Dr. Slaa: Kikwete mmiliki wa DOWANS...

've always said this country's leadership is rotten to the core. There it is. Rais fisadi. Duh! Unatemea nin kutoka kwa mawazir, RCs, DCs etc. Wanaiba bila wakuwakemea. Ndie maana Chenge na Mkapa hawakamatiki. Akiwakamata, watamwaga mboga!
 
Jamani si mmeona kama dr angeapishwa kuwa rais ina maana angeanza na kikwete kwanza.
 
Hard time is ahead of us just wait and see. Dowans is mzimu unaotutafuna wananchi mpaka kumaliza zote bilioni 185 kwa Dowans wananchi tutapigika kinoma. Mwaka Mpya na Mambo mapya yakulipa deni hewa la dowans, it is just like paying the left to right hand of the same person. Yaani unatoa mfuko wa kushoto pesa unaweka mfuko mwingine take care!
 
Upupu mtupu, unaongelea kodi? Unajuwa kuwa kwa miaka yote kabla ya Kikwete kodi inayokusanywa haikuchangia hata hamsini kwa mia ya bajeti yetu? Tumeona wakati wa Kikwete hali hiyo ikipanda hadi kufikia kuwa sasa tunachangia asilimia sitini ya bajeti yetu kama si zaidi. Tena kupunguka, bajeti imepanda maradufu! Au hilo hulioni?

Huyu Silaa anatafuta kuanzisha choko-choko za uvunjifu wa amani, kila analosema linaashiria kuwa si mwana-siasa bali ni limbukeni na sasa kapata sehemu ya malimbukeni wenzake nao wanamsikiliza bila kuhoji wala kupima. Akumbuke, hatuta ona amani ya Tanzania inavunjika kwa mtazamo wake hasi. Kama ana ushahidi wa hayo si apeleke bungeni na kama hana ushahidi na anaongea pumba ajuwe ndio mwanzo wa mwisho wa fitina zake. Atashughulikiwa kisheria.

Walisha kuwepo watu wa kanisa wenye choko choko kama yeye, mfano ni Mtikila, huyu kwisha nyamazishwa. Sasa huyu hayaoni hayo, na yeye inapaswa sasa anyamazishwe kama mtikila. Na hivyo ndivyo itavokuwa maana kushindwa kwake kura sasa analeta chokochoko.

I highly doubt..hajaanza leo! mbona hajashitakiwa!?? ama ni yale ya Sokoine!??
 
katika katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania na kanuni za bunge kuna kifungu kinacho wakilishwa na mbunge bungeni cha kumtoa rais madarakani,na huwa wanajadili wabunge wote na wale wanaompinga wafikie asilimia 20%
Ni kweli Katiba ya sasa ya Jamhuri Ibara ya 46A (3) (b) inatoa mamlaka kwa Bunge kuunda kamati ya kuchunguza mashtaka dhidi ya rais kwa hoja ya kutokuwa na imani naye. Hoja ambayo lazima kwanza isainiwe na asilimia 20 ya wabunge kisha mtoa hoja aitoe Bungeni kabla ya kupigiwa kura na kuungwa mkono na theluthi mbili. Ninachojiuliza jee wabunge wa Upinzani hawafiki 20%? kama wanafika kwa nini isitengenezwe hoja nzito ya kusababisha yote yawe hadharani hata kama hiyo thelusi mbili haitapatikana wakati wa kupiga kura ili kupata kamati ya kumchunguza, sisi wananchi tutafahamu fika kuwa Rais ameokolewa na wabunge wa CCM bali ukweli tayari utakuwa wazi. Hilo litakuwa pigo takatifu.
 
Naogopa ban otherwise ze utam could be absolutely right?
Hata mimi nahisi wanweza ku-ban like ze Utamu nawombeni wataalamu mtuhamishie wiki leaks Ulimwengu mzimz wayajue haya mambo maana toka jana ile thread ya Invisible na hii ya Rutashubanyuma zinatisha.
Bado naogopa kusema ............ kule Dodoma jirani na ofisi za Makao Makuu ya CCM brbr ya One way kuna Hotel ya hadhi ya Nyota ghorofa la Mnguu nasikia si lake ila la mzee wa kaya linaanzia na herufi K.
Bado naogopa ................... maji ya mvua kwenye mabwawa ya Mtera ni yetu kweli, maana wanasema hata magreda ya kuchimbua tope yaliyoagizwa enzi za IPTL yalinywewa, sasa tope litaacha kujaa?
haijawahi kutokea masika tukawa na mgawo, ipo siku tukimchekea nyani tutakuta mabua ni nani anatumaliza umeme haupo hata mahospitalini.
Kama kweli Mzee Pinda ana uchungu na Nchi hii atazame kwanza Watanzania na wakazi wa jimbo la Katavi je? wana Umeme agome kuidhinisha malipo hayo ya Tanesco asije jibebea lawama kama mtoto wa mkulima maskini kwani 2015 hatasogea popote (fomu ya Urais) tutabakia kupikia kuni tu
 
Upupu mtupu, unaongelea kodi? Unajuwa kuwa kwa miaka yote kabla ya Kikwete kodi inayokusanywa haikuchangia hata hamsini kwa mia ya bajeti yetu? Tumeona wakati wa Kikwete hali hiyo ikipanda hadi kufikia kuwa sasa tunachangia asilimia sitini ya bajeti yetu kama si zaidi. Tena kupunguka, bajeti imepanda maradufu! Au hilo hulioni?

Huyu Silaa anatafuta kuanzisha choko-choko za uvunjifu wa amani, kila analosema linaashiria kuwa si mwana-siasa bali ni limbukeni na sasa kapata sehemu ya malimbukeni wenzake nao wanamsikiliza bila kuhoji wala kupima. Akumbuke, hatuta ona amani ya Tanzania inavunjika kwa mtazamo wake hasi. Kama ana ushahidi wa hayo si apeleke bungeni na kama hana ushahidi na anaongea pumba ajuwe ndio mwanzo wa mwisho wa fitina zake. Atashughulikiwa kisheria.

Walisha kuwepo watu wa kanisa wenye choko choko kama yeye, mfano ni Mtikila, huyu kwisha nyamazishwa. Sasa huyu hayaoni hayo, na yeye inapaswa sasa anyamazishwe kama mtikila. Na hivyo ndivyo itavokuwa maana kushindwa kwake kura sasa analeta chokochoko.

Ok Profesa do us a favor tutajie basi mmiliki halisi wa Dowans kama sio JK. Vinginevyo huwezi kututoa kwenye agenda
 
Hii ndiyo ile ambayo kamati ya Dr. Mwakyembe alisema mengine hawakuyatoa hadharani kwa sababu za kiusalama ( wa Taifa)!!!! Hivi usalama wa Taifa ni usalama wa Kikwete au wa wananchi? Ni usalama gani wa taifa wakati mkulu mwenyewe ndiye anayetusaliti?

Haha now you are talking. Bonge umesema sawia kabisa. Usalama wa Taifa si usalama wa taifa, ni usalama wa CCM, and to be more specific na wa baadhi ya watu ndani ya CCM. Ukiangalia issue nzima ya umeme kwa Tanzania, inaweza kuwa ni moja ya top prioroties za usalama wa Taifa, lakini angalia jinsi Usalama wa taifa wenyewe wanavyoiangalia na kuishughulikia, si prioroties kabisa. I can not believe tunarudia tena ujinga uleule tuliou-face wakati wa Richmond, kama kweli uslama wa taifa wangefanya kazi yao tusingekuwa na tatizo hili.
 
Upupu mtupu, unaongelea kodi? Unajuwa kuwa kwa miaka yote kabla ya Kikwete kodi inayokusanywa haikuchangia hata hamsini kwa mia ya bajeti yetu? Tumeona wakati wa Kikwete hali hiyo ikipanda hadi kufikia kuwa sasa tunachangia asilimia sitini ya bajeti yetu kama si zaidi. Tena kupunguka, bajeti imepanda maradufu! Au hilo hulioni?

Huyu Silaa anatafuta kuanzisha choko-choko za uvunjifu wa amani, kila analosema linaashiria kuwa si mwana-siasa bali ni limbukeni na sasa kapata sehemu ya malimbukeni wenzake nao wanamsikiliza bila kuhoji wala kupima. Akumbuke, hatuta ona amani ya Tanzania inavunjika kwa mtazamo wake hasi. Kama ana ushahidi wa hayo si apeleke bungeni na kama hana ushahidi na anaongea pumba ajuwe ndio mwanzo wa mwisho wa fitina zake. Atashughulikiwa kisheria.

Walisha kuwepo watu wa kanisa wenye choko choko kama yeye, mfano ni Mtikila, huyu kwisha nyamazishwa. Sasa huyu hayaoni hayo, na yeye inapaswa sasa anyamazishwe kama mtikila. Na hivyo ndivyo itavokuwa maana kushindwa kwake kura sasa analeta chokochoko.

Itakuwa jambo la kheri serikali ikichua hatua huko ndo kuzuri tutajua mbichi na mbivu Dr wa ukweli hajakurupuka bila ubishi unayatambua mambo ya EPA walimtishi Dr. Kuwa watamburuza mahakamani wewe mwenyewe nishahidi wa halihalisi mpaka kufikia kujiuzuru kwa PM.
 
Slaa: JK anamiliki Dowans
• Asema hana nia ya kuunda Katiba mpya

na Mwandishi wetu

amka2.gif
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willbrod Slaa amesema kuwa Rais Jakaya Kikwete ni dikteta.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Dk. Slaa, alisema kitendo cha Rais Kikwete, kutangaza kuwa ameunda tume ya kuanzisha mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya na atateua kiongozi na wajumbe kinaashiria kuendeleza udikteta wa uongozi.
Alibainisha kinachotakiwa kuanzishwa hivi sasa ni Constitutional Assembly au Baraza la Katiba (Bunge la Katiba) ambalo ndilo litakalokuwa na wajibu wa kuratibu kura za maoni ya wananchi juu ya uundwaji wa Katiba mpya.
Alisema kitendo cha Rais Kikwete, kutangaza kuunda tume ni kiini macho na kinadhihirisha hana nia ya kutaka kuundwa kwa Katiba mpya.
"Huyu Rais wetu haonyeshi kama yuko 'serious' katika uundaji wa Katiba mpya, anataka kuweka viraka ili aendelee kututawala kidikteta!" alisema.
Aliongeza kuwa kwa kawaida Baraza la Katiba ambalo hapa nchini halipo ndilo lenye jukumu hilo na linatakiwa lifanye mchakato huo kwa kuishirikisha serikali, Bunge, wadau na wananchi.
Alisema hakubaliani na tume ya kuratibu mchakato huo, kwani inaweza kufanya kazi kwa utashi wa aliyewateua na hata Bunge pia linaweza likatumbukia kwenye mtego wa kupitisha kitu kisichokuwa matakwa ya wananchi kwa sababu ya wingi wa wabunge wa chama kimoja.
Alisema katika nchi zote zilizoandika upya Katiba au kutengeneza zilipitia njia ya 'National Constitutional Congress au Convention' (Constitutional Assembly) ambapo ilikubaliwa kati ya serikali, Bunge, wadau mbalimbali na wananchi katika majukwaa yao.
"Constitutional Congress ni chombo kitakachoratibu maoni ya wananchi na wadau mbalimbali na siyo mtu aliyeteuliwa na Rais ambaye anafanya kazi kwa ajili ya kumfurahisha jambo ambalo ni kuendelea kuweka viraka" alisema.
Alisema baada ya chombo hicho kuundwa, maoni ya wadau, wananchi mbalimbali hukusanywa kwa njia itakayokubalika.
Dk. Slaa alisema kuwa 'Constitutional Congress hukaa tena kupitia maoni yote kipengele kwa kipengele na kukubaliana na siyo Rais Kikwete na tume atakayounda jambo ambalo liliwahi kutokea huko nyuma.
Alisema inawezekana Rais Kikwete, hafahamu au kwa makusudi amepuuza kilio cha wananchi ndiyo maana ameunda tume inayowajibika kwa maslahi yake.
Alisema kuwa Katiba siyo mali ya Rais wala ya serikali iliyoko madarakani, bali ni mali ya wananchi.
Dk. Slaa alisema wananchi wanatakiwa kufahamu kuwa wanahitaji chombo chao ambacho kinaweza kuwekewa utaratibu na Bunge, baada ya kupitishwa na Azimio la Bunge, lakini siyo mtu au watu wa tume wanaochaguliwa na Rais.
"Tume hiyo haikubaliki kabisa tunachotaka tunajua hakitakubalika kwa maana hakuna serikali duniani itakayounda tume ya kujinyonga yenyewe, mabadiliko makubwa kwa vyovyote, hayakupendwa na serikali iliyoko madarakani" alisema.
Alisema ana imani kuwa tume hiyo haiwezi kuleta Katiba mpya hivyo kutoa nafasi kwa Rais Kikwete kuendelea kuongoza katika sura ya kidikteta kwa kupitia Katiba ya sasa iliyopitwa na wakati.
Dk. Slaa alisema kuwa inashangaza katika hili ambapo hata Zanzibar wamepiga hatua kwani waliweza kuruhusu kukusanya maoni ya uundaji wa serikali ya kitaifa na si kuundwa kwa tume.
Alisema Katiba mpya haiwezi kamwe kupatikana kwa njia ya tume hiyo (Constitutional Review Commission) kwani zilishawahi kutokea tume za aina hiyo na hakuna kilichofanyika.
Alibainisha kuwa jambo hilo halina tofauti na tume zilizowahi kuundwa na Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi pamoja na ile ya Benjamin Mkapa ambapo matokeo yalikuwa ni kuweka viraka kwenye Katiba tuliyonayo hivi sasa.
"Uzoefu wa Tume za Mwinyi na Mkapa ni kuwa maoni yalikusanywa kwa upendeleo, hojaji zilipelekwa kwenye matawi ya CCM, halmashauri za wilaya vyombo ambavyo vyote ni vya CCM, hatimaye serikali ikatoa mapendekezo ya vifungu vya kurekebishwa na vingine kuachwa, alisema na kuongeza: "hatua hii inawezekana kwa kuwa tume ni ya Rais, na Rais kama alivyosema mwenyewe ndiye atakayepeleka marebisho kwa vyombo husika (Bunge) ambalo karibu lote ni la CCM bado wana wabunge wengi pamoja na kuwa wapinzani wameongezeka sana" alifafanua.
Katika hatua nyingine, Dk. Slaa alisema ameshangazwa na kitendo cha Rais Kikwete kushindwa kufafanua kuhusu suala la kulipwa kwa Kampuni ya Dowans sh bilioni 185 na Shirika la UmemeTanzania (TANESCO).
Alisema fidia hiyo iliyoamriwa na mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya biashara (ICC) hivi karibuni kuwa TANESCO inapaswa iwalipe Dowans fedha hizo baada ya kuvunja mkataba wa kununua umeme.
Alisema kimsingi uvunjwaji wa mkataba huo na sakata zima ni uzembe ambao unapaswa uwekwe wazi na watu wachukuliwe hatua lakini Rais Kikwete haonyeshi kushtushwa na jambo hilo.
Alisema kutokana na majibu ya kiongozi huyo inaonyesha kuwa naye ni sehemu ya kampuni ya Dowans.
Alisema Rais anaonyesha udikteta kwa kuamua kulibeba shirika la umeme nchini (TANESCO) huku wananchi ambao ni walalahoi wakiendelea kunyongwa na upandaji wa gharama hizo.
"Hasemi kuwa kitendo cha kulipa kampuni hiyo kimesababishwa na uzembe wao wenyewe kwa kuleta mitambo ya Richmond iliyozaa Dowans huku yeye akiwa sehemu ya kampuni hizo ameamua kuficha uovu wao" alieleza.
Alisema wataendelea kuhamasisha maandamano pamoja na kupinga gharama kwa kuwa vyama vya upinzani havikusajiliwa kwa Rais bali vimekuwepo kwa mujibu wa sheria ili kuhakikisha vinakataa uozo unaofanywa na serikali.
Dk. Slaa alisema Rais Kikwete amesahau hali ngumu inayowakumba wananchi imetokana na maamuzi mabovu yaliyoanzishwa na wanasiasa wenzake kwa kukubali kufanya mchakato wa IPTL.
"Eti Rais Kikwete anasema upandaji wa umeme ni suala la kibiashara na wanasiasa wasilizungumzie kisiasa inawezekana hana uchungu na Watanzania wanaoshindwa kununua umeme kwa ajili ya kuendeleza biashara zao" alisema.
Alisema vyama vya upinzani vina haki ya kujadili masuala mbalimbali na siyo kama anavyodai kufanya hivyo ni kuendeleza malumbano na ikiwa hataki vyama vifanye hivyo basi hana budi kuvifuta.
Wakati huo huo Chama cha Wananchi (CUF), kimemtaka Rais Jakaya Kikwete, kutekeleza kwa vitendo ahadi yake aliyoitoa juu ya kupata Katiba mpya itakayokuwa na maslahi ya Watanzania wote.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF, bara, Julius Mtatiro, alisema kuwa kitendo cha Rais Kikwete, kukubali kuundwa kwa Katiba mpya kuendane na vitendo hasa kuiunda upya na sio kuifanyia marekebisho kama ilivyokuwa awali.
Alisema Tanzania imefanya marekebisho mara 14 lakini bado kumekuwa na malalamiko hali inayoweza kuleta machafuko nchini na kuipa nchi doa.
Alisema ni kipindi kizuri kwa Rais Kikwete kuiga mfano wa Rais wa Zanzibar wa awamu ya sita Amani Karume kwa kuridhia maridhiano yaliyoleta sura mpya ya Zanzibar.
Alisema suala la Katiba mpya limekuja wakati muafaka, kabla ya kutokea kwa misukosuko inayoweza kuchafua hali ya utulivu na amani ya nchi hatua itakayofanya kupoteza sifa hasa pindi amalizapo muda wake mwaka 2015.
Hata hivyo chama hicho kilimtahadharisha Rais Kikwete kuhakikisha anatembea katika kauli zake hasa kwa kuunda tume makini itakayokuwa huru na isiyokuwa na upendeleo au agenda ya kuibeba CCM, hasa kwa kufanya maamuzi ya upande mmoja.
Aidha katika hotuba yake Rais Kikwete aliahidi kuunda Tume Maalum ya Katiba (Constitutional Review Commission), itakayoratibu mchakato kwa kushirikisha wananchi wote ili waweze kutoa maoni yao juu ya yale wanayotaka yaingizwe katika Katiba mpya.
 
Most of them(people) follow nothing except conjecture; but surely conjecture can be no substitute for truth; and Allah is well aware of whatever they do.
S.10(Yunus): 36
 
Ni kweli Katiba ya sasa ya Jamhuri Ibara ya 46A (3) (b) inatoa mamlaka kwa Bunge kuunda kamati ya kuchunguza mashtaka dhidi ya rais kwa hoja ya kutokuwa na imani naye. Hoja ambayo lazima kwanza isainiwe na asilimia 20 ya wabunge kisha mtoa hoja aitoe Bungeni kabla ya kupigiwa kura na kuungwa mkono na theluthi mbili. Ninachojiuliza jee wabunge wa Upinzani hawafiki 20%? kama wanafika kwa nini isitengenezwe hoja nzito ya kusababisha yote yawe hadharani hata kama hiyo thelusi mbili haitapatikana wakati wa kupiga kura ili kupata kamati ya kumchunguza, sisi wananchi tutafahamu fika kuwa Rais ameokolewa na wabunge wa CCM bali ukweli tayari utakuwa wazi. Hilo litakuwa pigo takatifu.

Wanafika lakni ili wabunge wa CCM waiunge mkono ni lazima ipate msukumo wa wapigakura..................wananchi wakianza kudai maandamano ya kumng'oa JK itafika wakati hata wabunge karibu wote wataiunga mkono hoja hiyo..................na hapo Jk atalazimika kujiuzulu mwenyewe...........Nionavyo mimi huko ndiko tunakoelekea............

Nchii haiwezi kuvumilia ufisadi mkubwa ambao JK anauendesha....itafika mahali itabidi hili zigo tulitue tu hatuna namna..............na haitachukua miaka miwili kuanzia sasa.............
 
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Dk. Slaa, alisema kitendo cha Rais Kikwete, kutangaza kuwa ameunda tume ya kuanzisha mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya na atateua kiongozi na wajumbe kinaashiria kuendeleza udikteta wa uongozi.
Alibainisha kinachotakiwa kuanzishwa hivi sasa ni Constitutional Assembly au Baraza la Katiba (Bunge la Katiba) ambalo ndilo litakalokuwa na wajibu wa kuratibu kura za maoni ya wananchi juu ya uundwaji wa Katiba mpya.
Alisema kitendo cha Rais Kikwete, kutangaza kuunda tume ni kiini macho na kinadhihirisha hana nia ya kutaka kuundwa kwa Katiba mpya.

Hizi ni hajo nzito sana kutoka kwa kiongozi mwenye maadili na anayelijali taifa lake.....................Aidha Mkutano wa Kikatiba ulioandaliwa na sheria iliyopitishwa na Bunge............or Jk akaae pembeni asubiri kukamatwa kwa ufisadi mkubwa aliotufanyia na kutuongezea umasikini wa kutupwa................
 
Chonde wabunge wetu! Kikwete hafai kuongoza nchi na hawezi kuondoka mwenyewe.....anzeni mchakato wakumwondoa.......vinginevyo hamna uchungu na nchi hii. Pinda naye aondoke tu.....anashindwaje kutaja wa miliki wa dowans wakati anajua? aliapa kuwa akila rushwa mungu amchukue je hili halifanani na rushwa? hebu fanya maamuzi kabla mungu haja amua kutimiza ombi lako
 
Kumbe!!!!!!!!!!!!!!!! sasa naanza kumwelewa Slaa alipotuambia kumrudisha Kikwete ni maafa.
 
Back
Top Bottom