Elections 2010 Dr Slaa: Live Dodoma leo saa 10.00 alasiri!

minda

JF-Expert Member
Oct 2, 2009
1,068
65
dk slaa anasubiriwa na umati wa watu hapa mjini dodoma kwenye viwanja vya barafu, vinavyopakana na uwanja wa jamhuri; uwanja uliokuwa mali ya mlipa kodi wa nchi hii ukapokwa.

inesemwa ya kwamba dk ws atawasili hapa majira ya saa 10:00 alasiri akitokea iringa.


nusu saa iliyopita nilikuwa hapo uwanjani nikashuhudia haya:

  • umati wa watu ni mkubwa sana na hasa vijana.
  • kuna malalamiko kuhusu kununuliwa kwa bendera za chadema kwa gharama kati ya sh.2000 hadi 10000 na watu ambao mshereheshaji anawaita mafisadi (unawajua!!!).
  • wagombea udiwani wa kata mbali mbali wamepata nafasi ya kuwasalimia wananchi na kuomba kura kwa chadema.
  • msisitizo umeelekezwa kwenye AMANI; ambapo wananchi wameombwa na wagombea, viongozi wa chadema na mshereheshaji kutokuwa chanzo cha machafuko.
  • eneo la upande wa magharibi (uwanja wa jamhuri) na kusini kuna bendera za ccm.
  • magari ya mashabiki wa ccm yanapita mara kwa mara yakifungulia sauti ya juu wimbo wao ule maarufu wa wa kuwachanachana watanzania wazalendo wanaoamua kujiunga na vyama vya upinzani kwa mujibu wa sheria za nchi hii.
  • kuna umati wa wapanda baiskeli na wale wa pikipiki zenye bendera ya chadema.

nawasilisha!!!
 
Mkuu safi sana, endelea kutupa habari, kama unaweza kutuwekea picha tuwekee mkuu. Hizi ndo lala salama. CCM bye byee, see you in the hell.
 
Minda tunaoomba picha mkuu, kazi yako ni nzuri sana, huo ni mji mkuu picha ni mhimu sana
 
Mkuu tunaomba picha si kwamba hatukuamini, hapana tunataka kuweka kumbukumbu kuwa haya yanayotokea
 
Mi sina la ziada ila nanukuu kama ifuatavyo"slaa ndiyo mpakwa mafuta wetu.ndiye aliyempendeza bwana mungu tumsikilize yeye"
 
CCM lazima wapite na vipaza sauti kwa uchokozi tu ktk mikutano ya CHADEMA, ni kweli CHADEMA lazima wawe waangalifu maana uchokozi wa CCM sasa upo waziwazi ili kutafuta shari. Safi Mkuu tupo pamoja. akianza kuhutubia turushie walau picha mbili tatu.
 
Kikwete na kundi lake wanajitahidi kufuta kile wanachoita nyayo za Slaa, sasa afuate NYayo hizi vyema, Toka Dar, Lindi , Mtwara , Dodoma, Mbeya na wilaya zake , na kumalizia MKUTANO WA MWISHO PALE KWA MR 2 , SUGU MBEYA MJINI, Aje nyuma, ataliwa na manyigu
 
Kikwete na kundi lake wanajitahidi kufuta kile wanachoita nyayo za Slaa, sasa afuate NYayo hizi vyema, Toka Dar, Lindi , Mtwara , Dodoma, Mbeya na wilaya zake , na kumalizia MKUTANO WA MWISHO PALE KWA MR 2 , SUGU MBEYA MJINI, Aje nyuma, ataliwa na manyigu
afya yake ya mgogoro hawezi...
 
sasa na hao ccm wanajipitisha nini hapo yani wasione kichaka...nnya inawabana!!!
asante minda kwa updates
 
Back
Top Bottom