Dr Slaa: Haijawai kutokea ktk serikali ya CCM

SOKON 1

JF-Expert Member
Dec 28, 2010
1,134
331
Dr Slaa anasema chama chochote cha upinzani kazi yake sio kukipigia makofi serikali iliyoko madarakani bali ni kuikosoa pindi inapoenda mrama kwa hiyo tangu miaka 50 ya uhuru haijatokea chama kukukosoa ama kuonesha kutokuwa na imani na serikali yao kama nchi zingine zinavyofanya pindi serikali inavyofanya hovyo na kutowajali raia wake.
Kutokana na chadema kuanza kuonesha izo movement kwa vitendo imewafanya waanze kuingiwa na hofu na badala ya kujibu hoja zao wao wanawaachia polisi ili iwazibiti pamoja na msajili wa vyama.Dr Slaa amewaambia huo ni mwanzo na wataendelea mpaka wawatoe watanzania gizani dhidi ya serikali yao na wala hawatishwi na lolote.
My take;
Kweli ccm inaongozwa na vipofu wasiojua watokapo na waendapo iweje washindwe kujibu hoja za chadema na pia baada ya kushauriwa wa Sumaye naye wamempinga. Hawa sio viongozi bali bora uongozi
Nawasilisha
 
Siku hizi kujadili vilaza waccm nashindwa naweza pigwa bun bure!
 
Hukosoi chama tawala kwa kusema uongo na ufataani na kuhubiri uvunjifu wa amani.
 
Njia sahihi ya kmja dikteta ni kuwajelimisha wananchi haki zao. Hapo atajitokeza balabala kwa kutoa kauli za kogopesha. Nimeanza kona CCM inaelekea huko.
 
Bado wanausingizi wa serikali niya chama kimoja hawataki kubadilika!
 
Hukosoi chama tawala kwa kusema uongo na ufataani na kuhubiri uvunjifu wa amani.

Billion 94, mabilioni ya kagoda,meremeta, tangold, EPA, ni uongo????!!!! kama ni uongo ccm na serikali wafafanue hayo mabilioni yaliliwa na nani na kwa nini??!!! Kinachofanywa na CDM siyo kuchochea vurugu; bali kuwaeleimisha wananchi kuelewa serikali yao ilivyo na namna ya kulinda maslahi na haki zao, period! Think!!!!!!!!
 
Hukosoi chama tawala kwa kusema uongo na ufataani na kuhubiri uvunjifu wa amani.
Chukua hali halisi ya Tanzania sasa kisha kama Dr Slaa anazungumza uongo juu ya serikali toka nianze kumsikia Dr sijawai kuona akiukumiwa ama kukamwatwa kwa anachokisema ila CCM wanapaki wakimuita mropokaji ila sasa maji yamewafika shingoni kwa kusingizia uvunjivu wa amani ili usijue maovo ya serikali.
Najua wewe ni mojawapo ya wale ambao bado wapo wamelala so stil naping
 
Tatizo ni kama mkuu mmoja alivyowahi kusema humu jamvini kuwa hawa ccm wanaishi kwenye karne ya analogue wakati sasa tupo kwenye digital sasa hawawezi kukaa pamoja na sisi.
 
Dr Slaa anasema chama chochote cha upinzani kazi yake sio kukipigia makofi serikali iliyoko madarakani bali ni kuikosoa pindi inapoenda mrama kwa hiyo tangu miaka 50 ya uhuru haijatokea chama kukukosoa ama kuonesha kutokuwa na imani na serikali yao kama nchi zingine zinavyofanya pindi serikali inavyofanya hovyo na kutowajali raia wake.
Kutokana na chadema kuanza kuonesha izo movement kwa vitendo imewafanya waanze kuingiwa na hofu na badala ya kujibu hoja zao wao wanawaachia polisi ili iwazibiti pamoja na msajili wa vyama.Dr Slaa amewaambia huo ni mwanzo na wataendelea mpaka wawatoe watanzania gizani dhidi ya serikali yao na wala hawatishwi na lolote.

My take;
Kweli ccm inaongozwa na vipofu wasiojua watokapo na waendapo iweje washindwe kujibu hoja za chadema na pia baada ya kushauriwa wa Sumaye naye wamempinga. Hawa sio viongozi bali bora uongozi
Nawasilisha

CCM ndio wanatakiwa wafutwe na Msajili wa vyama na viongozi wake wakamatwe na Polisi kwa kukosa sifa ya kuwa chama cha siasa, kuongozwa na viongozi karibu wote wanatuhumiwa kwa ufisadi, wanachochea udini na ndio wamelipeleka taifa na jamii nzima ktk janga kubwa la umaskini, maradhi na ujinga wa kupindukia na wanataka watanzania wabakie wajinga na waoga siku zote.

Hawa ni Viongozi gani wa chama ambao wanajitapa wapo wengi nchi nzima, na wamejaa uzoefu wakati wanashindwa kujibu hoja za viongozi wanne wa ngazi za juu za Chadema? Hicho ni chama kweli au mizimu inafurahia jasho na rasilimali za taifa?
 
Naunga Hoja mkono. CCM wameshachoka kwa kuwa hawana kipya tena ila ni majungu, fitina, kutokusikiliza ushauri na hata kuonyesha dharau kwa sis Watanzania wenye nchi yetu.
Doctor wa UKWELI na CDM endeleeni kutufumbua macho Watanzania tuliolala usingizi fofofo la sivyo tutastuka wakati chama cha matumboni wamemaliza kila kitu!.

GO CHADEMA GO!.
 
serikali haiwezi kuzuia movement za chadema, imeshindwa kuzuia kupanda kwa bei ya sukari na bidhaa kadhaa zinazozalishwa hapa nchini, imeshindwa kuzuia upandaji wa mafuta na nauli za mabasi, inaweza kuzuia nini serikali yetu? imeshindwa kuzia mgao wa umeme? kuzuia malipo ya dowans? hebu niambie serikali yetu inaweza kuzuia nini?
 
Hukosoi chama tawala kwa kusema uongo na ufataani na kuhubiri uvunjifu wa amani.

Mkuu,
Amani kwako unaitafsiri vipi?
Maana sioni maana halisi ya mani pale maisha yanavyokuwa magumu...
Vyakula bei juu... maji ndo kama wimbo wa taifa... umeme pamoja na kupanda bei..... bado unapatikana kwa mgao (mgao ambao hauna mwisho)... mashule yamebaki kuwa sehemu ya kupigia siasa.....
Yote haya bado unasema una amani mkuu....

Serikali yetu imekosa dira na muelekeo, ni kama vile tumebaki kusubiri kudra za Allah!!! Mwanye nchi badala ya kutulia na kutumia watu wake kutatua matatizo haya, ndo kwanza anapaa kwenda ulaya.... wewe bado umelala na ngoma za amani!!!

Amani?....my foot. %***s*en.#%^&&...
 
Chadema na wananchi lao moja sasa mbona CCM inaogopa kuwasema wananchi wanaoambatana na Viongozi wa Chadema kwenye maandamano wanaogopa nini, au wanakijua wanachokiogopa
 
Hukosoi chama tawala kwa kusema uongo na ufataani na kuhubiri uvunjifu wa amani.

Toa ushahidi... wapi, lini na nani na useme kilichozungumzwa cha uvunjifu wa amani. Hivi watu wakiambiwa kitu hiki kingetakiwa kiwe hivi (kuelimishwa) ni uvunjifu wa amani??? Ndo maana Serikali hii inatoa elimu duni tena kwa wachache (haiwezeshi) ili wananchi waendelee kubaki katika SIFAHAMU lengo lao asitokee anayehoji ili wabaki madarakani milele? Kumbukeni hakuna marefu yasiyo na ncha.. Mwisho wa utawala dhalimu wa CCM ni huu na inabidi wakubali tu.
 
Back
Top Bottom