Elections 2010 DR.Slaa Kuunguruma Jangwani Kesho tarehe 07/08/2010

Mimi nilikuwa kwenye mkutano. Sikuwa na network huko. Ila mambo yalinoga kweli kweli.

Kwa taarifa yenu, Slaa kapata wadhamini zaidi ya milioni 1.3; na zoezi bado linaendelea. Mahali kama Zenji wamepata wadhamini elfu chache tu. Lakini sio mbaya, kwani minimum ni mia mbili kila mkoa. Nami nimejiandikisha leo kuwa mmoja wa wadhamini.
 
Ndiyo maana mwandishi wa habari hizo kaandika Moshi mjini, Mbeya mjini, Mtwara na Songea mjini!!!
Sijaona neno vijijini.

I hear you ,lakini mimi naona wangekuwa wanaenda kila kiiji labda mpaka sasa wangekuwa bado mkoa mmoja au ww unaonaje.
Labda kipindi cha kampeni wajaribu kwenda vijiji zaidi kwa kuwa muda utakuwepo kiasi.
 
Ndiyo maana mwandishi wa habari hizo kaandika Moshi mjini, Mbeya mjini, Mtwara na Songea mjini!!!
Sijaona neno vijijini.
Unataka kila kijiji wanachopita wakipige picha halafu wakutumie wewe vipi, hata rais huwa haletewi picha za vijiji vyote.
 
Mimi nilikuwa kwenye mkutano. Sikuwa na network huko. Ila mambo yalinoga kweli kweli.

Kwa taarifa yenu, Slaa kapata wadhamini zaidi ya milioni 1.3; na zoezi bado linaendelea. Mahali kama Zenji wamepata wadhamini elfu chache tu. Lakini sio mbaya, kwani minimum ni mia mbili kila mkoa. Nami nimejiandikisha leo kuwa mmoja wa wadhamini.

Mkuu, kuwa mkweli na hali halisi ya jangwani leo ukifananisha ni mikoani ambako watu walikuwa wanakuja kushangaa kwa kuwa hawana kazi za kufanya muda huo Slaa anajipitisha! Elezea hali halisi ya Zenj na mustakabali wa Urais wa Slaa. Be straight to the point na nadhani ndiyo maudhui ya JF. Ndiyo ukweli na uwazi ambao tunautegemea. Hamna campaign hapa kwani wote tuko macho,,, noma!
 
This is one of the most strange posts I have ever seen here in the forum. Yaelekea CCM maji ya shingo.
 
Mkuu, kuwa mkweli na hali halisi ya jangwani leo ukifananisha ni mikoani ambako watu walikuwa wanakuja kushangaa kwa kuwa hawana kazi za kufanya muda huo Slaa anajipitisha! Elezea hali halisi ya Zenj na mustakabali wa Urais wa Slaa. Be straight to the point na nadhani ndiyo maudhui ya JF. Ndiyo ukweli na uwazi ambao tunautegemea. Hamna campaign hapa kwani wote tuko macho,,, noma!
Mwaka huu hadi kieleke hakuna kulala, wewe huzijui siasa za zanzibar mwambie Kikwete aende Pemba kama hataambulia rangi ya kijani tupu tena walioletwa kwa chai maharage.
 
Yaani, bado tupo tupo sana mzee.
Hata mimi naona kweli mpo mpo tu kama hamupo hakuna la maana mnalolifanya likaonekana, eti tunaambia CCM imejichimbiwa sijui mstuni si waseme tu wamejichimbia kaburini kwani nani hajui, kanyaga twende chadema hakuna kulala.
 
Hata mimi naona kweli mpo mpo tu kama hamupo hakuna la maana mnalolifanya likaonekana, eti tunaambia CCM imejichimbia sijui mstuni si waseme tu wamejichimbia kaburini kwani nani hajui, kanyaga twende chadema hakuna kulala.

Quinine
CCM hakuna kitu. Ni chama kilichooza; ila tu kinapumua kwa nguvu ya dola.
 
Hata mimi naona kweli mpo mpo tu kama hamupo hakuna la maana mnalolifanya likaonekana, eti tunaambia CCM imejichimbiwa sijui mstuni si waseme tu wamejichimbia kaburini kwani nani hajui, kanyaga twende chadema hakuna kulala.

Let me put it in clearer fomat. CCM ipo mpaka kizazi cha sasa hivi cha JF kitakapokuwa hakipo. Yaani ipo sanaa. Take my words, I will back with the same words in November 3rd 2010.
 
Mimi ni mpemba
Wewe mpemba mwangalie rais wako anakusalimia

chadema8.jpg
 
Huyu bwana Slaa. Disqualification zake:
1. kwanza alikuwa padre, akahasi. Hiyo ni dalili kubwa sana ya udhaifu. Anaweza uza nchi huyu kwa kuwa hana msimamo.
2. Alikuwa CCM, mpaka leo sisi tunajua tuko naye. Alipogigwa chini 1995 akahamia upinzani. Siyo mpinzani halisia. Mkewe anataka kufuata hiyo.
3. Analalamika kuhusu mishahara midogo ya waalimu, yeye hatuwahi sikia amechangia chochote kwa lolote katika maendeleo ya popote
4. Sidhani kama mtu yoyote hapa JF akipata file chafu akaenda mwembeyanga kutangaza, tukamwona safi kuanzia siku hiyo. Usafi ni tabia.
5. Huyu ana nyumba ndogo lukuki kila sehemu, disqualification kubwa sana. Dodoma ana wanawake watano.
6. Security-wise, baadhi ya mambo hata senators wa US hawawezi sema. He is incompetence. Tutamnyung'unyiaa hapo
7. Alikuwa hana mpango wa Urais. Amelazimishwa. Urais siyo wa kulazimshwa. Ni plans za miaka mingi. Anaweza tuyumbisha huyu
8. Watu alionao ni wachafu sana,, hatutegemei mtu kama yeye akawa na watu wa namna hiyo.
9.Anyway, hakuna room inaitwa "President from chadema this year".
10. Too late to do anyrthing.

Mungu Ibariki Tanzania. Mungu wape hekima watu wake waweze jua wanalofikiria
 
Pole sana na maumivu, hakuna lolote ulilosema hapo wote ni umbea tupu, kajiandae tena uje, mbwabwajaji mkuu wenu Makamba kanywea hana hata moja kwa Dr. wewe ndo utaweza, fisi kaushindwa mfupa wewe utauweza?
 
Huyu bwana Slaa. Disqualification zake:
1. kwanza alikuwa padre, akahasi. Hiyo ni dalili kubwa sana ya udhaifu. Anaweza uza nchi huyu kwa kuwa hana msimamo.

Hujui ni kwanini aliomba kuacha upadre. Unajua maana ya kuasi? Yeye aliomba kuacha daraja la upadre, mtu anayeasi huwa anaondoka bila kuaga au kutoa taarifa. Yeye alifuata taratibu zote zinazotakiwa.

CCM ndio waliouza nchi, nenda kwenye hifadhi za wanyapori vitalu vyote wameuziana wenyewe na vingine wamegawa kwa wazungu.

2. Alikuwa CCM, mpaka leo sisi tunajua tuko naye. Alipogigwa chini 1995 akahamia upinzani. Siyo mpinzani halisia. Mkewe anataka kufuata hiyo.

Kama mnajua mko nae kwanini anawaumiza vichwa na ilihali ni mtu wenu. Kosa la kumpiga chini mpaka leo hii linawatesa CCM na amebaki kuwa tishio kwao miaka yote.

3. Analalamika kuhusu mishahara midogo ya waalimu, yeye hatuwahi sikia amechangia chochote kwa lolote katika maendeleo ya popote

Nenda Jimboni kwake ukaone jinsi alivyochangia maendeleo ya Jimbo lake. Yeye alikuwa Mbunge wa Karatu so mchango wake wa maendeleo uko Jimboni kwake. Pamoja na hayo, hakuishia huko bali pia alikuja kuwatumikia wananchi wote kwa kufichua ufisadi ambao ulikuwa umefunikwa na serikali ya CCM. Kama siyo Dr. Slaa CCM wangekuwa wanajiandaa kuchota EPA nyingine BoT na wala wasingekuwa na wasiwasi na hela ya kampeni.

4. Sidhani kama mtu yoyote hapa JF akipata file chafu akaenda mwembeyanga kutangaza, tukamwona safi kuanzia siku hiyo. Usafi ni tabia.

Wenzako walipewa wafanye kazi ya Richmond, wakafanya nusu. Yeye akipata credible information anaifanyia kazi mpaka mwisho. Muulize Spika wako Mzee Sitta aliyedai kwamba viambatanisho vya tuhuma za ufisadi vilikuwa vya kughushi, akapeleka polisi ili wachunguze, mpaka leo hakuna feedback, sana sana ni swala la kuibuka kwa EPA na akina Mama Meghji kumwaga sembe.

Unajua kama mtu ni mchafu hawezi kuwa na jeuri ya kumnyooshea kidole mtu mwingine. Ndiyo maana waziri Sofia Simba alisema ndani ya CCM hakuna msafi hata mmoja, wote ni wachafu. Kwa hiyo wasinyoosheane vidole. Kama Dr. Slaa angekuwa na madudu angeishapelekwa mahakamani siku nyingi sana.

5. Huyu ana nyumba ndogo lukuki kila sehemu, disqualification kubwa sana. Dodoma ana wanawake watano.

Hayo ni maisha binafsi ya mtu, pamoja na hayo inaweza kuwa ni uzushi. Labda tukuulize wewe kwamba kulikoni Mkuu wa Kaya kila siku anajitetea kwamba hajaoa mke mwingine na ilihali kwenye magazeti kuna habari hizo? Kama ni habari za uzushi, kwanini haendi mahakamani kufungua kesi za madai ama kupeleka malalamiko ili magazeti hayo yafungiwe?

Ukianza kuongelea nyumba ndogo, hakuna kiongozi wa CCM kuanzia ngazi za juu na serikalini ambaye atasimama na kuonyesha usafi/uadilifu wake. Kwa hiyo kwenye hiyo angle itakula kwenu maana uchafu huo ni mkubwa sana ndani ya CCM na serikalini. Ndiyo maana ukipeleka hiyo hoja huwa inapigwa majibu ya kiswahili.

6. Security-wise, baadhi ya mambo hata senators wa US hawawezi sema. He is incompetence. Tutamnyung'unyiaa hapo
Mambo yepi? Hawasemi mambo yanayogusa usalama wa nchi yao, lakini kama kuna ufisadi kwenye deals za majeshi watasema. Kama kile anachosema Dr. Slaa kingekuwa kinahatarisha usalama wa taifa, sasa hivi angekuwa gerezani siku nyingi. Hakuna mahakama inaweza kumfunga kwa kusema kile ambacho kina maslahi kwa nchi na wapiga kura wake na ndiyo maana hata yale madudu ambayo serikali inaita ni SIRI yeye anayo na anatembea nayo na alimwambia Mh. Pinda aende kumshika maana ana manyaraka kibao yenye nendo ya serikali na mhusi wa SIRI.

7. Alikuwa hana mpango wa Urais. Amelazimishwa. Urais siyo wa kulazimshwa. Ni plans za miaka mingi. Anaweza tuyumbisha huyu

Ni kweli hakuwa na mpango wala wazo, ni wananchi wenye uchungu na nchi hii ambao wamemuona ana uchungu na nchi yake ndio waliomuomba, hawakumlazimisha. Mipango ya muda mrefu hiyo ndio ilituletea mafisadi ambao bado tunao mpaka leo. Mkapa alipochukua fomu hakuna aliyetegemea kwamba angepita na hakuwa amefanya maandalizi yoyote. Kwani unajiandaa ili uandae mafisadi ili ukichaguliwa waje waifisadi nchi?

8. Watu alionao ni wachafu sana,, hatutegemei mtu kama yeye akawa na watu wa namna hiyo.

Uchafu wao ni nini? Hivi kuna watu wachafu kama vigogo wa CCM? Ufisadi umewazunguka kila kona, hakuna ufisadi unafanyika bila kuona majina yao na hao ndio vipenzi wa JK na ndio waliomzunguka.

Tafuteni hoja nyingine za kum-disqualify Dr. Slaa na siyo hizi ambazo hazina mashiko.
 
Back
Top Bottom