Rostam inamilikiwa kwa ubia wa yeye pamoja na Lowassa , na ndio maana utaona jinsi ambavyo mkuu wa mkoa wa Singida alikuwa mstari wa mbele kuibeba kampuni hii ya Rostam na Lowassa .

Hili limepelekea CHADEMA kumfikisha mkuu wa mkoa mahakamani na tangu jana alishapelekewa barua ya kusudio la kuburuzwa mahakamani baada ya kumtukana mwenyekiti wa kijiji hicho pamoja na viongozi wa CHADEMA kwenye mkutano wa hadhara.

Kampuni hii ya PE na ile ya wakina Mwakyembe wako kwenye kupigania kupata eneo kwenye kijiji hicho.

Mengine nitawaeleza zaidi baadae.
 
Sasa mbona nilisoma kuwa akina Mwakyembe wameuza hilo eneo kwa Wakorea? Au hilo ni eneo jingine? Ama kweli hapa mmoja anadanganya au mie nimeachwa Solemba!!
 
Sikonge eneo linaitwa kijiji cha KISASIDA kipo wilaya ya singida mjini , ndio hapo hapo kamapuni ya wakina Mwakyembe na Rostam wanataka kupata eneo.

Kuhusu hii ya wakina Rostam , ukweli ni kuwa Rostam aliiba mradi huu kwa watanzania ambao walifanya utafiti kuhusu kuzalisha umeme wa upepo , lakini walipoanza harakati za kutafuta pesa baada ya study yao kufanyika walijikuta wanaangukia mikononi wa Rostam , ndipo alipowaambia kuwa kama wanataka wanapaswa kusajili kampuni mpya ili awape pesa , na aligoma kutoa pesa kwenye ile ya awali ambayo sasa inamilikiwa na wakina Mwakyembe.

Mwakyembe kusikia wameenda kuchukua pesa kwa Rostam , ndipo alipowaeleza wenzake wazi kuwa hatapenda kuwa sehemu ya mradi huo na wao kwa kuwa wametoka wote eneo moja waliamua kumtii na kujitoa kwenye mikono ya Rostam na ndipo alipoamua kuendelea na mapambano kwa ajili ya kuhakikisha kuwa anazalisha umeme yeye kwenye kijiji hicho.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom