Dr Slaa Jibu tuhuma hizi...!

a) Wagonjwa wanaotibiwa kwa mwaka wanakadiriwa kufika 1,080,000 katika hawa zaidi ya nusu ni kutoka katika mikoa ya kasikazini ikiongozwa na moshi na arusha.(branch ya CCBRT iko moshi


Mtoa hoja nina maswali machache ya ufahamu,
Mosi, Kama unasema branch CCBRT iko moshi, iweje wasukuma wa Shinyanga wawe wengi kutibiwa ktk hosp iliyoko Moshi walipo wachaga? Automatically mahali hosp. ilipo ndopo weneyeji wa mahali pale wanakuwa wengi. Labda unahoji kwanini ilijengwa Moshi, na mimi nakuuliza, (uzuri mimi si mchagga) kwanini isijengwe Moshi? wachaga hawaumwi? Hilo tawi lingekuwa Mbulu au Karatu kwa ndugu zake na shangazi zake at least hoja dhaifu ingepatikana. Other wise, hapa hujaitendea haki RUZUKU ya Nape aliyekutuma.

Pili, Dr Slaa siyo katibu wa Bodi ni m/kiti wa Bodi/ Rais wa Bodi hivyo,hahusiki na utendaji wa Kila siku ikiwepo kuajiri. Yeye kila siku yuko Chadema, tumhoji kuhusu Chadema.

Tatu, Dr Slaa siyo mchagga, yeye ni mwiraq wa Karatu. Karatu kijiografia iko mkoa wa MANYARA ambao uko kati ya mikoa ya kati na Kaskazini. Hata hivyo, enzi ya akina SUMAYE NA Mkapa walipeleka karatu Mkoa wa Arusha kwa sababu zao (za kisiasa?).
 
Ni kweli kabisa mkuu, angalia kwa mfano siasa za usukumani John Cheyo anasupport timu ya ngoma za kisukuma ndo manifesto yake UDP kwa kawaida Bariadi kuna timu mbili ya kina Ng'wani inayopiga kura ccm na hiyo ya Cheyo, matoeko tunajaua wote. Waacheni wachaga, wahaya, wanyakyusa wapete vingine we have to pull up our socks
Na fursa za kisiasa pia mkuu au?
 
Tuhuma kama hizi zilishaletwa kwa Dr Slaa miaka 4au3 iliyopita na CCM wakati huo Kinana akiwa kinara wa kampeni za Kikwete lakini zilikuwa hazina ukweli tunataka ukweli zaidi ya huu. Hata hivyo sitaki nimsemee yeye ana domo kubwa tu:lol:
 
nimetapika mara 2 kabla hata sijamaliza kusoma hii thread,
huu ni upuuzi, msitake kuleta ukabila wenu hapa,
 
WE NI MBUMBUMBU SANA...
Hivi docta slaa ni mchaga?!
Acha umbumbumbu wewe. Kwani ile ccbrt ni ya kwake? We vipi unaanza kuugua tukuwahishe apolo!. Eti wachaga ndo wanatibiwa wengi mbona hata wakimbizi ni wengr mno wanaotibiwa ccbrt?. We kama huwajui wachaga nyamaza tu, hawa jamaa ni noma wamesoma sana kila idara wapo, jk mwenyewe alisema ukiona sehem mchaga hayupo hapafai kuishi, kama nchi yetu ingekuwa na watu wote kama wachaga tungekuwa mbali. Ebu waangalie 2 kwenye biashara utawajua, NDG YANGU ACHA UMBEA FANYA KAZI ACHANA NA WACHAGA WATAKUUMIZA KICHWA.

WE Tandale one (aka Lowasa wa Tandale) hili ndilo jibu lako kutoka kwa Dr slaa
 
Mpelekeni milembwe labda anaupungufu wa kichwa kidogo.....

Dr.Slaaa sio mtu wa hivyo wewe fanya utafiti wa kina kwanzaaaa. Alaaahaaaa!
 
Sidhani kama haya mapesa yanayotolewa na wafadhili huwa yanafika yote!! Ngoja Dr. Slaa aje atueleweshe!!
Huyu jamaa ni zaidi ya Mpuuzi. Anakuja na Uongo na Majungu yaliyotukuka. Juma lililopita nilikwenda na mzee wangu CCBRT ana tatizo la CATARACT. Tumelipia fast track TShs 70,000(elfu sabini tu) kwa ajili ya kufanyiwa CATARACT SURGERY. Sasa yeye hiyo figure kaipata wapi! Hata kama anatumiwa huenda hata masaburi yake si salama nayo yanatumika tu. Kwa hili ninalolijua nimeshaona amedanganya, je atakuwa amedanganya mangapi kwenye huo upuru wake aliyouweka hapo juu?
 
Nimepita katika group moja katika facebook nikakuta kuna post ambayo inazungumzia tuhuma za ufisadi uliofanywa na watu mbalimbali kutoka vyama vya upinzani akiwemo Dr Slaa..,si vibaya tuhuma hizi nikizileta hapa jamvini kwa kuwa Dr Slaa yupo na naamini wapo pia watu wenye uelewa katika haya yaliyozungumzwa wanaweza kuchangia ama kusaidia katika kukanusha ama kusahihisha ama kukiri tuhuma hizi..,

extracted from TANURI LA FIKRA

Kuchukua tuhuma za mwanachama na kuivesha tuhuma hiyo kwa chama ni makosa na hili linafanywa makusudi na wapinzani ili waendelee kichafua CCM.,haiwezekani ufisadi unasibishwe na CCM hali ya kuwa katika kila chama watu wa AINA hiyo wapo; Nikianza moja kwa moja na katibu mkuu na mgombea URAIS wa chadema Bwana WILBROD SLAA ambaye ni kiongozi mkuu wa taasisi ya CCBRT (katibu wa bodi ya wakurugenzi) ambayo inapatiwa ruzuku ya shilingi za kitanzania; 1,000,000,000/= kutoka kwa serikali kila mwaka kwa kuiendeleza taasisi hiyo kwa manufaa ya watanzania wote na taifa kwa ujumla na pia inapata misaada na harambee mbalimbali kutoka kwa watu binafsi na mashirika makubwa ndani na nje ya TANZANIA kama EUROPEAN UNION,IRISH AID, AUSTRARIAN GVT, AusAID, CBM, JOHNSON&JOHNSON nk, ili kuwaendeleza watanzania katika nyanja ya afya,.tofauti na malengo hayo taasisi hii chini ya Dr Slaa imekuwa ikitoa huduma za jamii kwa ubaguzi mkubwa na kukosekana kwa usawa; nitabainisha kama ifuatavyo;
a) Wagonjwa wanaotibiwa kwa mwaka wanakadiriwa kufika 1,080,000 katika hawa zaidi ya nusu ni kutoka katika mikoa ya kasikazini ikiongozwa na moshi na arusha.(branch ya CCBRT iko moshi)
b) Operesheni zilizofanywa kati ya mwaka 2003-2007 ni kama ifuatavyo.,macho 31,200 napo pia zaidi ya nusu ya wagonjwa walitoka maeneo hayo. Mimi sidhani kuwa moshi kuna watu wenye matatizo ya macho zaidi ya Dodoma, Singida na sehemu nyingine za tanzania ya kati.
c) Operesheni za orthopaedic&plastic surgery kati ya 2003-2007 ni 6,520 bado wagonjwa wengi walitokea kaskazini
d) Na waathirika waliokuwa wakihudumiwa na CCBRT kati ya 2003-2007 zaidi ya 60% ni kutoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro (ripoti ya Tom Varnneste 24 jully 2008)
e) Taasisi hii pia inakadiriwa kuwa na waajiriwa 320 napo hapa ni uchaga, na ukaskazini umetawala, mchakato wa uajiri ukisaidiwa na Jacqueline Kweka(Advocacy Officer) uliona kuwa hakuna watu waliosoma na kustahili kufanya kazi CCBRT ila ni wachaga na watu wa kanda ya kaskazini. Katika utafiti uliosimamiwa na CCBRT, Radar development pamoja na DISABILITY AID ABROAD umeonyesha kuwa ni asilimia 0.7% ya waajiriwa ndio watu wenye ulemavu(CCBRT ikiwemo kwa kutoajiri walemavu ingawa ni taasisi ya kusimamia walemavu nchini)
f) Lakini kama hilo halitoshi gharama za matibabu ni za juu sana katika hospitali zilizo chini ya CCBRT, takwimu zipo; Gharama ya matibabu kwa CCBRT mtu binafsi anatakiwa kulipa kati ya dola 400-714 sawa na 600,000-1,071,000/= gharama hii ni kubwa ajabu kulingana na pato la kawaida la mtanzania na pia ni gharama ya juu hata kuzidi hospitali zingine hapa nchini ambazo hazipati msaada serikali wala mashirika makubwa ya nje na pia hazifanyiwi harambee kama CCBRT.,mfano CATARACT SURGERY HINDU MANDAL 400,000/=, AGA KHAN 315,000/= REGENCY 300,000/= MISSION MIKOCHENI 180,000 WAKATI CCBRT 680,000(Tom Venneste Appendix iii-nov 2008)

Pia CCBRT imekuwa haiko tayari kuwa wawazi juu ya kiasi cha mapato kinachochangiwa kutoka katika taasisi hizi kubwa duniani (dalili kubwa ya kuwepo ufisadi ndani yake)


Ama ukiacha hayo ambayo yanamgusa moja kwa moja Dr Slaa, pia kuna yanayowahusu viongozi wengine wa CHADEMA kama vile DIWANI WA KATA YA SERENGETI,MKOANI MARA KUKAMATWA AKIMILIKI AK47 KINYUME CHA SHERIA kiuhalisia huu pia ni ufisadi na hata yule MBUNGE WA CUF ALIYESHUTUMIWA KUINGIZA NCHINI MAGARI YA WIZI NA KISHA KUKWEPA KODI huu pia ni ufisadi ila inapotokea mambo kama haya yakifanywa na viongozi au wanachama wa CCM yatatangazwa vyombo vyote vya habari na pia suala hilo litabebeshwa kwa chama badala ya mtu binafsi.


Tuhuma zozote,mazungumzo yoyote na fikra zozote zinasikilizwa.Ila sio zote ziko sawa na mzungumzaji hazuiwi kwa namna yoyote ile asiwasilishe katika vyombo vya kijamii.
Mwalimu Nyerere wakati fulani alituhumiwa kula njama za kuipindua serikali ya Kenya chini ya uongozi wa Bwana Moi.
ALIWAULIZA WANAHABARI:MKIAMBIWA MIMI NI BABA YENU,YAANI NI MUME WA MAMAAKO UTAANDIKA NA KUAMINISHA WATU HIVYOHIVYO?
Pimeni kwa vipimo vilivyokamilika kabla hamjatoa taarifa kwa ajili ya michango ya wanaJF
 
Chagga people are leading for nepotism and favouritism among African societies, study suggests. Famous research conducted and compiled by the late Zimbabwean professor Julius Mambubwa on 'the effects of nepotism to the economic growth of Africa' documented that 50 percent of the employed Chagga people have had their current jobs through the influence of their fellow Chagga relatives.

Additionally, it went on showing that in nearly each of the public office which is headed by a Chagga, 45 percent of the workers are coming from Chagga tribe apparently getting their employment after someone at the top had pulled strings for them.
Hii ni kweli kabisa... nakubaliana na wewe kwa 100%
 
Haya maswala ya Ukabila na kazi Nyerere alielezea vizuri sana hapa chini,


“..the work of the civil servants and people in the parastatal organizations does require education..it so happened that the Tanzanians who had the opportunity for higher education under the colonialists were mostly Wahaya, Wachagga, and Wanyakyusa. And because most of the education was provided by missionaries, most of these people are also Christians. That was our inheritance. These conditions will change, but they have not changed yet. And for these reasons, when we get rid of the Europeans who were doing responsible jobs, and give these jobs to Tanzanians, the people who get them come mostly from one or other of these three tribes”.

“Therefore, if you ask me why Wahaya, Wachagga, and Wanyakyusa have most of the jobs which require higher education, the answer is very obvious. They were the ones who received higher education during colonial times. I’d say: investigate the position in politics where a man is not asked about his educational qualifications. Look at the Parliament, the National Executive and Central Committee of TANU, and at the Cabinet. How many Wanyakyusa, Wahaya, or Wachagga are members? You will find that perhaps there aren’t any, or there are one or two. This is the truth”

“.. if a Mchagga, a Mhaya, or a Mnyakyusa young man were refused work simply because of his tribe – when he is capable and there is no other Tanzanian with the qualifications – then we would be practising a very stupid and very evil kind of tribalism such as that which caused the establishment of Biafra. I beg you, my brothers, avoid ANYTHING WHICH COULD BRING OUR COUNTRY INTO THIS KIND OF DISGRACE”


(From: Uhuru na Maendeleo pp 76,77)

NB :: Part ya thread ya Mwanakijiji, sijapata link yake original but check hapa

Wahaya, Wachagga, Wanyakyusa Wengi Maofisini Ishara ya Ukabila?
 
Huwezi kuwakwepa wachaga kwenye ofisi yoyote hapa bongo unless walaumuni wazazi wenu kwanini hawakujenga shule na kuwapeleka shule.
 
CCM imarisheni chama chenu ujinga huu...siku hizi watanznia hamtawapata.
Nashangaa ujinga huu kuja hata humu, maana niezoea kuusikia wakiuongea watu wasio na upeo kabisa wakiuongea mitaani!
 
Swala hili ingawa limeletwa kwa kumtumia Dr.Slaa lakini ukweli unabakia kwamba kuna mchezo mchafu unachezwa dhidi ya wananchi hasa ktk maswala ya ELIMU na AFYA. Haiwezekani serikali kutoa ruzuku kubwa ktk kusaidia kuyaendesha mashirika haya lakini bado wananchi wanalipa gharama kubwa kuliko hata za private Hospitals..

Kinachotarajiwa na wengi ni kwmaba serikali inatoa ruzuku hizo ili kuwapunguzia gharama za matibabu wananchi na sio kusaidia chombo hicho kupata mtaji wa kufanya biashara. Ni lazima serikali iliangalie upya swala hili na hasa ktk Elimu na Afya, maswala ya exemption tax zifutwe kwa vyombo vyote walipe kodi kwa sababu mbali na ruzuku wanazopewa ukiongezea na exemption inatugharimu mara 10 na mlengwa hapa inaonyesha sio kuwapa huduma bora wananchi bali kulikuza shirika hilo. Na hakuna sababu ya kuwapa urahisi huu ikiwa bado wananchi inawagharimu sawa na kutotumia kodi zao kukiendesha chombo hiki.

Kama Dr.Slaa anafanya haya na lawama hizi ni za kweli inabidi abadilishe muundo mzima kama mfano bora kwetu japokuwa anaweza kutokuwa na madaraka hayo. Kuwa katibu wa kurugenzi wa shirika hili haina maana Dr.Slaa ndiye anayeandika Policies na jinsi ya shirika hili litakavyo endeshwa, ila maadam yeye kama mgombea Urais ambaye aliwaahidi wananchi kuwa huduma za Afya na Shule zitakuwa bure basi mfano bora lazima uanzie kuonyesha msimamo wake ktk uendeshaji wa shirika unaloliongoza.
 
Sasa wewe MAPURENDE ni mngoni wa wapi? wangoni ninao wafahamu mimi wapo makini kwenye hoja. Hoja iliyotolewa hapa ni tuhuma sasa haya ya Nape na CCM unayatoa wapi. Usitupotoshe tunahitaji kuujua ukweli kuhusu hizo tuhuma.
Mbali na hilo la ungoni mimi ni kiongozi wa CCM nipo hapa Lumumba. Nilitaka kuwaonyesha kuwa pale CCBRT hakuna hilo la ukabila wala ukanda na pili hakuna hizo gharama kabisa.
Ndg zangu wana CCM mbinu za namna hii tulizitumia 1995 na 2000, 2005 na 2010 tumezitumia zimetuachia makovu ya udini, watu hawapatani. Juzi nilipita kwenye duka la mpemba mmoja pale Mabibo ninapoishi ili nipate mahitaji yangu ikiwepo vocha ya simu, akapita sister mmoja wa kanisa katoliki, na yeye akataka kununua vocha. Yule mpemba alikataa katakata kumuuzia akidai hana hizo vocha, alipoondoka yule sister yule Mpemba akasema siwapendi wakatoliki tena akasema siwapendi nduguzake Slaa.
Wana ccm wenzangu tufanye propaganda lakini za kuwagawa wenzetu kidini na kikabila ni ujinga. Na ujinga huu anao sana Nape. Ni bosi wangu lakini bado ana utoto unaosababishwa na kuvimbiwa
 
Back
Top Bottom