Dr Slaa hajapona mkono?

sijamuelewa mwanzishaji wa mada, je mahusiano ya mkono na kazi zake zakichama yanahusishwaje. Slaa ni binadamu na ataendelea kuwa binadamu, ama uanadhani kaugaganga kabagamoyo kanakowadosha watu kamemkaba?
 
Bwahahahahahahaaahaaa.....Utaelewa tu:)
 
Nilipoanzisha mada sikuwa na lengo la kumnyanyapaa kiongozi wangu. Labda ni namna nilivyoipresent mada. Kimsingi ni masikiyiko yangu kwa kiongozi huyu kwa hali aliyokuwa nayo ingawa haijamfanya kurudi nyuma kimapambano. Tangu kumalizika kwa kampeni za ule uchaguzi sikuwahi kumwona hadi jana nilipomwona kwenye taarifa ya saa mbili usiku.
Mimi binafsi naungana na wana CDM na Watanzania wote wapenda maendeleo ya nchi hii kumtakia kila la kheri aweze kupona na kurudia hali yake ya kawaida. Kama walivyotangulia kusema kuwa mkono uliofungwa POP hukawia kurudia hali ya kawaida, basi nami naamini kuwa hali itatengamaa haraka iwezekanavyo kwa mapenzi ya Rabana.
Ni ukweli usiopingika kuwa Dr Slaa ni mpiganaji wa kweli na mwenye uchungu na nchi yetu. Kwa wale ambao wanaishi kiujanjaujanja kwa migongo ya hao mafisadi wanatamani asipone kabisa. CAMARADERIE amesema kweli kuwa hatutaki ashike vitu bali aseme vitu. Nakubaliana sana na wewe mkuu.
Mpiganaji wetu tuko nawe na tunakutakia kila la kheri upone haraka tuendeleze mapambano.
Peoplesssssssssssssssssssss!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Heri rais aliye sinyaa mkono kuliko rais aliyesinya ubongo.Hivi mkuu Eeka Mangi unakumbuka ile mieleka ya hapa na pale ya mkuu? Hata siku ya Mei mosi kama uliangalia vizuri ile ngoma ilibuma ila alijiwahi kwenye ambulance, si unakumbuka alijishika tama muda mrefu na kunywa maji mara kwa mara kisha akatoweka kwa muda hivi? Basi habari ndiyo hiyo.
 
Ushauri wangu kwa viongozi wa Chadema,
Nimeangalia mikutano ya Chadema pamoja na maandamano ya Mwanza, Mbeya, Sumbawanga, Dk Slaa naona mkono wake wa kushoto bado ujapona hanapata shida sana kushika kipaza sauti na ni muda sasa toka aumie, ushauri tafuteni mtaalamu wa tiba ya mifupa, misuli, viungo (Ophopaedisti) bingwa au mpelekeni India kwa mabingwa wa tiba ya mifupa. ARTEMIS HOSPITAL au APOLLO HOSPITAL ni ushauri tu wana JF
 
Nimeyaamini macho yangu kaka. Kwa walioona taarifa ya habari ya saa mbili watakubalina nami mkuu.
Jamani hebu kama kuna mweny taarifa za uhakika kuhusu maendeleo ya huo mkono atujuze, mimi pia nilishtushwa sana jana. Mungu amlinde na kumbariki
 
Ni kweli hajapona ila si kweli kwamba umri unasababisha kutopona haraka.Chadema mmeshindwa kumtibu Rais kwa miezi yote tisa au mnataka Magamba NEPI ajenge hoja zake dhaifu hapo?Aisee tupeni akaunti yake tumwezeshe ili uhuru uwahi tumechoka na ukoloni mpya
 
Ushauri wangu kwa viongozi wa Chadema,
Nimeangalia mikutano ya Chadema pamoja na maandamano ya Mwanza, Mbeya, Sumbawanga, Dk Slaa naona mkono wake wa kushoto bado ujapona hanapata shida sana kushika kipaza sauti na ni muda sasa toka aumie, ushauri tafuteni mtaalamu wa tiba ya mifupa, misuli, viungo (Ophopaedisti) bingwa au mpelekeni India kwa mabingwa wa tiba ya mifupa. ARTEMIS HOSPITAL au APOLLO HOSPITAL ni ushauri tu wana JF

Aliyemtupia jini lililo shindwa kumuondoa ili utabiri wake utimie na akaendelea kuminya kibuyu amekwisha yeya, hivyo atapona hivi karibuni kwa nguvu za Mungu.
 
Back
Top Bottom