Dr. Slaa kutikisa Shinyanga kesho.

Status
Not open for further replies.
Kiongozi wa Upinzani nchini Dr Wilbroad P.Slaa kesho anatarajiwa kuunguruma mkoani Shinyanga.Kiongozi huyo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA atatikisa katika mkutano wa kumnadi mgombea Udiwani wa CDM katika kata ya Mwawaza.
Habari za awali zinasema kuwa baba mzazi wa mgombea udiwani wa CDM anatarajiwa pia kupanda jukwaani kuelezea jinsi alivyohongwa ili amsingizie mwanae ni mwizi katika moja ya mikutano ya CCM.
Kuna shamrashamra kubwa hapa Shinyanga kuashiria ujio wa kiongozi huyo mashuhuri nchini.Mpaka sasa tathmini za awali zinaonyesha CDM ina uwezo wa kushinda kata hiyo kwa idadi kubwa ya kura.

Yaan yale ya A.Masharik yanatokea tena Shy, hawa magamba kweli wameishiwa badala ya kushindana kwa hoja wao rushwa.
 
Molemo, Jasusi, Pasco, Mzee Mwanakijiji,

..hivi Dr.Slaa a.k.a kibabu ana matatizo gani yeye haendi ulaya na marekani kufungua matawi kama wenzake? naona kizee hiki na shuka lake kimengangania hapahapa bongo tu nje hakitaki kwenda. au kinaogopa kupanda ndege??

Waulize CCM katibu wao Mukama yupo upande gani Ndani ya nchi hasikiki wala haonekani na hata huko nje haonekani wala hasikiki.
 
Huyu Dr. Bunduki/ Slaa mwanzoni nilisikia Geita leo tena nasikia Shinyanga, Geita ilikuwaje?. Huyu mzee naye kweli akipanda jukwaani kwa sera kama hii na akapigiwa makopi asifikili kaongea point bali atakuwa anazihakiwa. Hivi kweli hata kama ni ushawishi, utumiwe kumtukana mtoto wako au ni wakusingiziwa?.

Si kila aniitae Baba Baba atauona ufalme wa mbinguni.

Njaa mbaya. ZE KOMEDI walisema hata kama una mbio kiasi gani, huwezi kuikimbia njaa. Umaskini wa Watanzania ndio mtaji wa CCM. Maskini kupindukia na matajiri kupindukia si watu wa kuwategemea katika mapinduzi ya aina yoyote.
 
Sasa hivi hakuna cha ndoho tabu kamanda!! Wamesimama si mchezo

Yani nikipafikiria kwetu SHINYANGA walivyoamka nasikiaje raha kiukweli SHINYANGA ndio ngome ya CDM asante BOB MAKANI,SHELEMBI na MZEE LUHENDE Mungu awape amani ya milele uko mlipo kwani nyie ndio chachu ya haya tunayoyashuhudia SHINYANGA.
 
yani nikipafikiria kwetu shinyanga walivyoamka nasikiaje raha kiukweli shinyanga ndio ngome ya cdm asante bob makani,shelembi na mzee luhende mungu awape amani ya milele uko mlipo kwani nyie ndio chachu ya haya tunayoyashuhudia shinyanga.

amen...
 
Yani nikipafikiria kwetu SHINYANGA walivyoamka nasikiaje raha kiukweli SHINYANGA ndio ngome ya CDM asante BOB MAKANI,SHELEMBI na MZEE LUHENDE Mungu awape amani ya milele uko mlipo kwani nyie ndio chachu ya haya tunayoyashuhudia SHINYANGA.

Usinikumbushe marehemu Luhende kwani kipenga cha vyama vingi kilipopulizwa tu CDM ikaingia shinyanga chini ya marehemu FELIX NGELELA LUHENDE akiwemo bob Nyanga Makani( by then Makamu mwenyekiti taifa), watu wafahamu CDM imekuwepo shy town from day one 1992.Sasa ni muda wa kura matunda, tumesubiri sana opportunity hii.Mzee shilungushela wewe ndiyo umebaki kati ya waanzilishi.Karibu DR.SLAA hapa shy ndiyo nyumbani kwa CDM
 
Kiongozi wa Upinzani nchini Dr Wilbroad P.Slaa kesho anatarajiwa kuunguruma mkoani Shinyanga.Kiongozi huyo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA atatikisa katika mkutano wa kumnadi mgombea Udiwani wa CDM katika kata ya Mwawaza.
Habari za awali zinasema kuwa baba mzazi wa mgombea udiwani wa CDM anatarajiwa pia kupanda jukwaani kuelezea jinsi alivyohongwa ili amsingizie mwanae ni mwizi katika moja ya mikutano ya CCM.
Kuna shamrashamra kubwa hapa Shinyanga kuashiria ujio wa kiongozi huyo mashuhuri nchini.Mpaka sasa tathmini za awali zinaonyesha CDM ina uwezo wa kushinda kata hiyo kwa idadi kubwa ya kura.

Tunaomba feedback hasa picha ili tujiridhishe na kile kilichotokea huko.
 
Molemo, Jasusi, Pasco, Mzee Mwanakijiji,

..hivi Dr.Slaa a.k.a kibabu ana matatizo gani yeye haendi ulaya na marekani kufungua matawi kama wenzake? naona kizee hiki na shuka lake kimengangania hapahapa bongo tu nje hakitaki kwenda. au kinaogopa kupanda ndege??

hyo ni moja ya mbinu na mikakati cdm wemeiweka kutwanga kote kote...so ni mgawanyo wa kazi ndyo maana dr slaa anatwanga ndan na wengne wanatwanga nje..usikurupuke na kutoaaa viwazo vyako finyu..
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom