Dr Slaa kugombea Urais, mafisadi wajipanga kummaliza

Na Mussa Juma, Arusha

VUGUVUGU la kupata mgombea wa urais mwakani ndani ya Chedema linadaiwa kuanza huku Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa akipendekezwa kuchukua nafasi hiyo.

Habari zilizolifikia Mwananchi Jumapili zimeeleza kuwa Dk Slaa ametajwa kuwania nafasi hiyo akipambana na kiongozi mmoja wa juu serikalini ambaye ni mwanachama wa Chadema.

Mchakato wa kutafuta mgombea huyo, umeanza kutokana na uamuzi wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuamua kugombea ubunge katika Jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro hivyo kukosa sifa kikatiba kugombea urais.

Habari zilizothibitishwa na mmoja wa viongozi wa Chadema ambaye hakutaka kutajwa gazetini, zinaeleza kuwa suala hilo limekuwa likijadiliwa katika vikao vya juu vya chama bila mwafaka.

Ni kweli kuna viongozi wanamtaka Dk Slaa agombee pia kuna kigogo mmoja ameonyesha nia ya kuja Chadema na kugombea na kuna wanasiasa wengine maarufu hawajatoa uamuzi, lakini mapema mwakani nadhani tutakuwa katika hali nzuri ya kujua nani atagombea,”alisema kiongozi huyo.

Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa, Chadema imekuwa na wakati mgumu kumtangaza Dk Slaa kuwa atagombea urais mwakani hasa kutokana na hofu ya kupoteza Jimbo la Karatu.

Pia hofu nyingine inatokana na baadhi ya wana CCM kuanza kuonyesha nia ya kuondoka katika chama hicho kujiunga na Chadema, kutokana na mgogoro unaoendelea kukitafuna chama chao.

Inaelezwa kuwa kutokana na mgawanyiko mkubwa uliopo ndani ya chama hicho, huenda makada maarufu wakaamua kujitoa na kujiunga na upinzani, hali ambayo inaweza kuwafanya wakapata mgombea urais.

Akihutubia wananchi wa Karatu wakati wa kufunga kampeni za serikali za mitaa, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Phillemone Ndesamburo aliwataka wananchi wa jimbo hilo kumchagua mtu ambaye ataletwa badala ya Dk Slaa kwa sababu chama kimeamua kumpa majukumu mengine.

Hata hivyo, kauli hiyo ilipingwa na umati wa watu waliohudhuria mkutano huo, akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu, Titus Lazaro ambaye amekuwa akitajwa
kutaka kumrithi Dk Slaa.

Alisema hadi sasa anaamini hakuna mtu wa kumrithi Dk Slaa Karatu hivyo ni
bora akaachwa aendelee kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Lazaro ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alisema kuanza kutafuta mrithi wa Dk Slaa sasa kunaweza kulipoteza jimbo hilo ambalo limekuwa likinyemelewa na CCM.

Mimi sijafikiria kugombea ubunge kama Dk Slaa akigombea urais kwani najua ugumu wa jimbo hili na mikakati mingi ya CCM kulitaka jimbo la Karatualisema Lazaro.

Hata hivyo,kwa upande wake Dk Slaa aliliambia gazeti hili kuwa bado hajaamua kugombea urais mwakani.

Mimi huwa sipendi kuzungumza bila ya kufanya utafiti..ni kweli watu wanasema nigombee ila bado sijaamua na jambo hili linahitaji utafiti kwanza,alisema Dk Slaa.

Dk Slaa ambaye katika siku za hivi karibuni, amekuwa mmoja wa viongozi wanaoheshimika na wenye msimamo mkali ndani ya chama hicho na bungeni, alisema muda wa kutangaza kugombea urais haujafika na suala la urais ni zito sio la kusema bila kuwa na mikakati.

Umaarufu wa Chadema katika miaka ya hivi karibuni, umekuwa ukiongezeka hasa kutokana na kuanzisha Operesheni Sangara nchi nzima ambayo imekifanya chama hicho kupata wafuasi wengi.

Chadema ilianza kuweka mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 ikimsimamisha kuwania kiti hicho, Freeman Mbowe ambaye pia alisimama mwaka 2005, huku ikiweka rekodi ya chama cha upinzani kutumia helikopta katika mikutano yake ya kampeni.
Mkakati wa kumsimamisha Dk Slaa ni kutaka kuongeza idadi ya wabunge baada ya kumtumia Mbowe mara mbili.

Source:Mwananchi
n.b msisitizo ni wangu
 
Mzee mbona bado mapema sana kufanya hivyo,tunahitaji kuongezeka akina Slaa wengine katika bunge siyo kupungua...we still need you mjengoni plz.
 
Mwache agombee, ikiwa wapinzani wote watakuja nyuma yake, muungwana atakuwa na kibarua kigumu mbele yake. Kama wapinzani watasimamisha utitiri kama kawa, Dr. Slaa bora ujilindie Karatu yako maana bado unahitajika sana mjengoni.
 
Mzee mbona bado mapema sana kufanya hivyo,tunahitaji kuongezeka akina Slaa wengine katika bunge siyo kupungua...we still need you mjengoni plz.

Junius, wewe ni mwanaCUF vipi wapata hofu CHADEMA kupoteza jimbo la Karatu? Anza kumshauri Profesa Lipumba aende kulinda jimbo kule Tabora

Asha
 
Hapana, nililenga kutilia nguvu "serikali kivuli ya upinzani" iwe na watu makini zaidi kama Dr.Slaa,...unajuwa bado mbio za mageuzi ya kweli zina mwendo mrefu...vyama vya upinzani vina resource chache kufikia huko...wakati wenzetu CCM wana kila kitu...filimbi ikilia tu wao wanatutangulia kwa kasi,hapa unanielewa nilichokusudia...thus why we need Slaa in Parliament and more of his like...
 
Na Mussa Juma, Arusha

VUGUVUGU la kupata mgombea wa urais mwakani ndani ya Chedema linadaiwa kuanza huku Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa akipendekezwa kuchukua nafasi hiyo.

Habari zilizolifikia Mwananchi Jumapili zimeeleza kuwa Dk Slaa ametajwa kuwania nafasi hiyo akipambana na kiongozi mmoja wa juu serikalini ambaye ni mwanachama wa Chadema.

Mchakato wa kutafuta mgombea huyo, umeanza kutokana na uamuzi wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuamua kugombea ubunge katika Jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro hivyo kukosa sifa kikatiba kugombea urais.

Habari zilizothibitishwa na mmoja wa viongozi wa Chadema ambaye hakutaka kutajwa gazetini, zinaeleza kuwa suala hilo limekuwa likijadiliwa katika vikao vya juu vya chama bila mwafaka.

Ni kweli kuna viongozi wanamtaka Dk Slaa agombee pia kuna kigogo mmoja ameonyesha nia ya kuja Chadema na kugombea na kuna wanasiasa wengine maarufu hawajatoa uamuzi, lakini mapema mwakani nadhani tutakuwa katika hali nzuri ya kujua nani atagombea,”alisema kiongozi huyo.

Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa, Chadema imekuwa na wakati mgumu kumtangaza Dk Slaa kuwa atagombea urais mwakani hasa kutokana na hofu ya kupoteza Jimbo la Karatu.

Pia hofu nyingine inatokana na baadhi ya wana CCM kuanza kuonyesha nia ya kuondoka katika chama hicho kujiunga na Chadema, kutokana na mgogoro unaoendelea kukitafuna chama chao.

Inaelezwa kuwa kutokana na mgawanyiko mkubwa uliopo ndani ya chama hicho, huenda makada maarufu wakaamua kujitoa na kujiunga na upinzani, hali ambayo inaweza kuwafanya wakapata mgombea urais.

Akihutubia wananchi wa Karatu wakati wa kufunga kampeni za serikali za mitaa, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Phillemone Ndesamburo aliwataka wananchi wa jimbo hilo kumchagua mtu ambaye ataletwa badala ya Dk Slaa kwa sababu chama kimeamua kumpa majukumu mengine.

Hata hivyo, kauli hiyo ilipingwa na umati wa watu waliohudhuria mkutano huo, akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu, Titus Lazaro ambaye amekuwa akitajwa
kutaka kumrithi Dk Slaa.

Alisema hadi sasa anaamini hakuna mtu wa kumrithi Dk Slaa Karatu hivyo ni
bora akaachwa aendelee kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Lazaro ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alisema kuanza kutafuta mrithi wa Dk Slaa sasa kunaweza kulipoteza jimbo hilo ambalo limekuwa likinyemelewa na CCM.

Mimi sijafikiria kugombea ubunge kama Dk Slaa akigombea urais kwani najua ugumu wa jimbo hili na mikakati mingi ya CCM kulitaka jimbo la Karatualisema Lazaro.

Hata hivyo,kwa upande wake Dk Slaa aliliambia gazeti hili kuwa bado hajaamua kugombea urais mwakani.

Mimi huwa sipendi kuzungumza bila ya kufanya utafiti..ni kweli watu wanasema nigombee ila bado sijaamua na jambo hili linahitaji utafiti kwanza,alisema Dk Slaa.

Dk Slaa ambaye katika siku za hivi karibuni, amekuwa mmoja wa viongozi wanaoheshimika na wenye msimamo mkali ndani ya chama hicho na bungeni, alisema muda wa kutangaza kugombea urais haujafika na suala la urais ni zito sio la kusema bila kuwa na mikakati.

Umaarufu wa Chadema katika miaka ya hivi karibuni, umekuwa ukiongezeka hasa kutokana na kuanzisha Operesheni Sangara nchi nzima ambayo imekifanya chama hicho kupata wafuasi wengi.

Chadema ilianza kuweka mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 ikimsimamisha kuwania kiti hicho, Freeman Mbowe ambaye pia alisimama mwaka 2005, huku ikiweka rekodi ya chama cha upinzani kutumia helikopta katika mikutano yake ya kampeni.
Mkakati wa kumsimamisha Dk Slaa ni kutaka kuongeza idadi ya wabunge baada ya kumtumia Mbowe mara mbili.

Source:Mwananchi

Kumbe Freeman Mbowe kagombea uraisi kupitia Chadema mara mbili. Hii ni habari mpya kwangu.

Gazeti la Mwananchi kiboko!
 
BTW: Junius, hii habari yote umequote kutoka Mwananchi?

Tanzania hatuna waandishi wa habari ambao ni spin doctors wazuri, ingawa wao wanajaribu ku spin.

Kuwa spin master mzuri inabidi uwe na kumbukumbu. Thats rule number one.
 
Junius, wewe ni mwanaCUF vipi wapata hofu CHADEMA kupoteza jimbo la Karatu? Anza kumshauri Profesa Lipumba aende kulinda jimbo kule Tabora

Asha
Punguza jazba! Junius ametoa wazo zuri ambalo lina mantiki. Slaa ni chaguo zuri la urais lakini ana chance tu endapo ataungwa mkono na kambi nzima ya upinzani, kitu ambacho sidhani kama kitatokea kwa Tanzania yetu tunayoijua. Itakuwa ni pigo kwa upinzani in general kama Slaa ataamua kugombea urais na kushindwa (which is more likely kama CHADEMA itasimama peke yake) kwa sababu hatakuwa na nafasi tena ya kugombea ubunge Karatu ambako anaonekana kuwa na nafasi kubwa sana ya kutetea kiti chake. Ikitokea hivi maana yake ni kwamba kambi ya upinzani bungeni itakuwa imepoteza kiti, tena cha mbunge muhimu kama Slaa (arguably the most influential MP of 2005-2010). Ni muhimu sana kuwa na strong opposition bungeni ili kujaribu kuinfluence utendaji wa serikali kutokea mjengoni kuliko kukimbilia kuingia Ikulu bila strong base ya wapiga kura. Let's be realistic, kwa mazingira ya kisiasa yalivyo sasa TZ ni vigumu kuona upinzani wakishinda kura za urais bila kuunganisha nguvu.
 
Sina tatizo na mtu kama wewe unavyojenga hoja hivyo. Nina tatizo na watu kama Junius ambaye ukiangalia mtirirko wa michago yake humu ndani wakati wote ni kuiponda CHADEMA na kuwasifia wakina Lipumba. Sasa mtu kama huyo anapokosoa hoja unapaswa si tu kukosoa hoja iliyopo bali pia kuangalia hoja za mchangiaji. Kwa sababu wapo wenye dhamira ya kukosoa kwa kujenga na wapo wenye kukosoa kwa kubomoa. Ingia hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ombea-urais-mafisadi-wajipanga-kummaliza.html utanielewa

Asha
 
Ushauri wangu kwa CHADEMA ni kwamba Dk. Slaa asigombee urais kwa sababu yeye anahitajika sana bungeni kuongeza nguvu. Na ukichunguza hali ya vyama vya upinzani bado havijawa na sauti moja hivyo bado hawana uhakika wa kuishinda CCM kutokana na ukweli kwamba CCM ni majemedari wa wizi wa kura.

Nashauri Dk. Slaa agombee ubunge ktk jimbo lake na wamweke mwanasheria Tundu Lissu ktk nafasi ya urais ili wao akina Slaa ambao wana hoja za nguvu wampigie debe, hapo wanaweza kupata chochote, na hata wakishindwa urais bado ubunge watakuwa na wabunge wengi.
 
Mie wazo langu ni DOGO sana.

Kuna ile makala ya kusema "Sallim A.S" anatakiwa kugombe u-Rais wa Zanzibar.

Kwangu mie Sallim Ahmed Sallim huna cha kupoteza kwa sasa. Ingelikuwa ni BUSARA na heshima kwa Watanzania kama angeligombea kwa kupitia CHADEMA. Hii pia itaifanya CHADEMA isiwe na cha kupoteza.

Dr. Slaa agombee ubunge KARATU, Mbowe HAI. Idadi ya Wabunge itakuwa ile ile au hata kuongezeka. Kama CHADEMA kitakuwa na Rais, basi walau baadhi ya mambo ataanza kuyabadilisha. Kama akikosa, bado atakuwa ameusaidia UPINZANI kwa kuleta ARI na NGUVU MPYA.

Tafadhali, Dr. Sallim, angalia hili pendekezo ili UMUENZI Baba wa Taifa na kuyafanya maneno yake yatimie haraka kuwa 'UPINZANI WA KWELI UTATOKA NDANI YA CCM". Nina imani ukitoka wewe, utabeba na wengine wengi. Ila inabidi mkumbuke maneno ya Clinton aliyowaambia Wanyarwanda. Mkijitenga, hakuna UHAKIKA wa kwamba mtaiadilisha Tanzania kwa sasa. Ila MSIPOJITENGA basi ni ukweli kwamba mambo yataendelea kuwa kama yalivyo.
 
Sina tatizo na mtu kama wewe unavyojenga hoja hivyo. Nina tatizo na watu kama Junius ambaye ukiangalia mtirirko wa michago yake humu ndani wakati wote ni kuiponda CHADEMA na kuwasifia wakina Lipumba. Sasa mtu kama huyo anapokosoa hoja unapaswa si tu kukosoa hoja iliyopo bali pia kuangalia hoja za mchangiaji. Kwa sababu wapo wenye dhamira ya kukosoa kwa kujenga na wapo wenye kukosoa kwa kubomoa. Ingia hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ombea-urais-mafisadi-wajipanga-kummaliza.html utanielewa

Asha
You got it all wrong Asha...unapata tatizo kwa jambo usilolielewa na kuuliza hutaki...sijawahi kuiponda chadema at the expense of praising Lipumba, the way you think...hata hiyo link uliyoweka hapo haionyeshi chochote kuwa nawaponda Chadema...ukitazama mada yenyewe na bandiko langu,nilichotaka kuonyesha ni maoni yangu binafsi tu...kuwa sioni kuwa ni sawa kwa Chadema kufikiria kumsimamisha Dr.Slaa agombee urais..nikiamini kuwa akiwa bungeni, sauti yake inafika mbali zaidi...na hii inasaidia kuwafumbua macho watu ambao ndo mtaji mkubwa wa kisiasa...sasa kama unatatizo na mimi kwa hilo basi siwezi kukusaidia...kumbuka tu an enemy of my enemy is my friend na siku zote huwa namtakia mema.
Asha, kama Dr.Slaa kafanya mwenyewe uamuzi huo au anafikiria kufanya hivyo basi afikirie upya, na kama kuna mtu kamshauri hivyo au chama kinamshauri hivyo basi...ni ushauri mbaya....unless otherwise,katika fikira hizo au uamuzi huo, kuwe na mambo mengine binafi si kwa maslahi ya chama chenu.
Mjumbe hauwawi.
 
Slaa ni chaguo zuri la urais lakini ana chance tu endapo ataungwa mkono na kambi nzima ya upinzani, kitu ambacho sidhani kama kitatokea kwa Tanzania yetu tunayoijua. Itakuwa ni pigo kwa upinzani in general kama Slaa ataamua kugombea urais na kushindwa (which is more likely kama CHADEMA itasimama peke yake) kwa sababu hatakuwa na nafasi tena ya kugombea ubunge Karatu ambako anaonekana kuwa na nafasi kubwa sana ya kutetea kiti chake. Ikitokea hivi maana yake ni kwamba kambi ya upinzani bungeni itakuwa imepoteza kiti, tena cha mbunge muhimu kama Slaa (arguably the most influential MP of 2005-2010). Ni muhimu sana kuwa na strong opposition bungeni ili kujaribu kuinfluence utendaji wa serikali kutokea mjengoni kuliko kukimbilia kuingia Ikulu bila strong base ya wapiga kura. Let's be realistic, kwa mazingira ya kisiasa yalivyo sasa TZ ni vigumu kuona upinzani wakishinda kura za urais bila kuunganisha nguvu.

Sure, hapa umeongea nukta tupu! Kumpoteza Dkt Slaa Bungeni ni pigo kubwa mno kwa upinzania! Prof Lipumba na wapinzania wengine wote watumie approach ile ile aliyotumia Seif kule Zanzibar alipomtambua refarii (Rais Karume) katika dakika ya 88 ya mchezo, kwamba "tunafanya hivi kwa maslahi ya Zanzibar na Wazanzibari." Kwa hiyo wapinzania nako watoe nafasi kwa Dkt Slaa ya kugombea urais na waseme kwamba "tunafanya hivi kwa maslahi ya Tanzania na Watanzania." La sivyo Slaa, usijaribu a loosing battle!
 
You got it all wrong Asha...unapata tatizo kwa jambo usilolielewa na kuuliza hutaki...sijawahi kuiponda chadema at the expense of praising Lipumba, the way you think...hata hiyo link uliyoweka hapo haionyeshi chochote kuwa nawaponda Chadema...ukitazama mada yenyewe na bandiko langu,nilichotaka kuonyesha ni maoni yangu binafsi tu...kuwa sioni kuwa ni sawa kwa Chadema kufikiria kumsimamisha Dr.Slaa agombee urais..nikiamini kuwa akiwa bungeni, sauti yake inafika mbali zaidi...na hii inasaidia kuwafumbua macho watu ambao ndo mtaji mkubwa wa kisiasa...sasa kama unatatizo na mimi kwa hilo basi siwezi kukusaidia...kumbuka tu an enemy of my enemy is my friend na siku zote huwa namtakia mema.
Asha, kama Dr.Slaa kafanya mwenyewe uamuzi huo au anafikiria kufanya hivyo basi afikirie upya, na kama kuna mtu kamshauri hivyo au chama kinamshauri hivyo basi...ni ushauri mbaya....unless otherwise,katika fikira hizo au uamuzi huo, kuwe na mambo mengine binafi si kwa maslahi ya chama chenu.
Mjumbe hauwawi.

Junius

Kwanini usimshawishi Lipumba kugombea ubunge? Maana CUF inamkosa bungeni toka mwaka 1995, amegombea kwa vipindi vitatu.

Propaganda zako dhidi ya Dr Slaa huwa unazifanya kwa utaalamu mkubwa https://www.jamiiforums.com/habari-...-slaa-tatizo-lako-nini-hapa-2.html#post626929

na huwa unamjenga Lipumba kwa ustadi: https://www.jamiiforums.com/michezo-sports-and-games/42088-prof-lipumba-aula-madola.html#post629943

Tuachane na hayo, turudi kwenye hoja. Kama Dr Slaa kwa kugombea urais akiwezesha wabunge zaidi ya kumi kwenda bungeni, upi ni mchango mkubwa zaidi, wa yeye mwenyewe kuweza kuendelea kuwepo au kuongeza nguvu zaidi?

Kwa kuwa Lipumba amegombea mara nyingi zaidi, kwanini sasa Lipumba asigombee ubunge aje kuwa waziri mkuu kwenye serikali ya mseto ya CHADEMA na CUF Dr Slaa akiwa Rais?

Asha,
Nasisitiza tena as far as I personally respect Dr.Slaa na Chama chake...sijawahi kufanya propaganda na nia mbaya kwake na chama chake...hizo post ulizo site hapo juu ni fair comments na hiyo ya Prof.Lipumba...haionyeshi any negative stance against Dr.Slaa wala Chadema.

Any way, tuachane na hayo...ndo awali nikauliza sielewi chadema huwa inajipanga vipi?

Kama suala la kuongeza majimbo kwa staili ya kumtumia Slaa as party candidate kwasababu ya umashuhuri wake,uwezo wake wa kuongea na kujenga hoja na haiba yake kwa ujumla...hii kisiasa ni ku put cart before the hoarse, wakati wa kufanya hivyo mbona umepita...mlitakiwa muanze mchakato wa kutafuta majimbo kuanzia ngazi za chaguzi za serikali za mitaa na vijiji...ambako ndo msingi wa kura za ubunge na urais.

Kusubiri uchaguzi Mkuu,ambao ni ghali mno kufikia hilo lengo lenu, kwa kuwa CCM nayo itatumia nyenzo zake zote...za kichama na dola kupigania majimbo hayo hayo,provided kuwa CCM tayari ina mizizi maeneo ya vijijini,ambayo ni rahisi kumuuza mgombea wao kwa nguvu kidogo tu...kinyume chake,kama Slaa atapita maeneo hayo ambayo chedema si maarufu...itakuwa kama bahati nasibu tu na kutumia nguvu nyingi bure.
Angalieni,Kigoma kusini ambako Chadema imefanya vizuri katika uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji...kama chadema ingepata mafanikio kama hayo kwa mikoa walau 15,hapo mgombea wenu yeyote yule..angeliweza kushawishi hayo majimbo kumi unayosema na akauzika vizuri tu.

Kwanini isiwe Lipumba?
CUF,pengine wameanza kutafuta majimbo hayo kumi na zaidi kwa kujiimarisha vijijini...tusikatae ndo zilipo kura...kwa hiyo hata Lipumba akisimama tena,ndo maana ikawa hakuna haja ya yeye kwenda jimboni, ni rahisi kushawishi upatikanaji wa majimbo zaidi kuanzia huko....ambako tumetumia nguvu tangia mapema kwa ajili ya uchaguzi mkuu.
Asha,kujipanga ni muhimu...hypotheses katika siasa si mara nyingi kuleta matokeo mazuri.
 
Hypothesis yako imeijenga kwenye weak premise. Kwamba CUF imejijenga zaidi kushinda majimbo kuliko CHADEMA kwa hiyo Lipumba ni vizuri agombee urais; premise hii ina mushkeli.

Lipumba alianza kugombea toka mwaka 1995 lakini mwaka 2005 pamoja na kugombea kwake, CUF haikupata jimbo hata moja upande wa Bara. Lakini Freeman Mbowe ambae CHADEMA ilifanya vibaya sana uchaguzi wa mitaa wa mwaka 2004 akapata majimbo bara.

Kigoma Kusini, si kweli kwamba CHADEMA imefanya vizuri sana kuliko majimbo mengine. Kigoma Kusini ni moja ya majimbo ambayo kuna mgawanyiko mkubwa wa upinzani. CCM imefanya vibaya lakini nguvu ya upinzani imegawanyika baina ya NCCR na CHADEMA. Ingawa naamini CHADEMA inaweza kabisa kushinda jimbo lile. Sasa tukianza kuhesabu majimbo kwa maana ya kazi ya kisiasa kwa kulinganisha Operesheni Zinduka na Operesheni Sangara, CHADEMA kwa hakika ina nafasi ya kupata majimbo mengi kuliko CUF.

Tuanza kwa kuijadili Kanda ya Ziwa Mkoa kwa mkoa, eneo ambalo CUF ilikuwa na nguvu kabla. Mkoa wa Kagera mathalani, ambayo CUF ilikuwa na nguvu baadhi ya majimbo hali imebadilika kabisa. Tunaweza kuanza kutaja jimbo moja baada ya lingine tukalijadili. Katika mazingira hayo, chama ambacho kwa kweli kikiweka mgombea urais kitazoa kura nyingi kwa upande wa upinzani ni CHADEMA. Ndio maana nimekuuliza, unaonaje Lipumba akagombee ubunge Tabora halafu CUF iunge mkono CHADEMA kwenye urais mgombea akiwa Dr Slaa? Halafu Lipumba atakuwa Waziri Mkuu kwenye serikali ya mseto?

Asha
 
1. Ni masikitiko kuwa kura za wagombea urais ambao hawashindi zinapotea, bila wao kuwa wawakilishi bungeni. Hili lingefaa kuangaliwa upya kwa manufaa ya taifa letu.

2. Tusiwe tunafanya siasa za uoga na za kuviziana, la sivyo vyama vyetu havitakuwa. Slaa amekuwa na nguvu bungeni na nje ya bunge, pia Lipumba, Mbowe na wengine. Kujitolea kushiriki kinyang'anyiro cha URAIS ni sehemu muhumu sana kukijenga chama. Huku ndiko kuangalia maslahi mapana ya taifa na chama kuliko kujiangalia binafsi. Wakati Mbowe anagombe, alijua wazi kuwa asingeweza kuupata urais na kulikuwa hakuna ubishi kuwa asingepoteza ubunge. Kwa gharama ya demokrasi na kukijenga chama kama taasisi ingekuwa busara akagombea sasa. Akikosa ataendelea kuziratibu shughuli za chama na kutumia muda wake mwingi atakaokuwa nje ya bunge kukijenga chama.

3. Wajiandae mapema, na endapo atakuwa tayari kugombea urais, wamtafute mrithi wake Karatu, mwenye msimamo na mwenyekukubalika kwa jamii, na wananchi wamuelewe mapema, wasijekulipoteza jimbo hili muhimu sana kwao
 
Asha,
Hili swali la mwisho limenichekesha sana.
Nimekwambia hapo juu hypotheses katika siasa si mara nyingi kuleta matokeo mazuri...mm sitegemei sana...unaweza kuwa right hapo.
Rudi kwenye ile nukta yako kuwa Dr.Slaa akigombea naweza akashawishi majimbo kumi zaidi ya hilo moja la Karatu...sawa...nikakueleza kuwa kama ni hivyo basi,mbona mmefanya kinyume nyume...kama kusudi lenu ni majimbo na si kura za urais!
Kama kusudi ni majimbo, kura zipo vijijini na kama mngejiimarisha huko,mgombea yoyote anaweza kusimama akashawishi.
O.k, tuje kwenye operesheni sangara..ambayo kwayo unadai chadema inanafasi kubwa ya kushinda majimbo kuliko CUF,kama nitakubaliana na wewe kwa hili, basi ile hoja yako ya kuwa Dr.Slaa akisimama kama candidate wa urais atashawishi majimbo kumi zaidi,itakuwa haina mashiko hapa.
Kwa hiyo mum release Slaa katika kubeba msalaba huu.
 
Back
Top Bottom