Dr. Slaa asema maandamano ya wananchi kudai kura zao yapo

Jamani ugopeni sana mtu aliyeweka kiapo lakini baadaye akaasi kiapo hicho. Yaani hiyo dhambi ya Kumuasi Mungu ndio inayomtafuna na anataka kutuambukiza UASI na litimie lile la kumwaga damu.
Watakapo andamana akae mbele ili damu yake ndio imwagike ya kwanza akiingia hiyo IKULU akajitibu na siyo kuacha wananchi wakiwa vilema eti apate kiti ikulu. Dhambi ya UASI bado hajatubu kaanza kwa kumuasi mke wake wa kwanza sasa anawaambukiza wanachama.
Fungeni tumuombe toba ya kweli kwa Mungu ni mwingi wa REHEMA na atunusuru na hili.
 
Jamani ugopeni sana mtu aliyeweka kiapo lakini baadaye akaasi kiapo hicho. Yaani hiyo dhambi ya Kumuasi Mungu ndio inayomtafuna na anataka kutuambukiza UASI na litimie lile la kumwaga damu.
Watakapo andamana akae mbele ili damu yake ndio imwagike ya kwanza akiingia hiyo IKULU akajitibu na siyo kuacha wananchi wakiwa vilema eti apate kiti ikulu. Dhambi ya UASI bado hajatubu kaanza kwa kumuasi mke wake wa kwanza sasa anawaambukiza wanachama.
Fungeni tumuombe toba ya kweli kwa Mungu ni mwingi wa REHEMA na atunusuru na hili.

Wewe unamatatizo ya kiakili maana nawewe umewaasi watanzani na kuandamana na mafisadi, Huna maana yeyote kwetu.
 
mbona nimesikiliza video hii ya mwanakijiji tamko la SLAA kuhusu wabunge kutoka nje wakati raisi alizindua bunge, mwisho wa video SLAA anasema kwa mazungumzo ndiyo yatatumika kupata suluhusho kwa hiyo watu wawe watulivu. ni sauti yake mwenyewe
video ipo hapa sikiliza kipengele cha mwisho https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...zi-wa-wabunge-kugomea-hotuba-ya-jk-audio.html

sasa unaposema maandamano unaweza ukanipa source

Kama Slaa anasema mazungumzo ndio suluhisho pekee, mosi, hayo mazungumzo ya kutafuta suluhu yatafanyika kati ya Chadema na nani (CUF, PPT maendeleo, CCM )? Si serikali ambayo ya Kikwete kwani hawaitambui. pili, kama mazungumzo ndilo suluhisho pekee, kwa nini hawakutumia suluhisho hilo kutatua tatizo wanaloliona at the first place ( walkout inaimply kutokuwa tayari kusikiliza) tatu, CHADEMA either hamjui mnachokitaka au hamuelewi mnachokifanya, tafakarini kabla ya kutenda.
 
Ze Marcopolo hizo ni common nonsense! It's likely that you are not a great thinker but a lunatic fan of chichiem.
 
Hii nimenukuu kutoka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. CHADEMA tuna haki ya kudai mabadiliko ya Katiba kistaarabu ikiwemo Walkout.Soma

13.-(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki,bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.
Sheria ya Na.4
ya 1992 ib.8
Sheria ya 2000
Na.3 ib.5

(2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambaloni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.
(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya yawatu yatalindwa na kuamuliwa na Mahakama na vyombo
vinginevyo vya Mamlaka ya Nchi vilivyowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
Page 17

(4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya Mamlaka ya Nchi.
(5) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii neno "kubagua" maana yake ni kutimiza haja, haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao, kabila, pahala walipotokea, maoni yao ya kisiasa, rangi, dini,jinsia au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa aina fulani wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima, isipokuwa kwamba neno "kubagua" halitafafanuliwa kwa namna ambayo itaizuia Serikali kuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kurekebisha matatizo katika jamii.
(6) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria, Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia misingi kwamba:
(a) wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji kufanyiwa uamuzi wa Mahakama au chombo kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya mahakama au chombo hicho kingenecho kinachohusika.

Masharti ya Jumla

Haki ya wajibu
muhimu
Sheria
ya 1984 Na.15
ib.6
29.-(1) Kila mtu katika Jamhuri ya Muungano anayo haki yakufaidi haki za msingi za binadamu, na matokeo ya kila mtu
kutekeleza wajibu wake kwa jamii, kama zilzivyofafanuliwa katika ibara ya 12 hadi ya 28 za sehemu hii ya Sura hii ya Katiba.
(2) Kila mtu katika Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kupata hifadhi sawa chini ya sheria za Jamhuri ya Muungano.
(3) Raia yoyote wa Jamhuri ya Muungano hatakuwa na haki,hadhi au cheo maalum kwa misingi ya nasaba, jadi au urithi
wake.
(4) Ni marufuku kwa sheria yoyote kutoa haki, hadhi au cheo maalum kwa raia yeyote wa Jamhuri ya Muungano kwa misingi ya nasaba, jadi au urithi.
(5) Ili watu wote waweze kufaidi haki na uhuru vilivyotajwa na Katiba hii kila mtu ana wajibu wa kutenda na kuendesha shughuli zake kwa namna ambayo haitaingilia haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.

Mipaka kwa
haki
na uhuru na
hifadhi kwa haki
na wajibu
Sheria ya 1984
Na.15
ib.6
Sheria ya 1994
Na.34 ib.6

30.-(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
(2) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Sehemu hii ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wa binadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia sheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa mujibu wa sheria hiyo, kwa ajili ya: -

(a) kuhakikisha kwamba haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma haviathiriwi na matumizi mabaya ya uhuru na haki za watu binafsi;
(b) kuhakikisha ulinzi, usalama wa jamii, amani katika jamii, maadili


(3) Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika Sehemu hii ya Sura hii au katika sheria yoyote inayohusu haki yake au wajibu kwake, limevunjwa, linavunjwa au inaelekea litavunjwa na mtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anaweza kufungua shauri katika Mahakama Kuu.

(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika Katiba hii, Mahakama Kuu itakuwa na mamlaka ya kusikiliza kwa mara ya kwanza na kuamua shauri lolote lililoletwa mbele yake kwa kufuata ibara hii; na Mamlaka ya Nchi yaweza kuweka sheria kwa ajili ya-

(a) kusimamia utaratibu wa kufungua mashauri kwa mujibu wa ibara hii;
(b) kufafanua uwezo wa Mahakama Kuu katika kusikiliza mashauri yaliyofunguliwa chini ya ibara hii;
(c) kuhakikisha utekelezaji bora wa madaraka ya Mahakama Kuu, hifadhi na kutilia nguvu haki, uhuru na wajibu kwa mujibu wa Katiba hii.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
page 25

(5) Endapo katika shauri lolote inadaiwa kwamba sheria yoyote iliyotungwa au hatua yoyote iliyochukuliwa na Serikali au mamlaka nyingine inafuta au inakatiza haki, uhuru na wajibu muhimu zitokanazo na ibara ya 12 hadi 29 za Katiba hii, na Mahakama Kuu inaridhika kwamba sheria au hatua inayohusika,kwa kiwango inachopingana na Katiba ni batili au kinyume cha Katiba basi Mahakama Kuu ikiona kuwa yafaa au hali au masilahi ya jamii yahitaji hivyo, badala ya kutamka kuwa sheria au hatua hiyo ni batili, itakuwa na uwezo wa kuamua kutoa fursa kwa ajili ya Serikali au mamlaka nyingine yoyote inayohusika kurekebisha hitilafu iliyopo katika sheria inayotuhumiwa au hatua inayohusika katika muda na kwa jinsi itakavyotajwa na Mahakama Kuu, na sheria hiyo au hatua inayohusika itaendelea kuhesabiwa kuwa ni
halali hadi ama marekebisho yatakapofanywa au muda uliowekwa na Mahakama Kuu utakapokwisha, mradi muda mfupi zaidi ndio uzingatiwe.
 
chonde chonde chadema watuhakikishie wanataka mabadiliko ya katiba na kuundwa tume huru kweli au ndiyo wanataka post serikalini kama CUF . manake sisi ndiyo tutapigwa mabomu kwa kuandamana wakati wao wakiendelea kubembea mjengoni wakilamba mshiko wa siku sawa na mishahara ya miezi miwili ya kina sisi
 
Back
Top Bottom