Dr Slaa: Kuhusu bajeti, CCM imefikia mwisho wa kufikiri

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameiponda hotuba ya bajeti iliyosomwa bungeni juzi, akisema inaonyesha wazi kuwa serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), imefikia mwisho wa kufikiri.

Alisema kuwa kitendo cha serikali kushindwa kutafuta vyanzo vipya vya mapato na badala yake kuendelea kutegemea vinywaji laini na vileo na kuruhusu wananchi waweke majina yao kwenye pleti za magari badala ya namba za magari ni hatua kuwa hawana ubunifu wa kukuza uchumi.

Akizungumza na Tanzania Daima jana jioni kwa njia ya simu kuhusu bajeti hiyo, Dk. Slaa ambaye alikuwa mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo, alisema licha ya kwamba ni mapema kutoa maoni lakini bajeti imejaa matamko ya kisiasa.

“Hayo aliyosoma Waziri William Mgimwa ni matamko ya kisiasa si hotuba ya bajeti, kwani tunaoelewa bajeti ni vitabu vinne wanavyopewa wabunge, nami navingojea nimeomba nipatiwe ila kama ndiyo hivyo alivyosoma tuko kwenye hali mbaya,” alisema Dk. Slaa.

Alisema kuwa kinachoshangaza ni kuongezeka kwa deni la taifa halafu fedha zinazokopwa na serikali imezielekeza kwenye matumizi ya kawaida badala ya maendeleo.

“Taifa linakopa ili iweje, kulipana mishahara na posho ama? Hii ni hatari kwa vizazi vijavyo miaka 30 hadi 40 ijayo. Zamani hata serikali zilizotangulia zilikopa lakini mikopo hiyo ilitumika kujenga viwanda, shule, barabara na huduma nyingine, leo tunafanya hivyo?” alhoji.

Alisema inashangaza kuona serikali inakopa kutoka vyombo vya biashara halafu inapelekea fedha hizo kwenye uendeshaji jambo lililozifanya hata taasisi za fedha za kimataifa kuwanyima mikopo na hivyo wamekimbilia kwenye mabenki.

Alifafanua kuwa ni katika makosa kama hayo imenyimwa mkpo wa sh bilioni 480 kwa ajili ya Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO).

Kuhusu vyanzo vya mapato, Dk. Slaa alisema anashangaa kuona kila mwaka serikali akili yake inalalia kuongeza kodi kwenye vileo na kuacha sekta nyeti kama madini.

“Tumerudia vyanzo vile vile ukiacha hicho cha watu kuruhusiwa kutumia magari yenye majina yao badala ya namba za usajili, sasa labda walevi watakapogoma kunywa ndipo serikali itapata ubunifu wa kuangalia vyanzo vingine,” alisema.

Hata hivyo, Dk. Slaa aliponda chanzo kipya cha mapato cha kuwaruhusu watu kuweka majina badala ya namba, akidai kuwa hatua hiyo mbali na kuleta matabaka kisaikolojia kwa wenye fedha kujiona wameiweka serikali mfukoni lakini pia ina madhara kuichumi.

“Mafisadi hawaoni uchungu hata kidogo kutumia fedha ila jambo la msingi ni kwamba wamezipataje, sasa kwa hali kama hii watafurahi kwa vile wanaona serikali imewahalalisha bila kujali kama fedha zao ni haramu,” alidai.

Aliongeza kuwa hata, vipaumbele ambavyo serikali imeelekeza kwenye bajeti yake, utekelezaji wake utakuwa mgumu kwani fedha zilizotengwa ni ndogo ikilinganishwa na mahitaji halisi.
 
Serikali legelege matokeo yake ndio haya,
hapo wamefika mwisho wa kufikiri.
 
Kukopa kwa ajili ya kulipana posho huu ni uhuni ktk uchumi wa leo.
Mkopo ni kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Wa kubanawa apa ni TRA mapato mengi yanaenda mifukoni mwao no wonder wengi wa mamanager wake wawemewekeza kama wafanyabiashara.
 
Kukopa kwa ajili ya kulipana posho huu ni uhuni ktk uchumi wa leo.
Mkopo ni kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Wa kubanawa apa ni TRA mapato mengi yanaenda mifukoni mwao no wonder wengi wa mamanager wake wawemewekeza kama wafanyabiashara.
Kuna kazi kubwa sana ya kulijenga taifa, na ni wenye moyo tu ndio watalijenga na wenye meno wazuiwe kula uchumi huu!
 
Kukopa kwa ajili ya kulipana posho huu ni uhuni ktk uchumi wa leo.
Mkopo ni kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Wa kubanawa apa ni TRA mapato mengi yanaenda mifukoni mwao no wonder wengi wa mamanager wake wawemewekeza kama wafanyabiashara.

Serikali inakopa ili mkweree aweze kusafiri kwenda kubembea!! It is stupid!!!
 
Hivi kuna watu wanafikilia kwa kutumia makalio au.?kama wapo bac asilimia kubwa ya viongozi wa serikali hii wanatumia makalio mana inasikitisha sana kuona kiona kiongozi anafanya utumbo na anasema uvundo. Mwisho wao 2015 tu.. na kupanda gari lenye mamba T2015CDM.
 
I hate Tanzania with ths present presdent who think by using Masabuli. I love u Slaa, ni kwa mema na mawazo endelevu unayotupa sisi watanzania tunaotaka tz iwe angalau kama rwanda. God-bless u Slaa
 
Tena kwa mimi naona hiyo kodi ya ulevi na sigara ni ndogo sana. Mzee wa Kanisa anapotetea ulevi kuongezwa bei, anasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom