Dr. Slaa athibitisha EPA ni ya Mkapa Arumeru.

Losambo

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
2,612
864
WanaJF katika kufunga kampeni za jimbo la Arumeru Dr. W. P. Slaa alizungumzia kashfa kubwa sana juu ya rais mstaafu Benjamin W. Mkapa alisema wapinzani ni vifaranga!!!! Kauli hiyo ilikuwa ni kejeli na dharau kwa wapinzani jambo ambalo Dr. W. P.Slaa aliona asilifumbie macho na kuamua kumlipua katika mkutano uliofanyika USA kabla ya kwenda kuhitisha kampeni katika viwanja vya Patandi USA ambapo ilikuwa ni funiko bovu kwa jinsi watu walivyoitikia wito.

Hebu msikilize Dr. Slaa akimkaanga BWM.



Namshauri Mkapa kuachana na siasa ambazo hazina tija kwake hasa ukizingatia siyo kiongozi aliyekuwa msafi sana alipokuwa Ikulu yetu.

Nawakilisha.
 
Last edited by a moderator:
WanaJF katika kufunga kampeni za jimbo la Arumeru Dr. W. P. Slaa alizungumzia kashfa kubwa sana juu ya rais mstaafu Benjamin W. Mkapa baada ya yeye kuwananga wapinzani kuwa vifaranga!!!! Kauli hiyo ilikuwa ni kejeli na dharau kwa wapinzani jambo ambalo Dr. W. P.Slaa aliona asilifumbie macho na kuamua kumlipua katika mkutano uliofanyika USA kabla ya kwenda kuhitisha kampeni katika viwanja vya Patandi Tengeru ambapo ilikuwa ni funiko bovu kwa jinsi watu walivyoitikia wito.

Habari hii haikupata coverage kubwa lakini kama kawaida wanaJF tunajuzana, hatunyimani.

Hebu msikilize Dr. Slaa akimkaanga BWM.



Namshauri Mkapa kuachana na siasa ambazo hazina tija kwake hasa ukizingatia siyo kiongozi aliyekuwa msafi sana alipokuwa Ikulu yetu. Akikaa kimya mchango wake katika taifa hili unaweza kuendelea kuheshimika.

Nawakilisha.
 
Last edited by a moderator:
Mkapa ni fisadi hilo halina ubishi,nakumbuka kauli ya JK akimtetea Mkapa alisema TUKIANZA KUWASHITAKI MARAIS WASTAAFU BASI VIONGOZI HASA MARAIS WATAKUA WANANG'ANG'ANIA KUKAA MADARAKANI MILELE!!!
 
Akashitaki kama anaona kuna kosa na ana ushahidi

JK aliposema wezi walioia EPA warudishe fedha zetu alikuwa mjinga? Nchi tatizo kubwa ni kubebana ndiko kunakotuhangaisha hata kama kitu kitu kipo wazi. Au unataka Lusinde atoke Mtera aje akueleze na hilo?
 
Kampuni ya Mr. and Mrs. Benjamin Mkapa, "TanPower Resources Limited, S.L.P 15 Luthuli Street, Dar-es-Salaam, ambayo ni Ikulu yetu."

Nilidhani Ikulu iko mtaa wa Magogoni. Nafahamu anwani za marais wengine za 10 Downing Street na 1600 Pennsylvania Ave, n.k. lakini ya Ikulu ya nchi yangu mwenyewe siijui, aibu, you know? Nadhani tatizo ni poor media, hawaandiki vitu hivi. Sasa sijui hilo S.L.P 15 Luthuli Street ni plot namba ngapi.
 
Ipo siku wezi wote na wahujumu wa mali za nchi watafikishwa mahakamani, kwa hilo hakuna ubishi. Kwa sasa hivi bado hawajafikishwa kwa vile utawala wa sasa pamoja na vyombo vya dola vinawalinda. Pindi itakapokuja serikali yenye uongozi bora na yenye kufuata maadili, lazima watafikishwa mahakamani. Jambo hili ni lazima, hata kama itakuwa imepita miaka mingi. Kumbuka kesi ya Pinochet wa Chile na wengine. Wanaotuhumiwa kwa wizi, hujuma na mauaji, kaeni chonjo
 
Ipo siku wezi wote na wahujumu wa mali za nchi watafikishwa mahakamani, kwa hilo hakuna ubishi. Kwa sasa hivi bado hawajafikishwa kwa vile utawala wa sasa pamoja na vyombo vya dola vinawalinda. Pindi itakapokuja serikali yenye uongozi bora na yenye kufuata maadili, lazima watafikishwa mahakamani. Jambo hili ni lazima, hata kama itakuwa imepita miaka mingi. Kumbuka kesi ya Pinochet wa Chile na wengine. Wanaotuhumiwa kwa wizi, hujuma na mauaji, kaeni chonjo

Na hicho ndicho kinachowatia wazimu watawala wengi wa nchi za kiafrika. Wanapokuwa Ikulu hawawatumikii wananchi kwa usafi bali kwa ubinafsi. Kasumba hii isipoachwa, demokrasia ipo mashakani sana. Sauti ya watu kupitia masanduku ya kura inaweza kufunikwa au kupotezwa.
 
Back
Top Bottom