Dr. Slaa aonekana kuufyata mkia na kumkubali JK...kimyakimya....................

Msimlinganishe Slaa na Quattara. Quattara yeye alitangazwa na Tume ya Uchaguzi kuwa ndio mshindi , je Slaa alitangazwa hivyo???. Ndio maana Jumuiya ya Kimataifa imeisha toa kauli mbali mbali za kumshutumu Bagbo na kumtambua Quattara, je kwa Tanzania waliisha mshutumu JK na kumtambua Slaa???. Hii ina maana hata waangalizi wao waliona uchaguzi ulikuwa wa huru na wa haki, na lolote atakalo sema watampuuza tu.
Tume iliambiwa na JK,Kinana,Makamba na Usalama wataifa wamtangaze KIKWETE ,KIKWETE ni raisi wa tume sio wa watanzania
 
Dr. Slaa's best weapon are the courts of law...................silence means poor leadership.................If Dr. Slaa can't stand the heat he has no reason to complain...................hence he has no business being in the kitchen...................He impresses upon me as a whiner.....but nothing else....

CONSTITUION has stated clearly that president once declared by NEC no instrument can contest,when was the last time u heard slaa complaining?and what do u mean complaining?thats no complaining!thats a cry for justice
 
Kweli upeo wa kufikiri mdogo, Mungu akusamehe bureeee !!!!
Habari ndiyo hiyo Jakaya Kikwete mwenyewe anajua hajawahi kujibu tuhuma hadharani kwamba yeye hakuchakachua matokeo,alibambikizwa na Tume na hilo litamgharimu maisha yake yote yaliyobaki ya kuishi hap duniani kihoro kimemshika anakazana kukapua maji ya dawa kwenye glasi popote alipo
 
Haujakosea.

Hivi ulishajiuliza kwa nini wananchi walikuwa wakiandamana kushinikiza kutangazwa kwa matokeo ya ubunge wa baadhi ya maeneo lakin hawakuwa na haja ya kusubiri kusomewa matokeo ya uraisi katika majimbo yao?..wanaujua ukweli!!

Kuna hoja ya msingi ya kuwa na tume huru ya uchaguzi ili kuondoa mwingiliano wa tume na serikali iliyopo madarakani lakini atleast katika uchaguzi wa mwaka huu hakuna aliyeporwa ushindi wa uraisi, aliyeshinda ndiye aliyetangazwa na tume.
Acha kulinganisha matokeo ya Ubunge na Urais ni vitu viwili tofauti kabisa kwanini watu walikuwa wanaandamana kushinikiza kutangaziwa matokeo ya ubunge na si ya urais kwanza ya ubunge ni rahisi kuyapata na kura zake hata mtu wa lasaba anaweza kujitutumua kujumlisha imladi apate matokeo ya kata na kupata matokeo ya kata siyo vigumu sana hasa huku mjini.....Naendelea kusema JK na watu wake waliiba kura
 
Pamoja na haja ya kuwepo kwa katiba na tume huru ya uchaguzi lakini Dr. Slaa, Chadema na watanzania woote wenye akili timamu kwa ujumla wao wanajua kuwa Kikwete alishinda katika uchaguzi wa Rais, haya mengine yooote ni sirka tu za siasa za kiafrika, tutafika lakini!!
alishinda kwa asilimia ngapi?
 
You are simply suggesting we dont need to vote anymore!!

You mean Dr. Slaa will transform to be Mtikila in the court??

If you will recall and record down, Mtikila have done great and memorable things than any living and dead politician in opposition side, for this country! he have done so through COURT!!

so many things except u 4got to mention the money he borrowed from the very person he always accused of embezzlement...IRANIAN-CANADIAN-TANZANIAN,-ROSTAM AZIZ
 
Ni nani atasahau hizi picha.....................

pg17.jpg

Ni nani atasahau hoja hizi za Dr. Slaa.......................

Dk. Slaa apinga matokeo

*Asema Usalama wa Taifa wamechakachua kura
*Aeleza tofauti ya zinazotangazwa na za vituoni
*Sasa aiomba jumuiya ya kimataifa iingilie kati
*Ridhiwan asema ameshaona dalili za kushindwa

Na Maregesi Paul

MGOMBEA urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, ametoa tuhuma nzito za wizi wa kura akiihusisha Idara ya Usalama wa Taifa.

Amesema kuwa kitendo cha Idara hiyo kujiingiza katika siasa na kushiriki kubadili matokeo ya kura katika maeneo mbalimbali nchini ni cha hatari kwa kuwa viongozi wanaopatikana sio chaguo la wananchi.

Amesema kwamba kubadili matokeo kunaweza kuzua vurugu kwa kuwa wapigakura wanajua ukweli juu ya kinachofanywa.

Dk. Slaa alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Chadema, Kinondoni jijini Dar es Salaam, jana.

Mmoja wa watuhumiwa wa "uchakachuaji kura", Ridhiwan Kikwete, amejitokeza haraka kujibu tuhuma hizo, akisema Dk. Slaa ametoa madai hewa baada ya kuona kuna dalili zote za yeye kuukosa urais.

Ridhiwan alisema Dk. Slaa anachofanya ni kutapatapa kutokana na imani yake kwamba watu wengi waliokuwa wakifika kwenye mikutano yake wangempa kura.

"Asidanganywe na umati aliokuwa akiupata, awaulize kina Augustine Mrema au Freeman Mbowe, asichukulie kuwa wote aliowaona walikuwa wapigakura wake, wengine walifika kumshangaa mambo aliyokuwa akizungumza," alisema Rishiwan.

Maudhui ya mkutano wa Dk. Slaa yalikuwa kueleza jinsi Chadema isivyoridhishwa na mwenendo wa utoaji matokeo ya kura zilizopigwa Oktoba 31.

“Tumewaiteni hapa ili kuzungumzia mwenendo wa kura za urais kwani kwa mujibu wa Katiba yetu, Rais akishaapishwa hakuna chombo chochote kinachoruhusiwa kuhoji ushindi wake.

“Kwa kuwa NEC inaendelea kutangaza matokeo yanayoonekana kuwa na dosari, naomba nisema yafuatayo kwa kuwa ni ya msingi kwa mustakabali wa nchi hii.

“Kama wote tunaitakia mema nchi hii, naiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi ifute matokeo yote ya urais na kura zirudiwe upya kwa kuwa hayo yanayotangazwa sio matokeo ya wananchi.

“Hatuwezi kukubali matokeo ya dola, hizo si kura za wananchi, ni kura za Usalama wa Taifa ambao wameshiriki kuchakachua matokeo haya.

“Vile vile matokeo ya ubunge yaliyochakachuliwa katika majimbo yote, NEC iyafute na uchaguzi urejewe upya ili haki iweze kutendeka.

“Lakini, kama tabia hii ya kuchakachua matokeo haitakoma, siku uzalendo utakapotushinda na tukawaamuru wananchi waingie mitaani, tusilaumiwe.

“Hivi wananchi wakiingia mitaani nani atabaki, siyo CCM wala Chadema, CCM wasitake kutupeleka huko tusikotaka.

“Katika haya, jumuiya ya kimataifa lazima itoe hadharani ripoti yake, TEMCO nao wasiogope kuitoa, waitoe ili wananchi wajue kilichofanywa na CCM,” alisema Dk. Slaa.

Alimtaka Mkuu wa Usalama wa Taifa ajiuzulu wadhifa huo kwa maelezo kwamba ana hakika maofisa wa Idara yake wameshiriki kubadili matokeo ya kura zinazoelekea kumpa ushindi mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete.

Katika mkutano huo, mgombea huyo wa urais alitumia muda mrefu kueleza jinsi matokeo yalivyobadilishwa.

Alisema kuwa matokeo ya urais yanayotangazwa na NEC kutoka katika majimbo nchini yanatofautiana na matokeo yaliyoko katika vituo vya kupigia kura.

Katika hatua nyingine, alimtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Said Mwema, aongoze Jeshi hilo kwa mujibu wa Kitabu cha Haki na Wajibu kwa Mpiga Kura kilichotungwa na Jeshi la Polisi.

Ama kweli kimya cha Dr. Slaa kina mshindo mkuu......................

"CDM na Dr PhD" ninyi ni watu makini kuliko hawa wasioona mbali wanavyowaza!!!!!!!! Dr uzi ni ule ule!!!!! Tundu Lissu na team yake bungeni-wewe Dr na yule mwanasheria machachari Mabere kuelekea Jumuia ya Kimataifa na kwa Wananchi-hapa sisiemu hatapumua!!!!!!!!!!! Ukweli uko pale pale-matokeo aliyodandia kikwete hayakutokana na kura tulizopiga-mbona hazioani na matokeo yaliyobandikwa kwenye vituo!!!-wataumbuka tuuuuuu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Kazeni buti CDM ushindi halisi uko mlangoni-mtu asiwadanganye nanyi mkadanganyika!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Imani yetu sisi umma bado iko pale pale!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
CONSTITUION has stated clearly that president once declared by NEC no instrument can contest,when was the last time u heard slaa complaining?and what do u mean complaining?thats no complaining!thats a cry for justice

Wenye mamlaka ya kutafsiri hiyo katiba siyo wewe ila ni Mahakama kuu...................tafadhali tusiingilie kazi za wengine...........Mahakama hiyo hiyo mwaka 1995 kwenye kesi iliyofunguliwa na Mrema na wenzake kupinga Mkapa kutangazwa na NEC kuwa Raisi...........Mahakama Kuu ilisema ya kuwa hakuna kifungu chochote kile kitakachoizuiwa Mahakama hiyo kuchunguza kama NEC ilifuata sheria ya uchaguzi kama inavyowajibishwa na Ibara ya 41 (5)........................Mrema hakuwa na ushahidi wa ya kuwa NEC haikufuata sheria ya uchaguzi lakini safafri hii Chadema na Dr. Slaa walidai wanao......................sasa kwa nini wasitinge Mahakamani kama wao siyo matapeli?
 
"CDM na Dr PhD" ninyi ni watu makini kuliko hawa wasioona mbali wanavyowaza!!!!!!!! Dr uzi ni ule ule!!!!! Tundu Lissu na team yake bungeni-wewe Dr na yule mwanasheria machachari Mabere kuelekea Jumuia ya Kimataifa na kwa Wananchi-hapa sisiemu hatapumua!!!!!!!!!!! Ukweli uko pale pale-matokeo aliyodandia kikwete hayakutokana na kura tulizopiga-mbona hazioani na matokeo yaliyobandikwa kwenye vituo!!!-wataumbuka tuuuuuu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Kazeni buti CDM ushindi halisi uko mlangoni-mtu asiwadanganye nanyi mkadanganyika!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Imani yetu sisi umma bado iko pale pale!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Haya yote yatawezekana kama Mahakama imethibitisha hoja za Chadema kuwa NEC haikuzingatia sheria ya uchaguzi kama Ibara ya 41 (5) inavyoelekeza......mengineyo ni hisia tu ambazo hazitusaidi hata kidogo.................
 
Habari ndiyo hiyo Jakaya Kikwete mwenyewe anajua hajawahi kujibu tuhuma hadharani kwamba yeye hakuchakachua matokeo,alibambikizwa na Tume na hilo litamgharimu maisha yake yote yaliyobaki ya kuishi hap duniani kihoro kimemshika anakazana kukapua maji ya dawa kwenye glasi popote alipo

Ebu rejea ya GB hapo juu, usizidi kujivua nguo hadharani!!
 
Acha kulinganisha matokeo ya Ubunge na Urais ni vitu viwili tofauti kabisa kwanini watu walikuwa wanaandamana kushinikiza kutangaziwa matokeo ya ubunge na si ya urais kwanza ya ubunge ni rahisi kuyapata na kura zake hata mtu wa lasaba anaweza kujitutumua kujumlisha imladi apate matokeo ya kata na kupata matokeo ya kata siyo vigumu sana hasa huku mjini.....Naendelea kusema JK na watu wake waliiba kura

Bado haujanielewa..

Kura za urais, ubunge na udiwani zote zilikuwa zilibandikwa kwenye vituo vya kupigia kura baada ya kuhesabiwa; hivyo kila jimbo wananchi hao walikuwa wakiandamana walikuwa na data za matokeo ya ubunge, urais na udiwani kwa jimbo husika.

Cha kujiuliza, kwanini wananchi wale waliokuwa wanaandamana kuhakikisha kuwa matokeo ya ubunge katika jimbo lao yanatangazwa kwa haki lakini hawakuwa interested na matokeo ya uraisi?kwanini haja yao ilikuwa ni kutangazwa matokeo ya ubunge na sio ya urais?kwanini baada ya matokeo ya ujumla kudangazwa pamoja na Dr. Slaa kutoyatambua lakini wananchi hawakuonyesha kushtushwa na matokeo hayo na kuendelea na shughuli zao kama kawaida? wananchi hawa maskini, vijana hawa wa mtaani wanaujua ukweli.....
 
"Kama wote tunaitakia mema nchi hii, naiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi ifute matokeo yote ya urais na kura zirudiwe upya kwa kuwa hayo yanayotangazwa sio matokeo ya wananchi.

"Hatuwezi kukubali matokeo ya dola, hizo si kura za wananchi, ni kura za Usalama wa Taifa ambao wameshiriki kuchakachua matokeo haya.

"Vile vile matokeo ya ubunge yaliyochakachuliwa katika majimbo yote, NEC iyafute na uchaguzi urejewe upya ili haki iweze kutendeka.

"Lakini, kama tabia hii ya kuchakachua matokeo haitakoma, siku uzalendo utakapotushinda na tukawaamuru wananchi waingie mitaani, tusilaumiwe.

"Hivi wananchi wakiingia mitaani nani atabaki, siyo CCM wala Chadema, CCM wasitake kutupeleka huko tusikotaka.

"Katika haya, jumuiya ya kimataifa lazima itoe hadharani ripoti yake, TEMCO nao wasiogope kuitoa, waitoe ili wananchi wajue kilichofanywa na CCM," alisema Dk. Slaa.

Alimtaka Mkuu wa Usalama wa Taifa ajiuzulu wadhifa huo kwa maelezo kwamba ana hakika maofisa wa Idara yake wameshiriki kubadili matokeo ya kura zinazoelekea kumpa ushindi mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete.

Katika mkutano huo, mgombea huyo wa urais alitumia muda mrefu kueleza jinsi matokeo yalivyobadilishwa.

tatizo la chadema kila mara limekuwa ni utkelezaji wa dhamira zake....................hapa walilia na ujasusi wa ccm na jk wake...................lakini ahadi zote ziliishia patupu..........................hakuna utekelezaji au ufuatiliaji...............................hata hili la katiba mpya tusitegemee miujiza kwa hawa waheshimiwa ambao kero yao siyo kuhakikisha tume ya raisi inatoa fursa sawa kwa raia wote kufikiriwa bali na wao wapewe nafasi mbili za kusimika watu wao......................what a shame?
 
M-Mbabe............bana......................face the truth how can Dr. Slaa be a leader without possessing persuasive powers............Are you not questioning his influential credentials when you avers................wd stop short at the suggestion that Slaa can go all out and make big decisions singlehandedly without his party's consent.

Ushawishi wake uko wapi?

What is the use to make an an outrageous claim that a presidential election has been stolen and you renege to seek court intervention?
"Kimya Kingi Kina Mshindo"
Sijajua Unataka nini.kama Dr.angalifanya unayotaka nchi hii ingeingia katika matatizo makubwa na mwisho wa siku mngesema wapinzani wanasababisha vita..Hakufanya hivyo kwa sababu ya busara tu aliyokua nayo mnaanza tena chokochoko zenu.Watz hatutakua na akili mpaka tutandikane ndio tutakapoheshimiana.

Hilo la mahakama unataka liweje? Kama sheria inasema hakuna rufaa sasa unataka waende kufanya nini?ndio maana issue ya msingi hapa ilikua ni tume huru ambayo CCM hawaitaki kwa hali yoyote.Chukua mfano wa mgombea binafsi ni suala la kikatiba na liko wazi kabisa katika haki za binadamu.

Mahakama hiyohiyo unayoitaka wewe imefanya nini?Kwa hiyo wakati mwingine usikurupuke na kuongea kama vile umetoka kuanguka kwenye mti.
 
JK ni mtu asiyekubalika na mtu yeyote mwwnyw akili timamu,hata mtoto wa miaka mitatu anayeelewa mambo kidogo ,hamwamini na kumkubali iweje Dr Slaa.
Mnataka aongee nini mengi ya aliyowaambia ndio leo mnayashuhudia.
Mf.Mkiichagua CCM mtakuwa mmechagua majanga,leo hii Kila mtanzania analia hata wewe unaepost utumbo hapa,maisha ni magumu kila inapofika leo ni bora ya jana.Kwa kesi hii Dr aongee nini.

Ukimuelewa mtu utajua ufanisi wake,Dr si mtu wa kukurupuka na kuongea ovyo ni mtu anayetumia mda mwingi kutafakari na kutenda zaidi.Inawezekana hapa Mjini Dar hammsikii,lakini vipo vijiji na mikoa ambayo inamsikia Dr na kumuona akijenga Chama Chake.

Kazi kubwa aliyonayo sasa si kuendelea kuongea bali ni kujenga chama for your future.Alisema mengi sote ni mashahidi na yote aliyoyasema tunayashuhudia leo.Yapo maeneo tunapita wananchi wanakumbuka sana kama wewe unaeandika pumba hukumbuki njoo nikupe CD za hotuba zake.

Pili anachofanya ni kuhakikisha anautumia mda huu kujifunza zaidi ni njia zipi zitatumika kuirudisha Tanzania iliyokuwa ikifikiriwa na mwalimu Nyerere baada ya vibaka kufilisi nchi.
More than that hamumtendei haki.
 
Asante first lady wa ukweli, yaani mijitu ni migumu kuelewa halafu hii ndio inayozidi kuwaambukiza ujinga hata watanzania wa chini wenye kutaka mabadiliko. na hapo Kwenye Bold nazihitaji hizo CD nizipeleke kijijini kwangu maana nina mpango wa kugombea udiwani kwenye kata yangu ya Bumera jimbo la Bariadi Magharibi
 
Josephine, waganga njaa Tanzania ni wengi sana, wanahakikisha CCM inashinda ili wazidi kuneemeka na vi 10% ya mikataba feki!! wakiiuza tanganyika yao kwa ujira mdogo. nakumbuka darasa la nne niliposoma mikataba ya ulaghai niliumia sana kumbe bado hadi leo ipo; wasaliti walikuwepo enzi hizo na hata leo hii wapo na ndiyo hao wanaosafiri ulaya kusainisha mikataba feki tena usiku wa manane hotelini eti ni urgent as if madini yataoza wasipo sign usiku.

Nani asiyejua jamaa ni kaole?
 
Back
Top Bottom