Dr Slaa Apinga Matokeo Yanayoendelea Kutangazwa na Tume

Pamoja Dk, Uko sawa wameiba mno, bt cha msing we kusanya data zako zote kutoka kwa mawakala nchi nzima halafu tutajumlisha sisi kama chadema na kujua 2mepata nini ndo 2pambane fresh..
 
Dk tuelekeze tuingie msitu upi kwani hawa kuku hawawezi kuchezea mind za watu kiasi hii! Tuko tayari
 
Ukweli Haubadiliki kuwa uwongo VUVUZELA likilia..........Kama wamechakachua zitawatokea puani
 
mbona hkna hata diskashen ndefu hapa? ishu ni wa2 kuburuzwa mahakaman basi.
 
Hivi sasa ITV inapitisha tangazo kuwa Dr. Slaa amepinga matokeo ya Uraisi kuwa yamechakachuliwa na NEC na kuwa hayana uhusiano wowote ule na maamuzi ya wapigakura kura...........


... kwenu JK, EL, RA, ...., RZ1 kumbukeni tu kwamba hatimaye WaTZ hawadanganyiki tena. Wachache walidanganyika wakati fulani. Sasa hawadanganyiki tena. Jueni hilo. Mambo mlofanya ni HATARI sana. Waulizeni washauri wenu yaliyomo katika maandishi ya historia. Balaa mnayotaka kuleta hapa Tanzania bado inaepukika by doing the right thing. NGUVU ya UMMA mmeiona. Yalompata Ceausescu si mliyaona wakati ule?
 
na jk awambie hao mafisadi wenzake watengeneze barabara zao, hotel zao, la sivyo (iraq). kama mbwai mbwai tu. hatukubali katuuu. maisha yenyewe yako wapi bora ufe ukililia haki kuliko kufa kimyakimya. tumechoka
 
Dr Slaa wewe ni mkombozi wa taifa letu lililoharibiwa na hawa mafia ccm wakishirikia na nec serikali na vyombo vya dola..
Nina imani kuwa utachukua hatua zinazostahili kabla hiyo tume dhalimu haijato upupu uliochakachuliwa
 
Ni kweli matokeo hayako sawa na mahudhurio ya mikutano... mlidhani kila aliyekuwa anakuja kwenye mikutano amewapigia kura? I question uzalendo wa Dr. Slaa.
 
Humu ndani kuna usalama wa Taifa kibao.

Wanaandika kama vile wana uchungu sana.

Unamuuliza Dr. Slaa msitu upi uingie? Tena ndani ya JF iliyojaa UWT?

Labda tu kama na wewe ni Mwenzao. Wakitaka kuingia msituni, hawatatangaziana hapa JF.
 
Jamaa amejishusha credibility like big time... nampa pole sana kwa kweli...
 
Uchochezi ndio nini?! Yaani mtu anakudhulumu haki yako ukimpinga eti uchochezi!! Mat***ko yako! originally posted by coby

Ndugu yangu coby:Usiangaike na kauli za malaria sugu huyu ni "shake thoroughly before you use" uwezi kujifunza kitu chochote kutoka kwake kila akiongea, anaongea pumba
 
akapinge matokeo mahakamani sio ktk itv!!!
zubeda umenena,nahii Itv chadema wana shea au vp?mana hata wakat wakampeni walikua ni kupigia debe chadema na slaa,bahat yao jk hana visasi wangekoma itv ungekua ule utawala wa big ben che nkapa.
 
nilikuwa sijamskia Malaria Sugu muda. Naskia mko busy mnachezea data base ya NEC. I hope mna wataalamu wa Statistics vile vile kwasaabu so far upuuzi wenu umeanza kujidhihirisha hesabu hazi make sense kabisa.
 
JK has finished CCM kwa sababu uchumi wa nchi hii is going down to its knee! that was a very big mistake and CHADEMA is fighting a wining war strategicaly, It is done Selemani, way out for ccm.

AND JK AND CCM SHOULD UNDERSTAND THIS WE WILL NEVER COMPROMISE FOR OUR RIGHTS WE WILL DEMAND IT WHETHER THEY LIKE IT OR NOT, TRUST ME! soma hii analysis ya report ya waangalizi wa uchaguzi wa umoja wa ulaya

EU: CCM imebebwa na vyombo vya dola

Wednesday, 03 November

Elias Msuya

MWANGALIZI mkuu wa wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Ulaya, David Martin amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepata ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu baada ya kubebwa na vyombo vya dola, ikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Akitoa taarifa ya awali ya waangalizi hao jana jijini Dar es Salaam, Martin alisema uchaguzi huo, uligubikwa na kasoro nyingi licha kuendeshwa kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa.


Alipoulizwa na mwandishi wa habari wa gazeti hili kuhusu muundo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kama inatenda haki, Martin alisema hilo ameshaligusia katika taarifa yake.


"Hilo nimelisema kama umesoma kipengele cha nne cha taarifa yetu utaona kinasema, chama tawala kilinufaishwa na muundo wa utawala thabiti wa vyombo vya serikali ambao kiliurithi kutoka kwenye mfumo wa chama cha CCM enzi za chama kimoja ambao wakati mwingine ulikuwa hautambuliki vizuri," alisema.


Alisema kimsingi idadi kubwa ya viongozi wanaoteuliwa katika vyombo hivyo, wamekuwa wakiteuliwa na rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni mgombea katika uchaguzi, jambo ambalo linazua maswali kuhusu uhuru wa vyombo vya dola kukisaidia chama tawala.


Alisema CCM kilisaidiwa na vyombo vya dola katika kuendesha kampeni ikilinganishwa na vyama vingine vya siasa.


Kuhusu uhuru wa vyombo vya habari wakati wa uchaguzi, alitaja kitendo cha kutishiwa kufungiwa kwa gazeti la Mwananchi kutokana na kutoa taarifa hasi za serikali, alisema ilikwenda kinyume na uhuru wa kujieleza.


"Ujumbe wa Ulaya wa kufuatilia kwa kina uchaguzi mkuu nchini unadhania kwamba vitisho kama hivyo dhidi ya vyombo vya habari ni jaribio la kuuwekea mipaka uhuru wa kujieleza" alisema Martins.


Mapungufu mengine kwa mujibu wa Martin ni kuwalazimisha watu kugombea kupitia vyama bila kutumia chama ni kinyume na kanuni za kimataifa.


"Sharti hilo, linawanyima watu haki na fursa ya kusimama kugombea hasa wale ambao wangependa kushiriki katika uchaguzi kama wagombea binafsi. Matokeo yake linaiwekea mipaka ridhaa ya wapiga kura,"alisema.

Alisema tume hiyo, imesikitishwa na tabia yake ya kuchelewesha matokeo huku akitilia shaka uwazi katika kazi ya kukokotoa matokeo ya uchaguzi.

"Ucheleweshwaji wa kutangaza matokeo ni jambo lililotusikitisha kwasababu jambo hilo, limesabisha mashaka miongoni mwa wapiga kura na wagombea. Pia tuna mashaka na uwazi katika shughuli ya kukokotoa matokeo ya uchaguzi," alisema.


Naye kiongozi wa ujumbe kutoka Bunge la Ulaya, Maria Ndelcheva alishangazwa na kutojitokeza kwa wanawake kugombea urais licha ya wanawake hao kujitokeza kwa wingi kupiga kura.


"Japo tunaikaribisha hatua ya idadi ya viti vilivyotengwa katika Bunge la Taifa na katika Baraza la Mapinduzi, bado tunasikitishwa kutoona wanawake katika vyombo vya kusimia kazi nzima ya uchaguzi wala mgombea urais," alisema Ndelcheva.
 
ccm walishazoea kuiba then wana expect waliowaibia wanyamazeeee....Jk watchout unaweza ukakosa pakufikia,walianza na mawe kitakachofuata ni mabomu...mwaka huuitabidi juu ya gun proo uvae na anti mabomu jacket/nyavu kuzuia mawe:nono:
 
sio uchochezi huo?

akapinge matokeo mahakamani sio ktk itv!!!

Sasa aingie mtaani aone kilichomtoa kanga manyoya,teh teh teh.

Sio kutuvuruga huko? Ushindi wote huo haamini?

tutanata aende mahakamani na co blabla..................2...............

zubeda umenena,nahii Itv chadema wana shea au vp?mana hata wakat wakampeni walikua ni kupigia debe chadema na slaa,bahat yao jk hana visasi wangekoma itv ungekua ule utawala wa big ben che nkapa.

Siku hizi mnazidi kuongezeka naona madau mnayo pewa kumwaga upupu ni makubwa sana days are numbered
 
DR.tunaaamini uko makini usingekuwa makini hayo majimbo usingeyapata.Tunaomba utambue ushiriki wetu na tunakuhakikishia tuko pamoja songa mbele hadi kieleweke.Baada ya kuteuliwa kwako DR.kuongoza jahazi la kuitafuta ikulu binafsi nilifarijika kwani level yako si ubunge kwa sasa uko juuuuuuuuuuu sana.
  • Baada ya uchaguzi wansheria wako watafungua kesi ya kupinga matokeo
  • Wewe itabidi ufanye kazi ya katibu mkuu kwa kuzunguka nchi nzima kuwashukuru wananchi kwa kazi yao nzuri ya kukupigia kura bahati mbaya matokeo yamechakachuliwa
  • Itabidi uanzishe harakati za kuanzishe mashina ya nyumba ishirini shirini kwa kila kijiji ya chadema na kusajiri wanachama wapya
  • Sisi tuna uchungu sana itabidi ubuni utaratibu wa kuanzisha miradi ya kiuchumi ya chama ili tuanze kujiandaa kuimarisha chama kifedha
  • Itabidi uanzishe mipango ya kuinua uchumi wa chadema kwa muda mfupi, kati na mrefu
 
Back
Top Bottom