Dr Slaa asipogombea 2015 njia nyeupe kwa CCM

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,412
Histori inaonyesha wazi kwamba Viongozi wa Africa wanajaribu kugombea zaidi ya mara moja na wengi wao wanafanikiwa kuingia madarakani kwa sababu waligombea zaidi ya mara moja
mfano mzuri ni John Atta Mills wa Ghana,yeye aligombea mara tatu na akaibuka mshindi mara ya tatu
tunaona kwamba mgombea akigombea mara ya kwanza anakuwa kama anauza zaidi jina lake na uwezo wake kwamba anaweza kuongoza,mara ya pili anakuwa amekubalika kwa watu ambao hawakumkubali mara ya kwanza,
maana yangu ni kwamba Dr Slaa ana uwezo mkubwa wa kushinda kwa kuwa amekubalika zaidi tangu mara baada ya uchaguzi mkuu 2010,Chadema ikifanya makosa na kumsimamisha mtu mwingine itakuwa ni ngumu mno kushinda kwani inakuwa ni mara ya kwanza na historia inaonyesha jinsi ilivyo ngumu mpinzani kushika madaraka kwa mara ya kwanza
Rais Sata alishagombea zaidi ya mara mbili,na Wazambia walipata nafasi ya kumjadili kwa kuwa alithubutu mara ya kwanza na ya pili na kuwaonyesha wapiga kura kwamba ninaweza
alipokuja tena mara ya tatu alisomba kura zote kwani alishajijenga ndani ya mioyo ya wapiga kura kwamba anaweza
Uchaguzi wa madiwani umetufundisha kitu,Chadema mna kazi ya ziada,kukurupuka na kupiga kelele hakusaidii tena,ebu tukae chini tuanze kila kitu upya,fundisho hili ni kubwa mno kwetu wapenda mabadiliko,tulitegemea Chadema kuchukua zaidi ya kata 15,kazi inaendelea
 
Hii kitu wewe unacho jaribu kufanya kwa kizungu wanaita "coronations" na hii inatokana na enzi za ufalme ambapo mtu ambae hajapitia process yoyote anapewa utawala wa nchi kama mfalme. Kwa maana hiyo acha muda ukifika Chadema ipitia hatua zake za kutafuta mgombea wake na mmoja ashinde kidemokrasia. Hii ya kusema kwamba Slaa ni lazima apitishwe hiyo sasa itakua"coronation" na inaweza ika backfire kwenye uchaguzi mkuu. Kama kweli anakubali na wananchi wengi basi hata ndani ya chama chake atakua ana kubalika vya kutosha kupita kidemokrasia.
 
Histori inaonyesha wazi kwamba Viongozi wa Africa wanajaribu kugombea zaidi ya mara moja na wengi wao wanafanikiwa kuingia madarakani kwa sababu waligombea zaidi ya mara moja
mfano mzuri ni John Atta Mills wa Ghana,yeye aligombea mara tatu na akaibuka mshindi mara ya tatu
tunaona kwamba mgombea akigombea mara ya kwanza anakuwa kama anauza zaidi jina lake na uwezo wake kwamba anaweza kuongoza,mara ya pili anakuwa amekubalika kwa watu ambao hawakumkubali mara ya kwanza,
maana yangu ni kwamba Dr Slaa ana uwezo mkubwa wa kushinda kwa kuwa amekubalika zaidi tangu mara baada ya uchaguzi mkuu 2010,Chadema ikifanya makosa na kumsimamisha mtu mwingine itakuwa ni ngumu mno kushinda kwani inakuwa ni mara ya kwanza na historia inaonyesha jinsi ilivyo ngumu mpinzani kushika madaraka kwa mara ya kwanza
Rais Sata alishagombea zaidi ya mara mbili,na Wazambia walipata nafasi ya kumjadili kwa kuwa alithubutu mara ya kwanza na ya pili na kuwaonyesha wapiga kura kwamba ninaweza
alipokuja tena mara ya tatu alisomba kura zote kwani alishajijenga ndani ya mioyo ya wapiga kura kwamba anaweza
Uchaguzi wa madiwani umetufundisha kitu,Chadema mna kazi ya ziada,kukurupuka na kupiga kelele hakusaidii tena,ebu tukae chini tuanze kila kitu upya,fundisho hili ni kubwa mno kwetu wapenda mabadiliko,tulitegemea Chadema kuchukua zaidi ya kata 15,kazi inaendelea

Huyu PADRE hata akigombea mara kumi, hawezi kuwa Rais. Rais gani hata matatizo ya nyumbani kwake yanamshinda kutatua bwana?, Rais gani anafanyakazi kwa hisia? Rais gani anapambana na Vyombo vya dola? Rais gani mfitini, mchochezi, asiyeheshimu sheria za nchi?
 
Mkuu Dr Slaa na Prof Lipumba ni wagombea urais wa kudumu wa Chadema na CUF waendelee tu kugombea mpaka watazeeka lakini hakuna yeyote atakayekuwa rais wa Tanzania labda wagombea wengine.
 
Japo kuna ukweli fulani ndani yake ila ni vema tuache demokrasia ichukue mkondo wake.
 
Back
Top Bottom