Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema ameshangazwa na taarifa za tishio la wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) za kutaka kugomea kujadili muswada huo. Amesema endapo watayagomea marekebisho hayo na kuyarudisha kwa Rais Kikwete anaweza kuamua kuvunja Bunge kwa mujibu wa Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, juu ya taarifa za wabunge wa CCM kutishia kugomea mjadala wa marekebisho hayo. Alisema wabunge wa CCM wanapaswa kuzingatia utaratibu uliotumika kupata maoni mbalimbali yakiwamo ya vyama vya upinzani, taasisi zisizo za kiserikali ambazo zilitoa maoni yake.
Alibainisha kuwa wabunge wa CCM wasiozidi 300 hawawezi kuzuia maoni ya Watanzania wasiopungua milioni 40 na endapo watafanya hivyo watakuwa wanamwelekeza rais kuvunja Bunge. "Wabunge wa CCM wakumbuke kwamba serikali imepeleka muswada huo kwao si kwa sababu yametolewa mapendekezo na CHADEMA au chama cha siasa tu, umejadiliwa na Watanzania wengi. "Kama kweli wataugomea na kuurudisha kwa rais tena, rais anaweza kuamua kuvunja Bunge kwa mujibu wa Katiba," alisema.
Dk. Slaa alisema anashangazwa sana na wabunge wa CCM ambao wamekuwa wakijigamba kwamba serikali inayoongozwa na chama chao ni sikivu halafu hao hao tena washindwe kutekeleza yaliyofikiwa na serikali hiyo hiyo. Alisema wabunge ni lazima waonyeshe uzalendo wao kwa Watanzania kwa kujadili muswada wa mabadiliko ya sheria badala ya kushindana na mamlaka ya rais
SOURCE:TANZANIA DAIMA