Gurudumu
JF-Expert Member
- Feb 5, 2008
- 2,349
- 261
Nimetoka mazoezini sasa hivi. Nilipitia kibanda cha magazeti kununua machache. Kulikuwa na watu 8 niliokadiria umri wao kuwa Kati ya miaka 25 hadi 40. Mjadala ulikuwepo wenye hisia mchanganyiko kati ya furaha, hasira, matumaini, na kukata tamaa. Ilikuwa hivi;
mtu1. Yaani leo sijalala, hakiamungu. Furaha, mimi nilikuwa namsoma slaa kwenye magazeti tu na kwenye tv wanamtoa sentensi moja au mbili. Jana anaulizwa maswali live yani anajibu chap chap na majibu yake yameenda shule na yanaingia akilini. Yaani siamini, si mchezo mwanagu. Ulimwona?
Mtu 2: Mimi husikiliza zile hotuba za kikwete za kwenye tv za kila siku, sijui huwa ccm wanazilipia? Yaani Kama ulimsikiliza Slaa unagungua kikwete ni mzitooo! Anaongea Kama babu aliyeshiba mnazi anasimulia wajukuu hadithi jikoni usiku, na wajukuu wenyewe wanasinzia.
Mtu 1: nakuambia tusubiri hiyo tarehe 31, mimi nikitoka kupiga kura nakaa na radio yangu na kalamu na daftari, kuandika matokeo nchi nzima.
Mtu 3: shida ya ccm wapiga kura ni wengi mwaka huu kuliko wanachama wa ccm. Wengi vijana ambao hawajawahi kuhudhuria semina za ccm na kulipwa posho. Wanataka mustakabali wa maisha yao, wanahangaika maisha magumu, ccm haina majibu yenye akili.
Mtu 4: tumia dayansi bwana, sisi wazoefu. Vijana hawawezi kushinda kwenye foleni jua kali ili wapige kura. Hawatulii, wana mambo mengi biashara nini starehe, siyo rahisi. Lakini wazee, wamama? Yuko radhi kukaa tangu asubuhi hadi usiku hata bila kula.
(kunakuwepo ukimya fulani baadhi wakitikisa vichwa kuafiki)
mtu 5: lakini mnawajua ccm katika kuiba kura?
Mtu 1: Slaa kasema kila mtu alinde kura, Tena anasema mbona karatu, musoma, kigoma, na moshi wameweza kulinda kura?
Mtu 6: mnajidanganya, taratibu zimeshabadilika. Utalindaje kura wakati umeambiwa ukishapiga kura nenda nyumbani. Hakuna tena mambo ya kukaa mita 100. Unafikiri wao wajinga. Hao mawakala wenu watawekwa sawa, na nyie mtabaki kulalamika tu.
(kunatokea mjadala wa hasira kali wengine wakionesha kukata tamaa)
Kwa hiyo, iko wazi kwamba dr slaa atachaguliwa. Je, atashinda?