VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Hakuna Mahakama hata moja nchini Tanzania itakayotamka kuwa kifungu cha 160 cha Sheria ya Ndoa,1971 kinaonesha uwepo wa ndoa badala ya Dhanio la Ndoa. Hata Jaji Laurence Kaduri anajua vyema. Ni jana tu Jaji Laurence Kaduri wa Mhakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam alitupilia mbali Pingamizi la Awali la Dr.Wilbrod Peter Slaa dhidi ya Shauri lililofunguliwa na Rose Kamili(MB) dhidi ya Dr.Slaa na Mchumba wake Josephine Mushumbusi.
Katika shauri la Rose Kamili,msingi mkubwa wa shauri lake ni uwepo wa ndoa kati ya Dr. Slaa na Rose Kamili. Sheria ya Ndoa niliyoitaja hapo juu inabainisha wazi kuwa kuna aina mbalimbali za ndoa zikiwemo za kidini na za kimila. Nina uhakika,Mheshimiwa Rose Kamili hakuwahi kufunga ndoa na Dr.Slaa. Yeye ataegemea tu Dhanio la Ndoa chini ya kifungu cha 160 cha sheria ya Ndoa. Hiki hutumika tu pale panapotokea sintofahamu kwa watu wanaodhaniwa kuwa wameoana lakini kisheria sivyo.
Kimsingi,Rose Kamili anaweza kupata matunzo ya watoto lakini si kukataza ndoa ya Dr.Slaa. Kuzuia ndoa si jambo la mchezo.Ni hadi athibitishe kuwa aliolewa na Dr.Slaa tena kwa ndoa ya mke mmoja ima ya kidini,kimila au bomani. Hapo patamshinda Rose. Lakini,Rose aweza kulalia muda hadi kesi ya msingi kuisha.Wakili Msomi wa Dr.Slaa,Mutakyamirwa,awe makini.
Nimuombe Dr.Slaa kuvumilia kwa muda wa shauri hili ili aweze kuendelea na ndoa yake na Josephine. Hakuna haja ya kushtushwa na kutupwa kwa Pingamizi la Awali.Ni mambo ya kawaida Mahakamani. Ingawa ndoa iliyopangwa kufungwa tarehe 21/7/2012 imeshacheleweshwa vya kutosha,kama ipo ipo tu.Kama Dr. Slaa ameweza kuvumilia kwa muda wote uliopita,atashindwaje kuvumilia kipindi hiki cha kesi tu? Naamini hashindwi. Kila la kheri Dr.Slaa! Nakuaamini sana.