Dr Slaa atolea ufafanuzi Kuongezeka kwa posho za wabunge

Nipo naperuziperuzi makala ya Rugemelezaa Nshala MwanaHalisi ya J'5 Jana uk 13 aya ya 2 kutoka mwisho kabisa Namnukuu "Hata rais lazima alipe kodi.Msamaha wa rais kutolipa kodi ni dhana potofu inayomuona rais kama mfalme.Zawadi ambayo Rais Jakaya Kikwete anayoweza kuwapa Watanzania leo, ni kubadilisha sheria ya kodi ya Mwaka 2004 ili naye alipe kodi". Kumbe huyu Mbaba na Ukuu wote naye Mtoro wa Kodi??? Halafu sijui analipwa mi-dola mingapi jumlisha miposho,pamba & buti bure kabisa!!Siku CCM ikitoka madarakani itafilisiwa mpaka vibanda vyake vya chips kwa madeni ya kodi,tena tutamtumia yule yule Kitilya maana atakuwa anawajua vizuri jinsi wanavyokwepa kodi,ili awaumbue kama alivyotumwa na CCM wakati ule awadai CDM wakati anajua dhahiri chama chake hakijawahi lipa kodi hata senti,rejea mabango ya JK-2010 kutoka Canada na kwa Cameron!!
 
sifikiri kama atakuwa jipya zaidi ya kuanza kulia kodi za mshahara wake anaopokea.

Yeye anapata zaidi ya wabunge. Tsh milioni sabaa sio mchezo

Mimi binafsi huwa sitegemei jambo la maana kutoka kwa mujahidina. Kaka hapa hatuzungumzii ndoa, tunazungumzia mustakabali wa taifa letu.
 
Kumbe ule uvumi kwamba mshahara wake wa sasa unatokana kufanya mahesabu ya mafao ya ubunge..duh
 
Mshahara wake wa milioni 7 kwa mwezi na posho, ambao haulipiwi kodi nao kautolelea ufafanuzi?

labda mshahara huo unamlipa wewe weka data hapa ku justify your statement, otherwise nitakuchukulia kuwa au huelewi uanachosema au huna akili au vyote pamoja..
 
Tatizo la pro-Chadema JF ni upeo wa kupambanua mambo..

Hawataki kabisa watu wahoji mshahara wa Dr. Slaa pamoja na posho zake anazopewa Chadema, lakini wanataka Dr.Slaa yeye ndio awe mwenye mamlaka yakuhoji posho za wengine..

Mimi binafsi lazima nihoji posho zote ikiwemo mshahara wa Dr. Slaa sababu ndani hizo posho mishahara kuna kodi yangu nalipa serikali kuu

Hongeara sana bi S.S! Sikusikii siku hizi ukipiga mipasho kwenye media, imekuwaje? Au umeamua kumpigia debe EL ili nawe uupate U-PM kwa kigezo cha genda?
 
Nyie mnaopenda kuhoji mshahara wa Dr slaa fahamuni yule ana Presidential Status penda msipende,anatunzwa na chama kwa status hiyo na sio ukatibu mkuu tu! Kama mnabisha mtabishana na risasi one day! ebo!
 
mshahara wa dr.salaa upunguzwe...whatever you call it mshahara,posho etc etc,unamnyima somehow moral authority ya kuzungumzia mishahara ya wabunge...labda anielimishe mtu otherwise
 
Mwalimu Nyerere katuachia kazi kweli...kichwa kama hiki kinadhani kodi wanalipa matajiri tu...

Mkuu hata wewe ukinunua Soda, Sabuni, Vocha za simu, Mkate, Unga, Chumvi, unalipa kodi!

mkuu ritz unga ni exempt supply(kama sio zero rated)haulipiwi VAT unless ukiwa kwenye package...correct me if iam wrong
 
mkuu ritz unga ni exempt supply(kama sio zero rated)haulipiwi VAT unless ukiwa kwenye package...correct me if iam wrong

Pumba zingine bana...mkuu kwa hiyo unataka kuniambia ule Unga wa Sembe na Unga wa ngano unaouzwa na Mohamed Enterprise, Bakharesa, ukinunua ulipi kodi?
 
Mshahara wake wa milioni 7 kwa mwezi na posho, ambao haulipiwi kodi nao kautolelea ufafanuzi?

Tunasubiri utolee ufafanuzi wewe!!

CDM walishatoa ufafanuzi na humu ukajadiliwa. Au akili yako huwa haitunzi kumbukumbu!!!!
 
Nimepapenda hapo mwishoni anaposema "Wenye maaamzi ni watz amba kama waliwachagua kwa kishondo basi tusishangae kupigwa kwa kishindo hichohicho!"

Kiongozi bora anapimwa kwa hoja jinsi anvyojipambanu. Huyu mzee anatufaa.
 
Back
Top Bottom