Elections 2010 Dr. Slaa: CCM imebanwa Igunga; yajipanga kuchakachua kura

Ukiona mtu mzima tena ana PHD ya ucha mungu kutoka vatikan anadanganya ujue anazeeka vibaya na ndio matatizo ya kuanza mapenzi uzeeni haya.Kulalama kwa chadema na cuf ni alama tosha kuwa CCM imeisha shinda.

Sasa si ujitokeze kwa ile ID yako inayojulikana, inakuwaje kigogo wa chama kila unapotaka kutoa hoja za kipuuzi unajificha nyuma ya hii mi-ID????? This shows hata wewe unatambua unachokiongea ni pumba. Bado siku nne mkuu vp safari bado ipo??
 
Sasa si ujitokeze kwa ile ID yako inayojulikana, inakuwaje kigogo wa chama kila unapotaka kutoa hoja za kipuuzi unajificha nyuma ya hii mi-ID????? This shows hata wewe unatambua unachokiongea ni pumba. Bado siku nne mkuu vp safari bado ipo??

Ina mana hii pia ni ya nepi!
 
Ukiona mtu mzima tena ana PHD ya ucha mungu kutoka vatikan anadanganya ujue anazeeka vibaya na ndio matatizo ya kuanza mapenzi uzeeni haya.Kulalama kwa chadema na cuf ni alama tosha kuwa CCM imeisha shinda.
Muongo na mwizi wa kura ni wewe!
 
Kama ndivyo basi huwa mnashindwa kihalali . Mbinu mnazijua na mnasema mnazidhibiti halafu mnashindwa, hapo hakuna kuibiwa kura huwa mnashindwa kihalali.

Tukidhibiti mnakimbilia ohhh kavuliwa hijabu, oohhh wanaleta fujo......lakini hayo hayatutishi tutaendelea kudhibiti tena na tena.
Hoja yenu ya udini haina mashiko tena.

Mkuu umesikia kuwa Fatma Joseph Kimario ni Mkristu tena Mkatoliki. Mumewe ni Mzee wa Kanisa pale Mwenge, tena wanajihusisha na Ufugaji wa nyama pendwa ya nguruwe.
Fatma na mumewe ni ma-supplier wazuri sana wa bidhaa hiyo inayopendwa na watu wa dini zote hapa jijini.
 
CDM bana mkipingwa kidogo kwa hoja zenu dhaifu mnazoleta ndani, mnaanza kuwatishia watu kuwa ban, sasa hapo watu wataacha kuamini vp kuwa JF ni jukwaa la CDM? ni ngumu kulibishia hili labda uwe zuzu

Naomba uache kutumia hilo jina (geniusbrain) au ubadilike! Usipofanya hivyo nitakutolea uvivu.
 
Ukiona mtu mzima tena ana PHD ya ucha mungu kutoka vatikan anadanganya ujue anazeeka vibaya na ndio matatizo ya kuanza mapenzi uzeeni haya.Kulalama kwa chadema na cuf ni alama tosha kuwa CCM imeisha shinda.

Hivi huwezi kutoa hoja halisi bila 'personal attacks' ambazo zinapindisha hoja na zinaanzisha msururu wa 'more and more personal attacks'?
Kukujibu ni kuwa wewe umetumwa ndo maana unaandika usiyojajua. Be independent.
 
ZIKIWA zimesalia siku nne kabla ya wananchi wa Igunga kuamua nani atakuwa mbunge wao, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbroad Slaa amenasa siri nzito ya jinsi vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), walivyojipanga kuiba kura, Tanzania Jumatano limebaini.

Akizungumza na gazeti hili jana katika mahojiano maalum, Dk. Slaa alisema kwa takriban wiki moja sasa, CCM imekuwa ikifanya mbinu mbalimbali na juzi na jana walikuwa na vikao vizito kupanga jinsi ya kuiba kura baada ya kubaini kuwa chama hicho hakiwezi kushinda.

“Safari hii, CCM wamekabwa kwelikweli na ukiona mtu mzima (CCM), analalamika, ujue ameshikwa mabaya. Sasa kwa kujua hilo, wamepanga mikakati ya kuiba kura. Jana walikuwa na kikao cha siri kilichofanyika Peac Hotel na leo walikuwa na kikao kingine, mipango na kila walichojadili nimepata,” alisema Dk. Slaa.

Dk. Slaa ambaye amepata kuwa mgombea urais wa CHADEMA katika uchaguzi uliopita na kutoa ushindani mkubwa kwa mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, alitaja mbinu nyingine ya CCM kuhakikisha inapata ushindi kuwa ni pamoja na kutengeneza kura hewa, kuchoma karatasi za kula kama walivyofanya Msalala, kununua shahada na kuwapiga wafuasi wa CHADEMA.

“Kama mlivyosikia, tayari wameanza kuwapiga watu wetu, wameanza kuwapa vitisho, vijana wanakamatwa na kuwekwa ndani hovyo ili kuwatisha,“ alisema Dk. Slaa.

Kiongozi huyo wa CHADEMA, pia alisema mbinu nyingine inayotumiwa na CCM ni kumwaga pesa na kutolea mfano wa kijiji cha Karenga ambacho kimepewa sh milioni 10 kwa kisingizio cha kutumika kwenye miradi ya maendeleo, jambo ambalo alisema sio kweli.

“Katika baadhi ya vijiji jana nilishuhudia mwenyewe watu wa CCM wakigawa mahindi. Vijiji hivyo ni Mwamwapuli, Mwamwagogo na vingine ambavyo sivikumbuki kwa sasa, kote huko waligawa mahindi ili kuwarubuni wawapigie kura,” alisema Dk. Slaa.

Hata hivyo pamoja na mbinu zote hizo za kuiba kura, Dk. Slaa alisema chama chake kimejipanga vizuri na kuwahakikisha wanachama wake kuwa hakuna kura itakayoibwa.

“Nakuhakikishia, mbinu zote tunazijua, tumejipanga vizuri sana kuhakikisha hakuna hata kura moja itakayoibwa au kuchomwa moto. Tutapambana hadi tone la mwisho na tuko tayari kufia kwenye vituo vya kupigia kura,” alitamba Dk. Slaa.

Alilitahadharisha jeshi la polisi pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwa makini siku hiyo, vinginevyo taifa linaweza kuingia katika matatizo mazito sababu ya kuibeba CCM ambayo alisema kwa sasa haibebeki.

Malalamiko ya Dk. Slaa, yaliungwa mkono na Chama cha Wananchi (CUF) ambacho kimedai kuwa CCM ina mpango wa kuiba kura na inacheza rafu kwa kuleta malori saba ya sukari, kugawa mahindi na kuingiza Janjawid ili kuwatisha wananchi wa Igunga siku ya kupiga kura.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF bara, Julius Mtatiro, aliliambia gazeti hili kuwa malori hayo yako njiani kutoka Mara kuelekea Igunga kwa lengo la kugawa kwa wapigakura.

“Kwa sababu vyombo vya dola ukiripoti havitachukua hatua kwa vile wanailinda CCM, tumejipanga vya kutosha kuyadhibiti malori hayo, tunazo taarifa za kutosha tunajua yamelala wapi juu wameweka nini, chini wameweka nini.

“Tumewapanga vijana wetu na tutayakamata kwa nguvu zetu kisha tutawaonyesha waandishi wa habari na taifa lione, tunatoa tahadhari kwamba mbinu zao zimegundulika, makontena ya sukari yanaletwa Igunga ili kuigawa siku mbili kabla ya kupiga kura.

“Hatutakubali haki za Watanzania kuchagua kiongozi bora ziondolewe kwa sababu ya kilo za sukari…tunalishughulikia hili,” alisisitiza kiongozi huyo wa timu ya kampeni za CUF Igunga.

Aidha, ameionya CCM kuacha mpango wa kutaka kugawa mahindi Septemba 30 na Oktoba mosi kwa wakazi wa jimbo hili kwa kuwa hiyo ni rushwa wanayoitoa kwa mgongo wa njaa.

“Hapa tunaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuingilia kati; CCM imepanga miundombinu ya kuhakikisha wakazi wa jimbo zima la Igunga wanapatiwa mahindi; wanayo magari ya kutosha ya kugawa mahindi licha ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa kutetea jukumu hilo.

“Huwezi kuikamata serikali; inasema hapa pana njaa tumeliacha. Tunalo tatizo kubwa; walikua wanayagawa mahindi hayo kwa ngazi ya kata sasa wanataka kuwarubuni wapigakura kwa kugawa tena kwa jimbo zima.

“Kama watu wameweza kukaa kipindi chote hicho wakiwa na njaa hawawezi kufa tarehe 30 na tarehe mosi tuwaache wakapige kura halafu CCM wapite wagawe mahindi yao tarehe 3 hapo hatuna shida lakini wakiendelea na mkakati huo tumejipanga kuwazuia wasigawe mahindi hayo,” alisisitiza Mtatiro.

Naibu katibu mkuu huyo amelalamikia pia vitisho vinavyotolewa na vijana wa CCM aliowataja kuwa ni Janjawid ambao wamemaliza semina yao mjini Shinyanga huku akidai kuwa wataingia mjini Igunga leo usiku.

“CCM tumewakalia maji ya shingo hivyo wanahitaji vijana hao wafanyekazi ya kutengeneza vitisho kwa wananchi ili wasijitokeze kupiga kura hasa kwenye maeneo ambayo hawaungwi mkono.

“Tathmini yetu kwenye uchaguzi huu inaonyesha kati ya kata 26 tumebaini CCM hawaungwi mkono katika kata 19 kwa hiyo msistuke hapa tarehe 30 mkakuta watu wamekatwakatwa mapanga ili wasiende kupigakura…

Alisema wamejipanga kudhibiti wizi wa kura kwa kuwa na majina ya wapigakura kwenye vituo vyote 427 vya jimbo la Igunga, huku akiitahadharisha CCM kutafuta mbinu nyingine ya kuiba kura.

Akizungumzia madai ya CUF kwa njia ya simu, Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Makao Makuu ya Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Issaya Mungulu, amekana kupokea taarifa za Janjawid.

“Siku zote nasema hawa wanasiasa wanatuingiza kwenye propaganda zao, sisi polisi hatuna taarifa zozote kuhusu madai ya CUF wala Janjawid labda wamepeleka kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo,” alisema kamanda Mungulu
 
Tutajua tu.Bado ningependa wananchi wapewe nafasi na uhuru wote kuchagua wanayemtaka.KUKANDAMIZANA hakusaidii.UCHU NA UBINAFSI hausaidii.MAGUVU NA UDANGANYIVU navyo havisaidii.
 
wakati unapanga kuzuia kuibiwa kura nadhan plan B ni kufanya na wewe kura zako ziwe nyingi.
 
Tatizo la uzee ndio hili, kila kukicha anachanganya maneno. Je 2015 hiki kibabu sijui kitakuja na stori gani. Jamani CDM mlikua mnawasema wazee wa CCM sasa mbona mko kimya na huyu kikogwe wenu?
 
Mods isitoshe tu kuiondoa Post ya Omr isipokua mngempa Ban ya ukweli kwa sababu hawezi mtukana Dr Slaa ndio maana nilijaribu kureply nikaambiwa sina access hyo,kipi cha ajabu ambacho Dr Slaa kakosea juu ya hizo wakati inajulikana wazi kua CCM ni wezi wakubwa wa kura na wanajulikana na mbinu zao chafu za kuiba kura? Madai ya Dr Slaa yana ukweli kabisa sio kupuuza kama baadhi ya wana Magamba wanavyotaka kutuaminisha hapa.
Kazana wewe mtoto wa kiume, hatuko shule hapa kwenda kushitakiana kwa mkuu. Tizama maana ya mpumbavu ndio uanze kulalamika. Hakuna tusi hapo. Mtu akishaanza kuwa punguani ni sawa na mpumbavu.
 
Ukigundua njama mapema, na wewe weka njama. Kwani maana ya Siasa ni kukuachia wewe ushinde? Siasa ni njama, hata maandamano ya kila siku ni njama za kisiasa.
 
Ukiona mtu anaanza kuota kuibiwa ujue hayo ni maandalizi ya kufanya fujo watakaposhindwa waseme si tulisema wataiba kura?. Haiingii akilini umegundua njama, unajua njia zinazotumika kuoba, umeweka mawakala kila kona, kura zinahesabiwa vituoni mbele ya mawakala wa vyama vyote na tena umetangaza kuwa mmejipanga vizuri kuhakikisha kura haziibiwi halafu siku ya siku umeshindwa udai umeibiwa!...Uchaguzi kuna kushinda na kushindwa tuache uroho wa madaraka kwa gharama za damu na roho za watu..TUKUBALI MATOKEO
 
Umezeeshwa hivyo ndugu yetu...................yaanikm haupo duniani bvile

mmeanza kuleta visingizio sasa.chadema inatoa vitisho kuwa itapambana mpaka tone la mwisho, kwani tuko vitani?,tuko tayari kufia kwenye vituo vya kupigia kura,jamani hivi sinivitisho?.visingizio vya nini kama unauhakika wa kushinda?.nyie kila siku mnaibiwa na njia za wizi mnazifaham kwanini msizitumie kama mnazifaham sasa?.
 
Ukiona mtu analalamika kuwa amegundua njama za kibiwa kura ujue anaandaa kisingizio cha kufanya fujo matokeo yatakapotangazwa na kujikuta amegalagazwa. Haiingii akilini mtu umegundua njama na unajua wizi unavyofanyika then usubiri hadi uibiwe ndiyo utoe visingizio!
 
Tamko la Chadema baada ya October 2!
1.CCM ili iba kura kwa kutumia usalama wa Taifa
2. NEC ilipendelea CCM
3. Polisi walikuwa wanailinda CCM
4. CCM waligawa mahindi
5. Kulifanyika Uchakachuaji mkubwa
6. Kuna kiongozi wa ngazi ya juu katusaliti Chadema alipeleka mikakati yetu CCM
7. Mgombea wetu alikua hana haiba ya kuwa Mbunge na gharama zote hadi maji ya kunywa alitegemea Chadema
8. Kwa ujumla tumehujumia!
 
Inawezekana madai ya Dr Slaa yanaukweli usio weza kuthibitishika ndani yake

Lakini inawezekana pia ikawa ni siasa chafu za kuwaanda watu waamini CDM imeonewa pindi ikishindwa hata kihalali

Pia inawezekana ikawa ni inferior complex tu ya CDM.

All in all let wait and see
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom